KUVIMBA MIGUU WAKATI WA UJAUZITO.
Wajawazito wengi hukumbwa na tatizo la kuvimba miguu kutokana na sababu mbali mbali, mabadiliko ya homoni huelezwa kuchangia mabadiliko ya utendaji kazi wa mwili hii ni pamoja na mwili kuhifadhi madini ya sodium badala ya kutolewa nje.
Kuvimba miguu inaweza kuwa ni hali ya kawaida wakati waujauzito pia kunaweza kuashiria hali ya hatari Kama kuta ambatana na dalili za magonjwa mengine, uvimbe hutokea zaidi sehemu za miguu lakini wakati mwingine hata mikono. Kuvimba miguu huelezwa hutokea zaidi katika miezi ya mwisho ya mimba.
Nini husababisha kuvimba miguu?
Kuna sababu mbalimbali ambazo huelezwa kuchangia miguu kuvimba wakati wa ujauzito,sababu hizo ni Kama ifuatavyo:
Kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto, Kadiri ukubwa wa mtoto unavyozidi kuongezeka husababisha mkandamizo kwenye mishipa inayorudisha damu kwenye moyo kutoka sehemu za chini za mwili (vein) ikiwemo vena cava,pia mishipa inayobeba maji damu (lymph),hali hii husababisha damu kushindwa kurudi kwenye moyo na kukusanyika sehemu za miguu.
Magonjwa, magonjwa pia yaweza ikawa ni sababu ya kuvimba miguu na sehemu zingine za mwili wakati wa ujauzito, magonjwa hayo ni pamoja na:
.Shinikizola damu wakati wa ujauzito(pre eclampsia) kupanda kwa shinikizo la damu huleta athari kwenye figo hivyo kusababisha uwepo wa protini kwenye mkojo.
.Magonjwa ya figo.
.Magonjwa ya moyo mfano moyo kushindwa kufanya kazi vzuri husababisha maji na damu kukusanyika sehemu mbalimbali za mwili.
.Magonjwa ya ini husababisha maji kujaa katika ukuta wa mbele wa tumbo na hata mwili mzima.
Vihatarishi vinavyoweza sababisha kuvimba miguu.
Mambo mbalimbali hutaja kuchangia kuvimba kwa miguu wakati wa ujauzito, mambo hayo ni pamoja na:
.Kusimama kwa Muda mrefu bila kukaa.
.Kutumia kiwango kikubwa Cha madini ya sodium au chunvi, chunvi husababisha maji kubakizwa ndani ya mwili badala ya kutolewa nje.
.Matumizi ya chakula ambacho kina kiwango kidogo Cha potassium.
.Kufanya kazi kwa Muda mrefu wakati wa mchana bila kupumzika kazini au nyumbani.
Nini Cha kufanya ili kuondoa au kupunguza uvimbe ?
Kuna Mambo mbalimbali ambavyo hushauriwa kufanya ili kuondoa au kupunguza uvimbe wakati wa ujauzito, Mambo hayo ni:
.Epuka Kusimama Muda mrefu.
.Wakati wa kupumzika inua miguu yako kwa pillow ili kusaidia damu na maji yaliyo kusanyika kurudi kwenye moyo.
.Punguza Matumizi ya chunvi kwa kiwango kikubwa kwasababu chunvi hubakisha maji mwilini.
.Hakikisha unafanya mazoezi ili kungeza mzunguko wa damu mwilini mfano mazoezi ya kutembea.
.Kanda kwa maji ya moto sehemu zenye kuvimba.
.Hakikisha unakula chakula chenye kiwango Cha madini ya potassium ya kutosha mfano ndizi ,viazi n.k
.Usivae nguo zinazo bana Sana kwasababu nguo zinazo bana huzunguka kasi ya damu kurudi kwenye moyo ivyo kusababisha damu kukusanyika.
.Hakikisha unakunywa maji mengi,wakati mwingine figo hulazimika kuhifadhi maji kutokana na kutokujitosheleza kwa maji mwilini kwahiyo ukinywa maji mengi maji hujitosheleza hivo kuruhusu maji ya ziada kutolewa nje.
Ushauri
Kuvimba miguu pia kwa weza kuwa ni dalili mbaya ya ujauzito Kama kutakuwa kumesababishwa na magonjwa,kwahiyo ni vema kujichunguza mara kwa Mara na endapo utaona baada ya Muda uvimbe haujatoweka Ni vema kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.
KARIBU TUKUSHAURI.
0753891441/0712106789

No comments:
Post a Comment