Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Njia ya dharura ya uzazi mpango.



Utangulizi.

Pamoja na kuwepo kwa njia za uzazi zenye ufanisi,Wanawake wengi hupata mimba bila ya kutarajia/ kupangilia,mimba hizo huongeza idadi ya vifo na ulemavu kutokana na utoaji usio salama,hivyo basi mimba zisizo na mpangilio zaweza kuepukwa kwa Kutumia njia ya dharura ya uzazi.


Njia ya uzazi ya dharura ni nini?

Ni njia ambayo Wanawake wengi huitumia ili wasipate mimba baada ya kufanya tendo la ndoa katika siku za hatari za mzunguko wa hedhi au dirisha la uzazi.

Njia ya uzazi ya dharura ipo ya vidonge na lupu lakini ili njia hizi zitoa matokeo chanya ni lazima zitumike ndani ya siku tano tangu kufanyika kwa tendo la ndoa bila Kinga.


Njia ya dharura inaweza kutumika katika mazingira yepi?

Ili njia ya dharura iweze kuzuia mimba ni lazima itumike ndani ya siku tano tangu kufanyika kwa tendo,baadhi ya mazingira/ Sababu zinazoweza pelekea Kutumia njia ya dharura ni pamoja na:

.Kulazimishwa tendo au kubakwa.

.Kutokutumia Kinga/kondomu.

.Matumizi ya njia ya uzazi yasiyo sahihi mfano Kutumia kondomu lakini kwa bahati mbaya ikapasuka au ikavulika.

.Wenza kushindwa kujizuia kushiriki ngono katika dirisha la uzazi/ kushiriki tendo bila Kutumia Kinga.

.Mwanaume kushindwa kutoa uume ukeni kabla ya kufika mshindo.

.Kwa watumiaji wa sindano kuchelewa Kuchoma sindano kwa kipindi Cha mwezi mmoja au zaidi.

.Kwa watumiaji wa lupu ,lupu kutoka katika sehemu yake .

.Mwanamke hajameza vidonge vitatu au zaidi  vya uzazi wa mpango kwa wale wenye Kutumia dawa zenye vichocheo viwili.



Jinsi njia ya dharura inavyo fanya kazi?

Njia ya dharura hufanya kazi kwa namna tofauti tofauti.

Njia ya vidonge hufanya kazi kwa kuchelewesha/ kuzuia mayai kupevuka kutoka katika vifuko vya mayai.

Lupu hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume kukutana na yai / kwa kuzuia yai lililo rutubishwa lisijishikize katika kuta za mji wa mimba endapo mimba ikitungwa.


Ufanisi wa njia ya dharura.

Ufanisi wa njia ya dharura hutegemeana na kutumika ndani ya siku zilizo pangwa, endapo zikitumika ndani ya siku tano huwakinga Wanawake 98-99 Kati ya Wanawake 100 na wanawake 1-2 pekee wanaweza kupata mimba.


Nani anaweza Kutumia?

Wanawake wote wanaweza kutumia njia ya dharura ya uzazi ikiwa ni pamoja na wale ambao hawawezi Kutumia njia zingine za uzazi zenye vichocheo hii ni kutokana na kutumika kwa muda mfupi,vile vile zinaweza kutumika kwa wale wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.



Faida ya njia ya dharura.

.Ni salama kwa Wanawake wote.

.Haina madhara kiafya.

.Ni chaguo la pili la kuzuia mimba.

.Ipo chini ya uangalizi wa Mwanamke mwenyewe.



Maudhi yatokanayo na njia ya dharura.

.Kuhisi kichefu chefu.

.Kutapika

.Maumivu ya tumbo.

.Maziwa kujaa au kuuma.

.Maumivu ya kichwa.

.Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi ikiwa ni pamoja na hedhi kuwahi au kuchelewa.




Kurudi katika uwezo wa kupata ujauzito?

Kuna uwezekano mkubwa mwanamke kupata ujauzito endapo atameza vidonge vya dharura kabla ya kujamiiana.

Ikumbukwe vidonge vya dharura huzuia mimba kwa mwanamke aliye jamiiana ndani ya siku tano na siyo vinginevyo.


Njia ya dharura na  Magonjwa ya ngono.

Njia ya uzazi ya dharura haimkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya ngono na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI ,bali huzuia mimba pekee.


Jinsi ya kutumia njia ya vidonge.


Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts