Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Nini husababisha maumivu wakati wa hedhi?


Dysmenorrhea

Ni hali ya kupata maumivu siku chache kabla ya kupata hedhi au baada ya kupata hedhi ,au kabla na baada ya kupata hedhi.

Wanawake wengi katika siku za karibuni wamekuwa waki sumbuliwa na maumivu wakati wanapo karibia au wawapo katika siku zao,maumivu kabla ya hedhi huashiria muda wowote mwanamke atapata hedhi ,pia maumivu baada ya hedhi kwa kawaida hudumu kwa siku mbili hadi nne na baadae hukoma,hali hii ni kawaida lakini maumivu hayo yanapo zidi unashauriwa kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi.

Maumivu wakati wa hedhi  yanaweza yakawa ya kawaida au yanaweza yakawa yanasababishwa na uwepo wa matatizo mengine katika mfumo wa uzazi kwahiyo kama unapatwa na maumivu makali ya Mara kwa Mara nivema ukaonana na wataalamu watiba.



Aina za maumivu wakati wa hedhi na visababishi vya maumivu ago

Kuna aina mbili za maumivu ambazo wanawake hupata katika kipindi cha hedhi na maumivu hayo hutofautiana miongoni mwa wanawake nayo ni kama ifuatavyo:

.Maumivu ya awali (primary dysmenorrhea)

Ni aina ya maumivu ambayo huanza katika umri wa balehe, katika aina hii ya maumivu kuna kuwa hakuna ugonjwa au tatizo ambalo husababisha uwepo wa maumivu,aina hii ya maumivu Mara nyingi hutokea katika sehemu za chini ya tumbo na kiuno, pia huanza siku moja au mbili kabla ya kupata hedhi na hukoma baada ya siku tatu hadi nne.

Nini husababisha maumivu hayo?

Katika mzunguko wa hedhi kuna mabadiliko mbali mbali ambayo hufanyika ili kumpokea mtoto endapo mimba itatungwa, mabadiliko hayo ni pamoja na kuongezeka kwa unene katika moja ya kuta za  tumbo la uzazi (endometium), endapo mimba haito tungwa baada ya kupevuka kwa yai basi mazingira ambayo yali andaliwa kwa ajili ya kumpokea mtoto hujiengua na kutoka kama uchafu hapo ndiyo hedhi hutokea.

Katika kipindi cha hedhi kichocheo cha prostaglandins hutengenezwa kutokana na kumeguka kwa ukuta wa tumbo la uzazi (functional layer of uterus),Kutengenezwa kwa kichocheo hiki husababisha kukaza zaidi kwa tumbo la uzazi,kukaza kwa tumbo la uzazi ndiko husababisha maumivu pia hupunguza usafirishaji wa damu safi katika tumbo la uzazi,kukaza kwa tumbo la uzazi huendelea ili kuhakikisha uchafu wote unatoka kupitia shingo ya kizazi hadi nje kupitia uke wa mwanamke.


Maumivu ya pili (secondary dysmenorrhea).

.Ni aina ya maumivu ambayo hutokea miaka kadhaa baada ya kubalehe,aina hii ya maumivu husababishwa na kuwepo kwa tatizo au ugonjwa katika via vya uzazi vya mwanamke ,pia endapo tatizo au ugonjwa utakuwepo kabla ya umri wa balehe basi maumivu hayo yanaweza yakawepo pia katika umri wa balehe.

Pia aina hii ya maumivu yanaweza yakatokea katika umri wowote lakini hutegemeana na kuwepo kwa ugonjwa,Mara nyingi aina hii hujitokeza kwa wanawake wenye umri kuanzia miaka 20 hadi miaka 45, Pia ukomo wa maumivu haya hutegemeana na kupatiwa kwa matibabu kwa ugonjwa ambao unasababisha maumivu.



Soma:ujue-ugonjwa-wa-zinaa chlamydia.html


Nini husababisha maumivu haya?

Kama nilivyo sema aina hii ya maumivu hutegemeana na uwepo wa magonjwa katika via vya uzazi, uvimbe katika tumbo la uzazi ambao haujatokana na kuwepo kwa saratani ambao hutokeza katika tumbo la uzazi,uvimbe katika mfuko wa uzazi husababisha kubadilika kwa vichovheo vya mwili,Maambukizi sugu katika via vya uzazi(pid),ugonjwa wa endometriosis ambao seli za ndani ya mfuko wa uzazi huota nje ya mfuko huo,ugonjwa wa adenomyosis, kushambuliwa na magonjwa ya zinaa Mara kwa Mara bbila matibabu matokeo yake ni ugonjwa wa pid,matatizo katika kifuko cha mayai ,pia maumivu haya yanaweza sababishwa na matatizo ya shingo ya kizazi
 mfano mlango wa shingo ya kizazi kuwa mdogo husababisha damu au uchafu kushindwa kupita kwa urahisi zaidi ,wanawake ambao wapo hatarini kupatwa na matatizo ya shingo ya kizazi ni pamoja na wale ambao hupata hedhi ya kwanza katika umri mdogo zaidi na wale ambao hawaja pata mtoto hadi wakiwa na miaka 35 au zaidi.




Dalili za maumivu

Dalili hutofautiana kati ya mwanamke na Mwana mke maumivu hayo huambatana na:

.Kichefu chefu

.Kutapika

.Kuharisha katika kipindi cha hedhi

.Maumivu ya kichwa

.Maumivu ya mgongo

.Maumivu chini ya kitovu

.Maumivu ya nyonga

Maumivu hayo hutoweka baada ya Siku tatu hadi nne.



Vipimo

.Kuchukua historia kutoka kwa mgonjwa kwa wale ambao wana maumivu ya awali.

.Kipimo cha utrasound ili kuangalia ndani ya tumbo la uzazi kama kuna uvimbe hususani kwa wale ambao maumivu husababishwa na magonjwa.

.Endo cervical swab ,kuchukua sampuli kwenye shingo ya kizazi kwa kutumia pamba maalumu kisha kupeleka maabara ili kugundua kama magonjwa ya zinaa ni sababu ya maumivu hayo.

.Kipimo cha damu ili kuangalia uwingi wa damu ,ili kugundua kama kuna upungufu wa damu hususani kwa wale wanaopata  heavy bleed .

.Kipimo cha laparascopy




Ufanye nini pindi unapo kuwa na maumivu?

.Epuka kukaa katika mazingira yenye baridi ambayo yata kuongezea maumivu.

.Pata muda mwingi wa kupumzika.

.Epuka matumizi ya vinywaji ambavyo vina caffeine mfano vilevi vyote pia epuka matumizi ya sigara kwa watumiaji.

.Epuka kuwa na msongo wa mawazo katika kipindi cha hedhi.

.Fanya mazoezi Mara kwa Mara

.Zingatia lishe bora

.Kunywa maji ya kutosha

.Pia unaweza ukajikanda na maji ya moto.

.Matumizi ya dawa za kutuliza maumivu.





Ushauri:

Endapo maumivu hayo yatazidi unashauriwa kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi kisha upate matibabu sahihi kwasababu huenda maumivu yako yame tokana na uwepo wa matatizo mengine.
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts