Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Homa ya ini (hepatitis B) na Madhara yake.


Homa ya ini (hepatitis B)

Ni ugonjwa wa kuambukizwa ambao unashambulia ini na una sababishwa na wadudu waitwao hepatitis B virus (HBV), vile vile upo unaosababishwa na virus A,C,D,E na G.


Aina za ugonjwa wa ini (hepatitis).

Homa ya ini imegawanyika katika makundi matatu kutokana na visababishi vya ugonjwa huo ,makundi ayo ni.

.Homa ya ini inayotokana na wadudu (infectious hepatitis)

Homa hii husababishwa na wadudu wajulikanao kama virusi,wadudu hao wanapoingia kwenye ini hushambulia seli za ini na kusababisha mabadiliko ya seli izo,pia inaweza sababishwa na bacteria au fungus.

Aina hii imegawanyika katika makundi yafuatayo.

i.Hepatitis A inayo sababishwa na hepatitis A virusi(HAV).

ii.Hepatitis B inayo sababishwa na hepatitis B virus(HBV).

iii.Hepatitis C inayo sababishwa na Hepatitis C virus(HCV).

iv.Hepatitis D inayo sababishwa na hepatitis D virus(HDV).

v.Hepatitis E inayo sababishwa na hepatitis E virus(HEV)

vi.Hepatitis G inayo sababishwa na hepatitis G virus(HGV).


.Homa ya ini inayotokana na sumu (toxic hepatitis).

 Homa hii husababishwa na matumizi ya madawa, chemikali ,na sumu ambazo kipindi zinapoingia mwilini hupelekwa kwenye ini kuvunjwa vunjwa,sumu hizi kadiri zinavyo zidi kuwepo mwilini kutokana na matumizi ya mara kwa mara huathiri seli za ini matokeo yake mtu atapata ugonjwa wa ini.

Dawa ambazo huathiri seli za ini na zinaweza zika sababisha ugonjwa wa ini ni pamoja na,pombe ,tetracycline,chloroform,acetominophin,asprin,steroids,halothane,phenotheazine component n.k.

.Homa ya ini ina yotokana na mabadiliko ya mzunguko wa damu (circulatory hepatitis).

Hii inaweza sababishwa na matatizo kama vile mshtuko (shock),moyo kushindwa kufanya kazi(cardiac failure ),mambo haya husababisha seli za ini sizipate damu ya kutosha matokeo yake ni homa ya ini.



Soma/ujue-uhimu-wa-baba-kuhudhuria-kliniki.html



Vihatarishi vya kupata ugonjwa wa ini.

i.Homa ya ini inayo sababishwa na virusi (A)E.

Homa hii hutokana na kula chakula au maji au maziwa yenye vimelea vya ugonjwa  wa ini A au E.

ii.Homa ya ini inayo sababishwa na virusi(B),C,D,G,homa hii inaweza sababishwa na:

.Kufanya ngono isiyo salama na mtu ambae anavimelea vya ugonjwa huu au ana ugonjwa wa zinaa.

.Kuchangia vifaa vyenye ncha Kali kama nyembe na sindano.

.Kuchangia damu ambayo siyo salama.

.Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

.Kutoka kwa mama mjamzito mwenye virusi vya homa ya ini kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.

.Kunyonyana ndimi(oral sex).

.Kuchangia miswaki.

.Mapenzi ya jinsia moja.

Pia homa hii inaweza sababishwa na magonjwa mbalimbali,na matatizo ya metabolism.


Dalili za ugonjwa wa hepatitis.

Kuna baadhi ya watu hawaoneshi dalili hata kama wana ugonjwa huu dalili huonekana baada ya INI kuathirika dalili hizo ni.

.Kichefuchefu

.Kuwashwa .

.Kutapika.

.Kupoteza hamu ya kula.

.Kukojoa mkojo mweusi.

.Manjano viganjani na machoni.

.Maumivu ya mwili na viungo .

.Homa Kali.

.Maumivu ya tumbo upande wa juu kulia.



Vipimo vya ugonjwa wa hehepatitis.

.Kipimo cha damu kujua aina ya wadudu.

.Kipimo cha damu kujua ufanyaji kazi wa ini(liver function test).

.Picha(ultrasound) kuangalia ini kwa ujumla.


Madhara ya ugonjwa wa ini.

.Saratani ya ini (hepatocellular carcinoma).

.Ini kuvimba( cirrhosis).

.Magonjwa ya figo.

.Ini kushindwa kufanya kazi (liver failure).



Ufanye nini kuepuka homa ya ini(hepatitis B)?

.Chanjo dhidi ya ugonjwa wa hepatitis B inapatikana kote nchini.

.Hakikisha unajikinga unapofanya ngono.

.Epuka kuchangia vifaa vyenye ncha Kali kama sindano.

.Epuka kuchangia miswaki.

.Epuka mapenzi ya mdomo.

.Epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

.Epuka matumizi ya pombe.

.Epuka matumizi holela ya dawa na kemikali.

.Pia zingatia usafi.

.Kwa wafanyakazi wa afya kutumia vifaa vya kujikinga na magonjwa wanapo toa huduma kama mipira ya mikononi,maski,buti,na miwani.

.Kuhakikisha wagonjwa wana pata damu salama.



Matibabu

Unashauriwa kwenda hospitality ili ufanyiwe uchunguzi mapewa ili upewe dawa na matibabu muhimu.

Ugonjwa wa ini hauna tiba lakini matibabu yake hulenga kuzuia INI lisiathirike zaidi.

Dawa zinazotolewa  ni pamoja na interferons ambayo huongeza kinga za mwili,ant  viral na corticosteroids.

Dawa hizo ni pamoja na adenofir na lamivudine ambayo hutolewa kwa wale ambao adenofir haiwasaidii.

Dawa zingine ni pamoja na entercavir(baraclude) na tenofovir.


Whatsap:0712106789



Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts