Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Athari zitokanazo na uzito mkubwa au unene,sababu za kuongezeka kwa uzito,faida ya kupunguza uzito,na njia za kupunguza uzito.


Uzito mkubwa ni tatizo ambalo linawakabili watu wengi katika miaka ya karibuni katika jamii zetu na hii imesababishwa na jinsi tunavo yaishi maisha yetu ya kila siku. Kwahiyo kuwa na uzito mkubwa au unene kuna athari kubwa katika jamii yetu na hii ni kwasababu uzito mkubwa au unene ni chanzo cha magonjwa mengi katika  miili yetu.

Magonjwa ayo ni kama shinikizo la damu,kisukari ,kiharusi ,matatizo ya usingizi na kukoroma,upungufu wa nguvu za kiume,pumu,magonjwa ya moyo,saratani na mengineyo. Kwahiyo uzito mkubwa au unene husababisha kutokufanya vizuri kwa mifumo ya mwili,kwaiyo kufeli kwa utendaji huo ndiko husababisha kuwa katika hatari ya kupata magonjwa. Kutokana na athari izo watu hujikuta wanajaribu kufanya vitu tofauti ili kupata suluhu ya tatizo hili na wakati mwingine bila ya kupata mafanikio.

Uzito mkubwa au unene.

 Ni kuzidi kwa kiwango cha mafuta mwilini kupita kiwango cha kawaida ambacho mwili unakihitaji. Hii hutokea pale ambapo nishati kubwa huingia mwilini kuliko matumizi ya kawaida ya mwili. Miili yetu imeundwa na tishu mbalimbali Kama vide adipose tissue. Seli hizi hufanya kazi ya kufyonza vyanzo vya nishati kwa wingi  katika damu kama sukari na mafuta na kuufanya mwili uhisi njaa Kali hali hii hupelekea mtu ale zaidi ili kuziba kiasi cha nishati iliyo fyonzwa na seli hizi.Kadiri utakavyo zidi kula ndivyo seli hizi zinavyo zidi kufyonza kiwango cha nishati na kuhifadhi na matokeo yake uzito utaongezeka au utakuwa mnene. Shughuli hii yote huratibiwa na vichocheo mbali mbali vya mwili kama insulin, cortisol, leptin na ghrelin.


Nini hupelekea kuongezeka kwa uzito mwilini au kuwa mnene.?

Uzito uliopitiliza hutokana na kuongezeka kwa nishati mwilini,vyakula tunavyo kula kila siku hutengeneza nishati ambayo  hutumika katika shughuli mbali mbali za mwili.Kwaiyo uzito kupitiliza au unene hutegemeana na kiwango cha nishati ambacho hupatikana katika vyakula na vinywaji ambavyo tumekula na kiasi kinacho tumiwa na mwili.Kwaiyo ili usiwe na uzito mkubwa wala mdogo ni lazima kiwango cha nishati kinachoingia mwilini kilingane na mahitaji ya mwili wako ivyo basis uzito mkubwa hutokana na kula kiwango kikubwa cha nishati ikiwa matumizi ya nishati iyo mwilini ni kidogo.Zifuatazo ni sababu zinazopelekea kuwa na uzito mkubwa au unene nazo ni.

.Msongo wa mawazo.
      
Katika hali ya kawaida  msongo wa mawazo huathiri au huvuruga mfumo wa vichocheo vya mwili ivyo kupelekea kuvurugika kwa utendaji kazi wa mwili.Kichocheo cha cortisol hufanya kazi ya kuweka uwiano sawa wa nishati mwilini, ivyo Kuvurugika kwa kichocheo hisi hufanya mtu ahisi njaa muda wote jambo ambalo litapelekea kula zaidi na nishati kuhifadhiwa mwilini kwa wingi jambo ambalo hupelekea uzito kuongezeka.

.Kukosa usingizi.

Kukosa usingizi huongeza athari ya mtu  kuwa na uzito mkubwa, kwasababu usingizi husababisha kuwa na ulinganisho au uwiano kati ya vichocheo ambavyo vinamfanya mtu ahisi njaa na vile ambavyo vina mfanya mtu asihisi njaa.Vichocheo ambavyo humfanya mtu ahisi njaa huitwa Ghrelin na vichocheo ambavyo humfanya mtu asihisi njaa huitwa Leptin.Kwaiyo kukosa usingizi husababisha kuvurugika kwa uwiano mzuri uliopo katika vichocheo ivyo kusababisha kupanda kwa kichocheo(ghrelin) ambacho kinamfanya mtu ahisi njaa na kushuka kwa uzalishwaji wa kichocheo (leptin)  ambacho humfanya mtu asihisi njaa hali hii hupelekea mtu ale zaidi na kusababisha nishati kuhifadhiwa kwa kiwango kikubwa na matokeo yake ni kuongezeka uzito.Pia kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa chakula mwilini hupelekea kuathirika kwa utendaji kazi wa kichocheo (insulin) hali hii humfanya mtu  awe katika hatari ya kuugua ugonjwa wa kisukari ambao hutokana na jinsi mtu anavyo ishi maisha ya kila siku.

.Kutokufanya mazoezi.
       
 Ili uwe na afya bora mazoezi ni muhimu kwasababu husaidia kutoa taka mwili,huimarisha viungo vya mwili, huongeza kiwango cha msukumo wa damu,vile vile husaidia kupunguza uzito au unene. Kutokufanya mazoezi huufanya mwili kushindwa kutumia nishati inayopatikana katika chakula ulichokula jambo ambalo husababisha kuwepo kwa uwingi wa nishati mwilini nahivyo kupelekea nishati iyo ihifadhiwe kama mafuta mwilini jambo ambalo litapelekea uzito kuongezeka.

.Unywaji wa pombe na ulaji wa vyakula vya viwandani.  
                  
 Kuna makampuni mengi sana siku hizi ambayo hutengeneza vyakula na vinywaji katika viwanda vyao.Makampuni haya hutumia gharama kubwa kufanya matangazo ya bidhaa zao ,Kutokana na ushawishi mkubwa wa matangazo yao na bei nafuu ya bidhaa zao watu wengi hujikuta wanatunia bidhaa za makampuni kuachana na zile za kuandaa wenyewe. Vyakukula na vinywaji hivi vimetengeneza kwa kiwango kikubwa cha nishati.Pindi mtu anavyo tumia bidhaa hizi kwa wingi husababisha nishati kubwa iendelelee hifadhiwa mwilini wakati matumizi ya mwili ni madogo matokeo yake uzito huongezeka.

.Kutokuzingatia lishe sahihi. 
             
 Wakati mwingine unaweza kuongeza uzito kwasababu ya kutokula mlo sahihi,na kwa kiwango ambacho siyo sahihi na wakati ambao siyo sahihi.Baadhi ya watu uzito wao huongezeka japo wanakula kiwango kidogo cha chakula lakini wapo wengine hubaki na uzito ule ule japo wanakula mlo anbao ni sawa.Hii inaweza kuoanishwa na kiwango tofauti  cha shughuli za kikemikali mwilini au aina ya chakula ambacho mtu anakula na haina mahusiano na kiwango cha chakula ambacho mtu anakula isipo kuwa ni ubora wa chakula chenyewe hii humaanisha unaweza ukala chakula kidogo ukaongezeka uzito na mwingine akala chakula kile kile na akaongezeka uzito.

.Matumizi ya madawa.  
                      
 Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali.Tunatumia dawa kwa lengo la kutibu au kupata suluhu ya ugonjwa ambao unakusumbua.Dawa hizi huleta matokeo tofauti pamoja na kutibu tatizo ambalo lina kusumbua.Mbali na kutibu tatizo ambalo linakusumbua dawa hizi huleta maudhi madogo madogo na mahudhi hayo hutofautiana kati ya dawa na dawa na mtu na mtu na hii ni kutokana na vile tumeumbwa. Baadhi ya dawa mfano dawa za kisukari , dawa za kutuliza mihemuko (ant depressant) mbali na kushusha sukari dawa hizi husababisha kuongezeka kwa uzito.

.Ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kwa wingi.   
    
 Ulaji wa vyakula hivi kwa wingi huchochea deli za kuhifadhi mafuta ziendelee kuhifadhi mafuta zaidi na matokeo yake in kuwa mnene au kuwa na uzito mkubwa.
    
.Urithi.  
  
 Unene au uzito mkubwa unaweza ukarithiwa kutoka kwa moja kati ya wazazi na hii ni kutokana na tafiti ambazo zmefanywa.Pia endapo mama mjamzito atakula sana au hatokula sana hupelekea kubadilika kwa DNA ya mtoto na kusababisha athari katika utumiaji wa mafuta mwilini kwa baadae.




Soma/nini-husababisha-kichefuchefu-na.html




Upi  ni umuhimu wa kupunguza uzito mwilini? 

     
Ndugu msomaji kama tulivyo ona mwanzo ,kwamba uzito mkubwa huatarisha Afya yako kwasababu hukufanya uwe katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa mengi, kwaiyo ni vema kupunguza uzito kwa wale wenye uzito mkubwa ili kujitoa katika atari iyo.Tafiti mbalimbali zinaonesha kupungua kwa uzito kwa asilimia tano hadi kumi husababisha Afya yako iwe imara.      
 Zifuatazo ni faida zinazotokana na kupunguza uzito.  
                                  
 .Husaidia kujitoa katika atari ya kuugua kisukari kitokanacho na mtindo wa maisha.

Uzito mkubwa huenda sambamba kabisa na kuugua ugonjwa wa kisukari kwasababu uzito mkubwa huathiri utendaji kazi wa kichocheo cha insulin kuathiriwa kwa kichocheo hiki husababisha kiwango kikubwa cha sukari katika damu matokeo yake utapata kisukari.

.Hupunguza athari  ya ku shambuliwa  na ugonjwa wa viungo vya mwili.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya uzito mkubwa na viungo vya mwili tafiti ambazo zimefanyika huonyesha kupungua kwa uzito husababisha kupungua kwa maumivu katika viungo vya mwili hivyo kujitoa katika Atari ya kuugua ugonjwa wa viungo(arthritis).

.Hupunguza athari ya kushambuliwa na ugonjwa wa kiharusi(stroke).

 Mafuta mengi mwilini husababisha kupungua kwa kipenyo cha mishipa ya damu jambo ambalo hupelekea moyo usukume damu kwa nguvu kubwa,msukumo mkubwa was damu katika mishipa ya damu huenda ikapelekea kupasuka kwa mishipa iyo na kusababisha upungufu wa damu yenye hewa safi kwenye ubongo jambo ambalo hupelekea kufa kwa seli hai za ubongo.

.Hupunguza athari ya kupata ugonjwa wa saratani.

.Hupunguza  athari ya ku shambuliwa na ugonjwa  wa moyo.

.Husaidia kupunguza msongo wa mawazo.

.Husaidia kuongeza uwezo wa kufikiri.

.Husaidia kupata usingizi vizuri.





Ufanye nini sasa ili kupunguza uzito?

.Kuwa na mpangilio mzuri wa kula.

Mpangilio mzuri ni vile ambavyo mwenyewe  utajipangia,ule chakula gani,kwa muda gani na kwa kiwango kipi .Pia no vema ukaepuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja,pia jitahidi  kuzingatia ratiba ambayo umejiwekea .

.Epuka au punguza matumizi ya bidhaa za viwandani.

Kwasababu bidhaa hizi zimetengenezwa kwa iwingi mkubwa wa sukari jambo ambalo hupelekea kuhifadhiwa kwa nishati kubwa mwilini kuliko matumizi ya kawaida ya mwili.

. Fanya mazoezi ya mwili.
   
  Kufanya mazoezi husaidia kiwango cha nishati ambacho kimehifadhiwa mwilini nacho kitumike,kadiri utakavyo endelea kufanya mazoezi Mara kwa Mara ndivyo nishati ya akiba itakavyo tumika na hatimaye utapungua na kufanya kuwe na uwiano sawa kati ya nishati inayo ingia na inayohitajika na mwili.

. Muda mwingi wa kupumzika. 

 Hata kama upon bize katika mihangaiko ya kukuza uchumi wa familia ni vema pia ukatafuta muda wa kupumzika kwasababu kukosa usingizi husababisha kusiwepo kwa uwiano kati ya vichocheo vinavyo kufanya uhisi njaa na vina vyokufanya  usihisi njaa jambo ambalo husababisha kuongezeka.

.Epuka au punguza mawazo.  
              
Msongo wa mawazo husababisha kuburugika kwa vichocheo vya mwili na kama cortisol na kupelekea utendaji kazi was mwili kushuka.Kuvurugika kwa kichocheo cha cortisol ndiko hupelekea mtu ale zaidi ili apate nishati.Kwaiyo ni vema ukapunguza mawazo kwa kufanya mazoezi,kujihusisha katika shughuli, kukaa katika makundi ili upunguze uzito wako.

.Epuka au punguza ulaji wa vyakula vya wanga na sukari.

Kwasababu ulaji wa vyakula hivi kwa wingu huchochea seli za mwili zihifadhi mafuta zaidi jambo ambalo huongeza uzito ,kwa hiyo nivema ukatumia vyakula hivi kwa kiwango kidogo.

.Zingatia matumizi ya aina zote za chakula yaani mlo kamili.



 Mawasiliano whatsap : 0712106789
      
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts