Njia za kudumu
Ni njia ambazo huhusisha kufunga kizazi kwa mwanamke na mwanaume ambao hawahitaji kupata mtoto tena Katika maisha yao.
Njia hizi huitaji maridhiano / makubaliano Kati ya mume na mke / wenza.
Njia hizi huhusisha kufanyiwa upasuaji mdogo kwa mwanaume au mwanamke.
Kufunga uzazi kwa mwanaume( vasectomy).
Ni njia ambayo upasuaji mdogo hufanywa Kisha kufunga na kukata mrija unao beba mbegu za kiume kutoka kwenye kokwa hadi kwenye uume,
Jinsi inavyo fanya kazi
Kwakuwa mrija unao beba mbegu za kiume toka kwenye kokwa hadi kwenye uume umefungwa na kukatwa ,mwanaume atakuwa anatoa mbegu Kama kawaida lakini zitazuiliwa na fundo lililo wekwa,kwaiyo mwanaume atakuwa anafika kileleni kama kawaida ila hatoweza kutungisha mimba kwasababu maji maji yanayo tolewa yanakuwa hayana mbegu.
Ufanisi wa kufunga uzazi kwa mwanaume.
Ili njia hii itoe matokeo chanya ni lazima wenza/wapenzi wasishiriki tendo la ndoa bila Kutumia Kinga/ njia nyingine ya uzazi wa mpango katika miezi mitatu ya mwanzo,endapo watashiriki tendo la ndoa Katika miezi mitatu ya mwanzo Kuna uwezekano mwanamke akapata mimba Kama kawaida.
Wenza wasishiriki tendo la ndoa baada ya miezi mitatu ,uwezekano wa kupata mimba ni mdogo Sana,kati ya wanawake mia moja ambao watashiriki tendo la ndoa na wenza waliofunga kizazi ,Wanawake tisini na Saba hadi tisini na nane hawato pata mimba na wanawake watatu hadi wawili wanaweza kupata mimba.
Nani anaweza Kutumia/Nani asitumie
Wanaume wote wanaweza kufunga kizazi baada ya kupata ushauri na saa na kukubaliana na wenza wao kuwa hawa hitaji kupata mtoto tena ikiwa ni pamoja na walio oa kwa wasio oa wenye watoto kwa wasio na watoto,wenye Maambukizi na wasio na Maambukizi bila kujali wameanza Kutumia / hawatumii dawa.
Pia Kuna baadhi ya wanaume kutokana na matatizo ya kiafya hawashauriwi kufunga kikazi ikiwa ni pamoja na:
.Wenye Maambukizi ya wadudu tumboni/ kwenye damu.
.Wenye Magonjwa ya ngono/zinaa.
.wenye uvimbe kwenye mirija ya kubeba shahawa,uume au korodani(busha kubwa).
.Mwenye Maambukizi kwenye korodani.
.Mwenye ugonjwa wa matende.
.Ambaye korodani imejiingiza ndani haitaki kushuka.
.Mwenye ugonjwa wa kisukari.
.Kijana mdogo ambaye ni nguvu kazi ya kesho.
Faida za kufunga kizazi.
.Ni salama na ni njia ya kudumu.
.Humpa mwanaume uhuru wa kushiriki na kufurahia tendo la ndoa muda wowote.
.Maudhi madogo hutokea Mara chache Sana.
Maudhi yanayo weza jitokeza.
.Maumivu sehemu iliyo fanyiwa upasuaji lakini maumivu haya hutoweka baada ya muda.
.Maambukizi sehemu ya upasuaji.
Je naweza kutungisha mimba baada ya kufunga kizazi?
Kama nilivyo eleza hapo awali hii ni njia ya kudumu kwaiyo ,ukishafunga kizazi hakuna uwezekano tenah wa kusababisha Mimba,kwaiyo niwasihi ndugu wasomaji kabla hujachagua njia hii ni vema ukajiridhisha hauto hitaji watoto Tena kwa baadae.
Jinsi ya kufunga kizazi.
Kufunga kizazi ni lazima kufanywe na mtaalamu aliye pata mafunzo maalumu, kufunga kizazi hakukitaji dawa ya usingizi Bali mtaalamu atatoa dawa ya ganzi ili usijisikie maumivu,Mtaalamu atafanya mambo yafuatayo.
.Atasafisha sehemu ambayo upasuaji mdogo utafanyika kwa kutumia pamba iliyo na dawa ya kuua wadudu ili mteja asipate Maambukizi kwa baadae.
.Baada ya hapo atachoma sindano ya ganzi sehemu ambayo atafanya upasuaji ili kuondoa maumivu.
.Mtaalamu ata pasua kidogo na kuangalia mirija inayo beba shahawa kutoka kwenye kokwa zote mbili Kisha atafunga kila mmoja peke yake na kukata.
.Mtaalamu atafunga kidonda kwa kutumia uzi maalumu na kukizuia kwa pamba na bandeji.
Mambo ya kuzingatia baada ya kufunga kizazi.
.Pumzika kwa siku kadhaa bila kufanya kazi ngumu.
.Kagua sehemu ya kidonda ili kubaini Kama Kuna mabadiliko Katika sehemu iyo, utajisikia maumivu siku kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji lakini yataisha.
.Hakikisha sehemu yenye kidonda ni safi na hayapiti maji kwa siku kadhaa.
.Usijamiane siku kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo.
.Tumia kondomu au njia nyingine ya uzazi endapo utashiriki ngono katika miezi mitatu ya mwanzo.
No comments:
Post a Comment