Kitanzi/ lupu.
Ni plastiki ndogo yenye umbo la T ambayo huwekwa kwenye mji wa mimba na mtaalamu aliye pata mafunzo maalumu ili kuzuia Mwanamke asipate mimba,kifaa hiki kimetengenezwa kwa madini ya shaba.
Je lupu hufanyeje kazi?
Kitanzi chenye madini ya shaba husababisha mabadiliko ya kikemikali ndani ya mji wa mimba,mabadiliko hayo husababisha kuharibiwa kwa mbegu za kiume pamoja na yai kabla ya kukutana na kutengeneza kiumbe ,kwa lugha rahisi naweza kusema kitanzi huzuia kutokea kwa muunganiko Kati ya mbegu ya kiume na yai.
Ufanisi wa kitanzi/lupu.
Ni njia ambayo humkinga mtumiaji dhidi ya mimba kwa muda wa miaka kumi na mbili na ufanisi wake ni mkubwa Sana.
Kati ya wanawake mia moja watakao tumia lupu/ kitanzi Wanawake tisini na tisa hawato pata ujauzito na Mwanamke mmoja pekee anaweza kupata ujauzito.
Nani anaweza tumia/Nani asitumie kitanzi.
Kitanzi ni salama na hufaa kwa takribani Wanawake wote,ikiwa ni pamoja na wenye kunyonyesha,waliokwisha ugua ugonjwa wa pid wakapona,walio kuwa na maambukizi sehemu za Siri,wenye upungufu wa damu,waathirika wenye kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI n.k
Lakini kitanzi kina hitaji usafi wa hali ya juu kwaiyo hivyo kuto kuwa faa aina fulani ya watu kutokana na kazi zao wanazo zifanya,baadhi ya watu ambao hawa shauriwi kutumia lupu/kitanzi ni pamoja na:
.Wenye Maambukizi ya via vya uzazi baada ya kujifungua /mimba kuharibika,hawa hushauriwa kupata matibabu Kwanza Maambukizi yakisha toweka basi wanaweza kutumia
.Wenye kutokwa na damu ukeni isiyo ya kawaida bila chanzo chake kufahamika.
.Wenye matatizo ya kizazi mfano saratani ya shingo ya kizazi,saratani ya mfuko wa mayai,mwenye ugonjwa wa kifua kikuu katika nyongahawa hawa hushauriwa kutumia njia nyingine ya uzazi lakini kwa wale wenye kifua kikuu katika nyonga wanaweza kutumia baada ya kupata matibabu.
.Wenye Maambukizi ya virusi vya UKIMWI lakini hawajaanza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.
Lakini kwa wale wenye virusi hawajapata UKIMWI bado wanaweza wakatumia,vile vile Kama Mwanamke akapata UKIMWI Wakati ashawekewa kitanzi anaweza akachagua kubaki nacho au kuondolewa.
.Wanawake walio jifungua zaidi ya masaa arobaini na nane/siku mbili bila kuwekewa lupu ,hawatakiwi kuwekewa lupu hadi angalau wafikishe wiki nne au zaidi tangu kujifungua.
Faida za kutumia kitanzi/lupu.
.Ni salama na ufanisi wake ni mkubwa.
.Huzuia mimba kwa muda wa miaka kumi na mbili.
.Ni rahisi kuitumia kwasababu haimuitaji mtumiaji kufanya kitu chochote Mara baada ya kuwekewa.
.Hai ingiliani na tendo la ndoa.
.Mtumiaji anaweza kuamua kuiondoa muda wowote akihitaji.
.Ina punguza gharama,Mara baada ya kuwekewa kitanzi Mwanamke hutakiwa kurudi kuchunguza baada ya wiki sita,lakini ikimletea shida anaweza kurudi muda wowote.
.Ina tunza usiri wa mteja na kujizuia katika uzazi.
.Hakuna kuchelewa kupata mimba baada ya kitanzi/ lupu kuondolewa.
.Inaweza ikawekwa Mara baada ya kujifungua.
.Inaweza tumika na Mama anaye nyonyesha.
Maudhi yatokanayo na lupu/ kitanzi.
.Maumivu ya tumbo Wakati wa hedhi.
.Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi.
.Kupata hedhi kwa muda mrefu.
Lupu/ kitanzi na HIV
Mwanamke Mwenye virusi vya UKIMWI au yupo katika hatari ya kupata virusi anaweza Kutumia lupu bila tatizo.
Mwanamke Mwenye UKIMWI na anatumia dawa za kupunguza makali ya virusi na kiafya yupo vizuri anaweza Kutumia lupu bila tatizo.
Mwanamke Mwenye UKIMWI na hajaanza Kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi na kiafya hayuko vizuri hatakiwi Kutumia lupu/ kitanzi.
Endapo Mwanamke atapata UKIMWI akiwa tayari amewekewa kitanzi anaweza akachagua kuendelea kuzitumia / Kuacha kukitumia.
Watumiaji wa lupu ambao Wana UKIMWI ni lazima waje kuchunguza Mara kwa Mara ili Kama itaonekana wamepata Maambukizi katika via vya uzazi lupu iondolewe.
Kitanzi /lupu haimkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya zinaa na UKIMWI ,kwaiyo pamoja na Kutumia lupu mtumiaji hushauriwa kutumia kondomu kwa usahihi Katika kila tendo la ngono.
Kuweka kitanzi/ lupu.
Kitanzi huwekwa na kuondolewa na mtaalamu wa afya aliyepata mafunzo maalumu .
Mtoa huduma atafanya mambo kadhaa wakati kuweka lupu/kitanzi.
.Atafanya uchunguzi Katika sehemu za siri ili kujua Kama mteja anastahili kuwekewa kitanzi au hastaili,mtoa huduma ataangalia uuvimbe,michubuko au uchafu ukeni.
.Kisha atasafisha uke kwa Kutumia pamba yenye dawa ya kutoa wadudu.
.Ataweka kifaa maalumu(speclum) ukeni ili aweze kuona shingo ya kizazi na kuingiza kifaa maalumu hadi mwisho wa tumbo la uzazi na Kisha kukitoa kifaa icho.
.Kwa Kutumia kifaa kingine mtoa huduma ataingiza kitanzi hadi afike mwisho wa tumbo la uzazi,Kisha atatoa chombo icho.
.Atakata uzi wa kitanzi na Kuacha sentimita tatu zikiwa zina ning'inia nje ya shingo ya kizazi.
Mambo ya kuzingatia baada ya kuwekewa kitanzi.
.Hakikisha unajichunguza Mara kwa Mara ili kujua Kama lupu ipo mahala pake au imetoka.
.Hakikisha unarudi kwa mtoa huduma baada ya wiki sita tangu kuwekewa lupu.
-Baada ya kuwekewa kitanzi anaweza pata maumivu ya tumbo kwa siku kadhaa Kisha yakaisha.
-Pia mtumiaji anaweza kupata damu au matone ya damu kwa muda wa miezi mitatu hadi sita.
Chukua tahadhari mambo haya yakitokea.
Mara baada ya kuweka kitanzi Kuna mambo kadhaa yanaweza yakatokea nayo ni lazima uya chukulie hatua ili usipate matokeo hasi,uonapo mambo haya rudi haraka kwa mtoa huduma:
.Baada ya kujifanyia uchunguzi ukagundua uzi unaonekana au hauonekani ,hii huashiria lupu haipo mahala sahii.
.Kuhisi maumivu ya tumbo yanaongezeka kila baada ya siku.
.Maumivu wakati wa kujamiiana.
.Kutokwa na uchafu ukeni.
.Kuhisi homa kali.
.Kuhisi Kichefuchefu na kutapika masaa ya mwanzo Katika siku ishirini za mwanzo.
.Unahisi umepata mimba.
Kutoa lupu/ kitanzi.
Kitanzi hutolewa na mtaalamu wa afya baada ya ,
.Kuisha muda wake wa matumizi,miaka 12 baada ya kuwekewa.
.Kimemletea maudhi ya kiafya ambayo hayavumiliki.
.Mtumiaji anataka kutolewa mara baada ya lengo la uzazi kutimia.
Mtoa huduma wa afya atafanya mambo kadhaa wakati wa kutoa kitanzi.
.Atasafisha uke kwa Kutumia pamba safi yenye dawa ili kuzuia wadudu,kabla ya kukuingizia speculum.
.Kisha mtoa huduma atatumia kifaa kingine kuangalia uzi ulipo na kuushikwa kwa kifaa icho Kisha kuuvuta taratibu hadi nje ya shingo ya kizazi.
No comments:
Post a Comment