Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Vidonda vya tumbo


Vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo hutokana na mashambulizi ya bacteria wajulikanao kama helicobacter pylori au michubuko inayo tokana na chemikali zinazo patikana katika tumbo ambazo husaidia kumeng'enya chakula.Vidonda hivyo hutokea katika njia ya chakula yaweza kuwa kooni(oesophagus),kwenye utumbo mdogo (duodenum),pia katika utumbo au mfuko wa kuhifadhi chakula (gastric).


Aina za vidonda vya tumbo.

Kuna aina kadhaa ya vidonda vya tumbo navyo vimegawanyika kulingana na sehemu ambavyo vidonda hutokea navyo ni:

.Vidonda ambavyo hutokea kooni , kitaalamu hujulikana kama oesophagus ulcer.

.Vidonda ambavyo hutokea sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo kitaalamu hujulikana kama deudenal ulcer.

.Vidonda ambavyo hutokea tumboni au kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula kitaalamu vidonda ivyo hujulikana kama gastric ulcer.





Nini husababisha kutokea kwa vidonda vya tumbo?

Kwa kawaida vidonda vya tumbo hutokea kipindi bacteria (helicobacter pylori)  au asidi inapo shambulia sehemu za ndani za koo, utumbo mdogo  na utumbo wa huhifadhi chakula.Mashambulizi ya vijimelea ivyo au kemikali izo husababisha michubuko katika Tabaka  laini la kuta za njia ya chakula, kadiri vimelea hao na chemikali zinavyo zidi kushambulia tabaka hilo michubuko huzidi kukua na kutokea kidonda ambacho husababisha maumivu katika nyakati tofauti pia kutokwa na damu.Kazi kubwa ya tabaka ilo laini katika njia ya chakula ni kuhakikisha njia ya chakula halishambuliwi na bacteria ,pia hali haribiwi na chemikali ambazo huzalishwa ili kusaidia kumeng'enya chakula. Kwaiyo kunasababu mbalimbali ambazo huchangia mtu kupata vidonda vya tumbo nazo ni:



.Maambukizi ya bacteria.

Vimelea vya helicobacter pylori hupatikana  katika tabaka la mucus katika njia ya chakula ambalo huzikinga kuta za tumbo,katika hali ya kawaida vimelea hivi vinakuwa havileti madhara kwa baadhi ya watu lakini kwa watu wengine vimelea hivi husababisha wapate vidonda vya tumbo.
Kwa kawaida Kinga za mwili huulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa ,pia kutokana na sababu mbalimbali wakati mwingine Kinga iyo hushindwa kuwadhibiti vimelea hao,kwaiyo kushindwa kwa Kinga ya mwili kuwadhibiti wadudu hao husababisha Maambukizi ya kudumu katika kuta za tumbo.Kuharibika kwa kuta za tumbo husababisha Kichocheo Cha gastrin ambacho huchochea utolewaji wa tindikali ya hydrochloric kutoka kwenye kuta za tumbo kizalishwe kwa kiwango kikubwa na kusababisha michubuko ya kuta za tumbo. Kichocheo Cha gastrin huzalishwa na kuta za tumbo.



.Unywaji wa pombe.

Unywaji wa pombe huchangia kukwangua kwa utando laini wa kuta za tumbo ,pia huchochea uzalishwaji wa tindikali ya hydrochloric kwa kiwango kikubwa ambayo husababisha michubuko tumboni.

.Matumizi ya dawa za kutuliza maumivu kwa muda mrefu.

Dawa hutumika kutibu magonjwa,lakini licha ya dawa hizo kutibu maradhi hayo kwa upande mwingine dawa hizo huleta maudhi madogo madogo.Kwaiyo dawa za maumivu licha ya kutuliza maumizu dawa hizi huleta maudhi mfano kukwangua utando laini tumboni ambao hulikinga tumbo dhidi ya tindikali ,kuharibiwa kwa utando huo husababisha kuta za tumbo kukwanguliwa ,pia kadiri matumizi ya dawa hizi yanavotumika Mara kwa Mara ndipo husababisha kutokea kwa vidonda.

.Uvutaji sigara

Uvutaji sigara huongeza hatari ya kupata vidonda vya tumbo kwa wale ambao wana maambukizi  ya vimelea vya helicobacter pylori.

.Msongo wa mawazo.

Kipindi cha nyuma ili aminika kwamba mawazo husababisha vidonda vya tumbo,kutokana na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zimeonyesha mawazo siyo moja ya sababu ya kuugua vidonda vya tumbo bali mawazo huleta maumivu makali kwa wale ambao tayari wana vidonda vya tumbo, pia kuna baadhi hupatwa na mawazo kutokana na  sababu tofauti mfano kuungua moto ,au kufanyiwa upasuaji sasa kwa mujibu wa tafiti mawazo ya tokanayo na sababu hizi ndiyo huongeza hatari ya mtu kupata vidonda vya tumbo.


.Chakula.

Kuna baadhi ya watu huamini chakula husababisha vidonda vya tumbo jambo ambalo siyo kweli, bali aina ya chakula ambacho mtu anakula au anakunywa ndiyo husababisha hali ya vidonda kuwa mbaya zaidi.







Dalili za vidonda vya tumbo



.Maumivu  makali au kiungulia maeneo ya chembe ya moyo.

Maumivu haya hutofautiana kutokana na sehemu ambayo vidonda vimetokea.Mfano mtu mwenye vidonda tumbo (Gastric) hupata maumivu wakati wa kula au baada ya kula na mwenye vidonda katika utumbo mdogo hupata Maumivu makali anapokuwa hajapata chakula na hupata nafuu apatapo chakula.

. Kichefuchefu.

.Kutapika.

.Kupoteza hamu ya kula na Kupungua uzito.

.Tumbo kujaa gesi.

.Kupata haja kubwa yenye rangi nyeusi na yenye harufu mbaya Sana.



Soma,ujue-ugonjwa-ya-kisukari-na-madhara-yake.html

Vipimo vya vidonda vya tumbo


.kipimo cha damu ambacho hufanywa ili kuangalia uwepo wa vimelea vya helicobacter pylori.


.kipimo cha haja kubwa kuangalia vijimelea Kama vipo hai au vmekufa.


.Barium meal ili kuthibitisha uwepo wa vidonda.

.Gastroscopy kuangalia moja kwa moja kwenye tumbo la mgonjwa.











 Madhara ya vidonda tumbo

.kutoboka kwa kuta za tumbo na kupelekea vitu kuingia nje na mfuko wa tumbo.


.Kansa ya tumbo


.kuziba kwa njia ya chakula


.



Jinsi  ya kujikinga na vidonda tumbo

.Punguza matumizi ya dawa za kulevya,
mfano,pombe,kuchanganya  pombe dawa, uvutaji sigara.

.Epuka kupata maambukizi ya wadudu wanaosababisha vidonda japo haijawa wazi ni jinsi gani huenea.



Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts