Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Uzazi wa mpango kwa sindano




Njia ya sindano(depo provera).

Sindano ya uzazi wa mpango ime tengenezwa kwa kichocheo kiitwacho medroxyprogesterone ambacho hufanana na kichocheo cha progesterone cha asili katika mwili wa mwanamke.
Kwa kawaida sindano hutolewa kila Baada ya miezi mitatu,Baada ya Kuchoma sindano dawa taratibu huingia kwenye mzunguko wa damu.



Jinsi inavyo fanya kazi.

Sindano hutanya Kati katika namna tofauti, kwanza kabisa husababisha kuto kupevuka kwa mayai katika vifuko vya mayai,vile vile kichocheo Cha progesterone husababisha ute kuwa katika shingo ya kizazi hivyo kuzuia mbegu za kiume zisilifikie yai na kutungisha mimba.


Ufanisi wa sindano.

Ufanisi wa sindano hutegemeana na uzingatiaji wa mtumiaji Kuchoma kila baada ya miezi mitatu, kama mtumiaji atachoma sindano kwa kuzingatia muda ulio pangwa uwezekano wa kupata mimba hauto kuwepo.Pia endapo mtumiaji hato fuata mtiririko ulio pangwa wa Kuchoma sindano Uwezekano wa kupata mimba huwa mkubwa.

Endapo haito tumika kwa usahihi Kati ya Wanawake 100 Wanawake 97 hawato pata ujauzito na wanawake 3 pekee watapata ujauzito.

Pia endapo mtumiaji atachoma sindano kwa Wakati mwafaka Kati ya Wanawake 100 mwanamke 1 pekee atapata mimba Wakati Wanawake 99 watakuwa salama.



Nani anaruhusiwa Kutumia sindano?

Wanawake takribani wote wanaweza Kutumia sindano kwa usalama  na kwa ufanisi mkubwa ,ikiwa ni pamoja na wanawake wenye:

.Wenye/wasio na watoto.

.Walio/wasio olewa.

.Wanawake wenye kuharibikiwa mimba.

.Wenye kuvuta sigara bila kujalisha umri na idadi ya sigara anazo vuta kwa Siku.

.Wanawake wanaonyonyesha lakini kuanzia wiki sita tangu kujifungua.

.Wenye Maambukizi ya virusi vya UKIMWI bila kujalisha wameanza/hawajaanza dawa.



Nani haruhusiwi Kutumia sindano?

.Wanawake ambao wananyonyesha mtoto chini ya wiki sita tangu kujifungua.

.Wanawake wenye shinikizo la damu.

.Wenye matatizo ya ini  Kama uvimbe kwenye ini,ini kuvimba na kushindwa Kufanya kazi.

.Wenye ugonjwa wa kisukari zaidi ya miaka 20.

.Wanawake waliokwisha ugua kiharusi / wana kiharusi/stroke.

.Wenye mgando wa damu kwenye mapafu / miguuni au wanashambulio la moyo/ walishawahi kuugua.

.Wanawake wenye kutoka na damu ukeni ambayo huweza ashiria uwepo wa mimba/ Magonjwa.

.Wenye kuugua saratani ya titi.



Faida za sindano.

.Ni rahisi Kutumia kwasababu haitumiki kila Siku.

.Ni rahisi kutunza Siri.

.Haiingiliani na tendo la ndoa.

.Inaweza kutumika kwa Wanawake ambao hawatakiwi Kutumia njia yenye kichocheo Cha oestrogen.

.Haileti maudhi kwa Wanawake wenye kunyonyesha.

.Ufanisi wake ni wa kiwango kikubwa.

.Inapunguza hatari ya kupata saratani ya tumbo la uzazi.




Maudhi madogo madogo

.Kuongezeka uzito.

.Maumivu ya kichwa.

.Kizunguzungu.

.Kupunguza hamu ya tendo la ndoa.

.Maumivu ya tumbo.

.Mabadiliko ya hedhi ikiwa ni pamoja na hedhi isiyo na mpangilio/hedhi ya muda mrefu lakini hukoma ndani ya miezi mitatu hadi sita.



Je itachukua muda gani kupata mimba  baada ya Kuacha Kutumia sindano?

Njia ya sindano ni tofauti kidogo na zingine Katika kurudi kwa uzazi,kwa kawaida mwanamke akiacha Kutumia sindano humchukua takribani miezi isiyo pungua tisa kupata mimba.


Sindano na Vvu.

Njia ya sindano haimzuii Mwenye/mtumiaji wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI Kutumia,Pia licha ya kutumia sindano inashauriwa Kutumia kondom Katika kila tendo ili kuepuka kupata Maambukizi mapya na Magonjwa mengine ya zinaa.


Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts