Home »
» Maudhi madogo madogo katika kipindi cha ujauzito
Maudhi madogo madogo katika kipindi cha ujauzito
MAUDHI MADOGO KWA MJAMZITO.
Mwanamke kushika mimba huleta furaha Kati yake pamoja na mumeo na ukifikiri nikipindi ambacho kilisubiriwa kwa Muda mrefu pia Kila mmoja hufurahia kuwa mzazi Mara baada ya mtoto kuzaliwa.
Licha ya kuwa kipindi ambacho huleta furaha katika familia mwanamke anapokuwa ni mjamzito Kuna mabadiliko mengi ambayo hufanyika katika mwili wake,kutokea kwa mabadiliko hayo husababisha mjamzito apate karaha na pengine hata kupoteza furaha anayo kuwa nayo juu ya mtoto ambaye yupo tumboni.
Katika kipindi Cha awali Cha ujauzito , wajawazito wengi wana shindwa kukubaliana na mabadiliko ambayo yanakuwa yanaendelea kutokea katika miili yao ,lakini baadae hutambua kwamba maudhi ayo ni kiashiria Cha uwepo wa ujauzito.
Maudhi ayapatayo mjamzito ni ya kawaida na huitwa madogo kwasababu siyo yenye kuhatarisha uhai wa mama ,japo yakizidi yaweza yakahatarisha usalama wa mama pamoja na mtoto tumboni.Kwa upande mwingine maudhi haya huonekana ni makubwa kwa Mama kutokokana na karaha ambazo mjamzito mwenyewe huzipata ,pia katika kipindi hiki mjamzito anatakiwa kutafuta suluhu dhidi ya maudhi ayo ili yasije yaka athiri mambo mengine katika familia.
Maudhi hayo Mara nyingi huleta karaha zaidi katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito,Kuna mengine yaweza yaka koma japo Kuna mengine huwepo hadi kuzaliwa kwa mtoto pia maudhi hayo yaweza tofautiana Kati ya mjamzito .
Pia maudhi ayo hugawanyika kutokana na mifumo mbali mbali iliyopo katika miili yetu binadamu.
MAUDHI KATIKA MFUMO WA MKOJO.
Kukojoa Mara kwa Mara.
Hali ya mjamzito kubanwa na mkojo Mara kwa Mara hutokea zaidi katika kipindi Cha miezi mitatu ya awali ya ujauzito.Katika kipindi hiki Cha miezi mitatu ya awali ya ujauzito mfuko wa uzazi(uterus) unakuwa Bado upo ndani ya nyonga za mwanamke na kufanya kibofu kikose nafasi kutokana na mfuko huo kuongezeka ukubwa, kuongezeka ukubwa wa tumbo la uzazi huongeza mkandamizo katika kibofu Cha mkojo na kusababisha mjamzito kukojoa Mara kwa Mara.
Miezi mitatu inayo fuata Mara baada ya kumalizika kwa miezi mitatu ya awali hali ya kukojoa Mara kwa Mara hupungua kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo la uzazi,kadiri tumbo la uzazi linavyozidi kukua nafasi Kati ya tumbo ilo na kibofu Cha mkojo huongezeka hivyo kusababisha kupungua kwa mkandamizo katika kibofu ambao ulikuwepo awali.
Katika miezi ya mwisho ya ujauzito hali ya mjamzito kubanwa na mkojo Mara kwa Mara hurudi kwa Mara nyingine tena, kwasababu mtoto anakuwa anashuka tayari kwa kujifungua,kwahiyo mjamzito hukojoa Mara kwa Mara kutokana na mkandamizo unaotokana na mtoto,hali hii husababisha mjamzito kwenda haja ndogo Mara kwa Mara hata nyakati za usiku.
Pia katika siku za mwisho za ujauzito ,mjamzito anaweza akawa anatokwa na matone ya mkojo kwa kushindwa kujizui kipindi anapokuwa anakohoa,kupiga chafya au kuinua kitu kizito hali hii hutokana na kuongezeka kwa mkandamizo katika kibofu unao sababishwa na tumbo la uzazi.
USHAURI.
.Mjamzito ni vema akakojoa Mara kwa Mara ili kupunguza hatari ya kupasuka kwa kibofu Cha mkojo vile vile kupunguza hatari ya kupata maambukizi katika njia ya mkojo(uti).
.Mjamzito aepuke kunywa kahawa au kinywaji chochote ambacho kina caffeine ili asikojoe zaidi.
.Pia ili mjamzito apate kupumzika zaidi nyakati za usiku ni vema asinywe maji mengi nyakati za jioni au usiku.
.Kwa wale ambao hutokwa na mkojo katika miezi ya mwisho ya ujauzito wanashauriwa kufanya mazoezi mepesi ya kukaza na kulegeza misuli ambayo huzunguka uke na haja kubwa,Mazoezi haya pia yatasaidia kwa wajawazito ambao hutokwa na mkojo Mara baada ya kujifungua ,hali hii ni kawaida na huisha bila ya matibabu ,pia Kama hali hii haitoisha ni vema kuwajulisha wataalamu wa afya ili kupata matibabu zaidi.
.Pia mjamzito awapo katika chumba Cha uchungu anashauriwa kukojoa Mara kwa Mara ili kuepuka madhara ambayo yanaweza jitokeza.
.Maudhi madogo siyo hatari kwa afya lakini yanaweza yakawa hatari kwa afya ya Mama na mtoto kwahiyo uonapo Hali inadhidi nenda hospitali ukapate matibabu.
Pia usikose kuendelea kufatilia kipindi kijacho muendelezo wa maudhi madogo ya ujauzito.
Karibu.
No comments:
Post a Comment