Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Ugonjwa wa zinaa wa kisonono



Kisonono.

Ugonjwa huu kitaalamu hujulikana kama gonorrhoea,ni moja kati ya magonjwa ya ngono ambao huambukizwa baada ya kufanya ngono isiyo salama kati ya mtu mwenye vimelea vya ugonjwa huu na asiye na vimelea.Vimelea vinavyo sababisha ugonjwa huu ni bacteria wajulikanao kwa jina la Neisseria gonorrhoae,katika mazingira ya joto na unyevu unyevu bacteria hawa hukua na kuzaliana kwa haraka zaidi,mazingira ayo ni pamoja na shingo ya kizazi kwa wanawake ,njia ya kupitisha mkojo kwa wanaume,njia ya haja kubwa.

Pia waanga wakubwa was ugonjwa huu ni jinsia zote mbili,wanaume pamoja na wanawake,na huwa kumba zaidi kuanzia miaka 15 wanapo balee hadi miaka 29 kwasababu wanakuwa na hamasa kubwa ya kingono.





Vihatarishi vya ugonjwa wa kisonono.

Ugonjwa wa kisonono husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya ya kujamiiana,kujamiiana kinyume na maumbile  mfano mdomoni,njia ya haja kubwa n.k. Vihatarishi ivyo ambavyo huongeza nafasi ya mtu kushambuliwa na ugonjwa huu ni pamoja na:

.Kuwa na wapenzi wengi huongeza nafasi ya kupata maambukizi.

.Unywaji wa pombe kupitiliza na utumiaji wa madawa ya kulevya pia huongeza nafasi ya kupata maambukizi.

.Kuugua ugonjwa wa kisonono kabla.

.Kushuka kwa kinga za mwili huongeza nafasi ya vimelea vya ugonjwa kufanya mashambulizi.

.Kuwa na magonjwa mengine ya zinaa .

.Kufanya ngono kinyume na maumbile.

.Kufanya ngono na mtu mwenye mpenzi mwingine.

.Kuwa na mpenzi mpya.

.Umri (ujana).




Soma: lijue-tatizo-la-aleji-au-mzio.html



Dalili za ugonjwa wa kisonono.

Mara baada ya kupata vimelea vya ugonjwa wa kisonono dalili huanza kuone kana kuanzia siku ya pili hadi ya saba ,pia kutokana na sababu za kimaumbile dalili kwa wanawake zinaweza zisionekane mapema.

Kwa wanaume.

.Kuwa na homa.

.Kuvimba kwa korodani wakati mwingine.

.Kuchoma choma wakati wa kukojoa,pia kukojoa mara kwa mara kwakuwa mkojo hauishi.

.Maumivu makali wakati wa kujisaidia endapo maambukizi yametokea kwenye njia ya haja kubwa.

.Maumivu makali yanayo ambatana na kutokwa na uchafu wa njano au mweupe kwenye njia ya mkojo .



Kwa wanawake.

.Maumivu wakati wa kukojoa.

.Kuwashwa sehemu za haja kubwa.

.Maumivu ya tumbo chini ya kitofu.

.Homa ya mara kwa mara.

.Kutapika.

.Kutokwa na maji maji mengi yenye rangi ya njano au yenye ku changanyika na damu kwenye uke.

.Mabadiliko au mvurugiko wa mzunguko wa hedhi.



Madhara ya ugonjwa wa kisonono

.Kwa wanawake endapo ugonjwa hautatibiwa basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa pelvic inflammatory disease (pid) ambao ni chazo kikubwa cha utasa.

 .Pia kwa mama mjamzito kama hato pata matibabu itasababisha mimba kuharibika au kuzaa kabla ya wakati.

.Maambukizi katika kipindi cha mwisho cha ujauzito bila matibabu huweza msababishia mtoto upofu au kichomi au ugonjwa wowote.

 .Madhara kwenye viungo vya mwili kwasababu wadudu husafiri kwenye mishipa ya damu kwaiyo athari inaweza tokea.

 .Huongeza athari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

.Utasa kwa mwanamke na kushindwa tungisha mimba kwa mwanaume.



Ufanye nini kujikinga na ugonjwa wa kisonono.?

.Epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

.Epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

.Tumia kondom kwa uhakika na usahihi katika kila kitendo.

.Kwa wakina mama wajawazito nivema kuwahi kuhudhuria kliniki mapema ili ufanyiwe uchunguzi na endapo utagundulika upate matibabu.

.Pia ili kupunguza athari ya ulemavu au upofu kwa mtoto mama unashauriwa kupata matibabu mapema na kujifungulia hospitality ili mtoto apewe matibabu baada ya kuzaliwa.

.Hakikisha mpenzi wako mpya anafanyiwa vipimo kabla ya kushirikiana nae ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa.

.Kuwa na kawaida ya kupima maambukizi mara kwa mara angalau mara moja kwa mwaka.

.Epuka kufanya ngono isiyo salama na mpenzi wako endapo anaonesha dalili ya maambukizi.




Mwisho,Ugonjwa wa kisonono unatibika kwaiyo mara uonapo dalili ambazo siyo rafiki katika maumbile yako ni vema ukaenda hospitali ili ufanyiwe vipimo na kisha upewe matibabu sahihi,pia epuka matumizi ya dawa bila kupata vipimo kwasababu unaweza ukadhani una aina Fulani ya ugonjwa kumbe siyo,kwa taarifa tu dalili za magonjwa huwa zina fanana.


Pia kumbuka kama huwezi Fanya ngono salama ni vyema ukaacha kabisa kujihusisha na vitendo vya ngono kwasababu maradhi ni mengi siku izi.




Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts