Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Kwanini unashauriwa mnyonyesha mtoto miez sita ya mwanzo bila kumchanganyia chakula?


Umuhimu wa maziwa ya mama 

Maziwa ya mama ni sawa na kimiminika cha dhahabu,maziwa ya mwanzo hutoka katika kiwango kidogo lakini kiwango hiki ni sahihi kabisa kwa mtoto ambaye amezaliwa,pia maziwa haya hutoka kwa kiwango kikubwa siku kadhaa baadae kutokana na kunyonyesha mara kwa mara pia kutokana na aina ya chakula ambacho mama atakula (balance diet) na ulaji wa mara kwa mara.Maziwa ya mwanzo huwa yana asili ya kujata na huwa ya njano japo mwonekano wake ni tofauti lakini ndiyo chakula sahihi kwa afya bora na ukuaji wa mtoto ambae amezaliwa.Unyonyeshaji pia unafaida kwa mama pamoja na mwanae.

Kuna baadhi ya akina mama kutokana na uelewa mdogo wa umuhimu wa maziwa haya ya mwanzo kwa mtoto ,hukamua maziwa haya na kuyamwaga au kuyatupa kutokana na maziwa haya ya mwanzo kuwa na mwonekano tofauti na maziwa ambayo akina mama wengi wameyazoea.

Maziwa haya yana virutubisho muhimu vilivyotengenezwa kutoka katika mwili wa mama yake kwa ajili ya ukuaji ,maendeleo na kumkinga mtoto dhidi ya vimelea vya magonjwa kipindi kinga zake za mwili zinapokuwa zinatengenezwa au kuandaliwa,kwahiyo usimwage au kutupa maziwa hayo kwakuwa yanamwonekano ulio tofauti kwani kwa kutupa maziwa hayo unamkosesha mtoto virutubisho muhimu hivyo kusababisha ukuaji wake uwe duni na iwe rahisi kushambuliwa na vimelea vya magonjwa kama vichomi,kuhara nakadhalika.



Umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.

.Maziwa ya mama yanavirutubisho vyote kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto.

.Maziwa ya mama huyeyuka kwa urahisi zaidi tumboni mwa mtoto  hivyo hutumika kwa urahisi zaidi mwilini ukilinganisha na maziwa ambayo siyo ya asili.

.Husaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya mama na mwanae au husaidia kujenga ukaribu zaidi na mwanae.

.Maziwa ya mama yana kinga za mwili ambazo humkinga mtoto dhidi ya vimelea vya magonjwa.

.Pia unyonyeshaji husaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo vya watoto
 Walio chini ya miaka mitano kutokana na kupatwa na utapia mlo (malnutrition).

.Maziwa hupunguza uwezekano wa mtoto kuwa na uzito mkubwa akiwa bado mtoto na katika ukubwa wake.

.Maziwa huongeza uwezo wa kufikiri,kutokana na utafiti ulio fanyea imebainika kwamba watoto ambao hunyonya maziwa ya mama  ndani ya miezi sita ya mwanzo bila kuchanganyiwa chakula kingine wanauwezo mkubwa wa kiakili ukilinganisha na wale ambao hawajanyonya maziwa ya mama.



Umuhimu wa unyonyeshaji kwa mama.

.Maziwa ya mama hupatikana kwa urahisi zaidi kwaiyo hupunguza gharama na hutumika muda wowote mtoto anapoyahitaji.

.Maziwa ya mama siyo rahisi kuharibika katika ziwa la mama,pia katika joto la kawaida ya kikamuliwa yanauwezo wa kukaa masaa sita hadi masaa nane bila ya kuharibika  pia katika jokofu hukaa hadi masaa sabini na mbili bila  ya kuharibika.

.Maziwa ya mama hayahitaji maandalizi katika upatikanaji wake pia ni safi na salama kwa afya bora na ukuaji wa mtoto.

.Unyonyeshaji hupunguza uwezekano wa mama kupata saratani ya titi na shingo ya kizazi.

.Unyonyeshaji hupunguza uwezekano wa mama kupata mimba nyingine katika miezi sita ya awali endapo mama atanyonyesha kwa usahihi bila kupata hedhi.

.Unyonyeshaji husaidia kumuondoa mama na msongo wa mawazo.

.Unyonyeshaji husaidia mama apate muda wa kupumzika pamoja na mwanae.

.Unyonyeshaji husaidia kupunguza uzito wa mama endapo kipindi cha ujauzito aliongezeka uzito.

.Unyonyeshaji husaidia kutambua hali ambayo siyo ya kawaida  kwa mtoto hivyo humsaidia mama kuchukua maamuzi sahihi katika muda sahihi wa kumpeleka mtoto kupata matibabu.

.Husaidia kupunguza kiwango cha upotevu wa damu kutoka kwa mama kutokana na uwepo wa kichocheo cha oxytocin ambacho huzalishwa zaidi katika kipindi cha uchungu na kipindi cha unyonyeshaji hali ambayo husababisha tumbo la uzazi kurudi taratibu katika hali ya kawaida.



Mambo ya msingi ya kuzingatia katika unyonyeshaji.

Wakina mama wengi hujikuta wanafanya makosa kadha wa kadha wakiwa  wananyonyesha kwa kujua kwamba wanafanya makosa au kwa kutokujua kama wanakosea kwa kufanya ivyo.Makosa ayo yanaweza yaka msababishia shida mtoto hapo hapo wakati unamnyonyesha au yakajitokeza miezi kadhaa baadae au kabla ya kufikisha miaka mitano na pengine hata baadae katika utuuzima,kwaiyo ili kuepuka adha ambazo zinaweza jitokeza baadae ni vema mama akazingatia mambo yafuatayo.


.Kwanza kabisa hakikisha mtoto wako ananyonya mara tu baada ya kujifungua au ndani ya saa moja mara baada ya kujifungua.

.Hakikisha mtoto ananyonya ndani ya miezi sita ya mwanzo bila ya kumchanganyia kitu chochote ,mara baada ya kutimiza miezi sita waweza mchanganyia lakini endelea kumnyonyesha mtoto hadi atimize miaka miwili.

.Hakikisha humwagi maziwa ya mwanzo,kwasababu maziwa haya yanakiwango kikubwa cha protini na kinga mwili ambazo ni muhimu kwa ukuaji ,afya bora na kumlinda mtoto dhidi ya vimelea vya magonjwa.

.Hakikisha una keti kwa hali nzuri unavyo kuwa unanyonyesha.

.Hakikisha unamshika mtoto vizuri  pindi unamnyonyesha,hakikisha mkono mmoja unashika kichwa cha mtoto na vidole vinne vya mkono mwingine vinashika  sehemu ya chini ya ziwa la mama wakati kidole kimoja kinakuwa  sehemu ya juu ya ziwa la mama hii husaidia mtoto kuiingiza vizuri chuchu ya mama mdomoni ivyo kumfanya mtoto anyonye vizuri, wakina mama ambao hawa tumii njia hii husababisha mtoto kuvuta hewa wakati ananyonya ivyo kusababisha mtoto kucheua au kutapika muda mfupi baada ya kumaliza kunyonya.

.Pia epuka kunyonyesha mtoto ukiwa umejilaza,unyonyeshaji huu unaweza ukatumika kama haujasinzia.

.Ili mtoto aweze kupata virutubisho vya msingi kutoka kwa mama ,mama inabdi ahakikishe anammyonyesha mtoto ziwa moja hadi liishe ndipo amnyonyeshe katika ziwa lingine.


Karibu tukushauri


Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts