Jinsi ya kutambua tarehe ya matazamio ya kujifungua.
Kwa kawaida huchukua takribani miezi tisa hadi kumi tangu kutungwa kwa mimba hadi kujifungua.
Mimba hukadiriwa kutungwa katika tarehe ya kuanza kuona damu/ hedhi kwa mara ya mwisho,tarehe ya kwanza ya kuona hedhi kwa Mara ya mwisho huchukuliwa Kama siku ya kwanza ya mimba japo uwezekano wa kushika mimba huwa ni wiki mbili tangu kuanza kwa hedhi.
Kukadiria siku ya matarajio ya kujifungua siyo sayansi iliyo kamili kwasababu kuna Wanawake ambao wanaweza kujifungua Katika tarehe ya makadirio na wengine kushindwa kujifungua Katika tarehe zilizo kadiriwa.
Japo kuwa siyo sayansi iliyo kamili ,lakini ni vema kupata uelewa ni lini mtoto anaweza kuzaliwa,ili kuweza kuandaa mahitaji ya msingi ya Mama na mtoto mapema zaidi ,pia husaidia mama kujua ukuaji na maendeleo ya mtoto kulingana na mwezi.
Je nawezaje kujua tarehe ya matazamio ya kujifungua?
Unaweza kutambua tarehe ya matazamio kwa Kutumia njia kadhaa,njia izo ni:
.Njia ya hesabu.
Ni njia ambayo hujumuisha kukokotoa hesabu rahisi,hii hutumika kwa Wanawake ambao mizunguko yao ni siku ishirini na nane ,au yai huachiliwa katikati mwa mzunguko yaani siku kumi na nne,pia mizunguko yao haibadiliki badiliki.
Kuna kanuni maalumu ambayo hutumika kukisia tarehe ya matazamio ya kujifungua, kanuni hiyo huitwa naegele's rule.
Kabla ya kuitumia kanuni hii hakikisha unaijua tarehe ya kuanza kupata hedhi kwa mara ya mwisho,kisha andika kwenye karatasi ambayo utaitumia kufanya hesabu rahisi.
Baada ya kuandika tarehe husika kwenye karatasi /daftari lako ,ongeza/jumlisha Saba sehemu ya tarehe.
Sehemu ya mwezi toa tatu endapo ni zaidi ya miezi mitatu,yaani Kama itakua mwezi wa nne,tano,sita ,Saba na kuendelea,Kisha jumlisha moja sehemu ya mwaka.
Kama ni chini ya miezi minne yaani ni mwezi wa tatu,wa pili na wa kwanza, jumlisha tisa sehemu ya mwezi na sehemu ya mwaka usijumulishe namba yoyote,Bali utabaki mwaka uliopo.
Mfano,mteja "Y" alianza kuona damu kwa Mara ya mwisho tarehe 2/3/2019,je ipi ni tarehe ya matarajio ya kujifungua?
Tarehe ya kuanza hedhi kwa Mara ya mwisho. 2/3/2019.
+ Saba tarehe,na Tisa mwez 7/9
Tarehe ya matazamio ni 9/12/2019.
Mfano 2,mteja "B" alianza ona damu kwa Mara ya mwisho tarehe 10/9/2019,je ipi ni tarehe ya matarajio ya kujifungua?
Tarehe ya kuanza hedhi kwa mara ya mwisho 10/9/2019 .
+ 7 tarehe,-3 mwez,+1mwk 7/-3/+1.
Tarehe ya matazamio ni 17/6/2020.
Lakini hata ivyo Kama itakuwa siyo rahisi kufanya hesabu rahisi usiumize kichwa kwani mtoa huduma Katika klinic ya wazazi atafanya kwa ajili yako.
.Kipimo Cha tumbo.
Hiki ni Kipimo ambacho hupimwa ili kujua ukubwa wa tumbo la mama katika kila hudhurio,ukubwa wa tumbo huwakilisha ukubwa wa mtoto kwa kwa wiki,Kipimo hiki hupimwa na mkunga au daktari.
Kuna Sababu nyingi ambazo zinaweza sababisha tumbo likawa kubwa au dogo, kwaiyo si vema kujifanyia Kipimo hiki mwenyewe Bali mtaalamu ndio atakupima.
Uwepo wa maji mengi katika mfuko wa uzazi,uwepo wa watoto zaidi ya wawili na uwepo wa uvimbe vinaweza sababisha tumbo kuwa kubwa zaidi,kwahiyo njia hii siyo sahii Sana katika kukadiria ukubwa wa mimba ivyo kusaidia kukadiria tarehe ya matazamio.
.Kipimo Cha utrasound.
Hii ni njia ambayo huweza kutambua umri wa mimba kwa usahihi zaidi ivyo ni rahisi kukadiria tarehe ya matazamio ya kujifungua .
*Kama nilivyo sema awali wachache Sana wanaweza wakajifungua Katika tarehe za makadirio,lakini wengi hawatojifungua Katika tarehe ambazo hukadiriwa,kwa kawaida uchungu unaweza kuanza kwa kuwahi wiki mbili kabla ya tarehe ya makadirio au wiki mbili Baada ya tarehe ya matazamio.
Pia unaweza ukajiunga barua pepe yangu kupokea makala mpya moja kwa moja kwenye simu yako pindi tu zikiwekwa.
KARIBU.
No comments:
Post a Comment