Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Maandalizi muhimu wakati wa kujifungua.

Habari gani ndugu msomaji na mfatiliaji wa makala za mikathommedia matumaini yangu ni wazima wa afya tele.Leo tutajifunza 'Maandalizi muhimu wakati wa kujifungua'

Maandalizi ya kujifungua inabidi yafanyike mapema kadiri mimba inavyodhidi kukua na hadi kufikia miezi tisa inatakiwa yawe yame kamilika.Lengo kuu la kuandaa mahitaji aya ni kwamba muda wowote mama akipata tatizo litokanalo na uzazi au akiugua au uchungu ukimwanzia ghafla aweze kusaidiwa na atimaye aponywe au ajifungue salama.

Ndugu msomaji kama nilivo eleza,maandalizi ya kujifungua kwa mama mjamzito ni muhimu yakafanywa mapema kwa sababu matatizo yatoka nayo na uzazi hayatabiliki,lakini wapo baadhi ya akina mama hawafanyi maandalizi mapema bali hufanya hadi miezi tisa itimie kwa maana iyo endapo mama anaetoka katika familia hii akapatwa na tatizo ambalo linahitaji msaada wa haraka watashindwa msaidia ivyo basi kupoteza maisha ya mama na mtoto.Ili mama mjamzito aweze kujifungua salama mambo kadhaa inapaswa yaandaliwe nayo ni:

Sehemu ya kujifungulia:


Mama anashauriwa pindi tu agunduapo ni mjamzito kwa kushirikiana na mumewe pamoja na wataalamu wa afya waandae sehemu ya kwenda kujifungua,hii itakuwa rahisi kama atazingatia kliniki kama atakavoshauriwa na wataalamu wa afya.Lakini endapo mahudhurio yake yatakuwa hafifu kliniki basi hatopewa ushauri kulingana na hali ambayo inaweza ikatokea muda wowote katika kipindi cha ujauzito.Mama mjamzito pia anashauriwa aende akajifungue katika hospitali kubwa hususani kwa wale ambao ni mimba za kwanza na ambao wamebeba mimba zaidi yanne ili endapo watashindwa jifungua kawaida wafanyiwe operesheni ya kutoa mtoto ivo basi kusalimisha maisha ya mama na mwanae.

Watu wa kuchangia damu:

Hili nimojawapo ya maandalizi ya muhimu sana kwa mama mjamzito kwasababu endapo mama atagundulika ana uwingi mdogo wa damu itahitajika aongezewe damu na damu iyo itatolewa na watu hawa.Pia kipindi cha kujifungua kuna matatizo mbali mbali ambayo yana mkabili mama mjamzito na kutishia maisha yake matatizo ayo ni kama kutokwa na damu nyingi sana wakati wa kujifungua(pph) na wakina mama wengi wanapoteza maisha kutokana na tatizo hili ivyo basi kulazimika kuwekea damu ili kunusuru uhai wa mama,hapo ndipo umuhimu wa watu wakuchangia damu unapoonekana.

Pesa:

Pesa ni hitaji muhimu sana katika maisha yetu yakila siku kwasababu pesa hutatua shida nyingi sana katika maisha ya sisi binadamu.Ndiyo maana kila mwanadamu anajishughulisha katika shughuli mbali mbali ili apate pesa na ainue uchumi wa familia.Pesa hizi ambazo tuna zitafuta ndizo husaidia kutatua matatizo mbalimbali pindi yanapotokea na kuendesha maisha yetu ya kila siku.Pesa katika kipindi cha ujauzito hutumika kuandaa lishe bora kwa mama ili awe na afya bora,pia hutumika andaa vifaa vyote vya kujifungua ili mama ajifungue salama,Vile vile zitatumika kuandaa usafiri wa kumpeleka mama hospitali pindi uchungu ukimwanzia au tatizo lolote likijitokeza,Pia zitatumika kugharamia matibabu yote ya mama pindi akiugua na atajifungua kwa njia gani na inategemea kajifungua ktk taasisi ya serikali au binafsi.Tushaona umuhimu wa pesa katika kipindi cha ujauzito hivyo basi tunashauriwa tufanye kazi kwa juudi zote na tukisha pata pesa tuzitumie kwa uangalifu pia tujiwekee akiba ili zitufae wakati wa matatizo kwasababu matatizo yanatokea muda wowote.

Vifaa vya kumsaidia mama ajifungue salama: 

Mama mjamzito anashauriwa aandae vifaa vya kumsaidia ajifungue salama mapema kwasababu uchungu unaweza ukajitokeza muda wowote baada ya miezi tisa hususani kwa wakina mama ambao wamezaa zaidi ya mara moja ,uchungu unaweza ukajitokeza awapo njiani kuelekea hospitali au hata nyumbani ivyo basi kama vifaa vitakuwa vimeandaliwa basi mama uyu atasaidiwa ajifungue salama.Vifaa ivyo ni kama mpira wa kuvaa mkononi,Wembe,uzi,dishi,nguo za kumfunika mtoto,na mavazi ya mtoto.



Soma:dalili-za-hatari-kwa-mjamzito.html



Usafiri: 

Usafiri wa kumpeleka mama hospitali ni lazma uandaliwe mapema ili pindi mama atakavojisikia homa au uchungu aweze pelekwa hospitali kwa haraka. Kama unao usafiri binafsi ni jambo jema lakini kama huna usafiri ni vema ukaandaa pesa za kutosha zitakazo kusaidia tafuta usafiri wa kumfikisha mama hospitali kwa harka zaidi.

Watu wa kumsindikiza hospitali pamoja na watakao tunza familia mama awapo hospitali:

 Mama mjazito vile vile lazma aandae watu ambao watamsindikiza hospitali kwa ajili ya kujifungua.Ni jukumu la mama mwenyewe kumwandaa mtu ambae anaendana nae, anamwamini,atakuwa na uhuru nae kumweleza jambo lolote pindi atakavokuwa anahitaji msaada.Ndugu msomaji najua wajua kila mmoja kuna mtu ambae anamwamini na anakuwa na uhuru nae kumweleza jambo ,hata kama jambo hilo ni lasiri anawexa akamweleza kwakuwa tu ni mwaminifu na anaweza kumtunzia siri,siyo ivyo tu mtu huyu pia anaweza msaidia mama kufanya maamuzi na kumpa ushauri kwa ujumla.Pia lazma aandae mtu wa kuangalia familia pindi awapo
hospitali.

Mwisho

Kujifungua salama inawezekana kabisa,Mama mjamzito hakikisha unahudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito pamoja na mumeo au mwenza wako ili mkajifunze malezi pamoja na matatizo ambayo yanaweza jitokeza kipindi cha ujauzito na namna ya kuya kabili.Pia fanya maandalizi ya kuji fungua mapema iwezekanavyo hii ni pamoja na pesa za kutosha kwasababu matatizo yaweza jitokeza muda wowote.

Pia jitahidi kuwahi hospitali mapema uonapo dalili za hatari ili uweze kupewa msaada,Pia muda wako wa kujifungua ukifika wahi mapema hospitali ili kuepuka kuji fungulia nyumbani au barabarani pindi uelekeapo hospitali,kwasababu kunamatatizo mengi yatoka nayo na kujifungua ivyo ukijifungua nyumbani au barabarani endapo matatizo yakijitokeza kuna uwezekanao mkubwa wa kupoteza maisha yako ,lakini kumbe ukiwahi hospitali utasaidiwa hata kama matatizo yatajitokeza utakuwa salama"Ewe mama mjamzito unae tarajia kujifungua chukua hatua kujifungua salama inawezekana."




Mawasiliano whatsap: 0712106789
  
    
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts