Home »
» Nini husababisha upungufu wa damu(anemia)?
Nini husababisha upungufu wa damu(anemia)?
Anemia
Ni jina kwa ujumla ambalo humaanisha upungufu wa chembe chembe nyekundu za damu katika mzunguko wake au kupungua kwa uwingi wa haemoglobin mwilini kutokana na sababu mbalimbali.
Mwili wa binadamu hutengeneza seli mbalimbali ambazo hufanya kazi mbali mbali mwilini,mfano wa seli izo ni chembechembe nyeupe za damu ambazo huulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa, seli sahani ambazo husaidia kugandisha damu na chembechembe nyekundu za damu.
Chembechembe nyekundu za damu zina haemoglobin ambayo huipa damu rangi nyekundu,kazi kubwa ya haemoglobin ni kuzisaidia chembechembe nyekundu za damu kubeba hewa ya oxygen kutoka kwenye mapafu hadi sehemu mbalimbali za mwili na kubeba hewa ya carbondioxide kutoka sehemu mbalimbali za mwili hadi kwenye mapafu ili ipate hewa safi tena.
Kwa kawaida kiwango Cha damu hutofautiana baina ya mtu na mtu pamoja na jinsia.Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni mtu akiwa na damu chini ya viwango tajwa hapo chini basi mtu huyu huesabika anaupungufu wa damu kwa wanaume chini ya 13g/dl,kwa wanawake chini ya 12g/dl, kwa wajawazito na watoto chini ya 11g/dl.
Soma;mambo-ambayo-huatarisha-figo-yako.html
Nini husababisha upungufu wa damu mwilini?
Upungufu wa damu hutokea Kama damu haitokuwa na chembechembe nyekundu za damu au hemoglobin ya kutosha na husababishwa na Mambo ya fuatayo:
.Mwili wenyewe kuvunja vunja chembe chembe nyekundu za damu,Hali hi kitaalamu huitwa haemolytic anemia (upungufu wa damu unaosababishwa na kuvunjika kwa seli nyekundu za damu). Hali hii mtu anaweza akaipata kwa kurithi au katika maisha ya baadae kutokana na mabadiliko ambayo yanaweza yakajitokeza mwilini. Pia Hali hii inaweza ikachangiwa na magonjwa mbali mbali Kama vile malaria na saratani ya damu (lukemia). Vile vile inaweza ikatokana na chembe chembe nyekundu za damu kuwa na umbile ambalo siyo la kawaida kitaalamu huitwa sickle cell (seli mundu),pindi mtu anavyo kuwa na aina hii ya chembechembe yekundu za damu hukabiliwa na upungufu wa damu Mara kwa Mara kutokana na seli hizo kuharibiwa kirahisi na kufa mapema.
.Kutokwa na damu ambako husababisha mwili kupoteza damu kuliko kuzalisha damu. Hali hiyo huweza kusababishwa na vitu mbalimbali, mfano ajali,uzazi,(kupoteza damu kabla na baada ya kujifungua).
.Mwili wenyewe hushindwa kuzalisha chembe chembe nyekundu za damu.Hii inaweza ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini,damu hutengenezwa kwenye uroto mwekundu (red bone marrow) ambazo hupatikana ndani ya mifupa, kwa hiyo ili damu itengenezwe madini ya chima yanahitajika Zaid, hivyo upungufu wa madini hayo husababisha uzaoishaji wa damu kupungua.Pia hali hii inaweza sababishwa na uwepo wa minyoo mwilini,upungufu wa vitamini B12, upungufu wa folic na magonjwa sugu Kama vile; Saratani, HIV/AIDS, magonjwa sugu ya figo.
Dalili za upungufu wa damu:
Mara nyingi dalili hutofautiana kulingana na visababishi mbalimbali vya upungufu huo wa damu. Dalili hizo ni Kama;
.Manjano,kutokana na kuongezeka kwa uharibifu wa chembechembe nyekundu za damu.
.Uchovu.
.Kushindwa kupumua vizuri baada ya kazi ngumu au mazoezi.
.Mapigo ya moyo kwenda haraka.
.Moyo Kushindwa kufanya kazi endapo upungufu wa damu ni mkubwa nayo hupelekea mgonjwa kuvimba miguu na Kushindwa kupumua.
Athali za upungufu wa damu:
Tatizo la upungufu wa damu lisipopatiwa ufumbuzi huleta madhara mengi, Kama vile;
.Matatizo ya mimba,mfano mtoto kuzaliwa kabla ya wakati kutokana na ukosefu wa folic acid, pia kifo kwa mama mjamzito Kama upungufu huo utakuwa ni kwa kiasi kikubwa wakati wa kujifungua.
.Matatizo ya moyo,upungufu wa damu husababisha Mapigo ya Moyo kwenda Kasi bila mpangilio maalum, pia moyo Kushindwa kufanya kazi au kuongezeka ukubwa, kwa sababu upungufu wa damu husababisha moyo kufanya kazi ya ziada ya kusukuma damu.
.Matatizo ya Figo.
.Kifo, upungufu wa damu utokanao na sababu za kurithi mfano,seli mundu,pindi zinapotokea husababisha madhara ambayo huatarisha maisha na wakati mwingine kifo.
Nini ufanye ili kujikinga dhidi ya upungufu wa damu?
.Hakikisha unapata tiba dhidi ya ugonjwa wa malaria Mara tu baada ya kugundulika nao.
.Hakikisha unapata tiba dhidi ya minyoo.
.Hakikisha unapata lishe Bora ambayo ina vitamin ya kutosha pamoja na virutubisho vingine mfano matunda,mboga za majani, nyama na vingnevyo.
.Epuka matumizi ya chemical na dawa zenye kuleta athari sehemu za mifupa ambazo ndo msingi mkubwa was utengenezaji wa damu.
.Pia wakina mama wajawazito wanashauriwa kuhudhuria kliniki mapema na katika Kila udhurio ili wafanyiwe uchunguzi na endapo watabainika wana malaria,minyoo au upungufu wa damu wapate matibabu ili kuondoa athari ambayo inaweza ikajitokeza baadae.
.Vile vile wakina mama wanashauriwa kutumia njia za upangaji uzazi ili kuhakikisha wanakuwa na afya Bora kabla ya kuamua kuzaa kwa Mara nyingine kwa sababu kuzaa bila mpango ni miongoni mwa vihatarishi ambavyo husababisha upungufu wa damu.
No comments:
Post a Comment