Matumizi ya dawa Wakati wa ujauzito.
Kipindi Cha mimba ni kipindi ambacho hudumu kwa muda wa wiki 36 hadi wiki 42,katika kipindi hiki mtoto hutegemea kila kitu kutoka kwa Mama katika ukuaji na maendeleo yake tumboni.
Kipindi Cha miezi mitatu ya mwanzo mtoto hukua kwa haraka Sana na ndiyo kipindi viungo vya mwili hutengenezwa,Wakati huu mtoto huitaji virutubisho mbali mbali ili viungo vyake viweze kutengenezwa kiukamilifu.
Kwakuwa mtoto hutegemea kila kitu kutoka kwa mama yake ,basi kitu ambacho Mama hukitumia humfikia moja kwa moja mtoto bila ya kujali kizuri au siyo kizuri hivyo kuleta matokeo chanya/ hasi katika ukuaji wa mtoto.
Kuwepo kwa maduka ya dawa kumesababisha matumizi ya dawa ya holela pasipo kupata ushauri kutoka kwa wataalamu,dawa zilizo nyingi huwa hazina madhara kwa mtoto lakini kuna baadhi ya dawa ni hatari endapo zikitumika na kwani huweza leta shida Katika ukuaji na maendeleo ya mtoto na pengine kusababisha ulemavu kwa mtoto.
Moja ya dawa ambazo hutumiwa holela ni dawa za kutuliza maumivu,watu wengi hudhani dawa za maumivu haziwezi leta athari kwa mtoto, lahasha dawa hizi zinaweza kuleta athari Kama kawaida endapo mtumiaji hato pata maelezo kutoka kwa wataalamu.
Athari zitokanazo na matumizi holela ya madawa wakati wa ujauzito.
Utumiaji wa dawa holela unaweza ukamuathiri mtoto kwasababu dawa hizo humfikia mtoto moja kwa moja,athari ambazo zaweza tokea ni pamoja na:
.Kuharibika kwa mfuko wa uzazi (placenta) /makao ya mtoto,mfuko huu humsaidia mtoto kupata chakula,kupumua,kutoa taka mwili ,pia kumkinga mtoto dhidi ya vimelea vya magonjwa,kwahiyo kuharibiwa kwa mfuko huu husababisha mtoto kukosa mahitaji yake ya msingi Katika ukuaji wake hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto.
.Dawa huathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto hivyo kuongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu wa viungo kutoka na viungo kushindwa tengenezeka sawa sawa /kuzaliwa akiwa na afya iliyo dhoofu.
.Kuongeza uwezekano wa mimba kuharibika,kuna baadhi ya dawa hazishauriwi kabisa kutumika katika miezi fulani ya ujauzito na zingine Katika kipindi chote Cha ujauzito,endapo dawa hizo zikitumika huweza kusababisha mimba kutoka / kuharibika.
.Matumizi ya dawa pia yanaweza kusababisha Mama kupata uchungu na kabla ya wakati .
Hata hivyo kuathirika kwa mtoto hutegemeana na mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na:
.Aina ya dawa ambayo mama ameitumia, haimaanishi kila dawa yaweza leta athari kwa mtoto hapana ila Kuna baadhi ya dawa hazishauriwi kutumika na endapo zitatumika huleta athari moja kwa moja.
.Muda ambao dawa imetumika,Kadiri dawa ambazo hazishauriwi kutumika wakati wa ujauzito zinavyo endelea kutumika ndivyo kadiri athari kwa mtoto inavyo zidi kuongezeka.
.Kiwango Cha dawa ambacho kinatumika, daktari na wataalamu wengine wanajua kiwango cha dawa ambacho hutakiwa kitumike,lakini kutokana na kutumia dawa bila kupata ushauri unaweza kuzidisha kiwango Cha kawaida Cha matumizi ya dawa hiyo ,dawa inaweza ikawa haina madhara wakati wa ujauzito lakini endapo ikitumika kwa kiwango kikubwa inaweza leta athari kwa mama na mtoto.
.Dawa imetumika pekee yake au ime changanywa na dawa zingine,unaweza kutumia dawa moja/ mbili / tatu bila kuleta athari kwa mtoto endapo dawa hizo zitakuwa hazina madhara ,Lakini kadiri unavyo changanya madawa bila ushauri ndivyo uwezekano wa kutumia dawa isiyo sahii unavyo ongezeka.
.Ukubwa/umri wa mimba,Kuna baadhi ya dawa hazishauriwi kutumika katika miezi mitatu ya mwanzo,baada ya miezi mitatu ya mwanzo na zingine Katika miezi mitatu ya ujauzito,kwahiyo kadiri utakavyo tumia dawa wakati ambao siyo sahii kwa matumizi yake ,ndivyo kadiri itakavyo leta athari kwa mwanao tumboni.
.Afya ya Mama mwenyewe,ufinyu wa afya ya mama husababisha udhoofu wa ukuaji na maendeleo ya afya ya mtoto tumboni kutokana na kukosa virutubisho na uwezekano wa kushambulia na Magonjwa,vile vile utumiaji wa dawa Mara kwa Mara pasipo ushauri huleta athari kwa mtoto.
Nini ufanye Sasa kuondoa athari kwa mtoto.
.Hakikisha ukiugua wakati wa ujauzito usitumie dawa yoyote bila kupata ushauri kwa daktari,mkunga au mtaaalamu wa dawa.
.Pia Kama ulikuwa unatumia dawa yoyote awali na ukahisi ni mjamzito ,ni vema Kuacha Kutumia dawa izo au ukapata ushauri kwa wataalamu ili kujua Kama ni salama/siyo salama kwa mwanao.
.Katika kipindi cha miezi mitatu ya awali ya ujauzito ni ngumu Sana kutambua Kama ni mjamzito lakini endapo ukatambua inashauriwa pindi unavyo kwenda hospitali kupata matibabu ni vema kumueleza daktari kuwa ni mjamzito ili asikupe dawa isiyo takiwa ,kwa kuto kujua.
.Ili kuepuka Kutumia dawa Mara kwa Mara hakikisha unakula mlo kamili Mara kwa mara ikiwa ni pamoja na mboga na matunda yakutosha,vile vile hakikisha unafanya mazoezi mepesi ili kuimarisha Kinga za mwili.
.Acha Kutumia madawa ya asili,kwa imani watu wengi hudhani kitu ambacho ni asili hakiwezi kuleta madhara,sawa kinaweza kisilete madhara,lakini ikumbukwe dawa za asili hazina kipimo maalumu Cha dawa,kwahiyo unaweza kuzidisha kiwango na ikamletea shida mtoto, kwaiyo ni vema zikaepukwa.
.Vile vile acha kutumia sigara,pombe na dawa za kulevya kwasababu athari zake hufanana na zile zitokanazo na Utumiaji wa dawa holela.
KARIBU.
No comments:
Post a Comment