Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Ujue ugonjwa wa zinaa wa chlamydia

Chlamydia

Ni ugonjwa wa zinaa unao sababishwa na bacteria wa julikanao kwa jina la chlamydia trachomatis,wadudu hawa huleta athari mbali mbali hususani kushindwa kushika mimba kwa mwanamke na kushindwa tungisha mimba kwa wanaume.

Pia kwa wale ambao hupatwa na vimelea vya ugonjwa wa chlamydia katika hatua za mwanzo huwa hawaoneshi dalili za ugonjwa huu, pia ugonjwa huu huambatana na ugonjwa wa kisonono.


Vi hatarishi vya ugonjwa wa chlamydia.

Kama nilivyo eleza mwanzo ugonjwa wa chlamydia husababishwa na bacteria aina ya chlamydia trachomatis na husambaa kutoka kwa mtu mwenye vimelea hadi kwa asiye kuwa na vimelea kwa njia ya kujamiiana bila ya kutumia kondomu, kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto, Kujamiiana katika njia ya haja kubwa,mapenzi ya mdomo na Kutoka kwenye manyoya au vinyesi vya wanyama kama vile ndege wenye ugonjwa huu unao patikana kwa ndege kama Kuku,kasuku ,bata. Kwaiyo uwezekano wa kupata ugonjwa  huu ni mkubwa endapo.

.Utakuwa na mahusiano au mpenzi zaidi ya mmoja.

.Utakuwa na umri kuanzia miaka kumi na tano,kwasababu kuanzia umri wa balehe watu huamasika kufanya mapenzi zaidi.

.Kuwa na mpenzi mpya.

.Kuugua ugonjwa wa chlamydia awali.

.Kuugua ugonjwa wowote wa ngono.

.Kushuka kwa kinga za mwili.




Soma:ugonjwa-wa-zinaa trichomonasi.html


Dalili za ugonjwa chlamydia.

Ugonjwa was chlamydia huathiri wanaume kwa wanawake ,kwa asilimia kubwa watu wenye ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili,pia dalili endapo zitaonekana huanza kuonekukojoaoiki
 moja au tatu baada ya kupata vijimelea vya ugonjwa huu.

Dalili kwa wanaume:

.Kuchoma choma au kuwaka moto wakati wa kukojoa.

.Maumivu ya korodani.

.Maumivu wakati wa kukojoa.

.Maumivu sehemu za siri pamoja na kuvimba kwa tezi zinazo
patikana katika sehemu za siri.

.Kutokwa na maji yenye rangi ya njano ,kijivu au meupe kwenye mrija wa kutolea mkojo nje.


Kwa wanawake:

.Maumivu wakati wa kukojoa

.Maumivu wakati wa kujamiiana

.Maumivu sehemu ya chini ya tumbo

.Kuhisi kuwaka moto wakati wa kukojoa

.Kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya sehemu za siri.

.Maumivu na kuvimba kwa tezi katila sehemu za siri.



Vipimo

Vipimo vya ugonjwa wa chlamydia ni pamoja na:

.Urethra swab culture,ni kipimo ambacho maji kutoka katika uke wa mwanamke au katika uume kwa mwanaume huchukuliwa kwa kutumia pamba maalumu kisha kupelekwa maabara kwa uchunguzi.

.Kipimo cha mkojo.



Madhara ya chlamydia.

.Kwa wanaume kushindwa kutungisha mimba na wanawake kushindwa kushika mimba kutokana na kuziba kwa mirija ya uzazi na uwepo wa makovu katika mirija kama mgonjwa hato pata matibabu

.Kuwa katika hatari ya kupata maambukizi katika viungio (arthritis),kwa jina lingine hufahamika kama Reiler's syndrome.

.Maambukizi ya tezi dume.

.Huongeza hatari ya kupata magonjwa mengine ya zinaa mfano kisonono na virusi vya Ukimwi.

.Hatari ya kupata ugonjwa wa ( pid ),ugonjwa ambao hushambulia mirija ya uzazi,mji wa mimba ,kifuko cha mayai,ugonjwa huu husababisha maumivu kiuno na homa Kali,pia ugonjwa wa pid huongeza hatari ya mimba kutungwa nje ya tumbo uzazi.

.Kwa wajawazito husababisha kujifungua kabla ya wakati, pia kama hato pata tiba anaweza mwambukiza mwanae wakati wa kuzaliwa hatimaye mtoto akapata kichomi,maambukizi machoni jambo ambalo linaweza sababisha apate upofu kama hato tibiwa,na maambukizi sehemu za siri.

.Maambukizi katika mfuko wa kuhifadhi mbegu za kiume na korodani.





Ufanyeje kujikinga dhidi ya ugonjwa wa chlamydia?

.Epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

.Epuka au kuacha kufanya ngono kabisa.

 .Wale ambao wana mpenzi zaidi ya mmoja wanashauriwa kufanya uchunguzi Mara kwa Mara ili kujua kama wamepata maambukizi.

.Kwa wanawake wanashauriwa wasijikande na kuosha nyeti kwa maji ya moto na sabuni kwasababu huua wadudu ambao huukinga uke dhidi ya vimelea vya ugonjwa.

.Hakikisha unatumia kondomu kwa usahihi,pia epuka kujishika mikono machoni kwasababu utaendelea kusambaza wadudu.

.Kwa wale ambao wapenzi wao wana ugonjwa lakini yeye hana dalili yoyote wana shauriwa kupata matibabu.

.Wajawazito wanashauriwa kuhudhuria kliniki mapema na katika kila hudhurio ili kama watakuwa na ugonjwa wapate matibabu ili kuepuka kuwa ambukiza wakati wa kuzaliwa.





Mwisho ugonjwa wa chlamydia unatibika kwaiyo pindi unapo hisi mabadiliko katika nyeti zako nenda hospitali kapate uchunguzi na matibabu.
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts