Home »
» Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi husababishwa na nini ?
Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi husababishwa na nini ?
Mabadiliko ya mzunguko wahedhi.
Ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila mpangilio maalum.Tatizo hili huanza ghafla ambapo mwanzo alikua anaona siku zake kwa mpangilio maalum ,Mara mzunguko wake unakuwa haueleweki.Yawezekana mwanzo alkua anapata hedhi kwa siku tano lakini ikabadilika hadi kuwa siku saba au zaidi ya siku saba,pia wakati mwingine inaweza tokea akapata hedhi Mara mbili ndani ya mzunguko mmoja au akavusha mwezi mmoja au miwili na baadae anapata hedhi tena.
Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika maeneo makuu mawili nayo nikama ninavyo ya ainisha hapo chini.
Mzunguko unao pevusha mayai (ovulatorycircle).
Nimzunguko ambao yai hujiachia kutoka katika kifuko cha mayai Mara baada ya kukomaa tayari kwa utungwaji wa mimba kama wenzi watajamiana bila kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi.Pia katika mzunguko huu ute ute mwepesi ,wenye utelezi,na wenye kuvutika hutengenezwa ambao huashiria kupevuka kwa yai ili kuisaidia mbegu ya kiume kuogelea kirahisi na kulifikia yai.
Mzunguko usio pevusha mayai (un ovulatory circle).
Ni mzunguko ambao yai haliachiliwi kutoka katika kifuko cha mayai .Tofauti kati ya mzunguko huu na ule unaopevusha mayai ni kwamba ,ule usiopevusha mayai hauhusiswi na utengenezaji wa ute ute lakini unaopevusha mayai ute ute hutengenezwa ambao ni kiashiria yai limepevuka,kwahiyo katika mzunguko ambao haupevushi mayai mimba haiwezi ikatungwa kwasababu ya mabadiliko ya vichocheo vya mwili, japo katika mzunguko yote miwili mwanamke hupata hedhi kama kawaida.
Kukosa hedhi na kuvurugika kwa mpangilio wa hedhi huwakumba wanawake wengi kwa sasa na hii ni kutokana na mtindo wa maisha ambao ndio chanzo kikubwa cha matatizo ya kuvurugika kwa siku zao.Mpangilio wa hedhi huratibiwa na homoni au vichocheo mbali mbali ambavyo huzalishwa na ubongo na tezi mbali mbali katika mwili wa binadamu,kwahiyo yatupasa kuzingatia sana mitindo ya maisha yetu ambao huvuruga mfumo wa vichocheo vya mwili ili kuepuka kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi.
Sababu zinazopelekea mabadiliko ya mzunguko wa hedhi.
Ndugu msomaji kama nilivyosema mwanzo mvurugiko wa mzunguko wa hedhi ni tatizo linalo wakumba wanawake wengi katika miaka ya sasa,na hii ni kutokana na vile wanavyo endesha maisha yao ya kila siku ambacho ni chanzo kikubwa cha mvurugiko wa mzunguko wa hedhi ambayo ni matokeo ya kuvurugika kwa vichocheo mbali mbali ambavyo huzalishwa na ubongo na tezi za mwili.Kwa mwanamke ambae anaufahamu vzuri mzunguko wake wa hedhi ni rahisi sana kutambua pindi mabadiliko yanavyo jitokeza.Ili mwanamke ufahamu mzunguko wako ni lazima ujue lini unaanza kupata hedhi, inakoma kwa muda gani na lini unaanza kupata katika mzunguko mwingine.Tatizo hili linaweza likaanza kwa kuruka siku,au anaweza pata hedhi mwezi huu na unaofuata usione au unaweza kupata hedhi Mara mbili katika mzunguko mmoja au akapata kwa muda mrefu na mfululizo na huambatana na mabonge ya damu.Mabadiliko haya yaweza yakawa yanatokea kwasababu una moja kati ya mambo yafuatayo.
.Lishe duni (chakula).
Vyakula vyenye madini pamoja na vitamini husaidia tezi ya thyroid na adrenali zifanye kazi katika kiwango kinachofaa,kupungua kwa vyaakula vyenye madini na vitamini husababisha tezi hizi zifanye kazi kupitiliza ,kitendo hiki hupelekea kichocheo cha cortisol kitengenezwe kwa kiwango kikubwa.Kuongezeka kwa kichocheo cha cortisol husababisha kupungua kwa utengenezaji wa vichocheo vya uzazi ,kupungua kwa vichocheo vya uzazi huaribu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hivyo kupelekea mabadiliko ya mzunguko mzima wa hedhi.
.Msongo wa mawazo.
Pindi mwanadamu anavokuwa anamsongo wa mawazo au kuhofia jambo ambalo lipo mbele yake na kwa namna yoyote lazma alitatue jambo hilo kwa kukimbia au kupigana,Nishati kubwa katika mwili hutunzwa ili kuweza kukabiliana na changamoto ambayo ipo mbele.Kwahiyo msongo wa mawazo au hofu iyo hupelekea utendaji wa shughuli mbali mbali za mwili kupungua ikiwemo upevushaji wa mayai.Sasa kipindi mwanamke awapo katika msongo wa mawazo mwili hutengeneza vichocheo mawazo kwawingi kwakuwa uhai ni bora kuliko hedhi ili kukuandaa kukabiliana na changamoto iyo kwahiyo kadiri unavyokuwa na msongo wa mawazo ndivyo vichocheo vya mwili vinavozidi kubadilika matokeo yake mzunguko wa hedhi nao kuvurugika.
.Mazoezi kupitiliza.
Mazoezi humfanya mwanadamu awe na afya njema kwasababu husaidia kuimarisha kinga za mwili,huongeza msukumo wa damu mwilini pamoja na kutoa taka za mwili kwa njia ya jasho.Lakini ni vema mazoezi ago yakafanyika kwa kiwango bila ya kutumia kiwango kikubwa cha nishati ya mwili.Kufanya mazoezi kupitiliza husababisha kutumia kiwango kikubwa cha nishati ya mwili ,mazoezi hayo hupelekea kichocheo cha cortisol kizalishwe kwa wingi ili kujarbu kuziba kiwango cha nishati iliyopotea,kiwango kikubwa cha kichocheo cha cortisol hupunguza uzalishaki wa vichocheo vya uzazi na matokeo yake mvurugiko wa hedhi.
.Matatizo kwenye tezi ya thyroid (hypothyroidism).
Ni tezi ambayo hupatikana shingoni chini ya koromeo.Kazi kubwa ya tezi hii ni kuzalisha vichocheo vya triiodothronine(T3) na thyroxine(T4) .Vichocheo hivi hurekebisha mzunguko wa damu na kufanya kazi zingine za mwili.Kuzalishwa kwa vichocheo hivi kwa kiwango kidogo(hypothyroidism) hupelekea mabadiliko ya vichocheo cortisol na oestrogen,cortisol hupunguza utendaji kazi wa tezi ya thyroid sambamba na kuzuia uzalishaji wa vichocheo vya uzazi,matokeo yake utendaji kazi wa mwili hushuka na kufanya mayai yasipevuke.
.Uzito mdogo.
Ili kupata uzito ambao unakubalika kiafya kipimo cha body mass index(BMI) hutumika.BMI maana take uzito wako inabidi uendane na urefu wako.Bmi=uzito wako zidisha kwa mbili(2) gawa kwa urefu,kwakawaida inabidi iwe 18.5 ikiwa chini ya hapo ni uzito mdogo na zaidi ya 25 ni uzito mkubwa.Endapo mwanamke atakua na BMi chini ya 18.5 atakabiliwa na mvurugiko wa vichocheo vya mwili kama oestrogen.Kiwango kikubwa cha mafuta kina hitajika ili kuongeza uzalishaji wa kichocheo cha oestrogen .Kwahiyo watu wembamba na wenye kutokupenda kula ,mazoezi hufanya kuongezeka kwa uhitaji wa chakula mwilini,kutokana na mazoezi na kutokula hufanya uzito kupungua na kuwa Fanya wawe hatariini kupata mabadiliko ya vichocheo ivyo kuvurugika mzunguko wao.Pia wanawake wanene hupata hedhi Mara kwa Mara kwasababu wanakiwango kikubwa cha mafuta ambacho husaidia uzalishwaji wa kichocheo cha oestrogen kwa wingi.
.Polycystic ovarian syndrome.
Ni kutokuwepo kwa usawa wa vichocheo kwa wanawake ambako kuna pelekea mayai yasipevuke , mwanamke mwenye Tatizo hili hupelekea vichocheo vya oestrogen na progesterone vipungue,matokeo yake ni kuongezeka uzito na mabadiliko ya mzunguko wa hedhi.
Sababu zingine ni kama
.kubadilisha mazingira
.Matumizi ya njia za upangaji uzazi.
.Uvimbe kwenye tumbo la uzazi.
.Saratani katika tumbo la uzazi.
Soma/ kutokupata-mtoto-husababishwa-na-nini.html
Nini ufanye ili kuondokana na Tatizo la mvurugiko wa hedhi.
Kwa kiwago kikubwa matatizo ya kubadilika kwa mzunguko wa hedhi husababishwa na wanawake wenyewe.Kujua Tatizo ni mwanzo wa kujua namna ya kutatua Tatizo.Kwahiyo kabla hujaamua kwenda hospitali kutibiwa ni vema ukaamua jitathimini mweyewe kadiri unavyo endesha maisha yakoya kila siku.Ukisha Fanya tathimini juu ya maisha yako yakilasiku naukagundua mwenyewe siyo chanzo cha Tatizo basi nenda hospitali ukachunguzwe.Fanya yafuatayo kabla hujaenda hospitali.
.Kupunguza mawazo,kama nilivyo eleza mawazo husababisha matumizi makubwa ya nishati,matokeo yake mzunguko wa hedhi utavurugika.Unaweza punguza mawazo kwa kujiingika katika shughuli ndogo ndogo ,kukaa katika makundi ambako kutakufanya uwe bize mda wote,Kwahiyo kupunguza athari za uzalishwaji wa kichocheo cha cortisol ambacho huzuia uzalishwaji wa vichocheo vya uzazi.
.Kula mlo kamili, mlo kamili hujumuisha vyakula ambacho vinavirutubisho vyote kama mafuta na vitamini.Mafuta ni moja ya vyakula ambavyo huunda vichocheo vya mwili,ivyo hulaji wa vyakula vya vitamini na mafuta husababisha kiwango cha vichocheo vya uzazi vitengenezwe kwa wingi.Vyakula ivyo ni pamoja na maparachichi ,nazi ,mapapai nakadhalika.
.Ufanyaji mazoezi kiasi, mazoezi hufanya mtu aonekane imara,pia mazoezi hupunguza mawazo.Kwahiyo ufanyaji mazoezi kupitiliza lazma uepukwe kwasababu huchochea kwa kiwango kikubwa mvurugiko wa mzunguko wa hedhi.
.Kuhakikisha uzito wako unakuwa wa kawaida,uzito mdogo hupelekea mabadiliko ya mzunguko wa hedhi.Lakini kuna baadhi ya wanawake kwa matakwa yao wenyewe hujikuta wanajiingiza kwenye Tatizo hili wenyewe kwakuto kujua hususani kwa wale ambao hukaa muda mrefu bila kula wakihofia kubadilisha maumbile yao na matokeo take wanakonda.Tumeona kiwango cha mafuta mwilini ni muhimu kwa kuchochea uzalishwaji wa vichocheo vya uzazi.Hivyo wenye tabia hii nivema wakaacha kwasababu wanajitengenezea matatizo wenyewe.
.Kuepuka matumizi ya madawa ya urembo na mazingira hatarishi kama ya viwanda ambayo hutoa chemikali ambazo zinaweza. sababisha mabadiliko ya mzunguko wa hedhi.
.Mwisho endapo umefanya njia zote hapo juu na bado Tatizo lipo ni vema ukaenda hospitality ili ufanyiwe vipimo ili kugundua Tatizo lako linatokana na mini kisha upewe dawa ambazo zinaweza tatua Tatizo lako kama laweza tatuliwa kwa dawa,.Pia kama Tatizo lako litaitaji upasuaji basi ufanyiwe na hatimaye Tatizo lako liishe.
Mawasiliano whatsap: 0712106789
No comments:
Post a Comment