Home »
» Chanjo ya pepopunda(tetanus) kwa mjamzito.
Chanjo ya pepopunda(tetanus) kwa mjamzito.
Pepopunda ni moja ya ugonjwa ambao huelezwa kuchangia vifo na ulemavu kwa wajawazito pamoja na watoto wachanga hususani katika nchi zinazo endelea.Ili kupunguza vifo pamoja na ulemavu kwa wajawazito serikali kupitia shirika la afya ulimwenguni ikaleta utaratibu wa kuchanja chanjo ya pepopunda kwa wanawake wote katika umri wa uzazi pamoja na wajawazito.
PEPOPUNDA(tetanus).
Ni ugonjwa hatari ambao husababishwa na bacteria clostridium tetani,bacteria huyu anapoingia mwilini hutengeneza sumu ambayo huleta athari katika mfumo wa fahamu(nervous system) na kusababisha kukakamaa kwa misuli katika sehemu mbali mbali ikiwemo misuli ya tumbo na misuli inayoshikilia taya,pia ugonjwa huu husababisha kushindwa kupumua vizuri hivyo basi kuhatarisha maisha zaidi.
Njia za maambukizi.
Kuna njia mbali mbali ambazo wadudu hawa hupata kuingia katika mwili na kuleta athari,njia izo ni pamoja na:
.Wakati wa kuzaliwa mtoto ,endapo vifaa ambavyo vitatumika kukata kitofu vitakuwa siyo salama.
.Kuchomwa au kukatwa na kitu chochote chenye ncha kali ambacho kina kutu au kugusana na udongo.
.Kuweka udongo kwenye kidonda au kufunga kitambaa ambacho siyo kisafi na salama kwenye kidonda.
.Kuumwa na mdudu au mnyama mfano mbwa.
Vihatarishi vya pepopunda
Clostridium bacteria ndio wasababishi wakuu wa ugonjwa huu,bacteria hawa huweza kpatikana katika mazingira tofauti tofauti Kama vile kwenye udongo,vinyesi vya wanyama pia katika vifaa vya ncha kali vyenye kutu pamoja na mazingira mengine machafu,kwahiyo pindi ukipata jeraha katika mazingira ayo Ndipo huingia mwilini. Licha ya hayo Kuna mambo mbayo ni hatarishi ambayo yanaweza sababisha kupata wadudu wa pepopunda nayo ni:
.Kutokufuata mlolongo unaotakiwa wa upataji chanjo au kupata chanjo kwa mlolongo usio takiwa mfano kuruka chanjo ya pili na kuchanja ya tatu Jambo hili husababisha chanjo isifanye kazi vizuri.
.Kutokupata chanjo kabisa,Kutokupata chanjo ungali katika mazingira hatarishi huchangia kupata pepopunda kwasababu mwili utakuwa hauna uwezo wa kutengeneza kinga dhidi ya wadudu wa pepopunda.
.Kuwepo na jeraha lolote mwilini ambalo laweza kuwa chanzo Cha bacteria kuingia mwilini.
.Kuchomwa na kitu chenye ncha kali mfano msumari,kisu n.k.
Pia ugonjwa wa pepopunda unaweza kuwapata :
.watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kupitia ukataji kitofu hususani kwa wakina Mama ambao hawakupata chanjo ya pepopunda wakati wa ujauzito.
.Watu wenye majeraha yatokanayo na kupigwa risasi.
.Wenye majeraha yatokanayo na kung'atwa na wanyama au wadudu.
.Wenye majeraha yatokanayo na kujichoma kitu chenye ncha kali,mfano msumal au vijiti,pia kujichora tatoo pamoja na kujichoma sindano hususani kwa wajidunga.
.Majeraha yatokanayo na mvunjiko wa mifupa.
.Majeraha yatokanayo na kuungua Moto.
.Wenye vidonda vichafu au vidonda ambavyo vina maambukizi ya wadudu.
Dalili za pepopunda.
Dalili huanza kuonekana siku chache hadi wiki kadhaa Mara baada ya kupata maambukizi ya wa dudu wa pepopunda , pia kutokana na mfumo wa fahamu kupata athari kutokana na sumu inayo tengenezwa na wadudu hao dalili kadhaa huonekana, nazo ni:
.Kushindwa kumeza chakula kutokana misuli inayolizunguka taya Kukakamaa.
.Kukakamaa kwa misuli ya shingo.
.Kukakamaa kwa misuli ya tumbo.
.Kuhisi maumivu wakati misuli inapokakamaa.
.Kukakamaa kwa misuli ya kinywa.
.Kupata homa kali.
.Mapigo ya moyo kwenda kasi.
.Kutokwa na jasho.
Athari zitokanazo na pepopunda.
Mara baada ya sumu zitokanazo na bacteria wa pepopunda kushambulia mfumo wa fahamu ningumu mno kuzitoa hivyo huendelea kubaki ndani ya mwili na kusababisha madhara,madhara hayo ni pamoja na:
.Matatizo katika mfumo wa hewa ikiwa ni pamoja na kushindwa kupumua vizuri.
.Kuvunjika kwa mifupa na uti wa mgongo kutokana na Kukakamaa kwa misuli na kupigisha.
.Kuharibika kwa seli zinazounda ubongo kutokana na kukosa hewa ya oxygen.
.Maambukizi ya wadudu kwenye mapafu.
.Kifo,Inaelezwa kifo huweza kutokana na mgonjwa kushindwa kupumua kutokana na Kukakamaa kwa misuli kwahiyo mgonjwa kushindwa kupata kiwango Cha kutosha Cha hewa ya oxygen.
Jinsi ya kujikinga na pepopunda.
Turejee kwenye mada yetu,kwa wanawake waliopo katika umri wakuzaa na waja wazito njia ya kujikinga na pepopunda ni kuhakikisha wanachoma chanjo ya pepopunda kwa kufuata mtiririko ulio pangwa ili kuweza kuondoa kabisa madhara yapepopunda dhidi yao na watoto walio tumboni.
Chanjo za pepopunda hutolewa bila malipo kote nchini katika zahanati, vituo vya afya na hospitali zote kwahiyo ni wajibu wako Mama wakesho kuhakikisha unapata chanjo kwa afya yako na mwanao.
Mjamzito Mara tu ya kuanza kuhudhuria kliniki huchomwa chanjo ya pepopunda .
Ambaye alikuwa ashaanza Kuchoma kabla ya kuwa na ujauzito na kadi akawa nayo na hajaharibu mlolongo hatochomwa tena bali huendelea Kuchoma kadiri ya mlolongo unavo mwonyesha, lakini kwa ambaye hakupata kabisa huanza Kuchomwa ,vile vile ambae alisha wahi Kuchoma kabla ya kuwa mjamzito lakini aliacha hulazimika kuanzishiwa upya.
Kwa kawaida chanjo ya pepopunda hutolewa kwa awamu tano Kama dozi kamili ambayo Kila mjamzito na mwanamke katika umri wa kuzaa anatakiwa kupata.
Chanjo iyo hutolewa kwa mlolongo ufuatao hapo chini na niwasihi wajawazito na wanawake katika umri uzazi kufuata mlolongo huu bila kuruka .
Chanjo ya Kwanza: chanjo hii hutolewa Mara ya Kwanza kabisa mjamzito kwenda kliniki ,chanjo hii hutolewa kwa wale ambao hawakuwahi kupata kabisa au walipata baadae wakaacha.
Chanjo ya pili: Chanjo hii hutolewa wiki nne au mwezi mmoja Mara baada ya kupata chanjo ya kwanza,chanjo hii humkinga Mama dhidi ya wadudu wa pepopunda kwa Muda wa miaka mitatu.
Chanjo ya tatu: Chanjo hii hutolewa miezi sita baada ya kupata chanjo ya pili,chanjo hii humkinga Mama dhidi ya bacteria wa pepopunda kwa miaka mitano.
Chanjo ya nne: Chanjo hii hutolewa mwaka mmoja baada ya chanjo ya tatu,chanjo hii humkinga mama kwa miaka kumi.
Chanjo ya tano: Chanjo hii hutolewa mwaka mmoja baada ya chanjo ya nne,chanjo hii humkinga Mama kwa miaka ishirini.
Karibu.
Mawasiliano,0712106789
No comments:
Post a Comment