Njia za asili za uzazi wa mpango.
Ni njia ambazo hazihusishi aina yoyote ya chemikali au dawa au kifaa chochote chenye dawa au kisichokuwa na dawa ili kuzuia utungaji wa mimba.
Katika njia hizi za asili wapenzi wanaweza kushiriki tendo la ndoa bila Kutumia kinga bali hulazimika Kuacha kushiriki kabisa tendo la ndoa au kutumia mpira/kondomu Katika siku ambazo uwezekano wa kutunga mimba huwa mkubwa,kwaiyo matumizi ya njia za asili huusisha kutambua siku ambazo kunauwezekano wa mimba kutungwa.
Njia izo ni pamoja na kutambua siku za hatari/ rutuba ,kunyonyesha,kuangalia joto la mwili ,Kuacha kushiriki tendo la ndoa siku hatarishi ,mwisho kabisa ni kuchomoa /kutoa uume kabla ya kufika mshindo endapo itashindikana Kutumia njia zingine.
Je nawezaje kutambua siku za hatari/ rutuba?
Mwanamke anaweza kutambua siku zake za hatari/ rutuba Katika mzunguko wake kwa Kutumia njia mbili ambazo ni njia ya kufuata kalenda na njia ya Kutumia shanga.
Njia ya kalenda ni nini?
Ni njia ambayo ina husisha kufuatilia mzunguko wako wa hedhi kwa umakini zaidi kwa Kutumia kalenda ili kutambua lini dirisha la uzazi huanza na lini huishia ,ivyo kulazimika kulazimika Kuacha kushiriki tendo la ndoa au Kutumia kondom Katika siku za uzazi.
Jinsi njia ya kalenda inavyofanya kazi.
Kalenda hutumika Kama chombo Cha kumwongoza mwanamke kutambua lini atakuwa katika dirisha la uzazi,lini atakuwa Katika siku salama , lini hashauriwi kushiriki ngono bila kinga pia siku ambazo anaweza fanya ngono isiyo salama kwa uhuru.
Ufanisi wa njia ya kalenda upoje?
Ili njia ya kalenda iweze kuleta matokeo chanya ina hitaji utayari na uelewa wa kutosha Jinsi ya kuhesabu siku za mzunguko wa hedhi,vile vile ina hitaji ushirikiano wa kutosha Kati ya wenza hivyo basi uwezekano wa kupata mimba huwa ni mkubwa Kama wenza hawana uelewa wa kutosha pia Kama ushirikiano wao ni mdogo,kwamaana iyo uwezekano wa kutokushika mimba huwa mkubwa endapo uelewa na ushirikiano ni mkubwa.
Nani anaweza Kutumia njia ya kalenda?
Njia ya kalenda yaweza ikatumika kwa mtu yeyote lakini ni lazima awe na ufahamu wa kutosha juu ya mzunguko wake na ashirikiane na mwenza wake Katika kutambua siku za mzunguko.
Faida ya Kutumia njia ya kalenda.
.Husaidia kuzuia mimba kwa kuwa fanya wenza kutambua siku za dirisha la uzazi.
.Njia za asili hazina mauzi madogo madogo.
.Inasaidia kukuza uelewa wa kutambua mfumo wa uzazi kwa wenza.
Athari ya njia ya kalenda.
.Isipo tumika kwa usahihi uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.
.Pia njia ya kalenda haimkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya ngono na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI ,njia pekee inayo zuia kupata Magonjwa ya zinaa ni kondom ya kike na kiume.
Je itachukua muda gani kuweza kushika mimba baada ya Kuacha Kutumia kalenda?
Kwakuwa njia hii huusisha Kuacha kushiriki ngono Katika dirisha la uzazi basi uwezekano wa kushika mimba huwa mkubwa pindi tu ikiacha kutumika.
Je nitawezaje kuitumia njia ya kalenda?
.Ili ufanikiwe kuitumia njia hii kwa usahihi hakikisha una ujua mzunguko wako wa hedhi vizuri,siku uanzapo kuona damu ihesabu siku iyo Kama siku yako ya Kwanza ya kuanza kupata hedhi.
.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani wanawake wengi huwa na mzunguko Kati ya siku 26 -32 japo wa chache huwa na mzunguko chini ya siku 26.
.Siku ambazo uwezekano wa kupata mimba ni kuanzia siku ya 8-19 kwaiyo ni vema Kutumia kondom au Kuacha kujamiana Katika siku hizo.
. Siku ambazo uwezekano wa kunasa mimba haupo ni kuanzia siku ya 1-7 na kuanzia siku ya 20 na kuendelea tangu kuanza kwa mzunguko wa hedhi.
Njia ya shanga(cycle beads) ni nini?
Hii ni njia ambayo inatumia shanga ambazo zimetengenezwa kwa rangi tofauti ili kumsaidia mwanamke kutambua siku ambazo Kuna uwezekano wa kupata mimba Kama atashiriki tendo la ndoa bila kinga.
Je nitaitumiaje njia ya shanga?
.Kwanza kabisa shanga moja huwakilisha siku moja ya mzunguko wa hedhi,Katika shanga izo Kuna kipira hakikisha unasogeza kipira hadi kwenye shanga nyekundu ya Kwanza siku ya Kwanza unapoona damu hesabu siku iyo Kama siku ya kwanza ya hedhi.
.Endelea kusogeza kipira kwenye shanga zinazotuata bila kujalisha unapata damu au imekoma.
.Endelea kusogeza kipira kwenye shanga zinazotuata Kila siku hadi ufike kwenye shanga rangi nyeupe,shanga rangi nyeupe huwakilisha dirisha la uzazi au siku ambazo uwezekano wa kushika mimba ni mkubwa hivyo basi ni vyema Kuacha kushiriki ngono isiyo salama au Kuacha kabisa kushiriki ngono,siku hizo ni kuanzia ya 8- 19.
.Endelea kusogeza kipira hadi ufike kwenye shanga za rangi ya kahawia,shanga za kahawia huwakilisha siku ambazo uwezekano wa kutunga mimba haupo ,kwaiyo ni ruksa kushiriki ngono Katika siku hizi bila ya Kutumia kondom lakini kumbuka kondom ndiyo njia pekee ambayo huzuia mimba na Magonjwa ya zinaa na UKIMWI,siku hizo ni kuanzia siku ya 1- 7 na kuanzia siku ya 20 na kuendelea hadi siku moja kabla ya kuanza pata damu Tena.
.Rudia Kufanya Kama nilivyo eleza hapo juu Katika mzunguko unao fuata wa hedhi.
.Endapo mzunguko wa hedhi utaanza tena kabla ya ya kuifikia shanga ya kahawia mkolezo basi mzunguko wako ni chini ya siku 26 ivyo kushauriwa Kutumia njia nyingine ya uzazi kwasabu njia hii itakuwa haikufai tena .
.Pia Kama hauto pata hedhi tena kabla ya kufikisha kipira kwenye shanga ya mwisho ya kahawia basi ni dhahiri kabisa mzunguko wako wa hedhi ni zaidi ya siku 32 ivyo kulazimika kuchagua njia nyingine ya upangaji uzazi kwasababu njia hii haitokufaa tena.
NB: Mambo mengine yanayo baki Katika matumizi ya njia hii hufanana na ile ya kalenda.
Njia za uzazi wa mpango kwa kuangalia dalili za siku za rutuba.
Hizi ni njia ambazo mtumiaji hulazimika kuangali ishara au dalili ambazo huashiria kupevuka kwa yai ivo kulazimika Kuacha kushiriki /kushiriki tendo la ndoa kwa Kutumia kinga njia izo ni kuangalia joto la mwili pamoja na kuangalia ute ute ukeni.
Je njia ya kuangalia joto la mwili ni nini?
Kwa kawaida Wakati wa kupevuka yai joto la mwili la mwanamke huongezeka Kati ya nyuzi joto 0.5- 1, joto hili huendele kuwa juu hadi kuanza kwa mzunguko mwingine wa hedhi ndipo hushuka.
Kama unachagua Kutumia njia hii kujikinga na mimba unashauriwa kupima joto la mwili Kila siku ya asubuhi Wakati ule ule kabla ya kula chochote au kabla ya kuamka kitandani.
Ina shauriwa Kuacha kushiriki tendo la ndoa/ Kutumia kondom tangu utakapo baini joto la mwili limepanda hadi siku tatu,Kuanzia siku ya nne unaweza kushiriki tendo bila ya Kutumia kinga bila kujalisha kupanda kwa joto ilo .
Pia ikumbukwe pia joto la mwili linaweza likapanda kutokana na Sababu tofauti Kama vile kuwa na Maambukizi,mazingira ya sehemu uliyopo,matumizi ya baadhi ya dawa ,Maambukizi Katika via vya uzazi n.k.
Njia ya kuangalia ute ukeni ni nini?
Kwa kawaida ute hubadilika Katika siku za kupevuka kwa yai ,ute ambao huashiria kupevuka kwa yai huwa hauna rangi, mwepesi pia huvutika,ute huu utengenezwa Katika shingo ya uzazi ili kusaidia mbegu za kiume kuogelea kwa urahisi kuelekea kurutubisha yai ,pia husaidia kuzilinda mbegu ili zisiharibiwe.
Unashauriwa kuchunguza ute huu angalau Mara mbili kwa siku Yani asubuhi na jioni, pia unashauriwa kuingiza kidole au Kutumia karatasi safi mfano toilet pepar kuchunguza ute.
Mara uonapo ute aina hii ni vema Kuacha kushiriki ngono hadi siku tatu au Kutumia kinga, baada ya ute huo kuto onekana tena waweza kushiriki tendo la ndoa bila kinga.
Lakini ikumbukwe pia kutokana na Maambukizi ya wadudu Katika via vya uzazi wa mwanamke unaweza kusababisha mabadiliko Ya ute kwaiyo njia hii kuwa ngumu ivyo kutakiwa Kutumia njia nyingine.
Njia ya kuchomoa uume Wakati wa kujamiana.
Ni njia ambayo mwanaume hulazimika kutoa uume wake nje ya uke kabla ya kufika mshindo na kumwaga shahawa zake nje. Njia hii ina hitaji utimamu wa akili na kimwili kuitumia kwa Sababu siyo rahisi kama inavyo dhaniwa na watu wengi.
Hata ivyo uwezekano wa kusababisha mimba huwa mdogo endapo mtumiaji ataitumia kwa usahihi zaidi ,vile vile uwezekano wa kushika mimba huwa mkubwa Sana Kama haito tumika kwa ufasaha na uangalifu mkubwa.
Njia ya unyonyeshaji ni nini?
Hii Ni njia ya uzazi ya muda mfupi ambayo humkinga Mama dhidi ya ujauzito ndani ya miezi sita ya mwanzo toka kujifungua kwake, njia hii hufanya kazi kwa kuzuia mayai yasipevuke kwani Kadiri mama anavyo nyonyesha kichocheo Cha prolactin ambacho husaidia Katika utengenezaji wa maziwa huzalishwa kwa wingi hivyo kupunguza uzalishaji wa kichocheo ambacho husababisha kupevuka kwa yai.
Ili njia hii ifanye kazi ni lazima mtumiaji awe hajapata hedhi toka ajifungue,vile vile ni lazima ahakikishe ananyonyesha Mara kwa Mara mchana na usiku Kila siku pia ni lazima mtoto anaye mnyonyesha ni lazima awe chini ya miezi sita na siyo zaidi ya hapo.
Endapo mtumiaji hato zingatia vigezo husika basi njia hii haito msaidia kwahiyo uwezekano wa kushika mimba huwa mkubwa zaidi na endapo atazingatia vigezo tajwa uwezekano wa kushika mimba vile vile huwa ni mdogo,hivyo basi ili mtumiaji apate matokeo chanya ni lazima awe makini.
Faida ya unyonyeshaji.
.Njia hii haina maudhi madogo madogo.
.Pia ikitumika kwa ufasaha ufanisi wake ni mkubwa.
.Pia unampunguzia garama Mama.
.Pia njia hii huongeza ukaribu/ uhusiano Kati ya Mama na mwanae.
.Pia unyonyesha kupitia maziwa ya mwanzo humpa mtoto kinga ya mwili dhidi ya Magonjwa.
.Hupungua uwezekano wa Mama kupata saratani ya matiti.
Je nani anaweza Kutumia njia hii?
Njia ya uzazi wa mpango kupitia kunyonyesha inaweza ikatumika na mwanamke yeyote lakini sharti awe amekidhi vigezo vya Kutumia njia hii.
Inashauriwa mtoto kunyonyeshwa kwa miezi sita bila ya kumpa chakula chochote kile kwasababu maziwa ya Mama pekee yanatosha kumpa mtoto virutubisho vyote muhimu ambavyo vinahitajika.
Kwa wale ambao ni watumiaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI nao wanaweza wakatumia njia hii bila tatizo lakini ni lazima wahakikishe mtoto ananyonya maziwa ya Mama pekee bila kumchanganyia chakula ndani ya miezi sita ya mwanzo lakini endapo wata mchanganyia mtoto chakula uwezekano wa mtoto kupata Maambukizi kutoka kwa Mama huwa mkubwa ikumbukwe ya kwamba kwawakati huo viungo vya mtoto vinakuwa havijakomaa vizuri .
Pia ikumbukwe njia ya unyonyeshaji haimkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya zinaa na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI hivyo kumtaka mtumiaji Kutumia kondom akihitaji kushiriki tendo la ndoa.
KARIBU TUKUSHAURI.
Whatsap: 0712106789.
No comments:
Post a Comment