Mzio/Aleji
Ni matokeo ya mapambano kati ya kinga ya mwili dhidi ya vitu ambavyo havina madhara pindi vitu ivyo vinapo ingia ndani ya mwili au kugusa sehemu moja wapo ya mwili.Mapambano hayo husababisha mtu aone dalili za mzio au aleji.
Nini husababisha aleji/mzio?
Vitu ambavyo husababisha mzio(allergens) Mara nyingi huwa havina madhara katika mwili wa binadamu ,lakini husababisha kinga ya mwili kupambana dhidi ya vitu ivyo kwasababu mwili unahisi kama umevamiwa au kushambuliwa na vitu ambavyo siyo rafiki.
Mzio au alegi hutokea mtu akivuta,shika,meza ,jichoma au akagusa vitu vinavyo sababisha mzio na inaweza ikawa ya kawaida kali,au muda mwingine kuhatarisha maisha kutegemeana na kisababishi.
Kwa kawaida kinga ya mwili huukinga mwili dhidi ya uvamizi wa vimelea ambao husababisha magonjwa kama vile bacteria, fangasi na virusi,vile vile hupambana na vitu visivyo na madhara pindi vinapoingia mwilini.
Kwaiyo pindi mwili unapo pambana dhidi ya visababishi vya mzio histamine na chemikali zingine huzalishwa ili kupambana na aleji.Histamine hufanya kazi nyingi katika mwili , mfano kusafirisha taarifa kati ya seli za mwili.Mfano kwa mwenye mzio wa aina Fulani ya chakula histamine husababisha tumbo kutengeneza kiwango kikubwa cha acidi ili kukiyeyusha chakula icho kwa haraka.
Pia katika mapambano hayo immunoglobulin nayo huzalishwa ili kupambana na allergens na mishipa ya damu hutanuka ili kurahisisha chembe chembe nyeupe kuelekea sehemu ambayo uvamizi umetokea.
Kwaiyo kuna sababu mbali mbali ambazo zinaweza zikapelekea mtu akapata mzio,sababu za kimazingira na sababu za kibailojia mfano jinsi mtu alivyo umbwa au kuzaliwa katika familia ambayo wazazi wana tatizo la mzio huchukua nafasi kubwa ya mtu kupata aleji.Kuna baadhi ya watu hupatwa na aleji wanapo kuwa katika mazingira ya baridi na wengine hupatwa wakiwa katika mazingira ya joto.Pia kuna baadhi ya watu hupatwa na mzio wanapo kuwa wamevaa aina Fulani ya mavazi au mapambo mfano saa,chain,bangili,heleni n.k
Kwaiyo vitu vinavyo sababisha ni pamoja na kukaa au kupita katika mazingira ambayo yana mavumbi, moshi unaotokana na viwanda au uchomaji wa taka au mapori,pia matumizi ya baadhi ya dawa hususani zenye salfa ,matumizi ya baadhi ya vyakula,vile vile kuna ambao hupata mzio kutokana na kung'atwa na wadudu kama vile nyuki ,nyigu na wadudu wengineo, wengine hupata kutokana na kuvuta unga wa maua(pollen) na baadhi ya watu hupata kwa kugusa au kushika majani ya baadhi ya mimea.
Pia kuna baadhi ya watoto hupatwa na aleji Mara tu baada ya kuanza kunyonyeshwa maziwa ya ng'ombe na hii ni kutokana na kuwepo kwa aina Fulani ya protini kwenye maziwa ayo ya ng'ombe.
Dalili za aleji au mzio.
Dalili za mzio au aleji hutofautiana kulingana na sehemu ambayo shambulizi limetokea..
.Kama ni machoni dalili zitakazo jitokeza ni pamoja na macho kuvimba,kuwasha ,kutokwa na machozi na pengine kuwepo kwa uwekundu katika ngozi inayo lizunguka jicho.
.Vile vile kama ni mzio unaotlkana na aina fulani ya chakula dalili zitakazo onekana ni pamoja na kuharisha ,kutapika ,kichefuchefu, Pamoja na maumivu ya tumbo.
.Kama mzio katika ngozi dalili zitakazo onekana ni pamoja na kuwashwa,kuvimba,uwekundu,
mabaka pamoja na kubabuka kwa ngozi.
.Pia kama itatokea katika njia ya hewa dalili zitakazo onekana ni pamoja na kamasi,kukohoa,shida katika upumuaji .
Soma:maandalizi-muhimu-wakati-wa-kujifungua.html
Vipimo
.Kipimo cha kwanza kwa mwenye tatizo la aleji ni kuchukua historia yake ili kujua ni lini tatizo lilianza na kujua vitu gani vimesababisha aleji dalili ambazo zinajitokeza ili kuweza kutofautisha dalili hizo na matatizo mengine kwasababu anaweza akasema ana alegi kumbe siyo aleji bali ni tatizo lingne ambalo dalili zake hufanana na za aleji mfano anaweza akawa ana harisha au kutapika ukazani ni mzio lakini kumbe kumetokana na maambukizi ya wadudu kama bacteria.
.Kipimo cha kuangalia damu kwa ujumla wake(full blood picture) kuonesha kuongezeka kwa seli nyeupe za damu kama eosinophil na imunoglobulini huashiria kuwepo kwa mashambulizi dhidi ya visababishi vya mzio.
.Kipimo ambacho vitu ambavyo huisiwa kusababisha mzio katika ngozi hubandikwa katika ngozi au sindano yenye visababishi vya mzio huchomwa katika sehemu ya juu ya ngozi na daktari akiangalia kama mabadiliko yoyote yanatokea,kama yatatokea basi mtu uyo atakuwa na mzio dhidi ya visababishi vilivyotumika,aina hii ya kipimo hujulikana kama patch testing.
.Kipimo ambacho vitu vinavyo hisiwa kusababisha mzio huwekwa kwenye ngozi ya mgonjwa au huchomwa sindano na kuviruhusu vitu ivyo viingie huku daktari akiangalia kama kuna mabadiliko yoyote katika eneo I'll kama vile uvimbe au uwekundu,kipimo hiki hujulikana kama skin testing.
Madhara ya aleji
.Kushindwa kupumua vizuri (asma)
.Kushuka kwa shinikizo la damu.
.Matatizo ya mapafu.
.Kifo endapo mgonjwa atachelewa pata matibabu.
Ufanye nini kujikinga na mzio au aleji?
Njia bora na sahii ya kujikinga na mzio ni kutambua vitu gani ambavyo hukusababishia mzio,ukisha vitambua vitu ivyo basi kinacho takiwa na kuvikwepa ili ucje ukakumbana navyo na vikakuathiri,mfano kama aleji yako husababishwa na kula aina Fulani ya chakula kinachotakiwa ni kuacha kula chakula hicho,pia kama aleji yako inatokana na mavumbi basi unatakiwa kuepuka mazingira ambayo yana mavumbi. Aidha kuna baadhi ya tafiti ambazo zimefanywa huonesha Watoto ambao huzaliwa katika mazjngira yenye mavumbi wanauwezekano mdogo sana wa kupatwa na mzio unao tokana na mavumbi kama baadae wakiwa wakubwa wakiishi kwennye mazingira kama ayo,pia wale ambao wamezaliwa katika mazingira yasiyo na mavumbi kuna uwezekano mkubwa wa kupatwa na mzio endapo wataishi mazingira yenye mavumbi.
Vile vile kama mzio wako unatokana na kukaa katika mazingira yenye baridi au joto basi kinacho takiwa ni kuyaepuka mazingira yenye baridi ambayo yatakuletea shida,kwa wale ambao hupata shida katika mazingira ya joto basi wanashauriwa kuyaepuka mazingira hayo.
Kwa wale ambao mavazi au mapambo ndio chanzo cha mzio basi inabidi waepuke aina ya mavazi au mapambo ambayo huwa yanawaletea shida.Pia kwa wale ambao wana aleji ya aina fulani ya dawa basi pindi anapo kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu anashauriwa kumweleza daktar wake dawa ambazo zinamzuru ili asipewe pia ni vema akamwambia muuguzi kabla hajapewa dawa izo.
Pia aleji inayotokana na kuwapa watoto maziwa ya ng'ombe mapema ili kuiepuka wakina mama wanashauriwa kuwa nyonyesha watoto wao maziwa kuanzia miezi sita kisha kuanzia hapo wanaweza kuwapa maziwa ayo.
Kwa wale ambao chanzo cha aleji yao ni unga unga wa maua ni vema wakaepuka mazingira ayo.
Kuna dawa aina mbali mbali ambazo hutumika kuzuia au kutibu tatizo la aleji,dawa hizo zaweza tolewa kama sindano,kupuliza,kunusa ,vidonge matone au kwa kupaka inategemeana na mtaalamu wako ana pendelea ipi pamoja na ukubwa wa tatizo
uli lokuwa nalo, wapi aleji imetokea dawa hizo ni pamoja na steroids na ant histamine .
Dawa hizi hutumika kwa uangalifu mkubwa kwasababu zinaweza zikaleta athari kwenye moyo kama hazitotumika kwa uangalifu.
No comments:
Post a Comment