Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Kufunga uzazi kwa mwanamke.



Kufunga uzazi kwa mwanamke.

Ni njia ya kudumu ambayo huusisha upasuaji mdogo Kisha kufunga na kukata mirija inayo beba mayai kutoka kwenye vifuko vya mayai hadi kwenye mji wa mimba.


Jinsi inavyo fanya kazi.

Mayai yaliyo pevuka huzuiliwa kukutana na mbegu za kiume na kifundo  kilicho wekwa kwaiyo mimba haiwezi kutungwa.


Ufanisi wake.

Uwezekano wa kupata matokeo chanya ni mkubwa endapo mtumiaji akifuata maelezo atakayo pewa na mtaalamu hususani Katika siku za mwanzo,Kati ya Wanawake mia mbili mwanamke mmoja pekee anaweza kupata mimba katika siku za mwanzo na wanawake mia moja tisini na tisa hawato pata mimba.


Nani atumie/Nani asitumie.

Njia hii ni lazima itumike kwa wenza ambao hawahitaji Tena kupata mtoto baada ya kupewa ushauri, wakati mwingine inaweza kutumika kwa wale ambao wakibeba mimba hupatwa na matatizo ambayo huatarisha maisha yao.

Hata hivyo Kuna baadhi ya wanawake hawashauriwi kufunga kizazi ikiwa ni pamoja na:

.Mwanamke asiye na watoto/asiye fikia lengo lake la uzazi.

.Mwanamke ambaye hajaolewa.

.Mwanamke aliye jifungua ndani ya siku Saba hadi arobaini na mbili .

.Mwanamke Mwenye Maambukizi Katika via vya uzazi.

.Mwenye saratani ya shingo/tumbo la uzazi.

.Mwenye kutokwa na damu nyingi ukeni isiyo ya kawaida.

.Mjamzito.




Faida za kufunga uzazi.

.Ni njia inayozuia kupata mimba moja kwa moja.

.Haiingiliani na tendo la ndoa kwaiyo wenza hufurahia tendo la ndoa hata Katika siku za hatari.

.Haina madhara kiafya pia ni salama.



Maudhi madogo madogo.

.Kuhisi maumivu sehemu ulipo fanyika upasuaji ,lakini baada ya siku kadhaa maumivu hutoweka,maumivu yaweza tulizwa kwa dawa za maumivu.

.Wakati mwingine Maambukizi yanaweza jitokeza sehemu ya upasuaji endapo mteja hato zingatia ushauri wa mtaalamu japo ni Mara chache sana kutokea.



Kurudi katika uwezo wa kupata mimba.

Hakuna uwezekano tena wa kupata mimba baada ya kizazi kufungwa,kwaiyo kabla hujachagua njia hii ni vema kufikiria kwa kina kabla ya kuamua,na ikumbukwe kwamba kizazi kikisha fungwa hakiwezi kurudishwa tena.



Jinsi ya kufunga kizazi.

Kizazi hufungwa na mtaalamu(daktari) aliye pata mafunzo maalumu.

Mtaalamu atafanya uchunguzi Katika sehemu za Siri ili kubaini Kama mteja anakidhi vigezo.

Atasafisha sehemu ambayo upasuaji mdogo utafanyika  kwa kutumia pamba safi yenye dawa.

Kisha mtaalamu atatoa sindano ya ganzi sehemu ambayo upasuaji mdogo utafanyika.

Ataingiza kifaa maalumu ukeni hadi kwenye mji wa mimba ili iwe rahisi kupata mirija ya uzazi karibu kabisa na sehemu ya upasuaji.

Kisha mtaalamu atafunga na kukata mirija yote miwili baada ya kufanya upasuaji .

Atafunga sehemu ya upasuaji na kuweka bandeji .





Baada ya kufanyiwa upasuaji zingatia yafuatayo.

.Pumzika angalau kwa siku mbili bila kufanya kazi yoyote.

.Epuka kufanya kazi ngumu au kunyanyua vitu vizito angalau kwa wiki moja.

.Hakikisha kidonda kina kuwa safi muda wote na usikiloanishe,pia hakikisha una meza dawa ulizo pewa na mtaalamu kwa kuzingatia maelezo.

.Epuka kushiriki tendo la ndoa ndani ya siku Saba toka kufanyiwa upasuaji.

.Rudi kwa mtaalamu kwa uchunguzi wiki moja au mbili Baada ya kufanyiwa upasuaji.



Rudi kwa mtoa huduma endapo Mambo yafuatayo yatajitokeza.

.Homa kali ambayo haipungui wiki moja baada ya kufanyiwa upasuaji.

.Maumivu makali sehemu ya upasuaji  yasiyo pungua hata baada ya kutumia dawa za kutuliza maumivu.

.Utaona usaha sehemu ya upasuaji/ utatokwa na damu .




Maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kufunga kizazi.

Mwanamke Mwenye Maambukizi ya virusi vya UKIMWI na Mwenye ugonjwa wa UKIMWI na anatumia dawa anaweza kufunga kizazi bila tatizo japo maandalizi maalumu yatahitajika.

Pamoja na kufunga kizazi ni vema Kutumia kondomu Katika kila tendo la ngono kwasababu kufunga kizazi hakumkingi mtumiaji dhidi ya Magonjwa ya zinaa na UKIMWI bali kondomu pekee.



KARIBU.



Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts