Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Utumiaji wa madawa ya kulevya na athari zake.



Dawa za kulevya.

Ni chemikali ambazo pindi zinapo ingizwa mwilini huathiri ubongo wa mtumiaji,jambo ambalo husababisha awe na matendo ,hisia,fikra na muonekano tofauti na matarajio ya jamii.

Chemikali hizi hutokana na mimea ambayo ni muhimu katika mahitaji mengine ya binadamu pia kuna njia tofauti ambazo madawa haya hutumiwa na watumiaji nazo ni,kuvuta kupitia pua,kuvuta kwa kutumia mdomo, kujidunga sindano,na kula au kunywa.

Tatizo hili la utumiaji wa madawa ya kulewesha limekuwa kubwa kote ulimwenguni jambo ambalo linapelekea kuwa na waathirika wa jinsia zote na kupunguza nguvu kazi ya taifa kutokana na madhara makubwa yatokanayo na dawa hizo.



Nini husababisha mtu kutumia madawa ya kulevya?

Kila mmoja anasababu zake ambazo zina sababisha akawa mmoja kati ya watumiaji wa madawa , sababu izo ni kama.

.Hali ngumu ya maisha.
Kutokana na ugumu wa maisha watu wanajiingiza katika utengenezaji wa madawa ya kulevya  ili wajipatie kipato cha kuweza imudu familia,pia katika uandaaji huo nao hujikuta wanakuwa watumiaji wa madawa.Mfano wale ambao husafirisha dawa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

.Marafiki wa baya.
Kuwa na marafiki ambao ni watumiaji wa madawa huongeza hatari ya kuwa mtumiaji wa madawa kutokana na ushawishi mkubwa uliopo baina ya marafiki.

.Msongo wa mawazo.
Baadhi ya watu huamini ukitumia madawa mfano pombe pindi ukiwa na mawazo,mawazo hayo huisha,jambo ambalo limepelekea imani iyo kujengeka kwa wengi na kusababisha wanapo pata mawazo kutumia vilevi kwa ajili  ya kuondoa mawazo jambo ambalo siyo la kweli, hali hii husababisha watumiaji waendeleee kuongezeka.

.Upatikanaji wa dawa.

Upatikanaji wa madawa ya kulewesha umekua rahisi jambo ambalo husababisha kuwepo kwa watumiaji wengi wa madawa ayo.



.Dini
Kuna baadhi ya dini utumiaji  was kilevi siyo haramuharamu jambo hili husababisha kuongezeka kwa idadi kubwa ya madawa ya kulewesha.


.Mila ,desturi na tamaduni ndani na nje ya nchi.
Kuna baadhi ya makabila utumiaji was vilevi in kawaidakawaida,pia kuna baadhi ya nchi madawa yamehalalishwa kwa matumizi,kwahiyo kutokana na watu kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine hususani wageni wanao kuja nchini kwetu husababisha watu  kuiga tamaduni ambazo siyo za kwao .



Soma/mambo-muhimu-ya-kuzingatiwa-kwa-mama.html




Aina za dawa za kulevya na athari zake.


.Heroin

Dawa hii imetengenezwa kutoka katika mmea ujulikanao kama opium papy,pia dawa hii kwa jina lingine hujulikana kama diemorphine.Dawa ya heroin ikiwa katika mfumo wa morphine imehalalishwa kutumika hospitali kwa ajili ya kutuliza maumivu makali yatoka nayo na saratani ambayo ni sugu,pia hutumika kuondoa maumivu kwa wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji japo hospitality nyingi hutumia zaidi dawa ya pethidine pamoja na tramadol,pia hutumika kuondoa maumivu kwa mtu aliye pata ajali au aliyepata maumivu makali ghafla.


Dawa ya heroin hutumika katika njia zipi?

Kuna njia mbalimbali za kutumia dawa hii,lakini inategemeana na mtumiaji ameachagua njia ipi,njia izo ni kama:

.Dawa hii inaweza ikatumika kwa kuvuta kwa njia ya pua.

.Watumiaji wengine huvuta kama sigara kwa kutumia mdomo.

.Wengine hutumia heroin kwa kujidunga na sindano moja kwa moja kwenye mishipa ya miili yao.

.Pia watumiaji wengine huchanganya heroin na crack cocaine kisha kuitumia kitendo cha kuchanganya dawa hizi mbili hujulikana kama speedballing.



Je heroin hufanyaje kazi?

Pindi dawa hii inapokuwa imetumika  huingia kwenye mishipa ya damu na kusafirishwa moja kwa moja kwenye ubongo kwa haraka zaidi.Dawa hii ikishafika kwenye ubongo hukandamiza mishipa ya fahamu au neva za fahamu,jambo ambalo husababisha mfumo wa fahamu usifanye kazi yake katika hali ya kawaida na matokeo yake mtu hatohisi  maumivu tena.


Zipi ni dalili kwa mtumiaji wa heroin?

Dalili zifuatazo hapo chini huonekana kwa mtumiaji Mara tu ya kutumia heroin.

.Kukauka mdomo

.Kujihisi ni mwenye furaha(euphoria) na mwenye nguvu.

.Kuhema polepole

.Mikono na miguu kwa baaadhi ya watumiaji inakuwa mizito.

.Baadhi ya watumiaji hupata kichefuchefu na kutapika.

.Kulegea kwa kope pamoja na macho.



Madhara yatokanayo na matumizi ya heroin.

Mara nyingi madhara ya kutumia madawa hutokana na matumizi ya muda mrefu,kiwango cha dawa kinachotumika(overdose) na vifaa ambavyo vinatumika mara nyingi vinakuwa siyo salama jambo ambalo husababisha madhara makubwa kwa watumiaji,madhara hayo ni.

.Maambukizi ya magonjwa mbalimbali hususani kwa kuchangia vifaa ,magonjwa ayo ni kama Virusi vya Ukimwi ,Homa ya ini(hepatitis B ) na mengineyo.

.Maambukizi katika mfumo wa hewa kwa sababu chemikali  inayo ingia katika mfumo wa hewa huathiri utendaji kazi wa mapafu,kadiri mtumiaji atakavyo dhidi tumia dawa mara kwa mara anaweza pata saratani ya mapafu,ugonjwa wa kifua kikuu na mapafu kujaa maji.

.Maambukizi katika figo,mifumo ya mwili wa binadamu hufanya kazi sambamba au hutegemeana na mfumo mwingine,kwahiyo kipindi mfumo mmoja unaposhindwa kufanya kazi vizuri husababisha na mwingine ushindwe kufanya kazi mfano mapafu ya kishindwa Fanya kazi vizuri hata figo nayo itashindwa kufanya kazi yake vizuri ya kuchuja taka mwili matokeo yake nayo itaathirika.

.Maambukizi kwenye kuta za moyo jambo ambalo litasababisha moyo ushindwe kufanya kazi yake ya kusukuma damu vizuri na matokeo yake mtu huweza patwa na magonjwa ya moyo,kama msukumo mkubwa wa damu na mapigo ya moyo bila mpangilio.

.Vile vile mtumiaji anaweza akapatwa na matatizo ya akili kutokana na ubongo kuathirika na madawa,matatizo hayo yaweza kuwa kama msongo wa mawazo(dipression,na pengine ukuchanganyikiwa kabisa).

.Kwa wanawake lazima kutakuwa na mabadiliko ya mzunguko wa hedhi kwasababu madawa ya kulevya huvuruga mfumo wa vichocheo vya mwili,pia kama ni mjamzito mimba inaweza ikaharibika kabla ya kutimiza miezi tisa,pia endapo mimba itafika miezi tisa mtoto atakae zaliwa hatokuwa na Afya njema.

.Kushindwa kumudu tendo la ndoa kwa wanaume.

.Majipu kwasababu vfaa vinavyotumika siyo salama.

.Pia kuharibika kwa kuta za pua kwa wale ambao huvuta kupitia pua.




Cocaine.

Chanzo cha dawa hii ni mmea unaojulikana kwa jina la coca bush. Dawa hii huweza kutumika katika njia zifuatazo.


.Unga (cocaine hydrochloride), dawa hii mtaani hujulikana kama coke mtumiaji anaweza akatumia dawa hii kwa kuvuta puani kama unga au anaweza akachanganya unga huo na maji kisha akajidunga na sindano moja kwa moka kwenye mshipa was damu.

.Coca paste,dawa hii hutumika kwa kuvuta.

.Pia mtumiaji wa cocaine anaweza akachuma majani ya mmea huu na kuyatafuna kwa mdomo.

.Crack cocaine (freebase), dawa hii mtaani hujulikana kwa jina la rock or crack dawa hii hutengenezwa katika mfumo wa alkali kwa kutumia dawa maalumu,na mtumiaji anaweza kutumia dawa hii kwa kuivuta kama sigara.



Cocaine hufanyeje kazi?

Mara baada ya kutumika dawa hii huenda moja kwa moja kwenye ubongo kipitia katika mishipa ya damu, ikifika kwenye  ubongo huathiri ufyonzaji wa chemicali za serotonin, dopamine na nor epinephrine katika ubongo ambazo zimeungana pamoja hufanya kama kiunganishi cha kusafirsha taarifa kutoka neuron moja hadi nyingine (neurotransmitter) ,kuathiriwa kwa chemikali hizo humfanya ahisi in mwenye furaha(euphoria), uchangamfu kupitiliza,dawa zikisha maliza kufanya kazi hali hii huisha.


Dalili za mtu aliyetumia cocaine.

.Kuongezeka kwa msukumo wa damu.

.Kutokwa na jasho kutokana na kuongezeka kwa joto mwilini.

.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

.Kuhisi kichefu chefu na kutapika.

.Kujihisi mwenye furaha.

.Kupungua kwa uwezo wa kufikiri .

.Kusinyaa kwa mishipa ya damu.

.Anahisi kuguswa mwilini au akahisi anaona kitu chochote ambacho kiuhalisia hakipo (hallucination) jambo hili hutokea kwasababu kunakuwa na hisia kubwa kwenye ubongo jambo ambalo husababisha mfumo wa kukabiliana na vitu ushindwe kukabili hisia izo(coping mechanism au defence mechanism).

.Kuhamasika katika ngono.

.Dilated pupils.





Madhara ya matumizi ya cocaine.

.Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kutokana na kuchangia sindano mfano Ukimwi na homa ya ini na kusababisha kupungua kwa nguvu Kazi ya taiga.

.Kuwa tegemezi hatoweza Fanya jambo lolote bila kutumia madawa.

.Cocaine huongeza hamu ya mapenzi ,lakini mtumiaji pia anaweza akashindwa kufikia adhimio lake.

.Kusinyaa kwa mishipa ya damu kunaweza sababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu na kusababisha mishipa kupasuka,kupasuka mishipa hupunguza kiwango cha damu safi kwenye ubongo kwaiyo mtumiaji huwa katika hatari ya kupata kiharusi.

.Matatizo kwenye mfumo wa hewa kama Mafia yasiyo koma kutokana na kuwepo kwa viamshi mda wote,pia saratani ya mapafu na kifua kikuu.

.Kifo cha ghafla kinaweza tokea endapo mtumiaji atapatwa na shambulio la moyo au atatumia kwa kiwango kikubwa (overdose),mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio na kiharusi.

.Figo kushindwa kufanya kazi,mifumo ya mwli hutegemeana au hufanya kazi sambamba tatizo katka mfumo mmoja hupelekea tatzo katika mfumo mwngine.



Bangi

Bangi hutengenezwa kutoka katika mmea unaoitwa canab plant.Pia bangi ni miongoni mwa dawa zinazoleta njozi na kumfanya mtumiaji awe na tafsifi potofu za hisia.


Njia za kutumia bangi.

.Kuvuta kama sigara kupitia mdomo.

.Wengine hutumia bangi katika mchanganyiko wa chakula.



Dalili za mtumiaji bangi.

.Macho kuwa mekundu.

.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

.Kukauka mdomo.

.Kuongezeka kwa hamu ya kula.

.Kujihisi raha na mwenye nguvu.

.Kupungua kwa uwezo wa kufikiria.

.Kuhisi vitu ambavyo havipo (hallucination).

.Kujitenga katika jamii.



Madhara ya kutumia bangi.

.Kupata ugonjwa wa akili kutokana na kutumia dawa.

.Magonjwa katika njia ya hewa kama saratani ya pafu kutokana na madhara ya kemikali zilizopo kwenye bangi.

.Kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka.

.Kuwa tegemezi.

.Magonjwa ya moyo.



Pombe.

Ni kilevi ambacho huleta burudani na kinawatumiaji wengi hususani katika miaka ya sasa,Lakini pindi kilevi hiki kikitumika kwa wingi na kikafanya mtu ashindwe jizuia basi huwa na madhara makubwa sana.


Madhara ya utumiaji pombe.

.Chemikali ambazo zipo kwenye pombe husababisha ini kuharibika au kuvimba endapo pombe zitatumika mara kwa mara ini  ambalo kazi yake kubwa ni kuvunjavunja sumu mwilini uwezo wake wa kufanya kazi utapungua.

.Kupoteza uelekeo wa maisha hususani katika mambo ya kukuza uchumi.

.Pombe pia huchochea uhalifu.

.Unakuwa Mtegemezi.

.Pombe pia huchochea kufanya ngono zembe jambo ambalo huongeza uwezekano wa kupata magonjwa kama Ukimwi.

.Pia huongeza hatari ya kupata kisukari.

.Ugonjwa wa figo.

.Kuongezeka kwa uzito.



Madhara yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya kwa ujumla

Madhara yakutumia madawa ya kulevya ni megi mwanzo tumeona yanayotokana na afya madhara mengine ni.

.Kupungua kwa nguvu kazi ya taifa.

.Kuongezeka kwa idadi ya watoto was mtaani.

.Kupoteza uelekeo wa maisha.

.Kushindwa kujihusisha katika shughuli za kijamii .

.Kupata magonjwa mbali mbali.

.Madawa ya kulevya pia huongeza kwa kasi mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu.

.Pia huongeza uharifu na uharibifu wa raslimali katika jamii.

.Madawa ya kulevya pia husababisha kuendelea kuwepo kwa rushwa katika jamii.

.Madawa ya kulevya husababisha uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti na mmomonyoko wa udongo.



Ufanye nini kuepuka utumiaji wa madawa ya kulevya.?

.Epuka kuwa na marafiki ambao ni watumiaji  madawa.

.Fanya mazoezi ya viungo

.Epuka kufata mila desturi na tamaduni za wengine.

.Jishughulishe na shughuli mbali mbali.

.Tafuta njia sahihi ya kuondoa mawazo unapokuwa na msongo wa mawazo kama kufanya mazoezi.

.Pia tambua athari zitokanazo na kujihusisha na madawa.



Mawasiliano whatsap: 0712106789.
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts