Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Dalili za hatari kwa mjamzito.



Kipindi cha ujauzito ni kipindi cha furaha kwa mama na baba pia kwasababu wanajiandaa mpokea na kumlea mtoto ambae atazaliwa.Pia katika kipindi hiki kuna matatizo mengi ambayo yanatokea kutokana na mabadiliko ya mwili wa mama katika vipindi tofauti tofauti.Matatizo hayo yanaweza yakajitokeza wakati wa ujauzito au mara baada ya kujifungua.

Dalili za hatari kwa mama mjamzito.

Ni viashiria vya hali ya hatari ambavyo vyaweza mtokea mama mjamzito ambayo vinahitaji msaada wa haraka ili kuokoa maisha ya mama pamoja na mtoto.Kuna baadhi ya vitu ni kawaida katika kipindi cha ujauzito ,lakini kuna mambo ya muhimu ukiona mama mjamzito analalamika ni lazima ufanye maamuzi ya haraka ili umsaidie nayo ni kama ifuatavyo.

Kutokucheza kwa mtoto. 

Mtoto huanza kucheza tumboni mwa mama kuanzia wiki ya 16 hadi 25 na mpaka mama atakapo jifungua.Ukiona kuanzia muda huu mtoto hajaanza kucheza au alikuwa anacheza lakini kaacha ghafla au alikua anacheza mfano mara tano kwa siku na akawa anacheza mara moja na huenda asicheze kabisa ni wakati wako sasa wa kwenda hospitali ili ufanyiwe uchunguzi au upate matibabu kwasababu dalili hii huashiria mtoto anashida au amefariki.


Kutokwa na damu nyingi sehemu za siri.

Kutokwa na damu nyingi katika miezi mitatu ya mwanzo huashiria mimba kuharibika ,pia kutokwa na damu katika miezi ya mwisho ya ujauzito huenda kukaashiria mfuko wa uzazi umejiachia katika tumbo la uzazi ivyo basi mama anashauriwa aonane na daktari haraka ili aweze pewa msaada na kuokoa maisha ya mtoto.pia damu katika kipindi cha ujauzito ikiambatana na maumivu ya tumbo la chini huashiria mimba imetungwa nje ya mji wa mimba ivyo basi upasuaji utahitajika kwa mama huyu ili kuokoa maisha yake.



Soma:maambukizi-katika-njia-ya-mkojo uti.html




Kupasuka kwa chupa ya uzazi. 

Chupa ya uzazi ya uzazi inafanya kazi nyingi kwa mtoto ,maji yaliyopo katika mfuko wa uzazi humkinga mtoto asidhurike pindi udondokapo,pia mahitaji yote ya muhimu ya mtoto hutokana na mfuko huu.Kwaiyo kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya siku za kujifungua ni hatari kwasababu mtoto atakosa mahitaji yake ivyo anaweza kufa muda wowote.Mama mjamzito unashauriwa uonapo dalili hii wahi hospitali ili ukapewe msaada .

Uchungu kabla ya wakati.

Kuna uchungu wa kweli na usio wakweli,wajawazito wengi hushindwa kutofautisha aina hizi mbili za uchungu,uchungu usio wa kweli huambatana na maumivu ya tumbo na hauna muda maalumu wakujitokeza,lakini ukiona uchungu unajitokeza kila baada ya muda mfano dakika tano au kumi na unaongezeka kadiri muda unavyozidi kwenda basi huu ndo uchungu wa kweli.Mama mjamzito unashauriwa uende hospitali haraka ili upate kujifungua salama.

Kuvimba miguu na mikono. 

Kuvimba miguu ,mikono,na uso ni kawaida hususani katika kipindi cha mwisho cha ujauzito.Lakini kama kuvimba huku ni kwakiwango kikubwa kukiambatana na tatizo la kutokuona vizuri hizo ni dalili za kifafa cha mimba.Mama unashauriwa uende hospitali ukapate matibabu haraka,kwasababu kifafa cha mimba huuwa wanawake wengi sana katika kipindi cha ujauzito.


Kutapika mara kwa mara. 

Kuhisi kichefu chefu na kutapika ni kawaida katika kipindi cha ujauzito na hii ni kutokana na mabadiliko yanayotokea katika mwili wa mama,lakini endapo mama anahisi kichefuche na anatapika mara kwa mara na kusiko na ukomo nivema akapelekwa hospitali haraka kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Hakuna mabadiliko ya ukuaji wa tumbo. 

Katika hali ya kawaida tumbo la mama linaongezeka ukubwa kadiri mtoto anavyo kua tumboni.Lakini katika hali isiyo ya kawaida tumbo linaweza lisikue kulingana na ukubwa wa mimba japo hutokea mara chache,hali hii huashiria mtoto amekufa tumboni au ukuaji wake siyo mzuri ivyo basi mama anashauriwa aende hospitali afanyiwe uchunguzi zaidi ili kujua ni nini kimesababisha hali hii.

Homa kali.

Homa kali katika kipindi cha ujauzito huashiria umepata na maambuki hivyo basi mama anashauriwa aende hospitali kwa uchunguzi zaidi.




Mwisho,Ewe mama mjamzito uonapo dalili mojawapo kati ya nilizo zitaja hapo juu wahi haraka hospitali ukapate matibabu .



Mawasiliano whatsap: 0712106789
 

Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts