Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Ujue ugonjwa ya kisukari na madhara yake




Kisukari

Kisukari ni miongini mwa magonjwa ambayo huathiri afya ya watu wengi duniani kote , Tanzania ni miongini mwa nchi ambayo  wananchi wake ni waanga pia wa ugonjwa wa kisukari kutokana madhara makubwa yanayo letwa na ugonjwa huo.

Katika Hali ya kawaida sukari ni muhimu Sana katika maisha ya binadamu kwasababu ndicho chanzo kikubwa Cha nishati mwilini lakini sukari hiyo haitakiwi izidi kiwango Cha kawaida Cha uhitaji wa mwili, pindi kiwango Cha sukari kikizidi mwilini kuliko mahitaji ya kawaida ndipo hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari huongezeka.



Je  sukari hufanya kazi gani mwilini?


Sukari ni chanzo kikubwa Cha nishati kwa seli ambazo huunda misuli na tishu nyingine. Nishati katika mwili  hutoka katika vyanzo vikuu viwili ,kutoka katika chakula ambacho tuna kula kila siku na kingine ni kutoka kwenye ini,viungo mbalimbali katika mwili uhitaji sukari ili viweze kufanya kazi vizuri ikiwemo ubongo.

Sukari hufyonzwa na mishipa ya damu ili ikatumike kwenye seli na tishu za mwili kwa msaada wa kichocheo Cha insulin na kisha sukari ya ziada iliyo katika mfumo wa glucose hubadilishwa kwenda kwenye mfumo wa glucagon na kuhifadhiwa na I'm kwa matumizi ya baadae.

Pindi kiwango Cha nishati kinapokuwa kimepungua mwilini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuto kula kwa muda mrefu  ,nishati iliyo hifadhiwa na ini hubadilishwa na kupelekwa kwenye mfumo wa glucose kwa matumizi ya mwili.






Je kichocheo Cha insulin hufanyaje kazi?

Insulin ni kichocheo ambacho huzalishwa na tezi ya kongosho,Mara baada ya insulin kutengenezwa huingia kwenye mishipa ya damu kwa lengo la kuisaidia glucose ambayo imetengenezwa kutoka kwenye chakula kuingia na kwenda kutumika na seli na tishu mbalimbali ambazo huunda mwili,kwa kufanya ivyo ndipo insulin inakuwa imefanikiwa katika kazi ya kupunguza sukari kwenye damu na Kuacha kiwango kidogo Cha glucose  kwa matumizi ya kawaida ya mwili.





Je,ugonjwa wa kisukari hutokeeje?

Ugonjwa wa kisukari hutokea pale tezi ya kongosho inaposhindwa kuzalisha kiwango Cha kutosha Cha kichocheo Cha insulin au mwili kushindwa kutumia insulin iliyozalishwa na kongosho ili kudhibiti kiwango Cha sukari kwenye damu ,mwili kushindwa kutumia kichocheo hicho husababisha kuongezeka kwa kiwango Cha sukari kwenye damu.



Soma:chanzo-cha-ulemavu-wa-akiliupungufu-wa.html


Aina za ugonjwa wa kisukari.

i.Kisukari aina ya Kwanza.

Ni aina ya kisukari ambacho hutokana na kuharibika au kukosekana kwa seli ambazo hutengeneza kichocheo Cha insulin katika kongosho ivyo kusababisha kukosekana au upungufu wa kichocheo Cha insulin kwenye damu.Vitu ambavyo husadikika kusababisha aina hii ya kisukari ni pamoja na Kinga ya mwili wenyewe kuzishambulia seli ambazo huzalisha insulin( auto immune) kwenye kongosho Hali hii husababisha kuwepo kwa kiwango kidogo au isiwepo kabisa jambo ambalo husababisha kuongezeka kwa sukari kwenye damu.

Kwaiyo kutokana na kutokuzalisha au kuzalishwa kwa kiwango kidogo Cha insulin basi magonjwa mwenye aina hii ya kisukari hulazimika kutumia sindano za insulini ili kupunguza sukari katika maisha yao yote. Pia aina hii ya kisukari kwa jina lingine hujulikana Kama kisukari ambacho hutegemea insulin yaani insulin dependant diabetic melitus(IDDMT).



ii.Kisukari aina ya pili

Ni aina ya kisukari ambacho husababisha na vile mtu unavyo ishi  Mara nyingi aina hii ya kisukari hutokea ukubwani. Aina hii ya kisukari  hutokana na seli kushindwa kutumia insulin ambayo imezalishwa na tezi ya kongosho na matokeo yake sukari hukusanyika kwenye damu.

Sababu ambazo huchangia kupata aina hii ya kisukari  ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa na kutokufanya mazoezi.Jina lingine la aina hii ya kisukari hujulikana Kama kisukari ambacho hakitegemei insulin yaani non insulin dependant diabetic mellitus(NIDDM).


iii.Kisukari ambacho hutokana na mimba.

Ni aina ya kisukari ambacho  huwapata wakina mama wajawazito.Hata ivyo Kuna baadhi ya akina mama Mara baada ya kujifungua kisukari icho hukoma japo kunawengine kisukari huendelea hadi baada ya kujifungua na kupelekwa kuingia katika aina ya pili ya kisukari.




Nini husababisha kisukari?

i.Aina ya kwanza ya kisukari

Visababishi vya aina hii ya kisukari mara nyingi ni magonjwa ya kinga ya mwili kushambulia tezi ya kongosho ambayo huzalisha kichocheo Cha insulin, sababu zinazopelekea kinga ya mwili kushambulia tezi ya kongosho hazijafahamika bado lakini uhusiano uliopo kati ya mazingira na vinasaba huchangia kwa kiwango kikubwa Cha ugonjwa. Visababishi ambavyo huchangia ni pamoja na historia ya familia, huchangia kwa kiwango kikubwa kupata kwa ugonjwa wa kisukari. Pia kwa watoto wadogo, kuanzia kumpa maziwa ya ng'ombe  mtoto mdogo kabla hajatimiza miezi sita na kunywa maji ambayo yana nitrate huchangia kwa kiwango kikubwa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.


ii.Aina ya pili ya kisukari.

Maranyingi visababishi vya aina hii ya kisukari hutokana na vile mtu anavyo ishi,sababu Kama vile kuongezeka kwa umri,magonjwa ya Moyo,kuongezeka uzito au unene ulopitiliza ,kutokufanya mazoezi ,kisukari ambacho hutokana na mimba na maambukizi katika tezi ya kongosho huchangia kwa kiwango kikubwa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.





Dalili za ugonjwa wa kisukari.

Dalili za ugonjwa wa kisukari humtofautisha kutokana na kiwango Cha sukari ambacho kipo kwenye mkojo,dalili hizo ni Kama:

.Kuona mawenge mawenge au maluweluwe.

.Kichefu chefu

.Kutapika.

.Kunywa maji Mara kwa Mara (polydipsia).

.Kukojoa Mara kwa Mara(polyuria).

.Kula Mara kwa Mara (polyphagia).

.Uchovu wa Mara kwa Mara.

.Kupungua uzito.




Vipimo.

.Kwa mtu ambae ambaye hajala kitu chochote kiwango Cha sukari kwenye damu inatakiwa kiwe chini ya Saba.

.Kwa mtu ambaye amekula kiwango Cha sukari kwenye damu inatakiwa kiwe juu ya kumi na moja.





Je yepi ni madhara yatoka nayo na kisukari?

Madhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari huanza taratibu,kadiri unavyo kuwa na sukari na unavyo shindwa kuchukua hatua juu ya sukari iyo ndivyo hatari ya kupata madhara makubwa huongezeka,pia ikumbukwe madhara yatoka nayo na kisukari huweza kuhatarisha maisha ya mtu.Madhara ayo ni Kama:

.Matatizo ya Moyo na mishipa ya damu,mfano Shinikizo la Moyo,kiharusi, kusinyaa kwa mishipa ya damu.

.Figo kushindwa kufanya kazi vizuri (nephropathy),Figo imeundwa na vishipa vidogo vidogo vijulikanavyo kama glomerular,kazi kubwa ya vishipa ivi ni kuchuja taka kutoka kwenye damu,kwaiyo kiwango kikubwa Cha sukari kwenye damu huweza sababisha kuziba kwa vifuko ivyo na kusababisha Kupungua kwa utendaji kazi wa Figo.

.Matatizo ya macho(retinopathy).kiwango kikubwa Cha sukari katika damu pindi kikifika kwenye vishipa vidogo vidogo ambavyo hupatikana ndani ya jicho husababisha madhara kwenye jicho na matokeo yake no upofu.

.Matatizo ya ganzi na kupooza endapo kisukari kitaathiri mishipa ya fahamu.

.Kupungua kwa nguvu za kiume.

.Kuvurugika kwa vichocheo vya mwili.

.Hatari ya kupata maambukizi kutokana na kushindwa kufanya kazi vizuri kwa seli nyeupe za damu.

.Kwa wamama wenye kisukari kinacho tokana na ujauzito kupata  aina ya pili ya kisukari.

.Kifafa Cha mimba ambacho huambatana na Kifafa Cha mimba.






Ufanye nini kujikinga na kisukari?

.Acha au punguza matumizi ya pombe.

.Punguza matumizi ya chumvi kupita kiasi kwenye chakula.

.Hakikisha inakuwa makini Sana na vyakula vya wanga.

.Hakikisha unafanya mazoezi ili kupunguza uzito ambao hukuhatarisha kupata ugonjwa wa kisukari.


Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts