Home »
» Umuhimu wa kuujua mzunguko wa hedhi
Umuhimu wa kuujua mzunguko wa hedhi
Mzunguko wa hedhi
Ni mpangilio wa mabadiliko yanayotokea katika mwili wa mwanamke kila mwezi kwaajili ya maandalizi ya kuipokea mimba endapo itatungwa.
Hedhi
Ni kiwango cha damu kinachotoka katika tumbo la uzazi la mwanamke kupitia uke,ambayo ni matokeo ya kumeguka kwa moja ya ukuta wa tumbo la uzazi(endometriam) endapo mimba haitotungwa.
Mzunguko wa hedhi kwa kawaida huanza Siku ya kwanza ya hedhi ya kila mwezi na huishia au kukoma siku ya mwisho kabla ya kuanza kwa mzunguko mwingine.mzunguko was hedhi hutofautiana kutokana na siku au muda na kiwango cha damu ambacho hutoka kutokana na umri,uzito,kazi za kila siku,kiwango cha mawazo pamoja na maumbile ya mtu.katika kila mwezi mfuko wa mayai hutoa mayai yaliyokomaa au kupevuka tayari kwa utungwaji wa mimba endapo mwanamke atakutana na mwanaume katika siku za hatari.Pia kutokana na mabadiliko ya vichocheo vya mwili kila mwezi tumbo la uzazi huandaliwa ukuta mpya kwaajili ya kupokea mimba ambayo hutungwa.Sasa kama mimba haitotugwa ukuta huo umeguka ukiwa pamoja na damu na kutoka nje kupitia uke,kitendo hiki huitwa hedhi
Mzunguko wa kawaida wa hedhi huanza siku ya kwanza ya kutokwa na damu hadi siku ya kwanza kabla ya mzunguko mwingine japo kuwa mzunguko wa hedhi kwa kawaida in siku 28,pia ni jambo la kawaida kuwa na mzunguko wa siku pungufu au zaidi ya siku 28.Mzunguko huu hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.Mzunguko wa kawaida huwa ni wa siku 21 hadi 25 kwa wanawake wakubwa na hadi siku35 kwa wanawake wadogo.katika hali ya kawaida ni kawaida sana kwa wanawake walioanza kupata hedhi ya kwanza kuwa na mizunguko mirefu katika miezi kadhaa ya mwanzo lakini baadae hupungua kadiri ya siku na umri unavyo kwenda.
Lini msichana huanza kupata hedhi ya kwanza na lini hedhi hufika ukomo?
Msichana huanza kupata hedhi ya kwanza kuanzia umri wa miaka 11 hadi miaka 14.Japo siyo wasichana wote watapata hedhi yao wakiwa katika umri huo,kuna ambao watapata hedhi yao wakiwa na umri chini ya miaka 11 na wengine wanaweza wakapata hedhi ya kwanza wakiwa na miaka zaidi ya 14 hii inawwza ikatokana na vile mtu alivyo umbwa,na hata kuugua maradhi ya kudumu.Endapo msichana atatimiza miaka 15 hadi 16 na hajapata hedhi yake ya kwanza anashauriwa aende hospitali kwa uchunguzi zaidi pia kupata matibabu.
Mwanamke huanza kupata hedhi ya kwanza akiwa na umri wa miaka 11 lakini kadiri umri unavozidi kwenda hedhi hiyo inafika ukomo.Ukomo huo wa hedhi huanza mpata mwanamke akishafikisha miaka 45 hadi miaka 55.Lakini mwanamke akisha fikisha umri kuanzia miaka 40 mzunguko wake wa hedhi hubadilika kutoka katika mzunguko wa siku 3 hadi 5 na kuwa na mzunguko wa muda mrefu kuanzia siku 7 na hata zaidi ya hapo na baadae hedhi hiyo hukoma kabisa.Pia wanawake wengi hupatwa na ukomo wa hedhi wangali wakiwa na umri mdogo kwasababu mbalimbali kama vile,maradhi ya kudumu au kuugua kwa muda mrefu,upasuaji na baadhi ya matibabu kama ya mionzi.
Hedhi ya kawaida inakuwaje?
Wakati wa hedhi mwanamke hutokwa na damu ukeni yenye mchanganyiko wa ukuta wa tumbo la uzazi(endometrium) ulio meguka baada ya mimba kushindwa kutungwa.Kiwango icho cha damu huwa kinatofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.Katika hali ya kawaida wanawake wengi hupata hedhi inayo dumu kati ya siku 3 hadi siku 5.Pia kuna wengine ambao hupata hedhi inayo dumu kati ya siku 3 hadi siku 7 hii nayo ni kawaida inategemeana na mzunguko wao kwasababu mzunguko hutofautiana kati ya mtu na mtu.
Soma/homa-ya-ini-hepatitis-b-na-madhara-yake.html
Dalili za awali za hedhi
Baadhi ya wanawake hujisikia vibaya siku chache kabla ya kuanza kupata mzunguko wao wa hedhi wa kila mwezi.Dalili hizo wanazo zipata hujulikana kama dalili za awali za hedhi nazo ni kama maumivu ya matiti,tumbo la chini kujaa,USO kutoa mafuta mafuta pamoja na chunusi,maumivu ya misuli kwenye tumbo la chini au mgongoni,wengine huwa ni wepesi wa kukasirika hata kwa jambo dogo. Wanawake walio wengi hupatwa na dalili moja wapo kila mwezi lakini kuna baadhi yao hupatwa na dalili karibia zote. Mwanamke anaweza akapata dalili tofauti tofauti katika mwezi mmoja na mwingine.
Vitu vinavyo fanyika mwilini kwa mwanamke wakati wa hedhi.
Homoni
Ni chemikali huzalishwa au hutengenezwa na ubongo(kisehemu cha mbele cha tezi ya pituitari, hypothalamus,) na kifuko cha mayai katika nyakati tofauti za mzunguko wa hedhi.
Mzunguko wa hedhi huendeshwa na homoni au vichocheo mbalimbali vya mwili.Wakati wa mzunguko sehemu za ubongo(hypothalamus,na tezi ya pituitari) hupeleka taarifa za homoni au vichocheo kwenda kwenye vifuko vya mayai na kurudishwa kwenye ubongo, taarifa hizi hufanya tumbo la uzazi pamoja na kifuko cha mayai kiwe tayari kwa utungwaji wa mimba.Vichocheo au homoni hizo ni kama zilivyo ainishwa hapo chini na kazi zake.
.Gonadotrophine releasing factor (GnRF).
Ni kichocheo ambacho kinazalishwa na hypothalamus moja ya sehemu katika ubongo.Kazi kubwa ya kichocheo hiki ni kuhakikisha kiwango cha vichocheo Follicle stimulating homoni (FSH) na luteinizing homoni (LH) havizalishwi kwawingi sana na havizalishwi kwa kiwango cha chini zaidi.
.Follicle stimulating homoni(FSH).
Ni kichocheo ambacho kinazalishwa na kisehemu cha mbele cha tezi ya pituitari.Kichocheo hiki hufanya kazi kuu mbili,Kuchochea ukuaji wa kifuko cha mayai,baadae kifuko hiki cha yai kikisha komaa hupasuka na kuachia yai ambalo limekomaa tayar kwa mimba kutungwa.pia husaidia kuchochea seli za kifuko cha mayai kilicho kwisha pasuka kitengeneze kichocheo au homoni oestrogeni.Sehemu ambazo kichocheo cha follicle stimulating homoni hufanya kazi ni pamoja na kwenye ubongo,mayai,tumbo la uzazi na kwenye shingo ya uzazi.
.Luteinizing homoni(LH).
Ni kichocheo ambacho huzalishwa na kisehemu cha mbele cha tezi ya pituitari .Kichocheo hiki hufanya kazi kuu tatu,husababisha yai lipevuke na kuwa tayari kwa utungwaji wa mimba,pili hubadilisha kifuko cha mayai kilicho pasuka kiwe corpus luteum,tatu husaidia kuchochea corpus luteum itengeneze kichocheo cha Progestrone.
.Oestrogen.
Ni kichocheo ambacho huzalishwa kwenye seli za vifuko vya mayai vilivyo pasuka.Kichocheo hiki hufanya kazi kuu tatu,moja husaidia katika ukuaji wa mishipa ya damu katika kuta za tumbo la uzazi (endometrium) na kuongeza ukubwa wa ukuta wa endometrium kwa ajili ya kupokea mimba itakayo tungwa au kuongeza kiwango cha ukuta utakao meguka kama mimba haito tungwa,pili huongeza kiwango cha uteute mwepesi na wenye kuteleza na wenye kuvutika katika shingo ya tumbo la uzazi ,ute ute huu ni moja ya ishara ya kwamba yai limepevuka na kama mwanamke atakutana na mwanaume basi mimba itatungwa.Ute huu huisaidia mbegu ya kiume iweze kuogelea kwa urahisi Katika safari ya kurutubisha yai na kuifanya mbegu ya kiume iwe hai kwa muda.
.Progesterone.
Ni kichocheo ambacho huzalishwa na corpus luteum Mara baada ya kifuko cha yai kilicho pasuka kubadilishwa na kichocheo cha Luteinizing .Kichocheo cha progesterone hufanya kazi zifuatazo,moja huchochea ukuaji na maendeleo zaidi ya mishipa ya damu na tezi katika ukuta wa endometrium.Pili hufanya kiwango au kiasi cha ukuta wa endometrium ubaki katika kiwango kile kile bila kupungua wala kuongezeka.Tatu husaidia kupunguza kiwango cha ute ute ambao umezalishwa na shingo ya tumbo la uzazi na kuufanya ute ute huo uwe mzito hivyo kusababisha mbegu ya kiume ishindwe kuogelea na kulirutubidha yai na kuifanya ikose uhai kwa muda mfupi.Pia endapo kichocheo hiki kitazalishwa kwa kiwango kikubwa basi kitapunguza uzalishaji wa gonadotrophin na hivyo kupunguza kiwango cha Luteinizing na follicle.
Awamu kuu tatu za mzunguko wa hedhi.
Mzunguko wa hedhi kwa mwanamke una awamu kuu tatu,kuisha kwa mzunguko kwa awamu ya kwanza huashiria kuanza kwa awamu nyingine na nyingine na hatimaye mwanamke hujikuta anaingia katika mzunguko wake kwa Mara nyingine. Awamu hizo ni kama ninavyo ziainisha hapo chini..
.Awamu ya mzunguko wa hedhi (menstrual phase).
Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hutokwa na damu katika sehemu za siri Mara baada ya ukuta wa tumbo la uzazi kumeguka ikiwa ni matokeo ya mimba kushindwa kutungwa.Pia katika kipindi hiki kwa kuwa hakuna mimba ambayo inakuwa imetungwa basi hupelekea kiwango cha vichocheo vya Oestrogen na progesterone kuzalishwa kwa kiwango cha chini.Mwanamke akisha maliza kupata hedhi taratibu kiwango cha vichocheo hivi hutengenezwa kwa kiwango kikubwa hususani kuelekea katika siku ya 14 ambapo yai hupevuka.
.Awamu ambayo yai hupevuka au huachiliwa(proliferative/ovulatory phase).
Kipindi hiki ni kipindi ambacho yai hupevuka au huachiliwa tayari kwa utungwaji wa mimba endapo mwanamke na mwanaume watajamiana bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. Katika kipindi hiki kiwango cha vichocheo cha follicle stimulating homoni huzalishwa kwa kiwango kikubwa kwa lengo la kuchochea ukuaji wa vifuko vya mayai na kuchochea uzalishwaji wa kichocheo cha Oestrogen ili kutengeneza ute ute mwepesi na wenye kuvutika katika shingo ya uzazi,ute huu ni kiashiria yai limeachiliwa.
.Secretory phase
Kipindi hiki hutokea mara baada ya yai kuachiliwa.Kifuko cha mayai kilicho pasuka hubadilishwa kuwa corpus luteum ambayo huzalisha kiwango cha progesterone ambayo hulifanya tumbo la uzazi liwe tayari kukipokea kiinitete (embryo) na kujishikiza katika endometrium na kuendelea kukua hapo endapo mimba itatungwa.
Dalili kuu tatu za yai kuachiliwa
.Ute ute mwepesi,wenye kuvutika na kuteleza hii huashiria yai limeachiliwa.
.Nafasi ya mlango wa uzazi hubadilika wakati wowote wa mzunguko wa hedhi wakati yai linapo achiwa kutoka kwenye kifuko cha mayai.
.Kupanda kwa joto la mwili,joto la mwili wa mwanamke hupanda zaidi ya nyuzi 0.3 had 0.9 kutoka katika joto la mwili la kawaida.Kupanda huku kwa joto la mwili huashiria yai limeachiliwa ivyo mimba inaweza ikatungwa kama wana ndoa au wenzi watakutana bila kutumia njia yoyote ya kupanga uzazi.Kwa wenye mzunguko wa siku 28 basi mnashaurwa kukutana na mumeo angalau Mara tatu kuanzia siku ya 9 na ya 10 hadi siku ya 17.Kuanzia siku ya Tisa hadi ya 17 kuna uwezekano mkubwa wa kutungwa mimba.Pia kwa wale ambao wana mzunguko mfupi mfano siku 22 yai huachiliwa kuanzia siku ya 6 hadi ya 10 kwa iyo ndani ya hizi siku kuna uwezekano mkubwa wa kutungwa mimba.Pia kwa wale ambao wana mizunguko mirefu mfano siku 35 kuna uwezekano mkubwa yai kuachiliwa kuanzia siku ya 16 ya mzunguko hadi siku ya 23 ya mzunguko.
Mwisho
Endapo kama kuna mabadililo makubwa katika mzunguko wa siku zako,pengine damu kutoka kwa wingi,kutokupata siku zako kabisa ni vema wahi hospitality ukafanyiwe matibabu na vipimo.
Mawasiliano whatsap :0712106789
No comments:
Post a Comment