Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Jikinge na ugonjwa wa ini (livercirrhosis).

INI

Ni kiungo kikubwa sana katika mwili wa binadamu ambacho hupatikana upande wa kulia wa juu ya tumbo.

Ini hufanya kazi nyingi katika miili yetu wanadamu kazi izo ni pamoja na:

.Kuhakikisha kiwango cha mafuta nasukari kwenye damau kinakuwa cha kawaida.

.Ini pia hutengeneza nyongo(bile).

.Ini huukinga mwili usishambuliwe na vimelea vya magonjwa.

.Huvunja vunja chakula tunacho kula na kutengeneza nishati inayo tufanya tuonekane wenye nguvu.

.Pia ini hutengeneza enzyme na protini ambazo hufanya kazi nyingi mwilini.

.Huvunjavunja madawa na chemicali ambazo tunaziingiza katika miili yetu ili kutulinda tusipate madhara.

.Ini huzalisha kichocheo cha angiotensionogen ambacho huongeza msukumo wa damu wakati inapokutana na enzyme renin ambayo huzalishwa na figo pindi msukumo wa damu una poshuka.

.Hutengenesa chembe zinazozuia Luganda kwa damu kama fibrinogen,prothrombin na zinginezo.

Kwaiyo kutokana na kazi kubwa inayofanywa na ini kuna madhadhara makubwa ambayo yatatokea na ivyo kuhatarisha uhai wa mtu.


Liver cirrhosis.

Ni ugonjwa ambao hutokana na kuwepo kwa makovu(scar tissue) na fibroids ambazo husababishwa na majeraha au magonjwa ya ini ya muda mrefu.Makovu au scar tissue huchukua nafasi ya tissue hai za ini na kuzuia mzunguko wa kawaida wa damu ndani ya ini ivyo kusababisha ini lishindwe kufanya kazi yake vizuri.


Je nini husababisha cirrhosis?

Ugonjwa wa cirrhosis ni matokeo ya maisha tunayo yaishi kila siku jambo ambalo husababisha ini kuathirika ,sababu izo ni kama:

.Unywaji wa pombe kupindukia.

pombe imetengenezwa kwa chemikali kwaiyo kipindi chemikali izo zinapoingizwa mwilini huenda moja kwa moja kwenye ini,ini huzivunja vunja na kisha sumu izo kutolewa nje kwa njia ya mkojo,jasho na haja kubwa,kwaiyo matumizi ya pombe kupindukia na ya Mara kwa Mara husababisha ini lifanye kazi kuliko kiwango cha kawaida ,pia husababisha majeraha ndani ya ini,au ugonjwa wa hepatitis unaotokana na ulevi matokeo yake ini linazidiwa na linashindwa kufanya kazi vizuri.

.Homa ya ini( Hepatis B,C,D).

Ugonjwa ambao husababishwa na virusi vya hepatitis ambao huambukizwa,ugonjwa wa hepatitis B ndo chanzo kikubwa cha kupata ugonjwa wa cirrhosis.

.Auto immune hepatitis.

Huu ni ugonjwa wa ini ambao husababishwa na kinga za mwili kushambulia seli hai ndani ya ini,mashambulizi ya Mara kwa Mara yatokanayo na ugonjwa huu husababisha majeraha na mwishowe makovu hutokea.

.Madawa na chemikali tunazo zitumia.

Madawa na chemikali zinazoingia mwilini kwetu llazima yapite kwenye ini kwaajili ya kuvunjwa vunjwa na kisha hutolewa ili mwili usidhurike,matumizi ya Mara kwa Mara huongeza utendaji kazi wa ini na kusababisha majeraha katika ini.

.Magonjwa ya kurithi.

Kuna uwezekano mkubwa mtoto akapata magonjwa ya ini kama moja kati ya wazazi walikuwa nayo ,magonjwa ayo ni kama.

i.Hemochromatosis  ugonjwa ambao husababisha madini ya chuma kukusanyika ndani ya ini,mkusanyiko huo huathiri mzunguko wa damu na utendaji kazi wa ini.

ii.Wilson's disease,ni ugonjwa ambao husababisha copper kukusanyika ndani ya ini na kuathiri utendaji Nazi.

iii.Porphyria ni hali ambayo husababisha mashambulizi kwenye ini,uroto mwekundu(bone marrow) na ngozi pia hali hii huathiri utendaji kazi wa ini.

.Magonjwa ambayo hushambulia mirija inayo beba nyongo kutoka kwenye ini.

.Kushindwa kufanya kazi chemba ya kulia ya moyo.

Upande wa kulia wa moyo ndiko husukuma damu safi inayotoka kwenye mapafu ili ikatumike sehemu mbali mbali ikiwepo kwenye ini,kuathirika kwa upande huu husababisha ini lisipate damu ya kutosha matokeo yake seli hai zitaathirika na kupunguza utendaji kazi wa ini,hali hii inaweza sababishwa na magonjwa ya moyo ,pia shambulizi katika vizibo (valves) za moyo.

.Ugonjwa wa kichocho (schistosomiasis).

.Kukusanyika mafuta kwenye ini.

Hali hii huweza sababishwa na mtu kuwa na uzito mkubwa kupitilia au unene au kisukari ambacho husababisha mafuta ayo kugandamana kwenye ini na kuathiri utendaji kazi wake,vile vile utapia mlo wa protini kutokana na kupungua kwa ufyonzaji wa virutubisho mwilini.





Soma/athari-zitokanazo-na-uzito-mkubwa-au.html



Dalili za cirrhosis.

Dalili hutegemeana na kiwango gani ini limeathirika.Wagonjwa wengi katika hatua za mwanzo huwa hawaoneshi dalili na wanaweza wakagundulika na ugonjwa huu kutokana na vipimo vingine ambavyo vitakuwa vinafanyika kwa magonjwa mengine.

Dalili za awali zaweza kuwa:

.Kutapika

.Kukosa hamu ya kula

.Uchovu

.Kupungua uzito.


Kwahiyo kadiri ugonjwa unavyodhidi kuendelea ndivyo madhara ya cirrhosis yanavyodhidi kutokea.

Viashiria au dalili ambazo zinaweza jitokeza baadae sana baada ya ini kushindwa kufanya kazi yake ni pamoja na:

.Manjano(jaundise) hujitokeza kwenye ngozi na machoni na hujitokeza kwasababu ini limeshindwa kutoa bilirubini matokeo yake bilirubin hugandamana ndani ya ini.

.Mabadiliko ya ngozi(watu wengi huwa weusi zaidi) na muwasho kwasababu ya kuwepo kwa bile kwenye ngozi.

.Homa

.Kuharisha

 .Kutapika

.Maumivu ya tumbo kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa ini.

.Kukua kwa maziwa kwa wanaume,ini hufanya kazi ya kuharibu vichocheo vya jinsia ya kike kwa mwanaume,kutokana na kushindwa kufanya kazi vichocheo hivyo huwa Vinci kwenye ini matokeo yake maziwa hukua.

.Korodani kusinyaa kutokana na kupungua kwa utendaji kazi wa hypothalamus na tezi ya pituitaty, jambo ambalo husababisha uume usisimame,ugumba na kukosa hamu ya mapenzi.

.Tumbo kuongezeka ukubwa kutokana na kukusanyika kwa maji.

.Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi kutokana na kupungua vichocheo.

.Kutapika au kuharisha damu kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa kugandisha damu.

.Mabadiliko ya kucha mwonekano umbile na rangi badala ya kuwa na rangi ya pink huwa na rangi nyeupe.

.Kukauka mate.

Kuongezeka ukubwa wa bandama.



Vipimo vya cirrhosis

.Kupima utendaji kazi wa ini.

.Kipimo cha ultrasound

.Ct scan kuangalia kama kuna saratani

.Liver biopsy,sampuli huchukuliwa kwenye ini na kupimwa kama ini Lima saratani.

.MRI hutumika kuangalia mirija inayo beba nyongo kutoka kwenye ini.

.Kuangalia chembe chembe ambazo husaidia kugandisha damu.

.Kuangalia kiwango cha sukari na cholesterol.

.Gastroscopy kipimo cha kupitisha Mpira kwenye tumbo hadi kwenye duodenum na kuangalia kama kuna oesophagus varies.



Madhara yatokanayo na cirrhosis.

.Hepatic encephalopathy.

Kupungua kwa utendaji kazi wa ubongo husababisha kushindwa kufanya maamuzi,kuwa na hasira,kusahau pia kuona watu au vitu ambavyo kiuhalisia havipo,hii husababishwa na kuongezeka kwa ammonia kwenye damu.

.Saratani ya ini

.Kutokwa na damu

.Tumbo kujaa maji

.Utapia mlo

.Ini kushindwa kufanya kazi kabisa.

.Figo kushindwa kufanya kazi

.Osteoporosis (udhaifu wa mifupa ivyo kuwa rahisi kuvunjika)

.Premature menopouse(kufika ukomo wa kuona hedhi kabla ya miaka)

.Kisukari




Ufanye nini kuepuka cirrhosis?

.Epuka kufanya mapenzi bila ya kinga.

.Kuwa mwaminifu au kuwa na mpenzi mmoja.

.Acha au punguza unywaji wa pombe kupindukia.

.Hakikisha unapunguza uzito wako kama una uzito mkubwa.

.Fanya mazoezi ya viungo.

.Epuka matumizi holela ya dawa ,pia punguza matumizi ya paracetamol ambayo huleta shida kwenye ini.

.Kula mlo kamili ili kuepuka kupata utapia mlo.

.Kama bado hujapata chanjo ya hepatitis basi hskikisha unapata chanjo.

.Punguza matumizi ya vyakula vyenye protini kwa wingi.

.Punguza matumizi ya chunvi kwenye chakula.

.Epuka kuchangia vifaa vyenye ncha Kali pamoja na miswaki.

.Kama una magonjwa kama kichocho nenda hospitali ukapate tiba.

.Pia epuka kuwa na msongo wa mawazo.



Pia mgonjwa wa cirrhosis atawekewa ini lingine endapo madhara hayato dhibitiwa.


Whatsap;0712106789


Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts