Utangulizi
Matumizi ya uzazi wa mpango ni yasiyo pingika kote ulimwenguni,ili uweze kutumia njia za uzazi wa mpango ni lazima Kwanza uelimishwe njia za uzazi wa mpango zilizopo ndipo Sasa uchague kutokana na elimu ambayo umepewa.
Hata hivyo mambo yamekuwa tofauti watu wengi hutumia njia za upangaji uzazi pasipo kujua au kupewa elimu sahii juu ya njia ambayo anataka kuichagua,wengi wa watumiaji wamekuwa wakitumia njia za kupanga uzazi kwa kuiga kutoka kwa marafiki zao kwakuwa wameona marafiki zao wanatumia basi nao wanaamua kutumia au wanatumia tu kwakupewa elimu na marafiki zao bila ya kujua elimu iyo ni sahihi au siyo sahihi.
Changamoto hutokea endapo mtumiaji akapata maudhi au akapata mimba kutokana na matumizi yasiyo sahihi hivyo kuonekana uzazi wa mpango siyo sahihi hivyo maneno mengi kuzagaa juu ya njia za uzazi wa mpango.
Lakini ni kutoe hofu ndugu msomaji ,uzazi wa mpango ni salama kabisa ndio maana hata serikali yetu inaimiza Matumizi yake na ungekuwa haufai basi sidhani Kama serikali ingehamasisha watu juu ya Matumizi yake.
Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuchagua njia za uzazi wa mpango.
Kuchagua njia ya uzazi wa mpango kunaweza kuwa ni Jambo gumu kidogo ni lazima Kwanza ujue njia zilizopo Kisha uchague njia ambayo ni sahihi,ili ufanikiwe katika hili ni lazima uulize maswali yafuatayo:
.Je Kuna njia ngapi za uzazi wa mpango ambazo zinapatikana? Licha ya kuwa na mawazo yako pindi unapokuwa katika klinik ya uzazi wa mpango ni vyema kumuuliza mtoa huduma wako ili akueleze njia ambazo zinapatikana.
Kuna njia mbili za upangaji uzazi nazo ni:
*Njia za asili, hizi ni njia ambazo hazihusishi aina yoyote ya dawa au kifaa chenye dawa ili kuzuia mwanamke asishike mimba mfano wa njia izo ni njia ya kalenda,kuangalia joto la mwili,kuangalia ute wa uzazi,kunyonyesha,na kutoa uume kabla ya kutoa mbegu.
*Njia za kisasa,hizi ni njia ambazo hutegemea Matumizi ya dawa au kifaa chenye dawa au kisichokuwa na dawa ili kuzuia mwanamke kupata mimba,mfano wa njia izi ni kitanzi,vidonge,kondomu ,kipandikizi .
Vile vile njia hizi zimegawanyika katika makundi makuu matatu yaani:
-Njia za muda mfupi,hizi ni njia ambazo hushauriwa kutumika kwa wale ambao malengo yao ya kuzaa siyo chini ya miaka miwili na hayazidi miaka miwili,kwa watumiaji wa njia hii ni vema wakatambua njia hizi zinaweza kusababisha wakapata mimba wakiacha kuzitumia au zisipo tumika kwa usahihi.Mfano wa njia hizo Ni njia zote za asili,vidonge,kondomu za kiume na kondomu za kike na sindano.
Pia Kuna njia za dharura ambazo hutumika wakati wa dharura tuu.
-Njia za muda mrefu, hizi ni njia ambazo hushauriwa kutumika kwa wale ambao malengo yao ya uzazi ni kuanzia miaka mitatu na kuendelea hadi miaka kumi, watumiaji ,kwa watumiaji wa njia hizi uzazi hurudi Mara tu baada ya Kuacha au kutolewa kwa njia hizo.Mfano wa njia izo ni kipandikizi na kitanzi au lupu.
-Njia za kudumu, hizi ni njia ambazo hushauriwa kutumika kwa wale ambao wameshazaa watoto kadhaa hivyo hawahitaji tena kuzaa,njia hizi huusisha kufunga kizazi moja kwa moja na kizazi kikishafungwa haiwezekani tena kukirudisha kwaiyo unapo chagua njia ni vema kuangalia uhitaji kwa baadae.Njia hizo huhusisha kukata na kufunga mrija unao beba shahawa kwa mwanaume (vasectomy) na kukata mirija ya uzazi kwa mwanamke (tubal ligation).
.Je,ni Jinsi gani njia iliyochaguliwa inafanya kazi? Njia za uzazi wa mpango hufanya kazi kwa namna tofauti tofauti japo Kuna baadhi hufanana katika utendaji wake,baadhi ya njia hufanya kazi kwa kuhakikisha mbegu za kiume hazilifikii yai ili kutungisha mimba,zingine hufanya kazi kwa kuhakikisha ute ute mzito una tengenezwa na shingo ya uzazi kazi ya ute mzito ni kuzizuia mbegu za kiume zisilifikie yai ,na njia zingine hufanya kazi kwa kuzuia yai au mayai yasipevuke katika Kila mzunguko pia zingine huziharibu shahawa kabla hazijalifikia yai.
.Je ,ufanisi wa njia iliyochaguliwa ni wa kiwango gani? Ili njia iweze kuzuia mimba kwa asilimia kubwa zaidi ni lazima itumike Mara kwa Mara na kwa usahihi zaidi,njia ambazo hazihitaji jitihada zaidi katika Utumiaji wake ni kondom, kitanzi au lupu, kipandikizi na kufunga kizazi ,uwezekano wa kupata mimba ni mdogo katika njia hizi na hutegemeana na uwezo wa mtoa huduma au makosa ya mtumiaji mwenyewe. Lakini Matumizi ya njia za asili huitaji uangalifu na umakini zaidi katika Utumiaji wake kwaiyo zisipo tumika kwa uangalifu na makini uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.
.Je,Kuna uwezekano mimba kutungwa baada ya njia chaguliwa kutolewa?
Narudia unapochagua njia ya uzazi wa mpango ni vema kuchagua kulingana na malengo yako ya uzazi ,ikumbukwe kwamba Kuna baadhi ya njia mfano kufunga kizazi ukishachagua njia hii ujue endapo utahitaji kupata mimba haiwezekani tena,kwaiyo Kama huitaji tena kuzaa ni vema kuchagua njia hii,pia endapo utahitaji kuzaa baada ya miaka miwili ni vema kuchagua njia za muda mfupi vile vile Kama utahitaji kupata mtoto kuanzia miaka mitatu au zaidi ni vema kuchagua njia za muda mrefu .
.Njia iliyo chaguliwa itafaa? Unapo chagua njia ni vema kuangalia Kama itakufaa,kuna baadhi ya njia hazishauriwi kiafya kutumika kwa baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na wenye saratani ya titi ,saratani ya shingo ya kizazi ,wenye magonjwa ya ini n.k. Pi baadhi ya njia kama kitanzi kinahitaji usafi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuepuka kushiriki ngono na wapenzi wengi kwani kwa kufanya ivyo uwezekano wa kupata mimba huwa mkubwa na kupata magonjwa ya zinaa,pia njia za asili huitaji umakini mkubwa katika Utumiaji wake na njia ya vidonge vilevile kwahiyo ni vema kuchagua njia inayo kufaa kulingana na maisha yako.
.Uwezo wa kumudu maudhi madogo unao? Unapochagua njia ni vema kuangalia pia uwezekano wa kuyamudu maudhi madogo yatakayo jitokeza, maudhi yaweza tofautiana Kati ya njia moja na nyingine lakini pia Kuna mengine hufanana.Kwaiyo usichague njia ambayo unajua hutoweza imudu .
.Je inakukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa? Ikumbukwe kwamba kondom za kiume na kike pekee ndizo hukinga dhidi ya magonjwa ya ngono na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI,kwahiyo ni vema kutumia kondom kama njia ya nyongeza ili kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na kutumia njia nyingine ya upangaji uzazi!
.Je njia iliyochaguliwa itakubalika na mwenza wako? Mpenzi au mwenza wako yawezekana Kuna njia ya upangaji uzazi ambayo anaipenda zaidi na mwanamke akawa na njia ambayo anaipenda kwaiyo kusababisha kuwa na mpishano wa mawazo, Sasa ili kuepuka Jambo hili ni vema mwanamke kumshirikisha mwenza wako juu ya uzazi wa mpango ili mkashiriki wote kwa pamoja kuchagua njia ambayo inafaa.Pia suala la uzazi wa mpango siyo jukumu la mwanamke pekee Bali hata mwanaume kwaiyo ni vema kumhusisha.
Karibu tukushauri juu ya upangaji uzazi.
WhatsApp, 0712106789.
Asante.
No comments:
Post a Comment