Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito

MAUMIVU YA MGONGO WAKATI WA UJAUZITO.

Maumivu ya mgongo yamekuwa  yaki wasumbua wajawazito wengi,maumivu haya huelezwa hutokana na mabadiliko yanayotokea katika miili yao, pia maumivu ya mgongo huweza kutokea katika miezi ya awali ya ujauzito lakini hutokea zaidi kadiri mimba inavyo zidi kukua.

Maumivu huweza sababisha Mama kushindwa kufanya shughuli mbali mbali wakati wa mchana, pia kukosa usingizi wakati wa usiku na pengine kulazimika kutumia dawa za kutuliza maumivu ili kupata usingizi.


Nini chanzo Cha maumivu haya?

Kunasababu nyingi ambazo husababisha maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito, sababu hizo yaweza kuwa:

.Mabadiliko ya homoni,mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito husababisha kulainika kwa ukano(ligament) na kulegea kwa viungio(joints)  zinazo zunguka kiuno. Mabadiliko haya hutokea ili kusaidia mtoto kupita kwa urahisi wakati wa kuzaliwa, kwa upande mwingine mabadiliko haya husababisha kulainika na kulegea kwa maungio katika uti wa mgongo hivyo kusababisha maumivu.

.Kuongezeka kwa uzito,wanawake huongezeka  uzito wakati wa ujauzito , mgongo ndio egemeo au msaada mkubwa wa uzito huo hali hii usababisha maumivu , vile vile kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto  huongeza mkandamizo sehemu za chini za kiuno hivyo kusababisha maumivu.

.Mabadiliko ya mkao, mfano ukiwa ume beba ndoo za maji katika mikono yako miwili na ndoo hizo zikawa zina ujazo tofauti nguvu huelekea zaidi upande ambao unamzigo mkubwa hivyo kusababisha kutembea upande kutokana na kutokuwa kwa uwiano ulio sawa wa mzigo ulio bebwa, wakati wa ujauzito uzito pia huongezeka kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto hali hii husababisha Mama kubalili jinsi ya kutembea kutokana na kuongezeka uzito Hali hii husababisha maumivu.

.Msongo wa mawazo, msongo wa mawazo huelezwa kuchangia maumivu ya mgongo bila kujalisha ni mjamzito au siyo mjamzito,Inaelezwa msongo wa mawazo husababisha kukaza kwa misuli hivyo kusababisha maumivu hususani katika sehemu dhaifu. Kwahiyo kutokana na kulainika na kulegea kwa viungo(joints) katika uti wa mgongo husababisha Mama kuhisi maumivu ya mgongo wakati anapokuwa na msongo wa mawazo.



Ushauri

Ni vigumu Sana kuyaondoa maumivu ya mgongo moja kwa moja lakini Mambo ambayo tunafanya ni kujaribu kupunguza kiwango Cha maumivu hayo.Njia kadhaa hutajwa husaidia kutuliza maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito njia hizo ni:

.Hakikisha hunyanyui au hubebi mizigo mizito.

.Hakikisha husimami kwa Muda mrefu.

.Hakikisha unafanya mazoezi maalumu ya ujauzito ili kuimarisha misuli ya mgongo na tumbo mfano kutembea.

.Hakikisha unalala upande nasiyo kulalia mgongo.

.Hakikisha unapata Muda mwingi wa kupumzika.

.Hakikisha huvai viatu vyenye visigino virefu badala yake vaa viatu ambavyo havina visigino.

.Epuka kuinama unavotaka kuchukua kitu kilichopo chini badala yake kunja magoti na kukichukua .

.Hakikisha unavokaa kwenye kiti hupindi mgongo na ikiwezekana jiwekee kitu laini nyuma ya mgongo wakati unakaa.

.Hakikisha unatumia godoro ambalo halibonyei wakati wa kulala au Kama linabonyea Hakikisha unaweka kitu kigumu ambacho ni flat chini ya kitanda ili kuepuka kubonyea kwa godoro.

.Pia unaweza kujikanda na maji ya baridi au ya Moto .





Kama unaona maumivu yanazidi ni vema kwenda hospitali kwa matibabu zaidi.


KARIBU  TUKUSHAURI

Mawasiliano: 0753891441,0712106789
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts