Kondomu ya kike.
Ni mpira ulio tengenezwa kwa plastiki laini na yenye kuangaza ,una ringi pande zote mbili ringi la upande mmoja lipo wazi na la upande mwingine lipo wazi. Ringi la upande ulio zibwa husaidia kuingiza kondomu ukeni ,na ringi la upande wa wazi hushikilia kondom kwa nje.
Faida ya kondomu ya kike
.Ni salama na hutoa matokeo chanya endapo ikitumika kwa usahihi.
.Haina maudhi madogo ambayo ni hatari kwa afya.
.Inaweza kutumika na yeyote bila kuhitaji msaada wa mtoa huduma za afya.
.Haihitaji elimu ili Kutumia/ni rahisi Kutumia.
.Ina wakinga watumiaji dhidi ya Magonjwa ya ngono na virusi vya UKIMWI ikitumika Mara kwa Mara kwa usahihi.
.Haiingiliani na tendo la ndoa.
.Haipunguzi ladha ya tendo Kama ulivo mpira wa kiume.
.Siyo lazima utolewe Mara baada ya kufika mshindo.
.Inaweza kutumika Kama njia ya muda mfupi au ya ziada.
.Haina madhara yanayotokana na vichocheo.
.Mimba huweza tungwa Mara baada ya Kuacha Kutumia.
Ufanisi wa kondom ya kike.
Uwezekano wa kuzuia mimba na kujikinga na Magonjwa ya ngono pamoja na UKIMWI hutegemeana na matumizi ya Mara kwa Mara kwa usahihi.Pia watumiaji wachache wanaweza kupata mimba/ Maambukizi kutokana na kuvutika au kondomu kupasuka.
Ikiwa haitotumika kwa usahihi Kati ya wanawake 100 Wanawake 21 watapata mimba na wanawake 79 hawato pata mimba.
Vile vile ikitumika kwa usahihi Mara kwa Mara katika kila tendo la ngono Kati ya Wanawake 100 Wanawake 5 watapata mimba na wanawake 95 hawato pata mimba.
Pia kondomu ya kike huwakinga watumiaji dhidi ya Magonjwa ya zinaa pamoja na Maambukizi ya UKIMWI ikitumika kwa usahihi katika kila tendo la ngono.
Nani anaweza /hawezi Kutumia?
Wanawake wote wanaweza kutumia kondomu ya kike bila kujalisha hali zao kwakuwa haina madhara.
Pia kondomu ya kike haina maudhi kwa watumiaji wake.
Kurudi kwa uzazi.
Uwezekano wa Kupata mimba ni mkubwa Mara ya Kuacha Kutumia kondomu.
Jinsi ya Kutumia kondomu ya kike.
.Tumia kondomu mpya kwa kila tendo la ngono.
.Kabla ya kutumia hakikisha unaangalia Kama imechanika au kuharibikiwa Kama imeharibika usitumie,pia angalia Kama Wakati wake umepita Kama umepita basi usiitumie.
.Kabla ya kuingiza kondomu hakikisha unanawa maji na sabuni Katika mikono yako ili kuepuka kujiingizia wadudu.
.Fungua pakiti kwa uangalifu mkubwa bila ya kutumia meno ,kucha au kidole au kitu chochote ambacho kinaweza kuharibu kondomu.
.Kondomu ya Kike yaweza valiwa masaa nane kabla ya tendo la ndoa,wakati unavaa hakikisha unakaa Katika mkao unaofaa ili iwe rahisi kujiingizia kati ya mikao ambayo hushauriwa ni pamoja na kukaa,kuinua mguu mmoja au kulala chali.
.Shika bangili upande ulio fungwa Kisha ikunje hadi iwe ndefu na nyembamba.
.Kwa Kutumia mkono mwingine tenganisha mashavu ya uke kwa Kutumia vidole Kisha ingiza kondom taratibu.
.Kisha ingiza kidole ndani ya kondom na isukume taratibu ifike sehemu husika.
.Hakikisha uume unaingia katikati ya kondomu na siyo katikati ya kuta za uke.
.Wakati wa kujamiana Kuna uwezekano kondomu ikasogea endapo itasogea hakikisha unairudisha mahala pake.
.Mara baada ya kufika mshindo mwanaume atoe uume wake ,kabla hujaamka Shika bangili ya just ili kuzuia maji yaliyomo ndani kumwagika.
.Kisha viringisha kondomu iliyo tumika kwenye pakiti Kisha tupa kwenye ndoo ya taka.
.Kama utahitaji kurudia tendo tumia kondomu nyingine.
Karibu tukushauri.
No comments:
Post a Comment