Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Njia za uzazi wa mpango za muda mfupi



UTANGULIZI.

Njia za uzazi wa mpango za muda mfupi zipo za aina tofauti ambazo zime tengenezwa katika mifumo tofauti tofauti , njia hizo ni Kama ifuatavyo:

.Uzazi wa mpango kwa kutumia vidonge , vidonge navyo hugawanyika Katika makundi mawili , vidonge vilivyo tengenezwa kwa kichocheo kimoja na vidonge vilivyo tengenezwa kwa vichocheo viwili.

.Uzazi wa mpango kwa Kutumia  sindano (depo provera).

.Uzazi wa mpango kwa kutumia kondom/mpira ,mipira nayo hugawanyika Katika sehemu mbili yaani mpira wa kiume na mpira wa kiume.




Njia ya uzazi ya vidonge.

Kama nilivyo eleza Katika utangulizi vidonge hugawanyika Katika makundi mawili,ili mimba isiweze kutungwa mwanamke anashauriwa kumeza vidonge Kila siku Katika Wakati ule ule.

Vidonge hivi vimetengenezwa kwa mfano halisi wa vichocheo ambavyo hupatikana Katika mwili wa mwanamke pia hufanya kazi sawa sawa kabisa na vichocheo vya asili ndani ya mwili

Vile vile vidonge vya weza tumika Kama njia ya dharura ya uzazi wa mpango kwa wale ambao wanakuwa wameshiriki tendo la ndoa Katika dirisha la uzazi na hawapo tayari kuwa na familia.



Vidonge vyenye kichocheo kimoja (progestin only pill au pops).

Vidonge hivi vimetengenezwa kwa kiwango kidogo Sana Cha kichocheo Cha progestin, kwa kuwa dawa hii haina kichocheo Cha estrogen kwa hiyo inaweza tumika hata kwa Mama anaye nyonyesha  kwakuwa haitopunguza kiwango Cha utengenezaji wa maziwa.


Vidonge vyenye kichocheo kimoja hufanyaje kazi?

Vidonge vyenye kichocheo kimoja hufanya kazi kwa namna tofauti ,kwanza kabisa husababisha ute ambao hutengenezwa Katika shingo ya kizazi kuwa mzito hivo mbegu za kiume kushindwa kusafiri Katika ute huo na kushindwa kulifikia yai,Vile vile huzuia mayai kuto kupevuka kutoka Katika vifuko vya mayai.


Je nani anaweza Kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja?

Wanawake karibia wote wanaweza Kutumia njia hii ikiwa ni ni pamoja na:

.Wanawake wanaonyonyesha watoto baada ya wiki sita toka kujifungua.

.Wenye upungufu wa damu au walishawahi pungukiwa damu awali.

.Wanawake wanaovuta sigara bila kujalisha miaka yake na idadi ya sigara ambazo huvuta kwa siku.

.Ambao mimba zimeharibika pia waweza tumia.

.Wasio olewa / walio olewa ,wenye watoto kwa wasio kuwa na watoto .

.We



Je nani asitumie njia ya vidonge vyenye kichocheo kimoja?

Wanawake wenye matatizo yafuatayo hawashauriwi Kutumia vidonge hivi,bali hushauriwa Kutumia njia nyingine ambayo haina vichocheo.

.Wenye saratani ya maziwa/matiti.

.Wenye Kutumia dawa za kifua kikuu mfano Rifampicin ,vile vile wenye Kutumia dawa za kifafa mfano carbamezapine na zinginezo dawa hizi hupungua ufanisi wa kichocheo Cha progestin ivyo kuwa rahisi kupata mimba.

.Wenye matatizo ya kuganda damu miguuni au kwenye mapafu .

.Pia wenye matatizo ya ini Kama uvime kwenye ini,manjano,ugonwa wa ini,ini kuvimba na kushindwa Kufanya kazi , hawa pia hushauriwa kuchagua njia nyingine ya uzazi wa mpango ambayo haihusishi vichocheo.

.Wanawake ambao wana nyonyesha lakini watoto wao wapo chini ya wiki sita.

.Wanawake wenye maambuzi ya virusi vya UKIMWI lakini wamesha anza Kutumia dawa za kufubaisha virus wanaweza Kutumia Isipo kuwa wale ambao hutumia dawa Aina ya Ritonavir dawa hii hupungua kiwango Cha dawa ya progestin kwenye damu hivyo ufanisi wake kupungua .


Je ufanisi wa njia hii ni wa kiwango gani?

Ili njia hii iweze kutoa matokeo chanya hutegemeana na umakini wa mtumiaji mwenyewe ,vile Kama mtumiaji wa vidonge hivi Kama hatokuwa makini uwezekano wa kupata matokeo hasi pia huwa mkubwa.

Kwa Wanawake ambao wanatumia njia hii lakini wakapata hedhi uwezekano wa kupata mimba huwa mkubwa endapo watachelewa kumeza vidonge au wakaacha kabisa kuvitumia.

Kwa Wanawake ambao hawanyonyeshi endapo watatumia dawa Kila siku Katika Wakati uleule Kati ya Wanawake 100 , wanawake 99 hawato pata ujauzito kwaiyo mwanamke 1 pekee anaweza akapata ujauzito.

Pia kwa Wanawake ambao hawanyonyeshi lakini wanameza dawa kwa kuchelewa Kati ya watu 100  watu 90 hadi 97 wanaweza kupata matokeo chanya,kwahiyo watu 3 hadi 10  kunauwezekano wa kupata matokeo hasi.

Kwa Wanawake ambao wananyonyesha endapo watatumia kwa usahihi zaidi uwezekano wa kupata matokeo chanya ni mkubwa kuliko matokeo hasi,kati ya Wanawake 100 Wanawake 99 hawato pata mimba na mwanamke mmoja pekee atapata mimba.




Faida ya kutumia njia hii.

.Hutoa matokeo chanya endapo itatumika kwa usahihi kwa wanao nyonyesha na wasio nyonyesha.

.Ni salama kabisa kwa watumiaji wake.

.Haina mwingiliano na tendo la ndoa.

.Unaweza acha  itumia Wakati wowote ukiamua bila msaada kutoka kwa mtoa huduma za afya.

.Pindi mtumiaji akiacha Kutumia uwezekano wa kupata mimba huwa mkubwa kwa hiyo uzazi hurudi kwa haraka zaidi.


Maudhi yanayoweza jitokeza Wakati wa Kutumia njia hii.

.Kizunguzungu

.Maumivu ya kichwa

.Kichefuchefu

.Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi.

.Mabadiliko ya uzito wa mwili.


Jinsi ya Kutumia vidonge hivi.

.Hakikisha unameza kidonge kimoja kila siku kwa Wakati ule ule,pia baada ya kumeza kidonge chakwanza endelea kumeza kwa kufuata uelekeo wa mshale katika pakiti ya vidonge.

.Baada ya kumaliza pakiti ya kwanza hakikisha unaanza kumeza vidonge katika pakiti inayo fuata bila ya kuchelewa, kwani kuchelewa kumeza kidonge kutatoa matokeo hasi.



Je nifanyeje nikichelewa /nisipomeza ?

Ni rahisi Sana kusahau / kuchelewa kumeza vidonge,kwa iyo nimuhimu Sana mtumiaji kujua afanye nini endapo atachelewa /hatomeza kabisa,fanya ya fuatayo Kama umechelewa / umesahau kumeza.

.Meza kidonge ulichosahau Mara tu unapo kumbuka,Kisha endelea kumeza vidonge vinavyo fuata Kama kawaida, pia Kama huku meza kabisa unaweza kumeza vidonge viwili Kisha kuendelea na mzunguko Kama kawaida.

.Kama mtumiaji anapata hedhi ya Mara kwa Mara anashauriwa Kutumia njia nyingine ya uzazi au Kuacha kushiriki tendo la ndoa Katika siku mbili zinazo fuata,pia endapo ameshiriki tendo la ndoa Katika siku tano zilizopita anashauriwa Kutumia njia ya dharura ya uzazi.


.Kama ametapika ndani ya masaa mawili tangu kumeza dawa anashauriwa kumeza kidonge kingine Katika pakiti haraka iwezekanavyo.



NB: Njia ya vidonge haimkingi mtumiaji dhidi ya magonjwa ya zinaa na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI ,hivyo  pamoja na Kutumia vidonge ni vema Kutumia kondom kwa usahihi Katika kila tendo la ngono.


Karibu tukushauri

Whatsap,0712106789.

Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.