KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO.
Kupanga uzazi hujumuisha Mambo mengi ndani yake siyo tu kuzuia mwanamke asipate mimba zisizo tarajiwa Bali hata kujua idadi na jinsia ya watoto ambao wanahitajika katika familia.
Familia nyingi hutamani Sana kupata jinsia fulani ya mtoto kutokana na uhitaji wao, kushindwa kupata aina ya mtoto ambaye wanamuhitaji husababisha kuendelea kujaribu bahati hadi kupata mtoto wanaye muhitaji wakati mwingine kushindwa kupata kadiri ya mahitaji yao hivyo kusababisha kuzaa watoto wengi kuliko idadi iliyokuwa inahitajika au kuongezeka kwa ukubwa wa familia.
Pia kukosekana kwa mtoto anayehitajika huweza leta ugomvi mkubwa katika familia na pengine Kuvunjika kwa mahusiano au ndoa au kutoka nje ya mahusiano ili kujaribu kutafuta mtoto anae hitajika.
Njia ya kupata mtoto wa kiume/kike.
Kwanza kabisa ili mimba iweze kutungwa nilazima wenza wawe na afya njema,pia mbegu ya kiume iwe na uwezo na ubora unao kidhi kutungisha mimba.
Njia ya kalenda ni njia ambayo haina gharama katika kuamua jinsia ya mtoto ambaye anakuwa amechaguliwa kuzaliwa bali ili kuhakikisha jambo linafanikiwa, wahusika wanatakiwa kuwa makini Sana na ufuatiliaji wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke,Kutokuwa makini katika ufuatiliaji wa mzunguko wa hedhi kutasababisha kupata matokeo hasi au kupata mtoto jinsia tofauti na iliyopangwa.
Kwa kawaida mwanamke huzalisha mbegu za aina moja yaani "XX" ,lakini mwanaume huzalisha mbegu aina mbili ambazo ni "X" (mbegu ya kike) na "Y" (mbegu ya kiume).
Kwaiyo endapo mbegu ya kike "X" itarutubishwa na mbegu "X" ya mwanaume na kutengeneza muunganiko wa "XX" hapo mimba ya mtoto wa kike itakuwa imetungwa au mtoto atakae tarajiwa kuzaliwa ni jinsia ya kike. Pia endapo yai la kike "X" litarutubishwa na mbegu ya kiume"Y" na kutengeneza muunganiko wa "XY" hapo mtoto atakaye zaliwa atakuwa ni wakiume.
Pia mbegu ya kike (X) inayotolewa na mwanaume ni imara zaidi kuliko mbegu ya kiume(Y) mbegu X huelezwa huweza kukaa masaa sabini na mbili sawa na siku tatu bila kufa tangu kutolewa kwake,Pia huogelea kwa mwendo mdogo zaidi kuliko mbegu(Y) hivyo kuchelewa kulifikia yai zaidi.
Mbegu ya kiume Y siyo imara Sana Kama ilivyo mbegu X mbegu hii huelezwa huweza kukaa kwa masaa arobaini na nane tu toka kutolewa kwake,pia mbegu hii huogelea kwa kasi kubwa kuliko mbegu ya kike ivo kuwahi kulifikia yai mapema zaidi.
Kwaiyo ili kupata mtoto wa kiume au wa kike ni vema kufatilia kwa makini mzunguko wa hedhi wa mwenza wako.
Kuna baadhi ya watu hufikiri kufanya ngono katika siku ya kumi na nne tangu kuanza kwa hedhi ndiko husababisha kupatikana kwa mtoto wa kiume hivyo wengi kujaribu kufanya ivo bila kupata matokeo wanayo hitaji na pengine hata mimba yenyewe isitungwe.
Kitu Cha Kwanza kabisa ni lazima kuhakikisha unaujua vema mzunguko wa hedhi wa mwenza wako kwa sababu mizunguko ya hedhi haifanani kwa wanawake wote bali hutofautiana Kati ya mwanamke na mwanamke.
Kuna wanawake ambao hupata hedhi Kila baada ya siku ishirini na moja ,mzunguko huu hufahamika Kama mzunguko mfupi, pia katika mzunguko huu yai la mwanamke huachiliwa katika siku ya kumi toka kuanza kwa hedhi.
Wanawake wengine hupata hedhi Kila baada ya siku ishirini na nane ,mzunguko huu hufahamika Kama mzunguko wa hedhi wa kawaida,katika mzunguko huu yai huachiliwa siku ya kumi na nne tangu kuanza kwa hedhi.
Vile vile kuna wanawake ambao hupata hedhi Kila baada ya siku thelathini na tano, mzunguko huu hufahamika Kama mzunguko mrefu,katika mzunguko huu yai huachiliwa katika siku ya kumi na saba ya mzunguko tangu kuanza kwa hedhi.
Kwahiyo Kama wenza wanataka kupata mtoto wa kiume hulazimika kushiriki tendo la ndoa siku moja kabla ya kuachiliwa kwa yai,siku ya kuachiliwa yai yenyewe au baada ya yai kuachiliwa kwasababu endapo tendo litafanyika siku kadhaa kabla ya kuachiliwa yai mbegu ya kiume itakufa na kubaki mbegu ya kike.
Pia kwa wenza ambao wanahitaji kupata mtoto wa kike ni lazima washiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kuachiliwa,hii ikasababisha mbegu ya kiume(Y) kufa mapema zaidi hivyo mbegu X kulirutubisha yai .
KARIBU TUKUSHAURI.
0753891441/0712106789

No comments:
Post a Comment