KIUNGULIA WAKATI WA UJAUZITO.
Kiungulia ni miongoni mwa maudhi madogo katika mfumo wa chakula ambayo huwapata wajawazito wengi,hali hii hutokea Kama mabadiliko ya kawaida wakati wa ujauzito.
Kiungulia huweza tokea muda wowote katika ujauzito,lakini imebainika wanawake wengi hupatwa na kiungulia katika miezi ya mwisho za ujauzito.
Kwa kawaida kiungulia hutokea zaidi Mara baada ya kula,wakati kiungulia kinatokea mjamzito huhisi Koo au kifua kuchoma au kuungua kutokana na asidi za tumbo kurudi kwenye umio.
Baadhi ya Mambo ambayo huchangia kutokea kwa kiungulia.
Kuna baadhi ya Mambo huelezwa huchangia kutokea kwa kiungulia wakati wa ujauzito,Mambo hayo ni Kama.
.Ulaji wa chakula kingi kwa wakati mmoja.
.Mjamzito kula chakula ambacho kimepikwa kwa mafuta mengi.
.Kula na kunywa maji mengi wakati wa kula.
.Pia Kula masaa machache kabla ya kwenda kulala.
.Kufanya mazoezi mda mchache baada ya kula mfano kuinama.
.Uvaaji wa mavazi ya kubana katika ujauzito pia inaelezwa huchangia kutokea kwa kiungulia.
.Pia Unywaji wa vinywaji ambavyo vimetengenezwa kwa caffeine huchangia utokeaji wa kiungulia.
Je kiungulia hutokeaje?
Kama nilivyo eleza mwanzo kipindi Cha ujauzito mabadiliko mbali mbali hutokea katika mwili wa mjauzito ili kuruhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto pia ikiwa ni maandalizi ya mtoto kuzaliwa.Moja ya mabadiliko ambayo hutokea ni mabadiliko ya homoni au vichocheo mwilini hususani kichocheo Cha progesterone.Katika kipindi Cha ujauzito kichocheo hiki huzalishwa kwa kiwango kikubwa mwilini,lakini moja kati ya athari ya kichocheo hiki ni kulainisha sehemu mbali mbali za mwili. Katika mfumo wa chakula moja ya sehemu ambazo huathiriwa na kichocheo hiki ni pamoja na vali iliyopo Kati ya umio (oesophagus) na utumbo,kazi kubwa ya vari hii ni kuzuia asidi za tumbo kurudi kwenye umio,kulainika kwa vari hii husababisha asidi za tumbo kurudi kwenye umio ndipo Mama huhisi Koo kuchoma au Moto kooni.
Pia kiungulia hutokea zaidi katika kipindi Cha mwisho Cha ujauzito,moja ya mabadiliko ambayo hutokea ni kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo la uzazi,katika miezi ya mwisho tumbo la uzazi huwa kubwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto,kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo husababisha uwepo wa mkandamizo mkubwa katika tumbo la chakula,kuongezeka kwa mkandamizo tumboni husababisha vari Kati ya umio na tumbo kuzidiwa ivyo kuruhusu asidi za tumbo kwenda kwenye umio ivo mjamzito kuhisi Koo kuungua.
Sehemu nyingine ambayo huathiriwa na kichocheo Cha progesterone ni utumbo ambao shughuli za umeng'enywaji wa chakula hufanyika,kuathiriwa kwa utumbo husababisha chakula kumeng'enywa taratibu ivyo kusababisha mabaki ya chakula ambayo hutolewa Kama uchafu wa mwili kukaa zaidi ndani ya mwili,hivyo nirahisi zaidi kwa mjamzito kupata kiungulia.
Ushauri.
Ili mjamzito apunguze atari ya kupatwa na kiungulia Kuna Mambo kadhaa ambayo hutakiwa kuzingatia au kuyafanya,Mambo hayo ni.
.Kama kiungulia hutokea Mara kwa Mara Mama hushauriwa zaidi kutumia maziwa kwa wingi.
.Kutokana na uhitaji mkubwa wa chakula wakati wa ujauzito,Mama hula chakula kingi kwa wakati mmoja hivyo kuwa rahisi zaidi kupata kiungulia hivyo basi inashauriwa mjamzito kula chakula kidogo Mara nyingi zaidi ili kukidhi mahitaji yake na mtoto.
.Imezoeleka zaidi katika familia zetu Mara baada ya kula ni kulala hususani katika nyakati za usiku Jambo ambalo ni hatari kiafya,kwaiyo kwa mjamzito inashauriwa usile chakula Muda mfupi kabla ya kwenda kulala,kwasababu wakati wa kulala utendaji kazi wa mwili hupungua ivyo ni rahisi kupata kiungulia.
.Pia inashauriwa si vema kula na kunywa maji mengi kwa pamoja wakati wa ujauzito.
.Utumiaji wa vyakula ambavyo vimeandaliwa kwa mafuta mengi nao ni vema ukaepukwa.
.Inaelezwa pia Uvaaji wa nguo za kubana wakati wa ujauzito ni vema ukaepukwa, kwasababu nguo hizo huongeza mkandamizo tumboni ivyo kuwa rahisi kwa asidi za tumbo kurudi kwenye umio.
.Pia inashauriwa kukaa angalau nusu Sasa Mara baada ya kula.
.Siyo vema pia kuinama mara baada ya kula kwasababu Ni rahisi zaidi asidi za tumbo kuja kooni ivyo kuhisi kiungulia.
.Matumizi ya mto wakati wa kulala pia hushauriwa zaidi ili kuinua sehemu za juu za mwili.
.Unywaji wa vinywaji ambayo vimetengenezwa kwa caffaine Ni vema ukaepukwa.
.Matumizi ya pombe pia inashauriwa kuepukwa ,licha ya pombe kuleta athari kwa ukuaji wa mtoto tumboni pia pombe yaweza sababisha kulegea kwa vari ivyo asidi za tumbo kurudi kooni.
.Pia inashauriwa zaidi mjamzito kulala upande wake wa kushoto,tafiti mbalimbali zilizo fanywa zimeeleza kulala upande wa kulia tumbo huwa juu zaidi ya umio ivyo Ni rahisi asidi za tumbo kurudi kooni.
Endapo utazingatia Mambo tajwa hapo juu na kiungulia kikawa kinasumbua Bado ni vema kumwona daktari wako akupe dawa za kupunguza asidi tumboni.
Pia usikose kufuatilia muendelezo wa somo hili wakati ujao.
Vile vile Kama unataka kujiunga katika kikundi Cha whatsap tuma neno NIUNGE kwenda namba 0712106789.
KARIBU TUKUSHAURI.

No comments:
Post a Comment