Home »
» Kuto kupata hedhi husababishwa na nini?
Kuto kupata hedhi husababishwa na nini?
Mwanamke katika hali ya kawaida akisha fikia katika umri wa kubalehe basi hupata hedhi yake ya kwanza kitaalamu huitwa menarche, na huendelea kupata hedhi hadi hedhi inapo fikia ukomo kitaalamu huitwa menopouse.
Hata ivyo wapo baadhi ya wanawake pamoja na kufikia umri wa balehe bado imekua changamoto kupata hedhi na jambo hili linaweza lika dumu kwa muda mrefu endapo halito patiwa ufumbuzi na kusababisha mwanamke kukosa uwezo wa kushika mimba tatizo hili kwa kitaalamu hujulikana kama amenorrhea.
Aina za amenorrhea
Kukosa hedhi kumegawanyika katika makundi mawili,kukosa hedhi kwa awali na kukosa hedhi kwa baadae.
.Kukosa hedhi kwa awali(primary amenorrhea).
Hii ni hali ya kukosa hedhi ambayo huwakumba wasichana ambao hawaja wahi kabisa kupata hedhi lakini wapo kwenye umri wa kuvunja ungo,pia yaweza endana na kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au mwanamke anaweza akaona mabadiliko yanayo ashiria balehe lakini akashindwa kupata hedhi.
.Kukosa hedhi kwa baadae (secondary amenorrhea).
Hii ni hali ambayo humkumba mwanamke ambaye alishakwisha kupata hedhi katika siku za nyuma lakini baadae akakosa hedhi kwa miezi mitatu mfululizo au zaidi,pia hutokea kwa mwanamke ambaye hatumii njia yoyote ya kupanga uzazi,siyo mjamzito ,ambaye hanyonyeshi pia hajafikia katika ukomo wa hedhi.
Soma:nini-husababisha-maumivu-wakati-wa-hedhi.html
Kukosekana kwa hedhi husababishwa na nini?
Kukosekana kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na uwepo wa sababu mbalimbali,baadhi ya sababu hizo huwa za kawaida katika kipindi cha maisha ya mwanamke lakini zingine zinaweza zikawa kutokana na maudhi yatokanayo na matumizi ya aina Fulani za dawa au ishara ya kuwepo kwa tatizo fulani kiafya ,sababu hizo ni kama:
.Kukosa hedhi kwa asili.
Katika maisha ya mwanamke anaweza akakosa hedhi kutokana na sababu ambazo kiasili zipo sababu hizo ni.
.Mimba
.Kunyonyesha
.Hedhi kufika ukomo.
.Matumizi ya dawa za upangaji uzazi.
Ni kawaida kwa baadhi ya wanawake wanao tumia dawa za upangaji uzazi kukosa hedhi,hata mara baada ya kuacha kutumia dawa izo huchukua muda kidogo kabla ya mayai kuanza kupevuka na kurudi kwa hedhi,pia sindano ,kipandikizi navyo husababisha kukosa hedhi.
.Matumizi ya baadhi ya dawa.
Kuna baadhi ya dawa endapo zikitumika huleta maudhi madogo madogo maudhi ayo yaweza kuwa mfano kukosa hedhi, dawa hizo ni pamoja na dawa za kutibu magonjwa ya akili (ant depressant na ant psychotic),pia dawa zinazo tibu ugonjwa wa saratani (chemotherapy),baadhi ya dawa za moyo( blood pressure drugs) na dawa za kutibu mzio au aleji.
.Sababu zitokanazo na mtu anavyo ishi.
-Uzito mdogo,kuwa na uzito mdogo kupitiza husababisha mvurugiko wa vichocheo vya mwili ambavyo husababisha kuto kupevuka kwa mayai,wanawake ambao wana matatizo ya ulaji mfano kula kidogo au kula sana huwa katika hatari ya kukosa hedhi kutokana na mvurugiko wa vichocheo vya mwili.
-Kufanya mazoezi kupitiliza, mazoezi kupitiliza husababisha mvurugiko wa hedhi kutokana na matumizi makubwa ya nishati.
-Mawazo,mawazo husababisha mabadiliko ya ufanyaji kazi wa hypothalamus,sehemu katika ubongo ambayo huratibu mfumo wa vichocheo vya mwili pamoja na vichocheo vinavyo sababisha kutokea kwa hedhi na matokeo yake mabadiliko ya hedhi au ukomo wa hedhi ,lakini pindi mawazo yanapo ishia hedhi hurudi katika hali ya kawaida.
-Hofu iliyo pitiliza pia huchangia kuvurugika kwa vichocheo hivyo kusababisha ukomo au mabadiliko ya hedhi.
-Unene uliopitiliza pia huchangia mgurugiko wa hedhi.
-Uvutaji sigara,unywaji wa pombe na utumiaji dawa kulevya.
-Magonjwa sugu pia yaweza changia kwa kiwango kikubwa.
.Matatizo yatokanayo na vichocheo.
Kwa kawaida matatizo mengi ambayo hugusa tiba husabababisha kuto kuwepo kwa uwiano wa vichocheo katika mwili mfano.
-Kuto kufanya kazi kwa tezi ya thyroid,tezi ya thyroid huzalisha vichocheo yaani T3 pamoja na T4 pindi vichocheo hivyo vinapokuwa havitengenezwi kutokana na tezi kupata shida husababisha mabadiliko katika hedhi ikiwemo kuto kupata hedhi.
-Uvimbe katika tezi ya pituitari,pia husababisha mabadiliko katika mfumo wa vichocheo au homoni na matokeo ni ukosefu wa hedhi.
-Polycystic ovarian syndrome,pia husababisha mwanamke akose hedhi.
-Ukomo wa hedhi mapema,ukomo wa hedhi katika hali ya kawaida huanza kuanzia miaka 50,japo Kuna wengine hupata ukomo kuanzia miaka 45.
-Kuzalishwa kwa Vichocheo vya kiume kwa wingi.
-Kuto kuzalishwa kwa mayai.
-Kuzalishwa kwa wingi kwa kichocheo cha prolactin, kichocheo cha prolactin huamasisha uzalishwaji wa maziwa kwa wingi,kwaiyo uwepo wa kichocheo cha prolactin kwa wingi husababisha kupungua kwa uzalishwaji wa vichocheo vinavyo husika na hedhi.
.Sababu za kimaumbile.
Matatizo katika via vya uzazi vyenyewe yaweza sababisha kukosekana kwa hedhi mfano.
-Kukosekana kwa viungo vya uzazi, matatzo mengine huanza kipindi cha uumbaji au ukuaji wa mtoto katika tumbo la mama ambayo huweza sababisha mtoto akazaliwa bila uwepo wa baadhi ya viungo vya uzazi mfano uterus,shingo ya uzazi n.k kwakuwa mfumo wa uzazi hauku kamilika ningumu kupata hedhi.
-Maumbile ya uke kutokuwa ya kawaida,mfano kuwepo kwa utandu (hymen )husababisha damu isitoke kirahisi.
-Kushikamana kwa kuta za tumbo la uzazi.
Dalili za kukosekana kwa hedhi.
Kukosekana kwa hedhi siyo ugonjwa Bali kunaweza kuka ashiria uwepo wa tatizo Fulani kwahiyo huambatana na:
.Kuongezeka uzito au kupungua uzito kwa kiwango kikubwa.
.Kuwa na mihemuko isiyo ya kawaida.
.Ukavu katkka uke.
.Kutoka jasho wakati wa usiku.
.Kutokupata usingizi.
.Maumivu ya kichwa.
.Mabadiliko katika uonaji.
.Maumivu ya kiuno.
.Kutokwa na maziwa wakati siyo mjamzito wala hanyonyeshi.
.Kuongezeka kwa vinywelea mwilini ambavyo huashiria kuongezeka kwa vichocheo vya kiume.
Vipimo
Msichana ambae yupo katka umri wa kuvunja ungo lakini hajaanza kuona mabadilioko anashauriwa kumwona daktari.
Pia kwa mwanamke ambae alikuwa anapata hedhi kama kawaida lkn ghafla hapati kwa miezi mitatu au zaidi anashaurwa kumwona Daktari kwa uchunguzi..
.Kipimo cha kuangalia vichocheo ambazo Huchochewa na tezi ya pituitari,mfano Lh,FSH ,TSH.
.Utrasound kuchunguza Matatzo katka tumbo uzazi.
.Ct scan au MRI kuchunguza kichwa kama kinashida ktk matezi ya pituitary.
.Kupima kiwango cha prolactin kwenye damu.
.Kupima utendaji kazi wa tezi ya thyroid.
Madhara ya kukosa hedhi.
.Kushindwa kushika ujauzito (infertility).
.Udhoofu wa mifupa (osteoporosisi) kama ukosefu wa hedhi utakuwa umetokana na uzalishwaji mdogo wa kichocheo cha oestrogen.
Ufanye nini ili kuondokana na tatizo hili?
.Wale ambao tatizo la ukosefu wa hedhi limechangiwa na kuwa na msongo wa mawazo wanashauriwa kutafuta njia sahii ya kuondoa msongo wa mawazo.
.Wale ambao ni kutokana na kufanya mazoezi kupitiliza wanashauriwa wafanye mazoezi kiasi.
.Tatizo lililo tokana na kula kidogo ili kupunguza uzito wanashauriwa kula mlo kamili ili kuimarisha afya.
.Kwa wanene au uzito mkubwa wanashauriwa kujipangia ratiba sahihi ya chakula na kula chakula sahihi.
.Pia kwa watumiaji wa pombe dawa kulevya wanashauriwa waache kutumia ivyo vitu.
.Pia epuka kutumia madawa holela bila ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.
.Kwa mwenye hofu anashauriwa kuondoa hofu kwa kugundua ni kitu gani haswa kinamsababisha awe na hofu .
Mwisho
Endapo hauto pata suluhu kwa kuzingatia nini kind kiss babushka tatizo,basi usisite kwenda hospitali kuonana na wataalamu ili upate ushauri ,uchunguzi wa vipimo na kisha upate matibabu kutokana na majibu ya vipimo kwa mfano dawa au upasuaji kwasababu huenda tatizo lako limetokana na uwepo wa tatizo lingine.
No comments:
Post a Comment