Home »
» Ugonjwa wa zinaa wa trichomonasi
Ugonjwa wa zinaa wa trichomonasi
Trichomonasi
Ni ugonjwa wa zinaa ambao hushambulia njia ya mkojo kwa wanaume(urethra) na kwa wanawake sehemu ya siri(uke) na wakati mwingine katika njia ya mkojo(urethra).Ugonjwa huu husababisha na vimelea aina ya protozoa vijulikanavyo kwa jina la trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu pia ujulikana kwa majina mengine kama trichomonas vaginitis au trich.
Wanaume wenye vimelea vya ugonjwa huu Mara nyingi huwa hawaoneshi dalili na hii ni kutokana na kuwepo kwa majimaji aambayo huzalishwa na tezi dume ,maji haya huwaathiri vimelea wa trich.Dalili za ugonjwa huu pia huonekana zaidi kwa wanawake, mama mjamzito mwenye vimelea vya ugonjwa huu ana uwezekano mkubwa wa kujifungua kabla ya wakati au kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo.
Vi hatarishi vya ugonjwa wa trich
Ugonjwa husababishwa na protozoa wa trichomonas vaginalis ambao husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye vimelea wa trich bila ya kutumia kinga.
Pia ugonjwa wa trich huwa athiri zaidi wanawake kuliko wanaume , wa athirika wengi ni kuanzia wale wenye umri wa miaka 15 hadi miaka 50. Kwahiyo hatari ya kupata ugonjwa wa trich huongezeka kutokana na:
.Kuwa na historia ya kuugua ugonjwa wowote wa zinaa kabla.
.Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
.Kuugua ugonjwa wa trichomonasi kabla.
.Kujamiiana bila ya kujikinga au kutumia kondom.
.Pia kushuka kwa kinga ya mwili.
Dalili za ugonjwa wa trichomonasi.
Dalili za ugonjwa huu huonekana siku tano hadi siku ishirini na nane baada ya mtu kuambukizwa vimelea vya ugonjwa,japo kuna baadhi ya watu huchukua muda mrefu zaidi hadi dalili kuonekana.
Kwa wanawake vimelea hawa hushambulia njia ya mkojo,shingo ya kizazi,sehemu ya siri(uke),tezi za batholin na kibofu cha mkojo. Kwa wanaume vimelea hushambulia njia ya mkojo ,njia ya kusafirisha mbegu za kiume,mfuko wa kuhifadhi mbegu za kiume na uume wenyewe.
Dalili kwa wanaume
Ni mara chache sana dalili kuonekana kwa wanaume,pindi zinapo onekana dalili huweza kuwa.
.Muwasho katika mrija wa kupitisha mkojo.
.Maumivu wakati wa kukojoa au kujamiiana hususani wakati wa kutoa mbegu za kiume(ejaculation).
.Kuwa na hamu ya kukojoa Mara kwa Mara.
.Kutokwa na uchafu au majimaji katika njia ya kutolea mkojo.
Dalili kwa wanawake
Kwa kuwa wanawake ndo wahanga wa kubwa na dalili kwa upande wao huonekana haraka, wanawake wengi hupata dalili moja au mbili lakini kuna wengine huweza kupata dalili zote kati ya hizi:
.Maumivu wakati wa kujamiiana
.Maumivu wakati wa kukojoa
.Muwasho katika sehemu za siri
.Harufu mbaya ukeni
.Maumivu chini ya kitofu
.Kutokwa na damu ukeni
.Kupata hamu ya kukojoa Mara kwa Mara
.Kutokwa na uchafu mweupe,njano au kijani ambao huambatana na harufu.
Soma:ugonjwa-wa-zinaa wa kaswende.html
Vipimo
.Kipimo cha damu kwaajili ya kuangalia prostatic specific ant gen,hizi ni aina ya protein ambazo hutengenezwa na tezi dume na utengenezwaji wake huongezeka kadiri tezi dume inavyo ongezeka ukubwa,maambukizi ya tezi dume na saratani ya tezi dume,pia kipimo hiki hufanyiwa wale wanao patwa na ugonjwa wa trichomonasi na wale wenye umri zaidi ya miaka 60.
.Kwa kutumia darubini,kipimo hiki hutumia kifaa maalumu kuingiza katika nyeti(uke) ya mwanamke kisha sampuli huchukuliwa katika shingo ya kizazi kwa kutumia pamba kisha sampuli hiyo hupelekwa maabara kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi,sampuli hiyo huchukuliwa na daktari.
.Kipimo cha mkojo
.Kipimo cha kuangalia damu kwa ujumla wake( full blood picture).
.Kipimo cha pap smear,hiki ni kipimo ambacho chembe chembe zinazopatikana kwenye shingo ya kizazi huchukuliwa na kufanyiwa uchunguzi kwa kutumia hadubini.
Yepi ni madhara ya ugonjwa wa trichomonasi?
.Ugonjwa wa trichomonas huongeza hatari ya mtu kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
.Kwa wakina mama wajawazito ugonjwa wa trichomonasi huongeza hatari ya mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya wakati.
.Pia ugonjwa wa trich kwa wanaume huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
.Kwa wanawake ugonjwa huu huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi.
.Pia kwa wanawake endapo hato pata matibabu huongeza hatari ya kuugua ugonjwa wa pelvic inflammatory disease (pid) ambao huongeza hatari ya mwanamke kuwa tasa,kuziba kwa mirija ya uzazi kutokana na kuwepo kwa makovu,na kuwa na maumivu sugu ya tumbo.
Ufanye nini kuepuka ugonjwa wa trichomonas?
.Hakikisha unafanya ngono iliyo salama au unatumia kondom kwa usahihi na kwa kila tendo.
.Epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kwa sababu wapenzi wengi huongeza hatari ya mtu kupanda magonjwa ya zinaa hivyo kuwa rahisi kupata ugonjwa wa trichomonasi.
.Fanya mazoezi au jishughulishe ,kufanya mazoezi humfanya mtu kuwa bize hivyo kumwondolea fikra za kuwaza ngono muda mwingi.
.Kwa wakina mama wajawazito wanashauriwa kuhudhuria kliniki mapema na kila hudhurio, kuhudhuria kliniki husaidia mama kufanyiwa vipimo katika kila hudhurio kwaiyo endapo atagundulika na vimelea vya ugonjwa wa trichomonasi basi atapata matibabu mapema ivyo kuondoa hatari ya mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya wakati.
.Pia epuka kufanya mapenzi ya jinsia moja au kinyume na maumbile.
.Pia kama utashindwa kufanya hayo yote basi unashauriwa kuacha kufanya ngono kabisa na kusubiri hadi pale utakapo mpata mwenza wako.
Ushauri
Ugonjwa wa trichomonasi unatibika kwaiyo ili kuepuka madhara tajwa hapo juu,ni vema ukawahi hospitali ili ufanyiwe vipimo Mara utakapo ona dalili ambazo siyo za kawaida katika nyeti zako na kisha upatiwe matibabu yaliyo sahihi, pia epuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.
No comments:
Post a Comment