Kaswende (syphilis).
Ni moja kati ya magonjwa wa zinaa ambao husababishwa na vimelea au bacteria aiza kwa kujamiana na mwenye vimelea vya ugonjwa au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika kipindi cha ujauzito, bacteria hao hujulikana kama Treponema pallidum.Ugonjwa huu huleta madhara makubwa endapo hauto gundulika na kupata matibabu mapema.
Pia endapo mwanamke mjamzito akapatwa na ugonjwa huu kuna uwezekano mkubwa wa kumwambukiza mwanae kupitia mfuko wa uzazi au aka mwambukiza wakati wa kuzaliwa, pia unaweza sababisha mtoto kufariki muda mfupi kabla ya kujifungua au muda mfupi baada ya kujifungua,watoto wanao zaliwa kwa mama mwenye maambukizi endapo wata zaliwa salama wanakuwa hawaoneshi dalili ya ugonjwa lakini baadae hupatwa na matatizo ya meno,vipele ,kubonyea kwa mfupa wa pua n.k
Vile vile ugonjwa wa ukimwi huenda sambamba kabisa na ugonjwa wa kaswende kwaiyo kuna uwezekano mkubwa sana wa mtu mwenye ugonjwa wa kaswende kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Vihatarishi vya ugonjwa wa kaswende.
Ugonjwa wa kaswende husababishwa na bacteria aitwae treponema pallidum kama nilivyo sema mwanzo ,na njia kubwa ya maambukizi ni kupitia kujamiana, vitu ambavyo humweka mtu katika hatari ya kupata vimelea by a ugonjwa huu ni pamoja na:
.Kutokuwa mwaminifu kwa mwenza au mpenzi wako au kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
.Kufanya mapenzi kinyume na maumbile mfano ,mapenzi ya mdomo(oral sex), mapenzi katika njia ya haja kubwa(anal sex).
.Kushuka kwa kinga ya mwili pia humfanya mtu awe katika hatari ya kupata ugonjwa huu.
.Pia mtoto anaweza akapata kutoka kwa mama mjamzito mwenye maambukizi wakati wa kuzaliwa.
.Kuugua ugonjwa wa kaswende awali.
.Utumiaji wa pombe pamoja na madawa ya kulevya.
Dalili za ugonjwa wa kaswende.
Ugonjwa wa kaswende hugawanyika katika hatua tofauti tofauti na kila hatua ikiwa na dalili tofauti tofauti,lakini wakati mwingine hakuna dalili ambazo hujitokeza kwa muda mrefu.Hatua za ugonjwa huu ni kama zilivyo ainishwa hapa:
.Hatua ya kwanza(primary syphilis).
Ishara ya kwanza ya ugonjwa wa kaswende ni uwepo wa kidonda,kidonda hiki hujulikana kwa jina la chancre,kidonda hiki hujitokeza sehemu ambayo bacteria wa ugonjwa huu wameingia,Mara nyingi watu walio wengi hupatwa na kidonda kimoja japo kuna wengine hupatwa na kidonda zaidi ya kimoja,kidonda hiki huweza jitokeza kuanzia siku ya kumi hadi miezi mitatu Mara baada ya kupata maambukizi.
Katika hatua hii watu wefngi huwa hawakioni kidonda hicho kwasababu kidonda hiki huwa hakina maumivu na huweza jitokeza katika shingo ya kizazi,ulimi,mdomoni ,kwenye uume au katika njia ya haja kubwa, pia kwa wale ambao hawapati matibabu basi huamia katika hatua ya pili.
Hatua ya pili (secondary syphilis).
Hatua hii hujitokeza wiki nne hadi kumi baada ya hatua ya kwanza. Katika hatua hii vipele visivyo na mwasho vyaweza jitokeza mikononi hususani kwenye viganja, vyaweza jitokeza katika nyayo za miguu pia vipele hivi vyaweza jitokeza sehemu yoyokte ya mwili au mwili mzima,homa, maumivu ya kichwa, uchovu, kidonda koo ,kunyofoka nywele, kuvimba matezi,maumivu ya viungo pia kupungua uzito vyaweza jitokeza katika hatua hii.
Pia endapo mgonjwa hato tibiwa katika hatua hii dalili izo hukaa kwa wiki kadhaa kisha hupotea pia yaweza jirudia kwa muda ndani ya mwaka mmoja au miwili na kama hato pata tiba tena huamia katika hatua nyingine.
Kaswende iliyo jificha(latent syphilis).
Katika hatua hii mgonjwa huwa haoneshi dalili zozote za kuwa na ugonjwa,Bali mgonjwa anaweza tambuliwa kwa kufanya vipimo maabara,pia katika hatua hii mgonjwa anakuwa hana uwezo wa kuambukiza wengine.
Kaswende Ya badae(tertiary syphilis)
Hujitokeza kwa wagonjwa ambao hawa kupata tiba katika hatua ya awali,hatua hii hujitokeza kuanzia miaka kumi na tano hadi thelathini baada ya maambukizi ya awali na husababisha athari nyingi katika viungo mbalimbali kama ubongo,macho n.k
Madhara ambayo yaweza jitokeza katika hatua hii ni pamoja na.
.Ugonjwa wa moyo.
.Upofu
.Ugonjwa wa akili.
.Kupungua uwezo wa kufikiri.
.Kifo.
.Matatizo katika mfumo wa kizazi na hewa.
Kaswende ya kurithi.(congenital syphilis).
Ni kaswende ambayo mtoto hupata kwa mama kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa,watoto wengi huwa hawaoneshi dalili japo wengne hupatwa na upele kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo za miguu,pia watoto hawa hufariki muda mfupi kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa.
Dalili za ugonjwa huu zaweza onekana baada ya kuzaliwa au wiki mbili hadi miezi mitatu baada ya kuzaliwa.
.Homa
.Kukasirika haraka
.Kutokuongezeka uzito
.Vipele viganjani au unyayoni
.Vipele mkononi ,sehemu za siri na haja kubwa.
Kwa watoto wa kubwa .
.Upofu
.Maumivu mifupa
.Kuwa kiziwi
.Ukungu kwenye mboni za macho.
.Mabaka meusi kwenye ngozi,mdomoni,sehemu za siri na sehemu za haja kubwa.
.Maumivu ya viungo.
Soma:Ugonjwa-wa-zinaa wa kisonono.html
Namna ya kugundua ugonjwa.
Ugunduzi hufanyika kwa kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa, kuchukua historia ya mgonjwa,vipimo vya damu na kugundua bacteria aina ya treponema pallidum.
Vipimo kwa wenye madhara ya kaswende hujumuisha x ray,vipimo moyo,ct scan,MRI n.k
Madhara ya tokanayo na kaswende.
Ugonjwa wa kaswende ni moja ya magonjwa ambayo huwa na madhara makubwa kama mgonjwa hatopata matibabu mapema,kadiri muathirika anavo Chelewa kupata matibabu ndivyo vijimelea vinavo zidi kusambaa mwilini na kuleta athari katika sehemu tofauti za mwili,athari ambazo hujitokeza ni pamoja na:
.Kwa akina mama wajawazito kuharibika kwa mimba Mara kwa Mara.
.Kuzaa mtoto mfu au mtoto kufariki muda mfupi kabla ya kujifungua.
.Upofu.
.Kupata magonjwa ya akili mfano kupoteza kumbukumbu
.Upungufu wa damu(anemia)
.Matatizo kwenye ubongo.
.Kupata magonjwa ya moyo.
.Kushindwa kusikia vizuri
.Matatizo ya mifupa
.Kuwa katika hatari ya kupata virusi vya ukimwi
.Kupata ugonjwa wa kiharusi
.Kupata ugonjwa wa uti wa mgongo.
.Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kwa wanawake.
.Utasa kwa wanawake na wanaume kushindwa tungisha mimba.
.Kwa wanaume kukosa msukumo wa kufanya mapenzi(impotence).
.Matatizo katika mfumo wa mkojo mfano kushindwa kuhisi mkojo umejaa kwenye kibofu.
.Matatizo kwenye ini.
.Kushindwa kuhisi maumivu au joto kutokana na mfumo wa fahamu kuathirika
.Kifo
Ufanye nini kujikinga na ugonjwa wa ?
.Tumia kondomu auu Mpira kwa usahihi katika kila kitendo ukifanyacho.
. Acha au epuka matumizi ya pombe au madawa ambayo huchochea ufanyaji wa ngono zisizo salama.
.Kuwa mwaminifu au kuwa na mpenzi mmoja,unapo kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja ndivo unavo jiongezea nafasi ya kupata ugonjwa.
.Pia epuka ufanyaji wa mapenzi kinyume na maumbile na jinsia moja.
.Pia Fanya mazoezi au kuwa bize na kazi zako jambo ambalo hupunguza mawazo ya ufanyaji wa ngono.
.Pia kama utashindwa kabisa ni vema ukaamua kuacha kufanya mapenzi kabisa hadi muda wa kuoa utakapo fika.
.Kwa wakina mama wajawazito wanashauriwa kuhudhuria kliniki mapema na katika kila hudhurio ,kwani kuhudhuria kliniki kuta saidia ugundulike mapema kama utakuwa na maambukizi kisha kupata matibabu mapema hivyo kuondoa uwezekano wa kumwambukiza mtoto kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa na kupelekea kupunguza idadi ya vifo vya watoto kabla na baada ya kuzaliwa,pia itasaidia kuondoa madhara ambayo mama mwenyewe anaweza akaya pata.
Ushauri!!
Ugonjwa wa kaswende unatibika kote nchini kwa iyo pindi uonapo mabadiliko hususani katika nyeti zako nivema ukaenda hospitali kufanyiwa vipimo ili kujua kama unaugonjwa wa kaswende au ugonjwa tofauti na ukapata matibabu ili kuondoa madhara ambayo yatajitokeza baadae sana.
Pia epuka matumizi holela ya dawa bila ya kupata vipimo ,kwasababu unaweza ukatumia dawa kwa kuhisi unaugua ugonjwa fulani lakini kumbe ukawa unaugua ugonjwa mwingine,pia kadiri utakavyo zidi kutumia dawa ndivyo kadiri wadudu wanavyo zidi kusambaa na kukuletea madhara, kwaiyo ni vema ukaenda hospitali ili kupata tiba sahihi.
No comments:
Post a Comment