Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Ujue uhimu wa baba kuhudhuria kliniki


Ndugu msomaji,athari au matatizo yatokanayo na ujauzito huwa hayatabiriki ni wakati gani yanaweza yakatokea.Kwa upande mwingine ufahamu wa jamii kuhusu athari hizi ambazo zinaweza jitokeza wakati was ujauzito kwa mama na kiumbe aliyoko tumboni bado umekuwa ni mdogo .Mwanaume katika jamii anaushawishi mkubwa kwasababu anakubalika katika jamii kwa haraka sana kuliko mwanamke ,kwaiyo basi kuhusishwa kwa baba katika kliniki inasaidia jamii iweze pata uelewa kwa haraka zaidi na anaweza akawa msambazaji wa athari ambazo zinaweza mkumba mama mjamzito katika jamii .

Mke na Mume wote kwa pamoja inatakiwa wahudhurie kliniki mapema kwasababu zifuatazo:

Kuhudhuria kliniki mapema husaidia kugundua na kutibu homa au ugonjwa unao mkabili mama mapema zaidi kabla ya ugonjwa haujawa sugu.

Vile vile kuhudhuria kliniki mapema kunaongeza usalama wa Afya ya mama pamoja na mtoto kwa sababu endapo mama atagundulika ni mgonjwa basi atapewa matibabu mapema na kufanya Afya take na mtpto iwe salama salimini .

Pia husaidia kukabiliana na changamoto au matatozo yatoka nayo na ujauzito kiipindi cha ujauzito na hata baada ya kujifungua kwa kutambua viashiria au dalili za hatari kwa mjamzito kabla kipindi cha kujifungua na hata Mara baaada ya kujifungua.


Hivyo basi kutokana na madhumuni makubwa matatu ya kuhudhuria kliniki baba unashauriwa uambatane  na mkeo kliniki  kwasababu zifuatazo hapo chini.



.Humfanya baba aweze kijali familia na kujihusisha zaidi katika suala la malezi ya familia ambayo ameipata.


.Humsaidia kujua madhara au dalili za hatari ambazo mwanamke anaweza akazipata katika kipindi cha ujauzito ,wakati wa kujifungua na Mara baada ya kujifungua ivyo basi kufikisha taarifa izo kwa wengine na hapo uelewa wa jamii juu ya madhara au dalili za hatari katika kipindi cha ujauzito unakuwa umeongezeka



.Husaidia aweze kuchukua hatua mapema kwa kushirikiana na mama mara tuu zitokeapo dalidi za hatari ivyo basi kuongeza usalama wa mama na mtoto .

.Humsaidia baba ajue na aandae mahitaji ya kujifungua mapema hii in pamoja na sehemu ya kujifungua,usafiri na pesa ya kutoka kwasababu baba ndie kichwa na mfanya maamuzi wa mwisho katika familia.

.Husaidia familia kujiandaa kumtunza mama na kumpa mtoto atakae zaliwa malezi bora na mahitaji ya msingi katika familia.

.Humfanya baba awe mwenye kujali na kuthamini familia aliyoipata ivyo basi hufanya upendo kati yake na familia kwa ujumla uongezeke kwa kiwango kikubwa tofauti na baba ambae hajali na kuthamini familia ,ambapo upendo katika familia hii utashuka kwa kiwango kikubwa.

.Itamsaidia baba aweze kumuimiza na kumkumbusha mama siku za kuhudhuria kliniki kabla na baada ya kujifungua endapo mama atasahau ivyo basi kuonekana baba bora wa familia

.Pia kwakuwa mwanaume anakubalika zaidi katika jamii ,akihudhuria kliniki yeye atakuwa ajent wa kusambaza taarifa kwa jamii ivyo basi ufahamu katika jamii utaongezeka.



Soma/utumiaji-wa-madawa-ya-kulevya-na-athari.html


Mwisho

Ndugu msomaji wa makala hii uwe baba au mama najua umepata ufahamu juu ya umuhimu wa kuhudhuria kliniki pamoja na mkeo au mumeo,kwahiyo kama we we ni mama nivema umkumbushe na kumuhamasisha mumeo kuhudhuria kliniki ili kupunguza madhara au matatizo yatokanayo na uzazi,Pia kama wewe ni baba tambua ni wajibu wako kuambatana na mkeo kliniki ili uwe baba bora wa familia na mwenye kujali,kuthamini na kulea familia katika misingi bora na atimae upendwe nafamilia yako wakati wa  sasa na baadae pia.



Mawasiliano whatsap:0712106789




Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts