Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Maambukizi katika njia ya mkojo(UTI).

Ugonjwa wa UTI.

Ni maambukizi ya wadudu au vijimelea vinavyo sababisha ugonjwa katika njia ya mkojo, vimelea hivyo hujulikana kama E.coli,vimelea hawa hupatikana katika njia ya chakula na hawawezi wakaleta athari yoyote wakiwa katika mazingira yao ya asili, Pindi vimelea hawa wakitoka katika mazingira yao ya asili na kuingia katika mazingira ambayo siyo asiliyao mfako katika njia ya mkojo vijimelea hivi husababisha maambukizi katika njia ya mkojo(uti).

Pia ugonjwa wa uti unaweza sababishwa na wadudu wengine kama fangasi au bacteria wengine ambao ni matokeo ya kuwa na magonjwa ya zinaa.


Aina ya maambukizi

Mfumo wa mkojo hujumuisha figo,mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye figo(ureter),kibofu cha mkojo(bladder) na mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu hadi nje (urethra).Kazi kubwa ya mfumo huu ni kutoa taka mwilini na kutoa maji ya ziada kwa njia ya mkojo.

Kwaiyo ugonjwa wa uti umegawanyika kutokana  na sehemu ambazo maambukizi yanatokea.


.Endapo maambukizi yatatokea katika njia ya kutolea mkojo nje kutoka kwenye kibofu hujulikana kama urethritis,dalili ambazo huonekana endapo maambukizi yatatokea katika njia hii ni pamoja na homa Kali,kutapika ,kutetemeka na kuhisi kuchomachoma kipindi cha kukojoa.

.Pia endapo vijimelea vya ugonjwa vitaingia na kushambulia kibofu cha mkojo hujulikana kama cystitis,pia dalili zake huwa ni kuwepo na damu kwenye mkojo,maumivu wakati wa kukojoa,kukojoa Mara kwa Mara na maumivu ya kiuno.

.Pia vimelea hivi vinaweza safiri hadi kwenye figo na kushambulia fiho hali hii hujulikana kama pyelonephritis,dalili zake huwa kichefuchefu ,kutapika,homa Kali,kutetemeka na maumivu pembeni juu ya mgongo.

Lakini Mara nyingi ugonjwa huu huathiri sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani kibofu cha mkojo na njia ya kutolea mkojo na Mara chache sana maambukizi kujitokeza sehemu ya juu ya mfumo mkojo.



Nini husababisha ugonjwa wa uti?

Ugonjwa wa  njia ya mkojo hutokea pale vijimelea vya magonjwa vinapoingia katika njia ya mkojo kupitia mirija inayotoa mkojo nje na kuzaliana kwenye kibofu cha mkojo kutokana na mazingira kuwa rafiki kwao.

Japo njia ya mkojo kuna kinga za mwili ambazo huulinda mwili usishambuliwe na vijimelea vya magonjwa,lakini kuna kipindi kinga hizo hushindwa kufanya kazi vizuri na kusababisha vimelea ivyo vizidi kuzaliana na kuendelea kushambulia njia ya mkojo.

Mara nyingi ugonjwa huu huwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume kutokana na maumbile yao kuwa karibu na njia ya haja kubwa,na nafasi kati ya mrija unaotoa mkojo nje na kibofu kuwa karibu.

Sababu kubwa ya ugonjwa huu ni kimelea aitwae E.coli na vimelea vingine ambavyo vinaweza ingia katika njia ya mkojo endapo mwanamke atajisafisha kutoka nyuma kwenda mbele baada ya kupata haja kubwa,pia endapo atakuwa na magonjwa ya zinaa ni rahisi sana wadudu wanao sababisha ugonjwa wa zinaa kama kisonono kuingia katika njia ya mkojo,pia anaweza akawapata wadudu wa ugonjwa kupitia kufanya mapenzi kinyume na maumbile au kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.


Vihatarishi vya ugonjwa wa uti

Vihatarishi vipo vingi na hii ni kutokana na umri,jinsia na mazingira ya mtu husika .Vihatarishi ivyo ni kama:


.Kufanya ngono zembe,ngono bila kinga huongeza hatari ya kupata vijimelea vya ugonjwa wa uti kwasababu hakuna ambae anajua Hali  ya afya ya mwenzie,pia wengine hawaoneshi dalili kwaiyo ni ngumu kugundulika,pia kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja huongeza nafasi ya maambukizi na kufanya mapenzi kinyume (anal sex) na maumbile husababisha E.coli watolewe katika mazingira yao ya kawaida na kuingia ukeni hivyo inakuwa rahisi kuingia katika njia ya mkojo.

.Maumbile,wanawake ni rahisi sana kushambuliwa na uti kutokana na ukarbu wa njia ya haja kubwa na uke na njia ya haja ndogo.

.Umri,watoto na wazee ni rahisi sana kushambuliwa na ugonjwa wa uti kutokana na kupungua kwa uwezo wa kinga zao za mwili kupambana na vimelea vya ugonnwa,pia mtoto anaweza akapata pindi akijisaidia na akakaa muda mrefu bila kusafishwa unyevu unyevu husababisha mazingira mazuri kwa ukuaji wa bacteria hivyo kuongeza nafasi ya maambukizi.

.Njia za uzazi wa mpango ,endapo muwekaji na mtumiaji wa njia hizo hato zingatia usafi husababisha wadudu kuzaliana.Njia izo yaweza kuwa kitanzi au njia ya kuua mbegu za kiume(spermcidal).

.Kuziba kwa njia ya mkojo kwa wanaume kutokana na kuwepo kwa mawe au kukua kwa tezi dume husababisha mkojo ubaki na kutengeneza mazingira ambayo wadudu wanaweza wakaishi na kusababisha uti.

.Matumizi ya mpira wa mkojo kwa muda mrefu hususani kwa wagonjwa ambao wamelazwa,pia wana matatizo katika mfumo wa neuroni na kusababisha washindwe kujizuia kupata haja ,pia kwa wagonjwa ambao wamepooza kutokana na kiharusi,hali hii husanabisha kuwepo kwa mazingira mazuri ya wadudu kuzaliana.

.Kupungua kwa kinga za mwili kutokana na magonjwa mengine kama kisukari na tb.

.Kuugua ugonjwa wa uti kabla huongeza nafasi ya kushambuliwa kwa Mara nyingine.

.Uchunguzi wa njia ya mkojo kwa kutumia vifaa tiba pia huongeza hatari ya kupata maambukizi.

.Mimba pia huongeza nafasi ya kupata maambukizi kutokana n a mabadiliko yanayotokea mwilini na inaweza ikasababisha mama akajifungua kabla ya wakati na mtoto akawa na uzito mdogo.

.Kuzaliwa na matatizo ya kimaumbile katika njia ya mkojo huongeza nafasi ya maambukizi.




Soma:jikinge-na-ugonjwa-wa-ini-livercirrhosis.html



Dalili za ugonjwa uti

.Maumivu wakati wa kukojoa na kuchoma choma.

.Kusikia hamu ya kukojoa mara kwa Mara.

.Maumivu ya kiuno na maumivu chini ya kitofu.

.Uchovu

.Homa Kali.

.Mkojo wa njano wenye kutoa harufu.

.kichefu chefu na kutapika.

.Pia baadhi ya watu huwa hawaoneshi dalili kabisa.

Kwaiyo Mara unapohisi dalili hizi ni vyema ukaenda hospitali kupata matibabu ili kupunguza madhara yanayoweza sababshwa na uti pia epuka kumeza dawa holela kwasababu zinaweza sababisha usugu  ,vile vile vipimo vya maabara vitaonssha unawadudu wa uti kweli au huenda dalili zinazoonekana ni za ugonjwa wa ngono kwasababu dalili hufanana.



Vipimo

.Utrasound ya tumbo kuangalia kibofu

.Kipimo cha mkojo kuangalia seli nyeupe za damu na vijimelea vya magonjwa ambavyo ni ishara ya kuwepo kwa ugonjwa.




Athari/madhara ya uti

.Mama mjamzito kupata uchungu kabla ya wakati na mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.

.Figo kushindwa fanya kazi vizur endapo maambukizi yatafka kwenye figo.

.Kusinyaa kwa njia ya mkojo(urethral stricture) kwa wanaume ambayo ni matokeo ya kujirudia rudia kwa homa hususani ya kisonono ambayo huacha makovu kwenye njia ya kutolea mkojo.




Ufanye nini kujikinga na ugonjwa wa uti.?


.Kunywa maji mengi na Mara kwa Mara.

.Hakikisha sehemu zako za siri ni safi kabla hujafanya mapenzi au unaweza ukatumia kondomu.

.Epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

.Mwanamke hakikisha una nawa kutoka mbele kuelekea nyuma baada ya haja kubwa .

.Hakikisha unakojoa Mara kwa mara ili kuwanyima wadudu sehemu ambayo wanaweza wakaishi na kuzaliana.

.Hakikisha unakojoa baada ya kufanya mapenzi.

.Hakikisha sehemu zako za siri ni kavu,pia epuka kuvaa nguo za ndani zinazo bana sana na zenye asili ya nailoni kwasababu hutengeneza unyevu ambao ni rahisi kwa bacteria kuishi.

.Pia hakikisha unabadilisha pampasi ya mtoto mara baada ya kujisaidia kwasababu unyevu hutengeneza mazingira rafiki kwa kuishi wadudu,pia kumbuka kumsafisha kutoka mbele kwenda nyuma.



Kumbuka ugonjwa wa uti unaweza ambukizwa kwa kujamiiana pia kwaiyo kwa wanandoa au wapenzi endapo mmoja ataugua ugonjwa huu basi hakikisha mwenza wako nae anapata vipimo na kupata matibabu sahii .


Unaweza ukatoa maoni yako hapa chini.


Mawasiliano whatsap.0712106789



Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts