Uzazi wa mpango.
Wanawake wengi wamekuwa wakipata mimba bila ya kutarajia kutoka kwa wanaume ambao siyo waume zao au michepuko au kwa kufanyiwa matukio ambayo katika jamii hayakubaliki Kama kubakwa na wengine hupata kutokana na ugumu wa maisha ili waweze kujipatia mahitaji yao.
Kutokana na kupata mimba bila ya kutarajia wengi wao wamejikuta wakiingia katika dhambi ya mauaji ili kunusuru mahusiano yao na wenza ambao wana wapenda na wengine hutenda dhambi ili kuhakikisha malengo waliyo jiwekea katika maisha yao yanatimia.
Licha ya kufanya ivyo ili kutimiza malengo yao wanasahau kwamba utoaji wa mimba unaweza ukawa na madhara makubwa katika afya zao ikiwemo kupoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi, kupoteza kizazi na pengine kushindwa tena kutimiza malengo endapo wakibainika kutokana na kushtakiwa na serikali,mbaya zaidi utoaji mimba husababisha kupungua kwa ukaribu baina yao na muumba wetu.
Kutokana na chunguzi mbalimbali huonesha wahanga wakubwa wa utoaji mimba ni wanawake ambao hawajaolewa na wamekuwa wakifanya ivo ili wapate kuolewa baadae,wanafunzi nao wametajwa kuwa ni miongoni mwa wahanga wa utoaji mimba ili tu wasiharibu malengo.
Baada ya kuona ya kuona mimba zisizotarajiwa kuongezeka nchini serikali kupitia wizara ya afya ikishirikiana na shirika la afya ulimwenguni wakaamua kuhimiza Matumizi ya uzazi wa mpango ili kuhakikisha watu wanatimiza malengo yao.
Nini maana ya uzazi mpango?
Ni maamuzi bila kulazimishwa au kushurutishwa ambayo hufanywa na wenza au wana ndoa ili kupanga idadi ya watoto ambao wanawahitaji,pia watoto ambao wanazaliwa wapishane kwa muda wa miaka mingapi ili kupunguza mimba zisizo tarajiwa.Maamuzi ya kutumia uzazi wa mpango pia yaweza fanywa na mtu yeyote mwenye uhitaji wakike au wa kiume lakini akiwa katika umri wa uzazi.
Je kuna kuna umuhimu wa kupanga uzazi?
Ndio,kuna umuhimu wa kupanga idadi ya watoto kwa baba mama pamoja na mtoto, umuhimu huo ni kama ifuatavyo.
.Husaidia kuongeza kipato katika familia, kwakuwa baba anakuwa anamuda mwingi wa kujikita katika shughuli mbalimbali.
.Husaidia kuimarisha afya ya mama kabla ya kuamua kushika mimba nyingine.
.Husaidia mtoto kupata malezi yaliyo bora kutoka kwa wazazi hivyo kufanya mtoto awe mwenye afya bora kimwili na kiakili.
.Husaidia kupunguza migogoro katika familia hivyo familia kuwa yenye upendo ndani yake.
.Husaidia watu kutimiza malengo yao waliyo jiwekea katika maisha kutokana kupungua kwa mimba zisizo tarajiwa.
.Uzazi wa mpango hupunguza ongezeko la vifo vya wakina mama pamoja na watoto.
.Maendeleo ya watu katika nchi husaidia pia kukuza uchumi wa nchi kutokana na kujikita katika shughuli za kimaendeleo.
.Pia uzazi wa mpango husaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa kupunguza mimba zisizo tarajiwa kwa waathirika wa virusi vya UKIMWI hivyo kupunguza idadi ya watoto ambao huzaliwa wakiwa wameambukizwa virusi vya UKIMWI.
Je nani anaruhusiwa kutumia njia za upangaji uzazi?
Uzazi wa mpango hauna masharti ya kuutumia bali mtu yeyote mwenye kuhitaji katika umri wa uzazi anaweza akatumia, awe mwanafunzi,awe ameolewa au hajaolewa,awe na watoto ,awe ana nyonyesha au hanyonyeshi,awe mlemavu au asiye mlemavu,awe mwenye maambukizi au asiye na maambukizi pia mwanaume au mwanamke.
Je yepi ni makundi yenye kuhitaji zaidi uzazi wa mpango?
Yeyote anaweza akatumia njia za uzazi wa mpango japo Kuna wenye uhitaji zaidi . Haya ni makundi ambayo endapo Kama hawata chagua au amua kutumia njia za upangaji uzazi basi maisha yao,afya zao,afya za watoto wao huwa katika hatari kubwa endapo watashika ujauzito ivyo kuathiri maisha ya watoto na familia kwa ujumla wake,makundi ayo ni:
.waliojifungu au wenye watoto,moja ya umuhimu wa kutumia uzazi wa mpango Ni kuhakikisha Mama anakuwa na afya bora kabla ya kuamua kushika mimba nyingine, kwa kawaida ili Mama aweze kuwa na afya bora ni angalau akapumzika kwa muda wa miaka miwili au zaidi ya miaka miwili awe amejifungua kawaida au kwa upasuaji, Hata ivyo Kuna ambao wanashika mimba tena kabla ya kutimiza miaka miwili hivyo afya na maisha yao kuwa katika hatari kubwa.
.Wanawake chini ya umri wa miaka ishirini,kiafya inashauriwa mwanamke kubeba mimba angalau akifikisha miaka ishirini kwa sababu viungo vyake vinakuwa vimekomaa vizuri hivyo kuweza kuhimili kubeba ujauzito,pia angalau akiliayao inakuwa imekomaa kwa kiasi ivyo kuweza kumudu baadhi ya changamoto katika maisha,japo Kuna ambao hushika mimba kabla ya kutimiza miaka ishirini hivyo kujiweka katika athari kubwa.
.wanawake wenye umri wa miaka thelathini na tano na zaidi lakini katika umri wa uzazi, kiafya hushauriwa kushika mimba kuanzia miaka ishirini hadi miaka thelathini na tano tu hii ni kwasababu kadiri umri unavyozidi kwenda ndiyo uwezekano wa kupata Matatizo ya kiafya unavyo ongezeka,Matatizo hayo huweza sababisha kupata shida wakati wa kulea mimba au wakati wa kujifungua na pengine kujifungua mtoto ambaye ni mlemavu,kwaiyo ili kuondoa athari hizi Ni vema kutumia uzazi wa mpango kwa wale ambao wana watoto tayari ,vile vile kwa wale ambao hawana mtoto hadi kufika umri kutokana na sababu mbalimbali au wale ambao hawajafikia lengo la uzazi ni vema kufanya uchunguzi kabla ya kuamua kushika mimba.
.Wenye watoto wanne na zaidi, hao nao ni vema wakatumia uzazi wa mpango ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza jitokeza wakati wa mimba au wakati wa kujifungua.
Je ,nini matokeo ya makundi tajwa hapo juu Kama watashika mimba?
Endapo makundi tajwa happy juu yataamua kutokutumia uzazi wa mpango na baadala yake kuamua kubeba mimba athari zinazo weza jitokeza ni:
.Mtoto anaweza kuzaliwa akiwa na uzito mdogo.
.Mtoto anaweza kuzaliwa kabla ya wakati.
.Mtoto anaweza kuzaliwa akiwa amekufa.
.Pia mtoto anaweza kuzaliwa akiwa na ulemavu wowote.
.Mama anaweza akapoteza maisha kabla au baada ya kujifungua.
.Anaweza kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
.Kupata upungufu wa damu.
.Anaweza kupata shinikizo la damu.
.Kupata magonjwa ya ngono ikiwemo virusi vya UKIMWI.
.Kupatwa na msongo wa mawazo baada ya kujifungua.
Karibu tukushauri,
Whatsap 0712106789.
Asante
No comments:
Post a Comment