Home »
» Nini husababisha kichefuchefu na kutapika katika kipindi cha ujauzito
Nini husababisha kichefuchefu na kutapika katika kipindi cha ujauzito
Kuhisi kichefuchefu na kutapika huanza katika wiki ya nne ya ujauzito hadi wiki ya kumi ya ujauzito na hukoma kabla ya wiki ya ishirini ya ujauzito na wengine hali hii huendelea had wakati wa kujifungua.Hali hii huweza sababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kichocheo cha chorionic gonadotrophic homoni.Hali hii huambatana na kupungua kwa uzito na kupotea kwa maji mwilini.
Katika kipindi cha ujauzito kuna mabadiliko mbalimbali ya kisaikolojia na kimwili hutokea kiutokana na vichocheo vya uzazi kuzalishwa kwa kiwango kikubwa. Mabadiliko hayo hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke na hutokea kwa kiwango tofauti katika mimba tofauti tofauti.
Pia kutapika katika ujauzito kunaweza kukawa ni kawaida kutokana na kwamba hali hii huwapata wengi,hali hii huwapata watu nane kati ya akina mama kumi kwaiyo ni jambo la kawaida.Hali hii ni kawaida kwa mjamzito na haina madhara lakini kama utaona hali hii inajitokeza zaidi ,Mara kwa Mara jambo ambalo huweza kutishia usalama wako na mtoto unashauriwa uende hospitali ukafanyiwe uchunguzi kwakuwa hali huenda imesababishwa na tatizo lingine.
Ni vigumu sana kuweza kuzuia hali hii kabisa kwasababu imetokana na mabadiliko ya mwili katika kujiandaa kumpokea mtoto ambaye anatarajiwa kuzaliwa.Kutokana na kuhisi kichefuchefu wakina mama wengi hujikuta wanapenda sana kula vyakula vyenye asili ya uchachu ili wasiendelee kuhisi kichefu chefu.
Kuhisi kichefuchefu na kutapika husababishwa na Nini?
Kuna magonjwa mengi ambayo yanaweza sababisha mtu akahisi kichefuchefu na mwishowe akatapika. Tatizo hili la kutapika Mara nyingi huanza pindi mimba ikiwa changa ,pia linaweza likakoma kabla ya wiki ya 20 ya ujauzito japo kunawengine hubaki na tatizo hili hadi wakati wa kujifungua.
Hadi sasa haijafahamika bado nini hasa husababisha tatizo hili litokee ,Japo kuna baadhi ya vitabu vinaeleza chanzo cha tatizo hili ni kuzalishwa kwa wingi kwa kichocheo cha human chorionic gonadotrophine (HCG) ,Kichocheo hiki hutengenezwa na kifuko cha tumbo la uzazi(placenta).
Lakini zipo baadhi ya sababu ambazo zinaweza zikamfanya mwanamke awe katika hatari ya kupata kichefuchefu na kutapika katika kipindi cha ujauzito nazo ni.
.Kurithi.
Kama katika familia kuna ambaye alipatwa na kichefuchefu na kutapika akiwa mjamzito,hali hii huongeza nafasi kubwa kwa wanafamilia wengine kupata kichefuchefu na kutapika kipindi watakavyo kuwa wajawazito.
.Kuwa na mapacha.
kuwa na mtoto zaidi ya mmoja katika tumbo la uzazi huongeza nafasi ya mama mjamzito kupatwa na kichefuchefu na kutapika.
.Uzito mkubwa kipindi cha ujauzito .
Uzito mkubwa husababisha kuvurugika kwa vichocheo vya mwili,jambo ambalo linaweza kupelekea kifuko cha uzazi kutengeneza kwa wingi kichocheo cha human chorionic gonadotrophine,kuzalishwa kwa wingi kwa kichocheo hiki husababisha mama ahisi kichefuchefu na atapike.
.Mimba ya kwanza(prime gravida) .
Uzao wa kwanza humweka mama katika hatari ya kukubwa na kichefuchefu na kutapika.
.Historia ya Matatizo ya ulaji.
Kama mama alikuwa anakula zaidi au kidogo sana kabla ni jambo ambalo linaweza sababisha akawa katika hatari ya kupata kichefu chefu na kutapika atakavyo kuwa mjamzito,kwasababu kula sana au kidogo husababisha awe na uzito kidogo au mkubwa jambo ambalo huaribu mfumo wa vichocheo vya mwili na litasababisha Kichocheo cha HCG kizalishwe kwa wingi.
.Kuongezeka kwa utengenezwaji wa kichocheo cha oestrogen.
Kuongezeka kwa oestrogen husababisha kupungua kwa mmeng'enyo wa chakula tumboni na utolewaji wa chemikali za tumbo zinazo saidia kumeng'enya chakula hali ambayo itasababisha mama ahisi kichefu chefu.
Soma/umuhimu-wa-kuujua-mzunguko-wa-hedhi.html
Dalili za kichefuchefu na kutapika
Siyo kwamba wakina mama wote wajawazito hukumbana na kichefu chefu na kutapika,kwa wale ambao wanapatwa na tatizo hili dalili zinakuwa kama hivi.
.Kukosa hamu ya kula.
.Kutapika zaidi ya Mara moja kwa siku.
.Maumivu ya kichwa na kizungu zungu.
.Kupungua uzito zaidi ya asilimia tano kutokana na kupoteza maji na kukosa hamu ya kula.
.Kupoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini.
Yepi ni madhara ya kuhisi kichefuchefu na kutapika katika ujauzito?
Madhara ya kutapika katika ujauzito yana weza kumpata mama pamoja na mtoto tumboni,madhara hayo hutokana na mama kupoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini kwa njia ya kutapika.
Pia madhara hayo yanaweza kutokea kwa wakina mama wachache kati ya wengi ambao ni wajawazito,na hii inategemeana na kiwango gani mama anatapika,kuto kufanya maamuzi ya kwenda hospitali kupata matibabu mapema kama tatizo hili litakuwa sugu.
Madhara hayo ni kama ifuatavyo:
.Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.
.Pia mtoto anaweza akazaliwa kabla ya miezi tisa haijakamilika.
.Mtoto anaweza akazaliwa akiwa mdogo ukilinganisha na umri wa mimba,kwakawaida tunategemea ukuaji wa mtoto uendane na ukubwa wa mimba,sasa endapo mama atakumbana na tatizo la kutapika bila matibabu atapoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini ,pia kupoteza hamu ya kula kutasababisha mtoto akose virutubisho vya msingi,jambo ambalo huathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto na matokeo yake mtoto atakae zaliwa baada ya miezi tisa atakuwa mdogo.
.Pia mama anaweza akapatwa na upungufu wa damu,kutokana na kukosa madini ambayo husaidia kutengeneza damu.
.Kupungua kwa kiwango cha sukari mwilini hii ni kutokana na kupoteza hamu ya kula.Chakula tunacho kula kina sukari ambayo hufanya kazi nyingi mwilini,kupoteza hamu ya kula kutasababisha mwili kutumia kiwango cha nishati ya ziada iliyo hifadhiwa mwilini na kusababisha upungufu wa sukari.
.Pia kupungua kwa maji mwilini husababisha utendaji kazi wa figo upungue.
.Kukosa hamu ya kula kutasababisha mama apatwe na upungufu wa virutubisho mwilini(malnutrition)
Ufanye nini unapokumbana na hali hii!?
Ukubwa wa tatizo hili hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke,Kwahiyo siyo kila utakapo patwa na kichefuchefu na kutapika utahitaji kumwona daktari. Unashauriwa mwona daktari kama tatizo lako linakuwa kubwa zaidi,pengine tatizo lako yawezekana limetokana na ugonjwa mwingine. Kwaiyo Fanya mambo yafuatayo .
.Kunywa maji mengi mara kwa mara.
Maji hufanya kazi nyingi katika mwili wa binadamu,kwaiyo kupotea kwa maji mengi husababisha kupotea kwa kiwango cha electrolyte mwilini,kwaiyo kupungua kwa electrolyte huathiri utendaji kazi wa mwili,Kwa iyo unashauriwa kunywa maji mengi Mara kwa Mara ili kuziba nafasi ya electrolyte ambazo zimepotea jambo ambalo hufanya mwili ufanye kaz vizur.
.Epuka kula na kunywa kwa wakati mmoja.
Unashauriwa kula kwanza baada ya nusu saa ndipo unaweza kunywa,kwasababu unavyo kuwa unakula na kunywa hususani vyakula vya sukari lazima utahisi kichefu chefu kwasababu vyakula vya sukari huleta kichefuchefu na vitakusababishia utapike.
.Pumzika muda mrefu.
Katika familia zetu mama ndo mtendaji mkubwa washughuli za nyumbani jambo ambalo humfanya awe bize muda wote ili kuhakikisha familia inapata mahitaji yake.Lakini pamoja na ubize au majukumu mengi katika familia anashauriwa apumzike kwa muda mrefu pale ambapo majukumu ayo huishia,kwasababu uchovu kwa mama anaetapika humsababishia ajihisi vibaya zaidi.
.Epuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja.
Kutapika hupoteza hamu ya kula jambo ambalo hupelekea nishati ya ziada itumike zaidi mwilini.Kupoteza hamu ya kula husababisha pasiwe na uwiano kati ya nishati inayoingizwa mwilini na inayohitajika kwa matumizi sahihi mwilini jambo ambalo husababisha mama kukosa nguvu.Kwahiyo unashauriwa ule chakula kidogo mara kwa mara ili kuupa mwili nguvu.
.Matumizi ya vitaminiB ,folic na Chuma.
Mama anashauriwa atumie vitamin folic na chuma ili kuepuka athari ya kupata upungufu wa damu,athari ya mtoto kuzaliwa na mgongo wazi.Pia matumizi ya vitamini husaidia kuimarisha kinga za msili hivyo kumwondolea hatari ya kushambuliwa na magonjwa mengine.
.Matumizi ya limau katika vyakula.
Limau inauchachu uchachu husaidia kukata kichefuchefu,kwahiyo mama anashauriwa atumie limau katika chakula ambacho anakula ili kuzuia asipate kichefuchefu.
Mwisho.
Pamoja na kufanya niliyo yataja hapo juu,na bado tatizo lako likawa ni kubwa basi unashauriwa uende hospitali ukafanyiwe vipimo huenda limesababishwa na magonjwa mengine,pili ukapewe ushauri juu ya matumizi ya dawa ya kuzuia kutapika(promethazine,metocropramide(MCP) ) kama hakutoleta madhara kwa mtoto ambae yupo tumboni,Pia kama umepoteza maji mengi uweze kuwekewa dripu ili kuleta usawa wa electrolyte mwilini.
Mawasiliano whatsap :0712106789
No comments:
Post a Comment