Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Njia za uzazi za muda mrefu




Njia za muda mrefu.

Ni njia ambazo huchukua kuanzia miaka mitatu hadi miaka kumi na mbili ili mwanamke aweze kupata mimba,njia hizo ni vipandikizi pamoja na kitanzi au lupu.


Kipandikizi ni nini?

Ni kipande chembamba Cha plastiki ambacho kimetengenezwa kwa kichocheo Cha progesterone,kipande hiki hufanana na njiti ya kiberiti,kipandikizi huwekwa chini ya ngozi sehemu ya juu ya mkono kwa ndani kidogo.

Kichocheo kilichomo ndani ya kipandikizi hufanana na kichocheo Cha asili kinacho patikana Katika mwili wa mwanamke na utendaji kazi wake huwa ni wa kufanana.

Kipandikizi huwekwa na mtoa huduma za afya aliye pata mafunzo maalumu,mtoa huduma hufanya upasuaji mdogo Sana sehemu za juu ya mkono na kuweka kipandikizi kwa uangalifu mkubwa.


Je Kuna aina ngapi za vipandikizi?

Nchini kwetu Kuna aina mbili za vipandikizi navyo ni implanon na jedelle.

.Implanon

Ni kipandikizi ambacho kimetengenezwa kwa kijiti kimoja pekee,kipandikizi hiki humkinga mtumiaji dhidi ya mimba kwa muda wa miaka mitatu tu,baada ya muda wake kuisha mtumiaji hulazimika kukitoka.

.Jedelle

Hiki ni kipandikizi kilichotengenezwa kwa vijiti viwili,kipandikizi hiki huzuia mwanamke kushika mimba kwa muda wa miaka mitano,baada ya muda kuisha nacho hutolewa.



Kipandikizi hufanyeje kazi?

Kichocheo Cha progesterone kilichopo Katika kipandikizi hutengeneza ute mzito Katika shingo ya kizazi hivyo kuzuia mbegu za kiume zisikutane na yai.
Vile vile kipandikizi huzuia upevushaji wa mayai kutoka katika vifuko vya mayai.


Ufanisi wa kipandikizi.

Kipandikizi ni moja ya njia ambazo ufanisi wake ni mkubwa Sana,Kati ya Wanawake 100 Wanawake 99 hawato pata mimba na mwanamke mmoja pekee anaweza kupata mimba.


Faida za kipandikizi.

.Huzuia mimba kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano.

.Kipandikizi hakileti karaha Wakati wa kujamiiana.

.Ufanisi wake mkubwa pia ni salama kwa afya.

.Uzazi hurudi kwa haraka baada ya kutolewa.

.Kinaweza kutumika na Mama anaye nyonyesha.

.Humkinga mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya via vya uzazi na upungufu wa damu unaotokana na ukosefu wa madini ya chuma.



Maudhi madogo yatokanayo na matumizi ya kipandikizi.

Wanawake wengi wanaotumia kipandikizi hupata maudhi madogo Mara kadhaa lakini baada ya muda maudhi hayo hutoweka kabisa ,kwa kawaida maudhi yatokanayo na kipandikizi siyo hatarishi kwa afya maudhi hayo ni:

.Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi ikiwa ni pamoja na hedhi isiyo na mpangilio, kupungua kwa siku za hedhi,au kukosa hedhi hususani Katika miezi ya mwanzo.

.Maumivu ya tumbo.

.Maumivu ya kichwa.

.Kuongezeka uzito wa mwili.

.Kizungu zungu.

.Kichefu chefu.

.Matiti kujaa au kuuma.



Nani anaweza Kutumia/ Kutokutumia kipandikizi?

Wanawake karibia wote wanaweza kutumia kipandikizi bila tatizo isipo kuwa wenye matatizo tajwa hapo chini hawa takiwi kutumia kipandikizi badala yake hutakiwa kuchagua njia nyingine ya uzazi.

.Mama Mwenye kunyonyesha mtoto chini ya wiki sita.

.Magonjwa ya ini,ini kuvimba pamoja na saratani ya ini.

.Mwenye matatizo ya damu kuganda miguuni na kwenye mapafu.

.Mwanamke anayetokwa na damu sehemu za Siri bila kufahamika chanzo Cha tatizo lake.

.Mwanamke Mwenye saratani ya titi.

.Mwenye shinikizo la damu.

.Mwanamke ambaye uzito wake ni zaidi ya kilo 80 au Mwenye uzito mkubwa.



Kurudi katika uwezo wa kupata mimba?


Kipandikizi kikitolewa uwezekano wa kupata mimba huwa ni mkubwa Sana.


Kipandikizi na Magonjwa ya zinaa.

Kipandikizi hakimkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya zinaa ,hivyo ni vema Kutumia kondomu Katika kila tendo la ngono ili kujikinga dhidi ya Maambukizi ya zinaa na UKIMWI.



Jinsi ya kuweka kipandikizi.

Kipandikizi ni lazima kiwekwe na mtoa huduma ambaye amepata mafunzo maalumu na siyo vinginevyo.Mtoa huduma atafanya Mambo yafuatayo Wakati was kuweka kipandikizi.

.Kwanza mtoa huduma atahakikisha mazingira ya kutolea huduma ni salama kwa mteja na yaliyo na usiri mkubwa.

.Kisha utakaa kwenye kiti au kulala Katika kitanda Cha kutolea huduma ,huelezwa kulala Wakati wa kuwekewa kipandikizi husaidia huduma ifanyike kwa urahisi zaidi.

.Mtoa huduma atasafisha eneo ambalo kipandikizi kitawekwa kwa Kutumia pamba yenye dawa ya kuondoa wadudu kisha kukausha tena eneo hilo kwa pamba kavu iliyo safi.

.Kisha mtoa huduma atakuchoma sindano ya maumivu sehemu ambayo kipandikizi kitawekwa ii kupunguza maumivu lakini zoezi hili huleta maumivu kidogo .

.Baada ya dakika kadhaa mtoa huduma ataingiza kipandikizi Katika eneo lile Lile ambalo lili wekwa dawa ya maumivu.

.Kisha mtoa huduma ataweka pamba safi na kufunga na bandeji ndogo.

.Baada ya kuwekewa kipandikizi hakikisha maji haya piti Katika eneo lililo wekwa kipandikizi angalau kwa siku nne hadi tano,unaweza kutoa pamba kuanzia siku ya pili lakini bandeji isitolewe hadi siku ya tano.


Rudi kwa mtoa huduma endapo Mambo yafuatayo yatajitokeza.

.Ukiona kipandikizi kina toka .

.Ukihisi maumivu makali zaidi yasiyo koma.

.Ukihisi joto,wekundu na kutokwa na usaha eneo lililo wekwa kipandikizi.




Kutoa kipandikizi

Kipandikizi kinaweza tolewa muda wowote pia kinaweza ondolewa kutokana na Sababu mbalimbali ,Sababu hizo ni Kama:

.Mteja mwenyewe ameamua kutolewa bila kujalisha kimemsababishia maudhi au hakija sababisha.

.Kimemletea maudhi ambayo huenda yakapelekea tatizo kiafya.

.Muda wake wa kufanya kazi umepita .




Jinsi ya kutoa kipandikizi.

Mtoa huduma atasafisha sehemu iliyowekwa kipandikizi kwa Kutumia pamba yenye dawa Kisha kukausha.

Kisha atachoma sindano ya kuondoa maumivu Katika eneo lililo wekwa kipandikizi.

Atakata sehemu ndogo ya ngozi Katika eneo lililo wekwa kipandikizi kisha kukitoa kwa Kutumia kifaa maalumu.

Kisha ataweka pamba safi na kufunga kwa Kutumia bandeji ndogo.


Pia endapo utaona wekundu ,usaha na kuhisi joto sehemu lililo tolewa kipandikizi ni vema kurudi kwa mtoa huduma za afya.





Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts