Ulemavu wa akili.
Ni tatizo la kiakili ambalo hutokea kabla ya kufikisha miaka 18,tatizo hili huambatana na kupungua kwa uwezo wa kiutendaji,uwezo wa kufikiri,uwezo wa kutambua mambo,na kushindwa kukua kwa tabia kutokana na mazingira ambayo yanamzunguka hususani kushirikiana katika jamii na kushindwa kuzitumia huduma za kijamii ili kutatua matatizo yake.
Ulemavu wa akili hutambulika kwa kuangalia kiwango cha utendaji kazi wa akili na uwezo wa mtu mwenyewe kutumia ujuzi alionao ili kukabili changamoto katika mazingira yanayo mzunguka.
Kipimo cha kutambua intelligent (IQ) ya mtu( uwezo wa kiakili) hufanywa kwa kuangalia fikra na matendo ambayo anayafanya.Kwa mtu ambaye uwezo wake wa kiakili ni kawaida ni lazima fikra na matendo yake yaendane na umri wake.Kwa walemavu wa akili Mara nyingi fikra na matendo yao huwa hayaendani na umri wao wa kawaida ,kwa kawaida watu hao uwezo wao wa kiakili (IQ) huwa chini ya 70 (<70) kwa iyo mtu yeyote ambaye uwezo wake wa kiakili ni chini ya 70 basi ana ulemavu au upungufu wa akili.
Kwa kawaida watoto wenye ulemavu wa akili hatua za ukuaji wao mfano kuongea,kutembea huchelewa zaidi kuliko ambao hawana ulemavu wa akili.Dalili za ulemavu wa akili zinaweza zikaonekana wakati wa kuzaliwa au baadae na kugundulika kwake hutegemeana na kisababishi cha ulemavu,kuna baadhi ya watoto inakuwa ngumu kuwagundua kama ni walemavu wa akili lakini hugundulika kwa baadae pindi wanapo kuwa wamefikisha umri wa kuanza shule,aina hii ya watoto huwa na mapungufu katika kuongea ,mahusiano na jamii na kupata shida katika masomo au kujifunza.Kwa watoto ambao ulemavu wao umetokana na matatizo katika mishipa ya fahamu kama vile meningitis hupata shida katika utambuzi na kubadilika kutokana na mazingira.Pia kuna baadhi yao wanaweza wakapata elimu maalumu na kubahatika kupata kazi lakini changamoto kubwa inayo wa kabili ni kutokuwa na uwezo wa kuthamini kazi ambayo wamepata na matokeo yake wanaweza wakafukuzwa kazi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kujali kile walicho nacho.
Kwaiyo kwa kawaida mtu ambae umri wake wa kawaida huendana na umri wa kiakili inabid awe na uwezo wa kiakili (IQ)=100 ,lakini kwa wale wenzetu ambao Wana vipaji uwezo wao wa kiakili (IQ) ni zaidi ya 100. Vile vile kwa wale ambao Wana uwezo wa kawaida IQ yao ni chini ya 100 lakini haipungui 85.
Hivyo,
Intelligent quotent (IQ)=umri wa kiakili(mental age )×100% ÷ umri wa mtu wa kawaida (chronological age).
Soma:nini-husababisha-upungufu-wa-damuanemia.html
Makundi ya ulemavu wa akili.
.Mild mental retardation(ulemavu akili).
Kwa asilimia kubwa watu wengi wenye upungufu wa akili hupatikana katika kundi hili,kwa kawaida watu hawa huwa na kiwango Cha akili (IQ) kuanzia 50 hadi 70.
Watu hawa wanaweza wakapata elimu ya kujifunza kusoma ,kuandika ,na kufanya hesabu rahisi katika shule maalumu.Mara nyingi katika elimu yao wanaweza wakaishia darasa la sita ,pia kutokana na elimu ambayo wanakuwa wameipata wanaweza wakaishi kwa kujitegemea wenyewe lakini wanahitaji uangalizi na usaidizi katika shughuli zao hususani pale wanapo kutana na changamoto kubwa katika maisha yao ,pia ni ni ngumu Sana kuwa tambua watu katika kundi hili.
.Moderate mental retardation( ulemavu wa Kati).
Asilimia 10 tu ya ja jamii yenye ulemavu wa akili hupatikana katika kundi hili,watu hawa kwa kawaida huwa na uwezo wa akili (IQ) 35 hadi 50.Watu hawa kutokana na kutokupata elimu maalum awali watu huwatambua Kama watu ambao hawafundishiki kutokana na kuwa na mawasiliano mabovu na jamii. Pia watu hawa wanaweza wakapata mafunzo maalumu katika shule maalumu mfano, kutamka majina yao na kuzungumza maneno rahisi, maranyingi katika mafunzo yao huishia darasa la pili .Pia katika mafunzo yao hujifunza zaidi vitu ambavyo havihitaji utumiaji wa akili zaidi japo mafunzo yao huchukua muda mrefu hadi kuweza kuya mudu mfano kunawa maji,kuvaa nguo ,piga mswaki n.k ,pia watu hawa inakuwa ngumu kuwaelewa pindi wakizungumza na watu wasio wazoea,lakini kutokana na elimu ambayo wanakuwa wameipata Sasa huwa na mawasiliano mazuri na jamii na Sasa hutambulika Kama kundi lenye kuelimika. Kwa kawaida watu hawa wanahitaji msaada ,na uangalizi katika shughuli zao na maisha yao kwa ujumla.
.Severe mental retardation(ulemavu wa akili mkubwa).
Asilimia tatu hadi nne ya walemavu wa akili hupatikana katika kundi hili.Kwa kawaida watu walio katika kundi hili huwa na IQ kuanzia 20 hadi 35.Aina hii ya watu ni rahisi Sana kuwa gundua kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutambua vitu, watu hawa wanahitaji mafunzo madogo madogo katika shule maalumu, baada ya kupata mafunzo watu hawa huweza kujitegemea kidogo Sana katika shughuli zao lakini kwa asilimia kubwa huitaji usimamizi na uangalizi wa hali ya juu katika shughuli na kipindi chote Cha maisha yao.
.Profound mental retardation( ulemavu ulopitiliza).
Asilimia 1 hadi 2 ya jamii ambayo ina ulemavu wa akili hupatikana katika kundi hili.Maranyingi kundi hili huwa na uwezo wa akili (IQ) chini ya 20. Tatizo lao hutokana na kuwepo kwa Matatizo katika mishipa ya fahamu moja kwa moja,pia watu hawa wanahitaji mafunzo maalumu ili waweze kupata misingi ya huduma za kujitegemea Kama kuzungumza.Pia watu hawa wanahitaji uangalizi na usimamizi wa Hali ya juu katika shughuli zao na maisha yao yote.
Nini husababisha ulemavu wa akili?
i.Kurithi,mtoto anaweza kupata ulemavu wa akili kutoka kwa wazazi moja kwa moja, mfano Matatizo ya chromosome Kama vile fragile x syndrome,pia mabadiliko (mutatio) vinasaba yanayo weza tokea katika maisha yanaweza sababisha ulemavu wa akili mfano downsyndrome ambayo ni matokeo ya mabadiliko ya chromosome namba 21.
.Madhara kwenye ubongo.
.Matatizo ya kimetabolism mfano phenyketonuria.
ii.Matatizo yanayo tokea kabla ya mtoto kuzaliwa, mfano.
.Unywaji wa pombe katika kipindi Cha ujauzito.
.Utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji sigara.
.Magonjwa Kama vile kaswende.
.Shinikizo la damu au uwepo wa sumu kwenye damu husababisha kupungua kwa kiwango Cha damu yenye hewa safi kwenye ubongo wa mtoto ,kadiri ubongo utakavo zidi kukosa hewa ya kutosha ya oxygen ndivyo unavyozidi haribiwa.
.Matibabu ya mionzi hususani katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito,mionzi husababisha athari katika seli za ubongo wa mtoto ,matokeo yake Kuna uwezekano mtoto akaipata ulemavu baadae.
iii.Matatizo wakati wa kuzaliwa mtoto.
.Mtoto kukosa hewa ya oxygen wakati wa kuzaliwa (birth asphixia).
.Kuvuja damu kwenye ubongo.
.Uchungu kwa muda mrefu.
iii. Matatizo baada ya mtoto kuzaliwa.
.Majeraha ya kichwa.
.Uvimbe kwenye ubongo.
.Magonjwa Kama vile Uti wa mgongo na encephalitis.
iv.Sababu za kimazingira,watoto ambao Wana ishi katika mazingira magumu wapo katika hatari ya kupata utapiamlo ambao huchangia kwa kiwango kikubwa mtoto kupata ulemavu wa akili,pia mazingira ambayo ni hatarishi kiafya huchangia kwa kiwango kikubwa,vile vile watoto katika mazingira ayo hukabiliwa na tatizo hili kutokana na kucheleweshwa kupata huduma za afya pindi wanapo kuwa Wana ugua ,kuugua Mara kwa Mara bila kupata matibabu ndiko husababisha watoto kuwa na ulemavu wa akili.
Ufanye Nini ili kuwakinga watoto dhidi ya ulemavu wa akili?
.Mama hakikisha Mara baada ya kujifungua mtoto anapata chanjo dhidi ya magonjwa Kama vile surua,vile vile hakikisha pindi mtoto anapokuwa anaugua unampeleka hospitali kupata matibabu.
.Pia kwa watoto ambao wanaishi katika mazingira rafiki kwa magonjwa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi Mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya huduma zao.
.Wakina mama wajawazito Wanashauriwa kuzingatia lishe bora kwa maendeleo na afya bora ya mtoto.
.Kuacha matumizi ya pombe,madawa ya kulevya ,uvutaji sigara katika kipindi Cha ujauzito ,vile vile wanashauriwa kupata matibabu pindi wanapohisi wanaugua magonjwa mfano magonjwa ya zinaa Kama vile kaswende.
.Pia wazazi wanashauriwa pindi mtoto anapogundulika kuwa na ulemavu wa akili apelekwe kwenye vituo maalumu vya kutoa elimu ili apewe mafunzo ya kujitegemea japo katika shughuli ndogo ndogo mfano kuvaa nguo,kula,kujifunza lugha ili kupunguza ukubwa wa tatizo.
Home »
» Chanzo cha ulemavu was akili/upungufu wa akili.
No comments:
Post a Comment