Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Mambo muhimu ya kuzingatiwa kwa mama mjamzito kwa uzazi salama na Afya bora ya mama na mtoto.

.MIKA.jpg
Habari gani ndugu msomaji na mfatiliaji wa mikathommedia ni matumaini yangu ni wazima wa afya.Leo tutajifunza "mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama mjamzito kwa uzazi salama na afya bora ya mtoto"

Kipindi cha ujauzito kuna mabadiliko mengi ambayo hutokea katika mifumo mbalimbali ya mama,hivyo basi kujiona yupo tofauti na alivyokuwa awali kabla hajapata mimba.Mabadiliko ayo ni pamoja na kukojoa mara kwa mara,kutapika ,kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo,matiti kujaa,kuvimba miguu,na mengineyo mengi,hivyo basi kutakiwa kuzingatia mambo kadhaa ili ajifungue salama,nayo ni kama yafuatayo;

Mahudhurio ya kliniki mara baada ya kupata ujauzito:

Mama mjamzito anapaswa kuhudhuria kliniki mara tu atambuapo ni mjamzito kwasababu atajifunza mambo mbalimbali,mfano namna ya kulea mimba pamoja na  mtoto,mambo ambayo yanaweza yakamkabili katika kipindi cha ujauzito na namna ya kuzigundua dalili izo za hatari kwake yeye na mtoto baada ya kujifungua,namna ya kujikinga na magonjwa kwake yeye pamoja na mtoto,namna ya kupanga uzazi ili kuinua kipato cha familia na malezi bora ya mtoto atakae zaliwa,pia atajifunzavitugani aandae ili aweze kujifungua salama.

Chakula Na Virutubisho:

Lishe bora katika kipindi cha ujauzito ni muhimu kwasababu hutumika kwa mama na mtoto anaendelea kukua vizuri tumboni,katika hali ya kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka katika kipindi cha ujauzito na namna ujauzito unavyoendelea kukua,kazi ya virutubisho ivyo ni kujenga mwili wa mama na mtoto hivyo lishe apatayo mama huathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto.Mama anashauriwa ale mlokamili kwa ajili ya maendeleo ya mjamzito na mtoto tumboni.Mlokamili hujumuisha vyakula vya wanga(nafaka kama ulezi ,mahindi,mtama,pia ndizi,mihogo,magimbi n.k,aina hii ya vyakula humpa mama nguvu).Protini(nyama,samaki,maharagwe,mayai ,karanga n.k ,vyakula hivi husaidia kujenga mwili hususani miezi minne had tisa mama anashauriwa atumie vyakula ivi),mafuta(karanga ,ufuta, nyama,alizeti,pamoja na matunda yenye asili ya mafuta kama parachichi vyakula hivi hujenga seli za mwili na kuupa nguvu mwili),vitamini(matunda na mboga za majani huimarisha kinga za mwili),madini na maji(husaidia kumengenya chakula,kutoa sumu mwilini na kumkinga mama na maambukizi ya njia ya mkojo kama uti).Pamoja na mlokamili mjamzito hupewa virutubisho vya ziada kwa ajili ya kuongeza madini kama foliki na chuma kwasababu huondoa athari ya mtoto kuzaliwa na mgongo wazi,kichwakikubwa n.k



Usafi na mavazi:

Mama mjaimzito anatakiwa kuzingatia  usafi wa mwili na mavazi pamoja na mazingira yanayom zunguka ili kuondokana na athari ya kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara katika kipindi cha ujauzito,pia mama mjamzito inabidi avae mavazi safi na yanayo sitiri mwili wake vizuri na aepuke mavazi ya kubana ambayo yanaonyesha maumbile yake.Mavazi ni pamoja na viatu kwa kawaida kina mama hupenda kuvaa viatu vyenye visigino virefu pindi wakiwa siyo wajawazito.Katika kipindi cha ujauzito mnashauriwa epukeni kuvaa aina hii ya viatu kwasababu kinaweza kikakusababishia ajali ya kuanguka ivyo kuhatarisha afya yako na ya mtoto.


Kufanya mazoezi na kupumzika:

Mama mjamzito anashauriwa afanye mazoezi mepesi ambayo hayato athiri afya yake pamoja na ya mtoto,mazoezi ayo ni kama kunyoosha mwili,kutembea ,na kufanya kazi nyepesi kwasababu husaidia mama aonekane ni imara asiye rahisi kushambuliwa na magonjwa,pia hufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri,pia husaidia katika shughuli nzima ya utoaji taka mwilini hususani kwa njia ya jasho,mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili,pia husaidia mama kujifungua kwa urahisi wakati wa kujifungua ukifika,pia anatakiwa apate muda wa kutosha wa kupumzika kwa afya yake na mtoto.


Kupima uzito:

Mama mjamzito anatakiwa apime uzito katika kila hudhurio kwasababu uzito mkubwa ni hatari kwa mtoto.Hapo juu tumeona chakula ni mojawapo ya mahitaji muhimu sana kwa mama mjamzito,kuna baadhi ya vyakula(ulaji mayai kupitiliza) vina asili ya kuongeza uzito endapo vitatumika mara kwa mara na kwa kiwango kikubwa,vyakula hivyo huifadhiwa sehemu mbalimbali za mwili na matokeo yake uzito wa mama huyu utaongezeka siku hadi siku kama hatozingatia ufanyaji wa mazoezi mepesi.Pia vyakula hivi vikitumika kwa kiwango kikubwa huweza sababisha mtoto kuwa mkubwa na mwenye uzito mkubwa hivyo huenda ikapelekea mama kushindwa kujifungua kawaida kwaiyo vyakula kama mayai inatakiwa vitumike kwa kiasi.


Matumizi ya dawa na chanjo:

Matumizi ya dawa kwa mama mjamzito inatakiwa yazingatiwe hususani katika miezi mitatu ya mwanzo kwasababu kuna baadhi ya dawa endapo zitatumika katika miezi mitatu ya mwanzo zinapelekea mimba kuharibika.Mama mjamzito anashauriwa aonapo dalili za homa epuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri au mwone daktari akuandikie dawa ambayo itakufaa kulingana na ukubwa wa mimba yako.Pia mama mjamzito unashauriwa pindi uendapo hospitali ni vema ueleze kuwa ni mjamzito ili kuepuka kuandikiwa dawa ambazo zitamdhuru mtoto aliye tumboni hususani katika kipindi ambacho mimba haionekani kwa macho .Pia mjamzito lazima uhakikishe unapata chanjo ya tetenus kabla na baada ya kujifungua,pia baada ya kujifungua hakikisha mwanao anapata chanjo ili kumkinga na magonjwa.



Soma /mabadiliko-ya-mzunguko-wa-hedhi.html


Matumizi ya pombe na dawa za kulevya:

Matumizi ya dawa za kulevya wakati wa ujauzito huathiri afya yako na ya mtoto,ivyo basi hushauriwi kutumia pombe ,sigara,dawa za kulevya, kwasababu endapo zitatumika katika kipindi cha ujauzito zinaweza sababisha kifo kwa mtoto,mimba kuharibika,afya dhoofu kwa mtoto,ulemavu na kujifungua kabla ya siku hazijatimia.



Unyonyeshaji:

Mara baada ya kujifungua mama anashauriwa anyonyeshe mtoto kwa muda wa miezi sita bila kumpa chakula kingine.Maziwa ya mama yana virutubisho vyote ambavyo humkinga mtoto dhidi ya magonjwa.Maziwa ya mama ni muhimu sana kwasababu yanapatikana bila gharama yoyote,pia yana jenga uhusiano mzuri kati ya mama na mtoto,pia ni mojawapo ya njia ya uzazi wa mpango ivyo basi mama akimnyonyesha mtoto mara kwa mara ndani ya miezi sita inamsaidia asipate mimba kwa haraka.Pia katika unyonyeshaji mama anashauriwa amnyonyeshe mtoto ziwa moja hadi liishe kisha amnyonyeshe ziwa lingine ili mtoto aweze pata virutubisho vyote muhimu.



Uzazi wa mpango:


Ni makubaliano kati ya mume na mke wazae watoto wangapi na wapishane kwa muda wa miaka mingapi ili waweze lea mtoto mmoja kabla ya kupata mtoto mwingine.Kwa kawaida watoto inabidi wapishane japo kwa miaka mitatu hadi mitano kabla hawajaamua kupata mwingine.Wiki sita baada ya kujifungua mama anashauriwa arudi kliniki na mwenza wake ili washauriwe juu ya uzazi wa mpango.Uzazi wa mpango husaidia mpate muda mwingi wa kumlea mtoto,husaidia kukuza kipato cha familia,pia inasaidia mama aweze kurudi katika hali yake ya kawaida kabla hajapata mimba nyingine,pia husaidia kupunguza matatizo na vifo visivyotarajiwa vitokanavyo na uzazi.Hivyo basi uzazi wa mpango ni muhimu kwa afya bora ya mama na mtoto ivyo basi ni vema ukapata huduma hii baada ya kujifungua.

 

Mawasiliano whatsap:0712106789
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts