Mimba hutokana na muunganiko unao tengenezwa baada ya mbegu ya kiume kukutana na yai,ili mimba iweze kutungwa ni lazima mayai/ yai liachiliwe kutoka katika moja ya vifuko vya mayai, mayai / yai huachiliwa katikati mwa mzunguko wa hedhi,pia mzunguko wa hedhi huto fautiana baina ya wanawake, kwa Mwanamke Mwenye mzunguko wa siku ishirini na nane tunategemea siku ya kumi na nne yai liachiliwe.
Kwa kawaida yai huachiliwa katikati mwa mzunguko wa hedhi wa Mwanamke,yai husafiri taratibu kupitia mirija ya uzazi kuelekea kwenye tumbo la uzazi,wakati yai linasafiri endapo Mwanamke atashiriki tendo la ndoa na mwanaume mwenye kutoa mbegu bora,basi Mwanamke atapata mimba.
Baada ya mimba kutungwa seli hugawanyika na kutengeneza seli zingine mpya,seli mpya nazo hugawanyika na kutengeneza kiini tete.Baadhi ya seli zilizo undwa hutengeneza maji Katika chupa ya uzazi na zingine huunda plasenta.
Nitajuaje Kama ni mjamzito?
Unaweza kutambua uwepo wa ujauzito kwa kuangalia dalili mbali mbali ambazo hujitokeza,dalili hizo ni pamoja na kuhisi kichefu chefu,kutapika, kukosa hedhi n.k.
Lakini hata hivyo huwezi kuthibitisha uwepo wa mimba kwa kuangalia dalili pekee kwa Sababu dalilli za magonjwa hufanana ,kwaiyo unaweza fikiri ana mimba kwasababu amekosa hedhi lakini ikawa siyo mimba,hivyo basi kipimo pekee kitathibitisha uwepo wa mimba.
Miongoni mwa vipimo hivyo ni pamoja na;
. Kipimo Cha mkojo (UPT)
Hiki ni kipimo ambacho kinaweza fanywa na muhusika Kwa kununua kutoka katika duka la dawa baridi,vile vile kipimo hiki hufanywa na wataalamu wa maabara katika kituo Cha kutolea huduma,na ndicho kipimo ambacho hutumika zaidi kutambua mimba.
Kipimo Cha mkojo hufanya kazi kwa kutambua uwepo wa kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin kwenye mkojo, kichocheo hiki hutengenezwa na kondo/ placenta Mara baada ya yai lililo rutubishwa kujishikiza kwenye mji wa mimba na uzalishaji wake huongezeka kadiri mimba inavyo kuwa.
Kwa kawaida kichocheo hiki huanza kuonekana kwenye mkojo baada ya wiki mbili tangu kutungwa kwa mimba. Chemicali iliyotumika kuunda kipimo hiki hubadilika rangi pindi inapokutana na kichocheo kilichopo kwenye mkojo.
Kwaiyo ili kupata majibu sahihi hushauriwa kupima baada ya kukosa hedhi,pia hushauriwa kupima zaidi asubuhi kuliko mchana kwasababu mkojo wa asubuhi huwa na kiwango kikubwa Cha kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin kuliko wakati wowote hivyo uwezekano wa kupata majibu sahii ni mkubwa kuliko wakati ambao kichocheo hiki kina kuwa kwa kiwango kidogo kwenye mkojo.
.Kipimo Cha damu.
Hiki ni kipimo kinacho fanywa na wataalamu wa maabara ili kutambua uwepo wa kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin kwenye damu,vile vile kipimo hiki hutambua kiwango Cha kichocheo Cha mimba(HCG) kilichopo kwenye damu.
Jinsi ya kutumia kipimo Cha mkojo.
Kipimo hiki hupatikana kwenye maduka ya dawa,na pharmacy kwahiyo kutokana na kupatikana kwa urahisi na gharama zake kuwa nafuu kina weza tumika hata nyumbani kwa kufuata maelezo bila uwepo wa mtaalamu wa maabara,lakini hata hivyo kutokana na kuto kuelimishwa namna ya kutumia kipimo hiki wakati mwingine kinaweza kutoa majibu ya uwongo, yafuatayo ni maelezo Jinsi ya kupima mimba kwa mkojo.
.Hakikisha unapima /unapimwa mkojo baada ya kukosa hedhi Katika mzunguko unaofuata.
.Hushauriwa zaidi kupima wakati wa asubuhi,japo unaweza kupima wakati wowote ule kwahiyo hakikisha unaweka mkojo Katika chombo kikavu pia kisafi.
.Kisha toa kipimo kutoka kwenye pakiti Kisha tumbukiza kipimo kwenye kifaa Cha mkojo upande wenye uelekeo wa mshale,hakikisha kipimo kina zama kwenye chombo hadi kwenye mstari,Kisha toa baada ya dakika moja.
.Subiri majibu kwa dakika chache,endapo ukatokea mstari mmoja Basi siyo mjamzito na ikitokea mistari miwili tambua ni mjamzito hivyo utalazimika kwenda Katika kituo Cha kutoa huduma ili wapate uthibitiwa na hatimaye uendelee na huduma zingine za clinic.
Usikose kufuatilia muendelezo wa somo hili wakati ujao.
KARIBU.

No comments:
Post a Comment