Ni hali ya mwanamke kushindwa kupata mimba au kubeba ujauzito ndani ya mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi au wanandoa ambao hufanya mapenzi au hujamiana bila ya kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango,(mfano mipira ya kiume au kike,kitanzi ,kipandikizi ,vidonge pamoja na sindano).
Tatizo la ugumba linaweza likatokea kwa jinsia yoyote kwa mwenza wa kike au wa kiume.Lakini kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa masuala ya uzazi na kujamiana kwa wapenzi au wana ndoa uliopo katika jamii zetu watu hudhania kwamba tatizo la ugumba humtokea mwanamke pekee jambo ambalo siyo kweli.Pia mahusiano au ndoa nyingi huvurugika kutokana na kukaa muda mrefu bila kupata mtoto kwasababu wanaume huamini wao wapo vizuri lkn mwanamke ndo huwa jamvi la tatizo hili.Lakini hatuwezi tukasema mtu ni mgumba bila kujiridhisha kuwa mimba haiwezi ikatungwa,kwahiyo ugumba unaweza ukatibika endapo utaenda hospitali kupata matibabu na kuyatendea Yale ambayo utaambiwa uzingatie.
Aina mbali mbali za ugumba
Kuna aina mbili za ugumba nazo ni kama nitakavo zieleza hapo chini.
i.Ugumba wa asili (primary infertility).
Ni aina ya ugumba ambao hutokea ambapo wenzi wawili hawaja wahi kusababisha au kutungisha mimba kwa muda wa mwaka mmoja japo kuwa wamejamiana bila kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi.
ii. Ugumba baada ya maisha(secondary infertility).
Ni aina ya ugumba ambao wenzi au wanandoa walishawahi kutungisha mimba au ujauzito ndani ya mwaka mmoja Mara baada ya kujamiana bila ya kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi,lakini baada ya hapo hawajawahi kutungisha mimba tena pamoja na kujamiana bila kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi.
Soma /ujue-ugonjwa-wa-kiharusi.html
Nini husababisha ugumba?
Tatizo la ugumba huweza mtokea mwanamke au mwanaume ,japo wanaume wengi huamini hugumba humpata mwanamke pekee jambo ambalo siyo kweli.
Ugumba kwa wanawake huwezasababishwa na.
i.Matatizo katika mji wa mimba na njia ya usafirishaji wa yai pamoja nambegu za kiume.
Via vya uzazi vya mwanamke hujumuisha uke,shingo ya uzazi,tumbo la uzazi,mfuko wa mayai,na mirija ya uzazi ambako ndiko mimba hutungwa kutokea kwa tatizo katika via hivi inapelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito.
Mfano, kuziba au kuharibiwa kwamirija ya uzazi ambako kwaweza sababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kaswende na kisono kunasababisha yai lisiweze kukutana na mbegu ya kiume ivyo basi mimba haito tungwa.
Pia,upasuaji katika mirija ya uzazihuacha makovu baada ya kidonda kupoa makovu ayo yanaweza ziba mirija ya uzazi ivyo kuzuia kabisa utungishwaji wa mimba.
Uvimbe katika tumbo la uzazi pia husababisha mimba isiweze tungishwa hata kama wanandoa wakakutana bila kutumia njia ya upangaji uzazi mwaka mmoja na zaidi.
Hali ya uke na shahawa, Ili mwanamke apate mimba mwanaume hukojoa shahawa kwenye uke wa mwanamke,shahawa husafiri kwenye uke wa mwanamke hadi kwenye mirija ya uzazi kwenda kurutubisha yai.Sasa ili mbegu ya kiume iwe hai au salama wakati inasafiri katika uke wa mwanamke nilazima ikute majimaji yanayo patikana ukeni yakiwa katika hali ya nyongo(alkaline),kama majimaji hayo yatakuwa katika hali ya tindikali(asidi) basi mbegu za kiume zitakufa kabla ya kulifikia yai ivyo basi hakutakuwa na utungwaji wa mimba. Pia uke usio wa kawaida mfano uke ulio tengana,bikira pamoja na uvimbe katika uke unaweza sababisha mimba isitungwe.
Shingo ya kizazi.
,Ni moja ya sehemu ambapo shahawa hupita kuelekea katika zoezi la urutubishaji,mwanamke anaweza asipate mimba endapo akashambuliwa na magonjwa ya kudumu bila ya kupata matibabu katika shingo ya kizazi kwasababu magonjwa katika shingo ya kizazi husababisha uteute unaotengenezwa na shingo ya kizazi utengenezwe kwa kiwango kidogo hivyo basi kupunguza uwezo wa mbegu za kiume kuogelea kuelekea kurutubisha yai na matokeo yake mimba haito tungwa,vile vile kuwepo kwa jeraha katika shingo ya uzazi ambalo limetokana na kuchukuliwa kwa sampuli katika eneo hili pia inaweza pelekea mimba isitungwe. Piakuwepo kwa uvimbe au kansa katika shingo ya kizazi kutapelekea mimba isitungwe.
ii.Mayai kutolewa kidogo aukutokutolewa kabisa.
Ili mimba itungwe ni lazima mfuko wa mayai uzalishe mayai yalio komaa mengi,kuzalishwa kwa wingi kwa mayai huongeza uwezekano mkubwa wa mimba kutungwa. Kwaiyo kuzalishwa kwa mayai kidogo hupunguza uwezekano wa mimba kutungwa na husababishwa na mambo mbali mbali kama vile umri mkubwa, mayai huzalishwa kwa wingi kipindi mwanamke akiwa na umri mdogo lkn kadiri umri unavyo sogea uzalisha wa mayai hupungua ivyo basi uwezekano wa kushika mimba hupungua vile vile.Uvutaji wa sigara,kansa ya mfuko wamayai,mabadiliko ya vichocheo vya mwili ambavyo huenda vikasababisha mwanamke apate hedhi bila kuzalishwa mayai, ugonjwa wa fuko la mayai kujaa maji,ugonjwa wa endometriosis na mayai kutokupevuka kutokana na kutokuwepo kwa yai navyo husababisha mimba isitungwe.
iii.Mayai kushindwa kujishikiza kwenye mji wa mimba.
Mimba hutungwa pale ambapo moja kati ya yai kutolewa katika kiwanda cha mwanamke.kitendo hiki hujulikana kama yai. kupevuka(ovulation).yai lililo pevuka husafiri hadi kwenye mji wa mimba kupitia mirija ya uzazi iitwayo fallopia.Pia mbegu moja ya kiume lazima iungane na yai au mayai ya kike pindi yanapo safiri katika mirija ya uzazi kuelekea kwenye mji wa mimba.Baada ya mbegu ya kiume na yai kuungana .Muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka hadi kwenye tumbo la uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kukua,kwahiyo kuwepokwa uvimbe ndani ya tumbo la uzazi,wadadu ndani ya endometrium ambao wametokana na ugonjwa wa kifua kikuu,tumbo la uzazi kuwa katika hali isiyo ya kawaida kama kutokuwepo kwa tumbo la uzazihusababisha kiinitete kishindwe kujishikiza katika tumbo la uzazi.
iv.Magonjwa mbalimbali kama vile kisukari,ugonjwa wa ini,figo kushindwa kufanya kazi ya utoaji taka mwilini hupelekea mimba ishindwe kutungishwa.
Sababu zingine ni kama
.Utumiaji wa pombe ulio pitiliza.
.Uvutaji sigara.
.Msongo wa mawazo.
.Utumiaji holela wa dawa
.Uzito mkubwa
.Kufanya mazoezi kupitiliza .
Tatizo la ugumba kwa mwanaumehuweza sababishwa na
i.Kushindwa kuzalishwa kwa shahawa au kuzalishwa kwa kiwango kidogo au kuzalishwa kwa shahawa ambazo hazina uwezo wa kutungisha mimba.
Kuzalishwa kwa shahawa kwa kiwango kikubwa na shahawa zenye uwezo wa kutungisha mimba huongeza uwezekano wa mimba kutungwa na kuzalishwa kwa shahawa kiwango kidogo na zisizo na uwezo wa kutungisha mimba mfano kukosa mkia,au kuzalishwa kwa shahawa zisizo komaa hupunguza uwezekano wa mimba kutungwa,tatizo hili husababishwa na vitu kama vileUtumiaji wa madawa kupitiliza,umri mkubwa kuanzia miaka 50 na zaidi,matibabu ya mionzi,matatizo ya kende ya kiume,mazingira ya joto hususani katika kende mbili za kiume ,kende za kiume zina hitaji joto la kawaida ili shahawa zisi athiriwe,kwaiyo wanaume tunashauriwa tuepuke nguo za kubana na zinazo sababisha joto Kali.
ii.Kuziba kwa mirija inayobeba mbegu za kiume kama vile epididimis,ejaculatory duct na vasdeferens husababisha mbegu za kiume zishindwe kutolewa na kulifikia yai kwa ajiri ya urutubishwaji hali hii husababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kaswende na kisonono.Pia kutokuwepo kwa uteute(semen) unaozalishwa na tezi dume na seminal vescles hufanya mbegu zishindwe kuogelea na kulifikia yai hivyo mimba haito tungwa,Vile vile kufanyiwa upasuaji(vasectomy) nako huongeza uwezekano wa MTU kushindwa kutungisha mimba.
iii.Matatizo ya kimaumbile.
Kila mwanaume ana maumbile yake ,kuna wenye maumbile makubwa wengne madogo,kuna baadhi ya wanaume mrija wa kupitisha mkojo na shahawa upo chini ya kichwa cha uume (hypospadiasis) maumbile ya mwanaume mwenye shida hii ni ngumu sana kutungisha mimba,pia kufika kileleni mapema zaidi (premature ejaculation) hupunguza uwezekano wa mimba kutungwa. Vile vile kuna wengine hukojoa maji maji pekee bila mbegu ,pia kuhasiwa(importance) au kushindwa kusimamisha uume,kwaiyo matatizo kama haya hupunguza uwezekano wa mimba kutungwa.
iv.Msongo mawazo pia hupunguza uwezekano wa mimba kutungwa.
Vipimo vya ugumba kwa mwanaume
Vipimo mbali mbali hufanyika ili kugundua chanzo cha ugumba vipimo hivyo ni kama
.semen analysis,kipimo hiki huangalia uwingi wa shahawa,maumbile ,namna zinavyo ogelea na uwezo wa shahawa kuogelea na kulifikia yai.
Vipimo Kwa wanawake
.Kupima kiwango cha vichocheo kwenye damu.
.Kipimo cha kuangalia uteute wa shingo ya kizazi ili kujua jinsi unavyo teleza na kama unavutika.
.Kiwango cha joto la mwili,kupanda kwa joto la mwili baada ya kumaliza hedhi huashirka kwamba yai limepevuka kwa iyo kuna uwezekano mkubwa wa utungwaji mimba wakati huo.
.Kupima vichocheo vya luteinizing kwenye mkojo ili kukadiria lini yai litapevuka.
.Hysterosalpingography ni kipimo ambacho hutumia dawa kuangalia kama mirija ya uzazi imeziba.
Matibabu ya ugumba
Matibabu ya ugumba huhusishwa na wenzi au wana ndoa wawili.pia yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu kwasababu wakati mwingne matarajio au mafanikio yanaweza yasipatikane kwa haraka .Matibabu ni kama ifuatavyo.
i.Elimu na ushauri nasaa kwa wapenzi au wana ndoa .matatizo mengi hutokea sababu ya ufahamu au uelewa mdogo juu ya uzazi na kujamiana.Kuna baadhi ya wanaume hufika kileleni kwa haraka ivyo kukojoa mapema kabla ya muda mwafaka.hii husababisha kutokupatikana kwa ujauzito na hupelekea lawama zote kubebeshwa mwanamke pasipo mwanaume kujijua.Kwaiyo mwanaume wa namna hii ni vema akajiandaa vzur kisaikolojia kabla ya kukutana na mwenza wake ili mimba itungwe .
ii.Kupunguza au kuacha unywaji pombe na matumizi ya madawa ya kulevya.
iii. Kupunguza unene ulio pitiliza.
iv. Kupunguza ufanyaji wa mazoezi uliopitiliza.
v. Kuacha kuvaa nguo zakubana sana kwa wanaume kwasababu nguo za kubana huleta joto Kali sehemu za siri ivyo kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume.
vi. Kutokufahamu ni lini haswa Sikh ya kukutana na mwanaume ili mimba itungwe.kuna baadhi ya wanawake hawajui hata nilini mzunguko wao wa hedhi huanza na lini mzunguko huo huisha na unakuwa wa siku ngapi.Ili kuongeza uwezekano wa mimba kutungwa unashauriwa kujamiana angalau Mara tatu mfululizo baada ya yai kupevuka.Yai hupevuka wiki mbili kabla ya mzunguko mwingne wa hedhi,kama mzunguko wako hutokea baada ya Sikh 28 basi ni vema kujamiana angalau Mara tatu kuanzia siku ya 8 hadi 17 baada ya hedhi kukoma.Angalia mchoro hapo chini.Rangi nyekundu huashiria idadi ya siku ambazo mwanamke anapata hedhi kawaida ni siku nne had tano lkn kunawengine huenda had siku saba kutegemea na mzunguko.kuanzia siku ya tano had 8 ni siku salama kwa mwenye mzunguko wa siku 28 lkn kuanzia siku ya Tisa had 17 ni siku za hatari zingne znazobaki ni siku salama.
 .Dawa,hii hutumika zaidi kutibu magonjwa ya zinaa ila inategemeana na kisababishi cha ugumba.Pia dawa inaweza ikatumika kwa wale ambao fuko la uzazi linashindwa zalisha mayai matokeo yake mayai mengi ya tazalishwa kwa kiwango kikubwa na matokeo yake kunauwezekano mkubwa yai zaidi ya moja likarutubishwa ivyo kuzaliwa mtoto zaidi ya mmoja.
.Kuzingatia ulaji wa mlo kamili
.Njia saidizi za uzazi kama vile,artifisialinsermination hii ni njia ya kitaalamu ambapo mbegu za kiume hukusanywa na kuingizwa kwenye mji wa mimba,njia hii hutumika pale ambapo mwanaume anauwezo mdogo wa kuzalisha mbegu za kiume.Pia in vitrofertilization, njia hii hutumika endapo mirija ya mwanamke imeziba kwakuwa haiwezi pitisha mayai.Mbegu za kiume na mayai hukusanywa kitalamu kisha kurutubishwa.Baada ya apo yai lililo rutubishwa hupandikizwa kwenye tumbo la uzazi.
Mawasiliano Whatsap. 0712106789
No comments:
Post a Comment