Vidonge vyenye vichocheo viwili(Cocs).
Hivi ni ni vidonge ambavyo vime tengenezwa kwa muunganiko wa vichocheo viwili yaani progesterone na estrogen, vichocheo hivi hufanya kazi sawa kabisa na vichocheo vya asili ambavyo vipo Katika mwili wa mwanamke.
Je njia hii ufanyeje kazi?
Vidonge vyenye vichocheo viwili hufanya kazi kwa njia tofauti,kwanza kabisa husababisha mayai yasipevushwe kutoka Katika vifuko vya mayai, pia husababisha ute ambao hutengenezwa Katika shingo ya kizazi kuwa mzito hivyo Kufanya mbegu za kiume zishindwe kulifikia yai .
Nani anaweza Kutumia njia hii?
Mwanamke yoyote Katika umri wa uzazi anaweza Kutumia njia hii ,ikiwa ni pamoja na:
.Walio olewa na wasio olewa.
.Wanawake wenye mzunguko wa hedhi mrefu na wenye mizunguko ambayo hubadilika Mara kwa Mara.
.Walio haribikiwa mimba.
.Wenye upungufu wa damu au walio wahi kuwa na upungufu wa damu.
.Wenye Maambukizi ya virusi vya UKIMWI bila kujalisha wameanza matibabu/ hawajaanza.
.Mama anaye nyonyesha kuanzia miezi sita toka kujifungua.
Nani haruhusiwi Kutumia njia hii?
.Wanawake wanaovuta sigara pia umri wao ni kuanzia miaka thelathini na tano na kuendelea pia wanavuta zaidi ya sigara kumi na tano kwa siku.
.Wanawake ambao wanahisiwa kuwa na mimba.
.Wanawake wenye saratani ya titi/ walisha ugua awali.
.Wanawake wenye matatizo ya ini mfano uvimbe kwenye ini, ini kuvimba n.k.
.Wanawake wanao nyonyesha lakini wapo ndani ya miezi sita toka wamejifungua.
.Wanawake wenye shinikizo la damu kuanzia 140/90 na kuendelea.
.Hanyonyeshi lakini yupo ndani ya wiki tatu toka kujifungua ,Kama ana afya njema anaweza kuanza Kutumia baada ya wiki tatu.
.Wanawake wenye tatizo la kuuma kichwa upande.
.Mwenye ugonjwa wa kisukari zaidi ya miaka 20.
.Anaye tumia dawa za kifua kikuu Kama Rifampicin ,vile vile Mwenye Kutumia dawa za ugonjwa wa kifafa Kama carbamezapine n.k.
.Mwenye Kutumia dawa za ugonjwa wa kiharusi au alishawahi kuugua kiharusi/ stroke awali .
.Mwenye mgando wa damu kwenye miguu au mapafu.
.Anae tarajia kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao utamfanya asitembee kwa muda wa wiki moja na zaidi.
Je ufanisi wake ni kwa kiasi gani?
Ufanisi wake hutegemeana na umakini wa mtumiaji,endapo itatumika kwa usahihi uwezekano wa kupata matokeo chanya huwa mkubwa,na endapo isipo tumika kwa usahihi uwezekano wa kutoa matokeo hasi huwa mkubwa.
Endapo vitatumika kwa usahihi Kati ya Wanawake 100 Wanawake 99 watapata matokeo chanya na mwanamke 1 atapata matokeo hasi.
Pia endapo havitotumika kwa usahihi Kati ya Wanawake 100 Wanawake 92 watapata matokeo chanya na Wanawake 8 watapata matokeo hasi.
Faida ya vidonge vyenye vichocheo viwili.
.Mtumiaji anaweza Kuacha Kutumia muda wowote bila msaada kutoka kwa mtoa huduma za afya.
.Uwezekano wa Kupata mimba huwa mkubwa baada ya Kuacha kutumika.
.Haiingiliani kabisa na tendo la ndoa.
.Mwanamke mwenyewe ndiye huamua Kuacha / kuendelea kuzitumia.
.Huzuia kupata mimba kwa asilimia kubwa Kama zikitumika kwa usahihi.
Maudhi madogo madogo ya njia hii.
Wanawake wengi hupata maudhi madogo kutokana na Kutumia dawa hii lakini mauzi hayo huweza kudumu kwa muda Kisha hutoweka kabisa,maudhi ayo ni:
.Maumivu ya kichwa.
.Kizungu zungu.
.Kuhisi kichefu chefu.
.Mabadiliko ya uzito wa mwili.
.Matiti kujaa au kuuma.
Jinsi ya kutumia
.Kwakawaida pakiti moja hujumuisha vidonge 28 Kati ya vidonge hivo 21 vina vichocheo na vidonge Saba vya Mwisho havina vichocheo pia vidonge vya Mwisho vina rangi tofauti na vidonge vingine.
.Hakikisha unameza kidonge kimoja kila siku katika Wakati ule ule bila kusahau/ kuruka kidonge chochote.
.Kisha endelea kumeza dawa kadiri mshale uliopo kwenye pakiti unavyo kuonesha, hakikisha huruki kidonge chochote.
.Ukimaliza kumeza vidonge katika pakiti moja anza kumeza vidonge katika pakiti nyingine bila kuchelewa katika Wakati ule ule ,endapo ukichelewa au ukiacha kumeza Uwezekano wa kupata mimba huwa mkubwa.
Nini ufanye endapo umechelewa/ hujameza dawa.
.Kama hujameza kidonge kimoja/ viwili / umechelewa kumeza Hakikisha unameza kidonge Mara tuu unapo kumbuka,Kisha endelea kumeza Kadiri ya mzunguko au unaweza kumeza vidonge viwili nayo ni sawa.
.Kama hujameza vidonge vitatu au zaidi katika wiki ya kwanza / ya pili hakikisha unameza dawa baada ya kukumbuka,pia unaweza ukatumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa muda wa siku saba ,vile vile Kama ulishiriki ngono katika siku tano zilizo pita unaweza Kutumia pia njia ya dharura .
.Kama hujameza vidonge vitatu au zaidi katika wiki ya tatu ,hakikisha unameza dawa unapokumbuka Kisha meza vidonge vilivyo baki vyenye vichocheo alafu tupa vidonge 7 vya Mwisho Katika pakiti ya vidonge 28 Kisha anza kumeza vidonge katika pakiti nyingine siku inayo fuata,vile vile unaweza Kutumia njia nyingine ya uzazi kwa siku saba .
.Pia Kama umetapika masaa mawili baada ya kumeza vidonge,hakikisha unameza kidonge kinachofuata Katika pakiti haraka iwezekanavyo Kisha endelea kumeza vidonge Kama kawaida.
NB:Njia ya vidonge haimkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya ngono na virusi vya UKIMWI,kwaiyo pamoja na Kutumia vidonge nivema Kutumia kondom kwa usahihi Katika kila tendo la ngono.
Karibu tukushauri.
No comments:
Post a Comment