Home »
» Ujue ugonjwa wa kiharusi
Ujue ugonjwa wa kiharusi
Kiharusi(stroke).
Ni hali ambayo hutokea kutokana na kutokana na kuathirika kwa mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo,jambo ambalo hupelekea kupungua kwa kiwango cha damu yenye kubeba hewa safi na kupeleka kwenye ubongo,hivyo kupelekea utendaji kazi wa ubongo kuathirika.
Pia ugonjwa wa kiharusi kwa jina lingine hujulikana kama Ajali ya ubongo na mishipa ya damu au shambulio la ubongo.
Aina za kiharusi(stroke).
Kiharusi au ajali ya ubongo na mishipa imegawanyika katika aina kuu mbili Nazi ni.
.Kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa safi(ischaemic stroke).
Ni aina ya kiharusi ambacho hutokea endapo kuna upungufu wa usambazaji wa damu yenye kubebe hewa safi kwenye ubongo jambo ambalo hupelekea seli za sehemu iliyo athirika kushindwa kufanya kazi vizuri.
.Aina hii ya kiharusi husababishwa na damu iliyo ganda kuziba mishipa midogo midogo inayopeleka damu kwenye ubongo jambo ambalo hupelekea kupungua kwa usafirishaji wa damu yenye oxygeni kwenye ubongo na kusababisha seli za ubongo kufa kutokana na ukosekanaji wa oxygen.
.Pia inaweza sababishwa na kumeguka kwa kipande cha damu na kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo.
.Vile vile aina hii ya kiharusi inaweza sababishwa na kusinyaa au kupungua kwa nafasi ndani ya mishipa ya damu(blood vessel lumen) jambo ambalo hupelekea kupungua kwa usafirishaji wa damu safi kwenye ubongo.
.Pia hali hii inaweza sababishwa na kuwepo kwa matatizo ya moyo(atrial fibrillation) jambo ambalo husababisha kuganda kwa damu.
.Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu (Hemorrhagic stroke).
Ni aina ya kiharusi ambacho hutokana kupasuka kwa mishipa midogo midogo ya damu ndani ya ubongo jambo ambalo hupelekea damu kusambaa ndani ya ubongo, seli za ubongo kukosa damu yenye oxygen ya kutosha na matokeo yake seli hizo zinakufa.
.Aina hii ya kiharusi inaweza sababishwa na kuwepo kwa shinikizo kubwa la damu lisilo zuiliwa kwa muda mrefu.Shinikizo kubwa la damu husababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu ndani ya mishipa jambo ambalo linaweza sababisha mishipa kupasuka na damu kuvuja badala ya kwenda kwenye ubongo.
.Pia aina hii ya kharusi inaweza sababishwa na mtu kupata ajali hususani ya kichwa,ajali inapotokea husababisha mishipa ya damu kupasuka,yaweza kupasuka kutokana na kipande cha mifupa kuichoma mishipa iyo jambo ambalo linaweza sababisha damu ikavuja ndani kwa ndani na hatimae damu hupungua kwenye ubongo na kusababisha seli za ubongo kufa.Pia mishipa ya damu inaweza ikawa imepasuka hata kama mtu hajapata majeraha makubwa jambo ambalo husababisha damu kuvuja ndani kwa ndani.
Vitu ambavyo humfanya mtu awe katika hatari ya kushambuliwa na kiharusi .
.Shinikizo la damu la muda mrefu bila kupata matibabu.
.Matatizo ya moyo mfano(atrial fibrillation) ambayo husababisha damu kuganda ndani ya chemba za moyo na damu hiyo husafirishwa sehemu zamwili inaposafirishwa inaweza ikaziba sehemu yoyote na kusababisha upungufu wa damu yenye oxygen kwenye ubongo.
.Ugonjwa wa kisukari.
.Kutokufanya mazoezi ya viungo.
.Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe kupitiliza,chemikali iliyopo kwenye madawa husababisha kuathirika kwa kuta za mishipa ya damu jambo ambalo linaweza sababisha mishipa iyo kupasuka kwa urahisi zaidi.
.Kuwa na uzito mkubwa, uzito mkubwa hutokana na kuhifadhiwa kwa wingi kwa nishati mwilini kuliko uhitaji wa mwili,mafuta mengi husababisha kukandamizwa kwa mishipa ya damu na kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu jambo ambalo husababisha kupungua kwa damu safi kwenye ubongo,pia uzito mkubwa humweka katika hatari ya kupata kisukari na magonjwa ya moyo ambayo ni chanzo kikubwa cha kiharusi.
.Kupata kiharusi cha muda mfupi(transient ischaemic attack) ambacho hupotea ndani ya masaa 24 na MTU kurudi katika hali ya kawaida,kwaiyo mtu aliyewahi pata kiharusi hiki yupo hatarini kupata kiharusi cha muda mrefu.
.Umri,hatari ya kushambuliwa na kiharusi huongezeka kadiri unavyokuwa na umri mkubwa.
.Jinsia.wanawake wapo katika hatari ndogo ya kushambuliwa na kiharusi kuliko wanaume katika umri mdogo,wanawake hupata kiharusi katika umri mkubwa jambo ambalo hupelekea wasipone na wafariki.
Dalili za kiharusi.
.Kupoteza ufahamu wa upande mmoja wa mwili,kulegea misuli ya uso,kuhisi ganzi,na kupungua kwa ufahamu wa hisia na kuhisi mitetemo.
.Kupungua kwa uwezo wa kuona,kitu kimoja kinaweza onekana viwili,kupotea kwa uwezo wa kuona inaweza tokea kwenye jicho moja au macho yote.
.Ugumu wa kufahamu kuzungumza pia kuelewa lugha.
.Maumivu makali ya kichwa ambayo huanza ghafla.
.Kupoteza kumbukumbu.
.Kuchanganyikiwa.
.Kutapika.
Vipimo vya ugonjwa wa kiharusi.
.Computer temograph (ct scan.
.Magnetic resonance(MRI).
.Mionzi.
Matibabu ya kiharusi.
Matibabu ya kiharusi hutegemeana na aina ya kiharusi ambacho kimemshambulia mgonjwa.
.Kiharusi ambacho husababishwa na kuganda kwa damu kuna dawa ambazo mgonjwa anapewa ili kuvunja vunja mgando wa damu na kuzifanya seli sahani zisiendelee kukusanyika na kusababisha mgando,dawa hizo ni kama asprin,clopidogrel,na dipryildamole.
Pia upasuaji wa kutoa damu iliyo ganda unaweza ukafanyika endapo dawa zitashindwa kufanya kazi.
.Kiharusi ambacho kimetokana na kuvuja kwa damu kinahitaji upasuaji ili kuangalia nini hasa chanzo cha kuvuja kwa damu na hatimaye waweze kukidhibiti.
Madhara yanayoweza sababishwa na kiharusi.
.Kupooza
Kupungua kwa damu safi kwenye ubongo,kunaweza pelekea mtu akapooza upande mmoja wa mwili na inategemeana na tatizo limetokea katika upande gani wa ubongo,pia anaweza shindwa control nyama za baadhi ya sehemu kama vile usoni na mikononi.
.Kushindwa kuzungumza au kumeza.
Mgonjwa atashindwa kuhimili jinsi nyama za kohoni na mdomoni zinavyo fanya kazi,jambo ambalo litasababisha ashindwe kumeza na kuzungumza.
.Kupoteza kumbukumbu.
Watu wengi walio ugua ugonjwa was kiharusi hupoteza kumbukumbu,kupatashida katika kufikiri,kushindwa kufanya maamuzi,kushindwa kuelewa mambo,na kushindwa kuchanganua mambo.
.Matatizo ya mihemko.
Watu wengi walio ugua kiharusi hushindwa kudhibiti mihemko yao na mwtokeo yake hujikuta wanakumbwa na msongo mawazo.
.Mabadiliko ya tabia.
Watu ambao wameugua ugonjwa wa kiharusi pia wanakuwa na tabia ya kujitenga katika jamii au kutopenda kujihusisha na kazi za kijamii,pia wakati mwingine wanajikuta wakipogeza uwezo wao wa kujitegemea hadi kuwa tegemezi kabisa katika huduma zao wenyewe,mfano kuogeshwa nazinginezo.
Ufanye nini ili kuepuka usishambuliwe na kiharusi.
.Fanya mazoezi ya viungo ili kuhakikisha unakuwa na afya iliyo bora.
.Epuka unywaji wa pombe,uvutaji sigara na dawa za kulevya kwasababu dawa izo huathiri kuta za mishipa ya damu na kukufanya uwe hatarini kushambuliwa.
.Hakikisha kama unashinikizo la damu unakuwa na mazoea ya kupima Mara kwa Mara.
.Punguza msongo wa mawazo hususani kwa wenye kisukari na msukumo mkubwa wa damu,kwasababu mawazo huvuruga mfumo wa vchocheo vya mwili na kusababisha kichocheo cha kuongeza Msukumo damu kizalishwe kwa wingi na kusababisha nishati iliyo hifadhiwa itolewe mwilini kwa wingi jambo linalo sababisha sukari kuongezeka kwenye damu.
.Hakikisha unakula vyakula vyenye mafuta kidogo.
.Kula vyakula vyenye chunvi kidogo,kwasababu katika maji maji yaliyo mwilini nje ya chembe hai(extracellular fluid) kuna kiwango kinachohitajika na mwili cha kemikali ya sodiam,na kwenye chunvi kuna sodiam pia kwaiyo ukila chunvi kwa wingi kiwango hicho cha sodiam mwilini hupanda jambo linalo sababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu.
.Kuwa na mazoea ya kupima kiwango cha mafuta mwilini.
Mawasiliano:whatsap
07121067 89
No comments:
Post a Comment