Home »
» Jikinge na ugonjwa wa fangasi sehemu za siri(vagina candidiasis)
Jikinge na ugonjwa wa fangasi sehemu za siri(vagina candidiasis)
Vagina candidiasis
Maambukizi ya fangasi sehemu za siri husababishwa na uwepo wa fangasi wajulikanao kama candida albicans,fangasi hawa katika miili ya binadamu hupatikana sehemu mbali mbali ikiwemo mdomoni, sehemu za siri(uume na uke) ,kwenye kibofu cha mkojo na sehemu zinginezo. Kutokana na kuwepo kwa bacteria walinzi katika miili yetu na uimara wa kinga za miili husababisha tusipatwe na magonjwa haya ya fangasi.
Fangasi jamii ya candida albicans huishi sehemu tofauti tofauti ya miili yetu bila kuleta athar au madhara yoyote, lakini wadudu hawa huleta athari au madhara katika miili yetu pindi tu mazingira yao yanapobadilishwa kutokana na sababu mbali mbali mfano mabadiliko ya ph katika uke, kushuka kwa kinga za mwili kutokana na magonjwa mbali mbali, matumizi ya muda mrefu wa madawa ya ant biotics n.k.
Vihatarishi vya fangasi kwa wanawake.
Watu ambao wapo katika hatari kubwa ya kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi ni pamoja na.
.Watu wenye upungufu wa kinga za mwili ambao umesababishwa na magonjwa sugu mfano saratani.
.Watu wenye ugonjwa wa Ukimwi.
.Watu wavaao mavazi ambayo huleta joto sehemu za siri kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na nguo za kuogelea, chupi zinazobana sana.
.Kufanya ngono kinyume na maumbile (haja kubwa) kisha kufanya katika njia ya kawaida jambo ambalo husababisha wadudu hao kubadilishiwa mazingira yao ya asili ambayo hupatikana na kuleta athari.
.Wanawake katika umri wa hedhi wapo katika hatari kubwa ya kupata fangasi kuliko ambao hawajaanza na wale ambao hedhi imefika tamati.
.Kuwa na msongo wa mawazo ulio pitiliza..
.Wanawake ambao ni wagumba wanaweza kupata fangasi kutokana na mihangaiko ya matibabu ya kutaka kubeba mimba.
.Matibabu ya vichocheo(homone replacement therapy )kutokana na sababu mbalimbali.
.Matumizi ya vifaa vya kusafishia uke kwa kutumia maji ambayo yamechanganywa na ant septic jambo ambalo husababisha kuua bacteria walinzi na kubadili mazingira ya sehemu husika na kufanya kuwa katika hatari ya kupata fangasi.
.Matumizi ya dawa za ant biotic na steroid kwa muda mrefu, matumizi ya dawa za ant biotic kwa muda mrefu mfano zile ambazo zina uwezo wa kuua aina zaidi ya moja za bacteria(broad spectrum antibiotics) dawa hizi husababisha kuuawa kwa bacteria walinzi jambo ambalo husababisha fangasi kuleta athari.
Vihatarishi vya fangasi kwa wanaume.
.Matumizi ya dawa ant biotcs na steroids kwa muda mrefu.
.Upungufu wa kinga mwilini.
.Ugonjwa wa Ukimwi.
.Magonjwa sugu mfano saratani n. k.
.Kujamiiana na mwanamke mwenye maambukizi ya fangasi.
Je, mwanamke atatambuaje amepata fangasi
Mwanamke anaweza kutambua au kuhisi amepata maambukizi ya fangasi endapo ataona dalili au ishara zifuatazo.
.Mwanamke mwenye fangasi hupata muwasho sehemu za siri.
.Kuhisi kuungua au kuwaka moto katika sehemu za siri.
.Pia hupata maumivu wakati wa kujamiiana na mwenza wake.
.Mashavu ya nje ya uke huvimba na kuwa na rangi nyekundu.
.Mwanamke hutokwa na uchafu mweupe au mweupe kijivu, uchafu huu waweza kuwa mwepesi au mzito ambao hufanana na jibini,pia uchafu huu huambatana na harufu yeyote isipo kuwa panapokuwepo na tatizo lingine kama magonjwa ya zinaa.
Je, mwanaume atajuaje amepata maambukizi ya fangasi?
Mwanaume anaweza hisi amepata maambukizi ya fangasi kama ataona ishara au dalili zifuatazo.
.Muwasho katika sehemu za siri.
.Uwepo wa vidonda kwenye uume.
.Kutokwa na uchafu sehemu ya juu ya uume.
.Ncha ya uume huvimba na kuwa na rangi nyekundu.
Soma,zijue-dalili-za-ujauzito.html
Matibabu ya maambukizi ya fangasi.
Maambukizi ya fangasi hutibika kwakutumia dawa za kutibu fangas(ant fungal drugs) kama vile dawa za kupaka kama vile cotrimazole, nystatin, fluconazole au ketokonazole.
Wenye maambukizi ambayo siyo makali wanaweza tumia dawa za kupaka kutoka katika dawa za fangasi jamii ya azole mfano wa dawa hizo ni, cotrimazole, muconazole n. k, dawa hizi hutumika kwa muda wa siku tatu hadi saba kutegemeana na aina ya dawa,pia mgonjwa anashauriwa kupaka dawa hizi maeneo jirani na uke na ndani ya uke akianza mbele kuelekea nyuma. Pia mgonjwa anaweza akapewa dawa za kuingiza ukeni ambazo atalazimika kutumia kwa muda wa siku tatu hadi kumi na nne dawa hizo ni pamoja na muconazole, terconazole, nystatin n. k.
Kwa wale ambao wana maambukizi makali kabla ya kupewa matibabu inashauriwa kufanyiwa kipimo cha kuotesha uchafu kutoka ukeni ili kujua ni aina gani ya fangasi wamesababisha maambukizi, mana yawezekana maambukizi yakawa yamesababishwa na aina nyingine ya fangas ajulikanaye kama candida glabrata licha ya kuwa msababishi zaidi ni candida albicans. Kama maambukizi yamesababishwa na candida glabrata ni ngumu kutibu kwa kutumia dawa za kawaida ivyo basi dawa mbadala zitahitajika. Wagonjwa jamii hii hutumia dawa za kupaka na vingine kuingiza ukeni kwa muda wa siku saba hadi kumi na nne au dawa ya fluconazole.
Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya fangasi.
.Epuka matumizi ya mara kwa mara ya nguo za kubana ambazo huleta joto.
.Epuka matumizi holela ya ant biotics na steroids kwa muda mrefu bila kupata ushauri kwa wataalamu.
.Epuka kufanya mapenzi na mpenzi ambaye tayari ana maambukizi ya fangasi.
.Tumia pedi pindi tu upatapo hedhi.
.Safisha sehemu zako za siri kwa kutumia kitambaa na maji safi kuanzia mbele kwenda nyuma.
.Vaa chupi ambazo zimetengenezwa kwa pamba pia hazibani sana.
.Badilisha nguo za ndani mara tu zipatapo unyevu.
.Kama wewe ni mtumiaji wa vifaa ngono na uzazi mpango mfano diaphram osha vifaa vyako vizuri baada ya kuvitumia ili kuepuka kupata maambukizi tena.
.Punguza msongo wa mawazo
.Hakikisha kila unapo kula unapata chakula chenye virutubisho aina zote.
.Epuka utumiaji wa maji ya moto.
.Epuka kufanya ngono kinyume na maumbile kisha kurudia kufanya katika njia ta kawaida.
.Epuka matumizi yoyote ya maji yenye mchanganyiko na ant septic yoyote kusafisha uke wako.
No comments:
Post a Comment