Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Kupevuka kwa mayai(ovulation) .



Kupevuka mayai(Ovulation) ni nini?

Ni kujiachia kwa yai au mayai kutoka kwenye moja kati ya vifuko vya mayai (ovari).Kupevuka kwa mayai hutokea katikati mwa mzunguko wa hedhi wa mwanamke,mayai huachiliwa katika Kila mzunguko, mayai hayo yaweza tolewa katika kifuko kimoja au katika mifuko yote kwa kuwa hakuna mpangilio maalumu wa utolewaji wa mayai.

Katikati ya mzunguko wa hedhi yai ambalo limekomaa huachiliwa kutoka katika kifuko Cha mayai na kusafiri kupitia mirija ya falopia ambapo ndipo utungwaji wa mimba hufanyika,mirija ya falopia huunganisha vifuko vya mayai na mji wa mimba.


Je mayai hupevuka lini na siku gani nipo katika hatari ya kushika mimba?

Mayai hupevuka kulingana na Jinsi mzunguko wako ulivyo na ikumbukwe mzunguko wa hedhi hutofautiana Kati ya mwanamke na mwanamke,michoro mingi inayosambazwa mitandaoni kuhusu upevushaji wa mayai huonesha aina moja ya mzunguko wa hedhi ambao ni Kila baada ya siku ishirini na nane,hii husababisha wanawake wenye mizunguko tofauti na huo unao onyeshwa kushindwa kujua tarehe sahihi ya yai kuachiliwa katika mizunguko yao,hivyo kupata shida katika suala la utungishaji wa mimba kutokana na kukosekana kwa taarifa ambazo ni sahihi.Kwa kawaida wanawake wana mizunguko mikuu mitatu.

Mzunguko mfupi,huu ni mzunguko ambao hutokea Kila baada ya siku ishirini na moja, Katika mzunguko huu yai huachiliwa katikati ya mzunguko wake toka kuanza kwa hedhi yani siku ya kumi,kwaiyo Kama wenza wamepanga kupata mtoto ni vema wakafanya tendo la ndoa siku tatu au mbili kabla ya kuachiliwa kwa yai au siku ya kuachiliwa yai,hii ni kwa wale tu ambao wana mzunguko wa siku ishirini na moja.

Mzunguko wa kawaida,huu ni mzunguko ambao hutokea Kila baada ya siku ishirini na nane,huu ni mzunguko ambao umezoeleka na watu wengi ,pia mzunguko huu umekuwa ukienea Sana mitandaoni. Katika mzunguko huu yai hupevuka au huachiliwa katikati ya mzunguko toka kuanza kwa hedhi ambayo ni siku ya kumi na nne,Kwahiyo Kama wenza wanataka kupata mtoto basi ili mimba ipate kutungwa ni vema wakashiriki tendo la ndoa siku ya kumi na nne au siku tatu au mbili kabla ya kuachiliwa kwa yai.

Mzunguko mrefu,huu nimzunguko ambao hutokea Kila baada ya siku thelathini na tano,katika mzunguko huu yai huachiliwa siku ya kumi na saba ya mzunguko tangu kuanza kwa hedhi,pia kwa mwanamke ambae ana aina hii ya mzunguko na anahitaji kushika ni vema akashiriki tendo la ndoa katika siku ya kumi na saba ya mzunguko au siku tatu au mbili kabla ya kupevuka au kuachiliwa kwa yai.



Je nitajuaje Kama yai limepevuka?

Ili zoezi la utungaji mimba liweze kukamilika ni lazima mwanamke afuatilie vizuri mzunguko wake wa hedhi na ajue mabadiliko ya mwili ambayo huanza kutokea siku kabla ya kupevuka kwa yai, mabadiliko hayo huashiria kufunguliwa kwa dirisha la uzazi kwahiyo Kama wenza walikuwa wana hitaji kupata mtoto basi muda unakuwa umewadia Sasa.

Mabadiliko ya ute kwenye mlango wa uzazi, wakati yai linapevuka mwili hutengeneza zaidi kichocheo Cha oestrogen, kichocheo hiki husaidia ute uwe wenye kuteleza na kuvutika pia ute unaokuwepo wakati wa kupevuka kwa yai unakuwa hauna rangi ,kazi kubwa ya ute huu ni kusaidia mbegu za  kiume kuogelea kirahisi kuelekea kulirutubisha yai katika mirija ya fallopia,kwaiyo uonapo ute umebadilika basi tambua ni dirisha la uzazi.

Maumivu ya tumbo,ni wanawake wachache ambao huhisi maumivu wakati yai linakaribia pevuka au linapevuka, unaweza ukahisi moja ya pande ambao kifuko Cha mayai kinakaa,Mara nyingi maumivu hayo huvuta na kuachia.

Kuongezeka kwa hamu ya kutaka kufanya tendo la ndoa,hii nayo ni dalili moja wapo ya kuachiliwa kwa yai,katika wakati huu mwonekano wa mwanamke hubadirika na kuonekana wa tofauti  ,mfano kupenda kupaka manukato ambayo yanaweza shawishi mwanaume.

Kuongezeka kwa joto la mwili pia huashiria yai limepevuka au kuachiliwa.



Kwa wale wanaohitaji kupata mtoto ni vema wakakitumia vizuri kipindi hiki kwa kujaribu kufanya tendo la ndoa  Mara kwa Mara  Sababu kadiri unavyofanya ngono katika dirisha la uzazi ndivyo uwezekano wa kutungisha mimba unavyokuwa mkubwa.



KARIBU TUKUSHAURI
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts