Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

  • This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ukuaji wa mimba hatua kwa hatua

Utangulizi

Kawaida hakuna mwanamke ambaye hatamani kujua maendeleo ya ukuaji wa mtoto wake kuanzia hatua ya awali mimba inapotungwa hadi wakati wa kujifungua.

Watu wengi hudhania swala la kujua maendeleo ya ukuaji wa mtoto tumboni ni suala la mjamzito pekee Jambo ambalo siyo kweli bali hata mwanaume ni wajibu wake kutambua ukuaji wa mwanae ili aweze kutoa msaada wa haraka pale atakapo gundua kuna tatizo Katika ukuaji wa mwanae pia wakati ambao mama atakuwa pengine hawezi kufanya hata shughuli ndogo.

Kupitia makala hii utajifunza hatua ambazo mtoto hupitia hadi kuzaliwa kwake tangu mbegu ya kiume inapo kutana na yai  na kutungisha mimba,nikusii fuatilia kwa makini makala hii ili angalau upate kujifungua machache Kati ya mengi ambayo nimekuandalia Katika makala hii.



Kutokea kwa ujauzito


Ili mimba iweze kutungwa ni lazima mbegu ya kiume kutoka kwa mwanaume mwenye afya njema na uwezo wa kutungisha mimba ikutane na yai kutoka kwa mwanamke mwenye afya bora na uwezo wa kushika ujauzito mara baada ya kujamiiana katika siku za hatari bila ya kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi.

Wakati wa tendo la ndoa Mwanaume hukadiriwa kutoka mamilioni ya mbegu, lakini Kati ya mbegu hizo ni mbegu moja tu ambayo hutungisha mimba.Mwanaume hutoa mbegu za  aina mbili,mbegu ya kiume na mbegu ya kike,kwa mantiki hii ni dhairi kabisa jinsia ya mtoto huweza kufaamika toka siku ya kwanza mimba inatungwa,kwahiyo kumbe mbegu za kiume ndizo ambazo huamua jinsia ya mtoto,baada ya mimba kutungwa yai lililo rutubishwa hujigawa kakita seli hai nyingi wakati linasafiri kuelekea kwenye tumbo la uzazi kujishikiza.


Maendeleo ya ujauzito Wiki ya nne .

Hiki ni kipindi ambacho endapo utaamua kujipima kwa Kutumia kipimo cha nyumbani ni dhahiri kabisa utapata majibu chanya.Pia ni wakati ambao sehemu mbali mbali za mwili wa mtoto huanza kutengenezwa sehemu hizo ni pamoja na moyo na mishipa ya damu,vile vile mtoto hutengeneza umbo la mwonekano wa sura pamoja na shingo.


Maendeleo ya ujauzito Katika wiki ya nane.

Wakati huu sehemu mbalimbali za mwili wa mtoto huendelea kutengenezwa,ngozi inayo funika macho huanza kutengenezwa, alama ya pua pia huanza kujitokeza kwa mbali,pia miguu na mikono vinakuwa vimetengenezwa lakini vidole ndo Kwanza vinaanza kujitokeza lakini vinakuwa bado vina utando Kama miuu ya bata ilivo.Pia wakati huu via vya uzazi vya nje hutengenezwa lakini bado jinsia ya mtoto inakuwa haijatambulika bado,moyo wa mtoto wakati huu unakuwa umeanza kudunda,kwa kawaida moyo huanza kudunda Katika wiki ya sita ya ujauzito.


Maendeleo ya ujauzito Katika wiki kumi na mbili.

Wakati huu mtoto anakuwa ameanza kucheza kwa mbali Sana japo siyo rahisi mama kutambua,pia mapigo ya mtoto yanaweza kusikika daktari au mkunga wako anaweza kusikiliza mapigo ya mwanao kwa Kutumia kifaa maalumu. Vile vile sehemu za Siri zinakuwa zishajijenga vyema Katika wakati huu hivyo basi unaweza kutofautisha kwa mwonekano wa nje,pia mtoto anakuwa ameanza kukojoa lakini Kuna uwezekano usionekane ndani ya mfuko wa uzazi(plasenta),pia ngozi ya macho hujifunga ili kuya Linda macho ambayo yanaendelea kutengenezwa.


Maendeleo ya ujauzito Katika wiki ya kumi na sita.

Wiki hii mtoto anakuwa anauwezo wa kuchezesha macho,moyo pamoja na mishipa ya damu vinakuwa vimekamilika, vidole pia vina kuwa vimeanza kutengeneza michirizi.Pia figo na kibofu Cha mkojo vinakuwa vinafanya kazi kikamilifu Kama ambavyo Inaweza ikathibitishwa na uwepo wa mkojo kwenye maji yanayo mzunguka mtoto.


Maendeleo ya ujauzito wiki ya ishirini.

Kipindi hiki mtoto anakuwa na uwezo wa kujinyoosha na kunyonya vidole,wakati huu pia mtoto anakuwa anacheza tumboni mwa mama ake pia mama anakuwa na uwezo wa kumsikia,vile vile wakati huu mtoto huonekana vizuri kwahiyo Kama ulikuwa unahitaji kufanya utrasound huu ni wakati mzuri,pia wakati huu unaweza kutambua jinsia ya mwanao kupitia kipimo Cha utrasound.wakati huu pia mkunga au daktari wako anaweza kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto wako kwa Kutumia kifaa Cha kawaida,utando unao fanana na maziwa hutanda Katika ngozi ya mtoto, vile vile nywele za mtoto huanza kutengenezwa .


Maendeleo ya ujauzito wiki ya ishirini na nne.

Kipindi hiki mfumo wa masikio wa mtoto unakuwa umeundwa kikamilifu na unafanya kazi hivyo basi mtoto huwa na uwezo wa kusikia sauti na kuweza kufuata uelekeo ambao sauti inatokea.Watoto huweza kutambua sauti wawapo tumboni na kujenga mazoea na sauti ambazo huzisikia Mara kwa Mara  hivyo huwa rahisi kwao kuzitambua baada ya kuzaliwa.


Maendeleo ya ujauzito wiki ya ishirini na nane.

Kutokana na taratibu za uzazi zilizowekwa na wizara ya afya mtoto akizaliwa chini ya wiki ya ishirini na nane huchukuliwa mimba imeharibika na halkuna uwezekano wa mtoto kuishi,lakini endapo mtoto atazaliwa  kuanzi wiki ya ishirini na nane Kuna uwezekano wa mtoto kuishi. Pia ni muda wa kujifunza nini unatakiwa kufanya pia nini hutakiwi kufanya ukiwa Katika chumba Cha uzazi,jinsi ya kumuhudumia/ kumlea mtoto wako ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha mtoto na kutambua viashiria vya hatari kwa mtoto wako.Pia Kuanzia wakati huu unashauriwa kutembea na taarifa zako zote  za uzazi popote unapo kwenda kwasababu unaweza kupatwa na uchungu wakati wowote ili uweze pata msaada kwa urahisi.Wakati huu mtoto huanza kufumbua macho.


Maendeleo ujauzito wiki thelathini na mbili.

Wakati huu mifupa ya mtoto inakuwa ishaundwa kwa ukamili lakini bado inakuwa laini,mtoto hufungua na kufumba macho Kulingana na mabadiliko ya mwanga,pia mwili wa mtoto huanza kuhifadhi madini muhimu Kama vile madini ya chuma pamoja na calcium,vile vile nywele laini zilizo jitokeza Katika mwili wa mtoto hutoweka,pia hadi kufikia wakati huu kichocheo Cha prolactin kinakuwa kishafanya maandalizi ya kutosha ya kutoa maziwa pindi mtoto atakapo zaliwa hivyo basi kuanzia wakati huu mama unaweza ukaanza kuona majimaji ya njano Katika chuchu zako hivyo usishangae uonapo hali hii.


Maendeleo ujauzito wiki ya thelathini na sita.

Wakati huu mtoto hugeuka kichwa chake huelekeza Katika mlango wa kizazi tayari kwa kujifungua.Wiki ya thelathini na Saba huchukuliwa Kama ni wakati mwafaka wa mtoto kuzaliwa japo Kuna wengine wanaweza wasijifungue wakati huu badala yake wakajifungua Katika wiki ya 38,39 hadi wiki ya 40


Kujifungua.

Safari ya ujauzito huishia Katika wiki ya arobaini japo kuna ambao wata jifungua kabla ya muda huu  na wengine wanaweza wakapitiliza hadi wiki ya arobaini na mbili, tarehe ya kujifungua hukadiriwa kutoka katika siku yako ya Kwanza ya kupata hedhi kwa Mara ya mwisho hivyo basi kunawengine wanaweza bahatika kujifungua Katika tarehe iyo pia wengine wanaweza wasijifungue Katika tarehe hiyo,lakini kwa kawaida unaweza kujifungua wiki moja au mbili kabla ya tarehe ya matazamio au wiki moja au mbili baada ya tarehe ya matazamio .
Share:

Je ,umepanga kushika mimba?je wajua mambo gani ni muhimu kufanya kabla ya kushika mimba?

Utangulizi.

Yawezekana wakati huu wewe na mwenza wako mnapanga kupata familia/ mpo Katika mahangaiko ya kutafuta familia /pengine mnatarajia kupata familia hivi karibuni,lakini Kuna mambo kadhaa ambayo ni lazima uyafikirie kabla ya kufanya maamuzi ,Jambo la Kwanza ni lazima ufikirie mwenza wako atakuwa tayari kukubaliana na wazo lako,Jambo la pili mtindo wa maisha hauta athiriwa na mimba ambayo utakuwa nayo,tatu hali ya uchumi inaruhusu kuwa na familia  na ukailea Katika misingi iliyo bora, na wakati mwingine ni lazima ufikirie afya yako kama haitoweza kuleta athari kwako au mtoto wakati wa mimba,kujifungua/baada ya kujifungua.

Wakati wa ujauzito ni lazima ubadilishe mtindo wa maisha ambao ulizoeleka kuuishi kabla ya kupanga kuwa mjamzito/ wakati wa ujauzito kwasababu mambo mengi ambayo utayafanya Katika mwili wako huenda kuleta athari moja kwa moja katika mwili wako na mtoto pia.

Kwa maana hiyo tunajifunza ,kumbe mwanzo mzuri wa maisha bora ya mama na mtoto wake wakati wote wa ujauzito ,kujifungua na baada ya kujifungua una tegemeana na maamuzi ambayo wenza/ mwenza aliyafanya kabla ya kuamua kushika mimba,hivyo basi kama ulifanya maamuzi yasiyo sahihi basi  kuna uwezekano mama na mtoto wakapata matatizo wakati wa ujauzito,kujifungua au wasipate malezi bora,lakini kumbe ukifanya maamuzi sahihi leo kabla ya kupanga na mwenza wako kupata mtoto uwezekano wa mama na mtoto kupata matatizo katika kipindi chote cha cha ujauzito mpaka malezi huwa ni mdogo hivyo familia yako kuwa yenye afya bora.



Mambo ya kufanya kabla ya kushika mimba.

Najua wachache watakuwa wanatambua mambo haya hususani wale ambao washaingia kwenye familia lakini wengi wetu hatujui mambo haya ambayo ni msingi wakati wote wa ujauzito na malezi, mambo hayo ni:

.Acha Kutumia uzazi wa mpango.

Kama ulikuwa unatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango ni wakati Sasa wa Kuacha Kutumia njia hizo,Kuna baadhi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango huchukua muda mrefu kushika mimba baada ya Kuacha kuzitumia,hivyo kadiri utakavyo chelewa Kuacha Kutumia njia hizo ndivyo utakavyo chelewa kushika mimba.

.Onana na mtaalamu wa afya.

Kabla ya kubeba ujauzito ni vema zaidi kupanga na kuonana na mtoa huduma wa afya ili kushauriwa mambo mbali mbali, wakati mwingine ni muhimu kuonana na mtaalamu kabla kuliko kuonana na mtaalamu baada ya kushika mimba,hii huondoa athari ambazo zinaweza kuathirika afya ya mama na mtoto.

Kwa kawaida wajawazito wengi huudhuria kliniki kwa kuchelewa Sana hii husababisha kuchelewa kupata baadhi ya huduma za msingi kwa ukuaji wa mtoto, kwa kawaida kipindi Cha mwanzo Cha ujauzito ndicho kipindi ambacho uundaji wa viungo mbalimbali vya mtoto hufanyika hivyo mama akichelewa Kuna uwezekano mtoto kuzaliwa akiwa na mapungufu.

Kuonana na mtaalamu kabla ya ujauzito hulenga kutambua viashiria hatari kwa mjamzito na kuandaa jinsi ya kukabiliana navyo Katika wakati wote wa ujauzito mfano umri zaidi ya miaka 35,umri chini ya miaka 20 n.k,pia huduma hii hutoa hutoa fursa ya kupanga na kufanya maandalizi kabla ya ujauzito,vile vile hutoa fursa kwa wenza kupima afya zao kabla ya ujauzito ili kujua Jinsi ya kuwa saidia endapo watakuwa  na tatizo,Pia hutoa fursa ya mama kuanza matibabu ya dawa na virutubisho vya kumsaidia Mama kwa ujauzito ikiwa ni pamoja na kutibu Magonjwa ambayo yanaweza kuleta athari kwa mimba.

.Pata chanjo .

Kuna magonjwa mengi ambayo yanazuilika, ambayo Kama endapo hauta pata chanjo yanaweza kuathiri afya ya mama na mtoto,kwaiyo moja ya Mambo ambayo ni lazima kufanya  ni lazima kuhakikisha unapata chanjo.

.Panga bajeti yako.

Wakati wa ujauzito huwa haueleweki  kwa kuwa Kuna mambo mengi ambayo yanaweza jitokeza wakati wowote,hivyo basi ni vema kuanza kujiwekea akiba kidogo kidogo pindi tu mnapofikiria kushika mimba ili pesa hizo zipate kuwafaa wakati wowote itakapo tokea dharura.

.Badilisha mtindo wa maisha.

Kama ulikuwa unakunywa pombe,unavita sigara,hufanyi mazoezi ni wakati Sasa wa kubadili mtindo huo wa maisha na kuishi maisha ambayo hayato kuwa na athari Katika afya yako na mtoto atakaye kuwa tumboni.

Acha Kutumia pombe,unywaji wa pombe huathiri afya yako pamoja na mtoto tumboni,chemicali zilizopo kwenye pombe huingia moja kwa moja Katika mfumo wa damu na kuleta athari za moja kwa moja kwa mwanao,athari ambazo zinaweza jitokeza ni pamoja na mimba kuharibika, mtoto kufia tumboni,mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo,mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu wa viungo vile vile mtoto anaweza kuzaliwa na ulemavu wa akili.

Acha Kutumia sigara,moshi ambao una tokana na sigara hutoa chemicali mbalimbali ikiwemo hewa chafu ya carbondioxide na nicotine,chemicali hizi pia huingia moja kwa moja katika mzunguko wa damu na kuathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto,chemicali hizi zinaweza sababisha kupungua kwa usafirishaji wa hewa ya oxygen kwa mtoto hivyo mtoto kukosa hewa Safi,vile vile nicotine huongeza mapigo ya moyo na shinikizo la damu kwa Mama hivyo mama kuwa Katika hatari na kupata shinikizo la damu wakati wa ujauzito,pia chemicali hizi zaweza sababisha kupungua kwa usafirishaji wa virutubisho vya muhimu kwa mtoto hivyo afya ya mtoto kudorora. Sigara huongeza hatari ya mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo Katika mfumo wa upumuaji mfano asthma,vile vile mtoto kuzaliwa mlemavu,kujifungua kabla ya wakati n.k,kwahiyo ni vema Kuacha Kutumia sigara kabla ya kujaribu kushika mimba na Kuacha Kutumia kabisa hata baada ya kujifungua kutokana na madhara niliyo yaeleza.

Anza kufanya mazoezi,kufanya mazoezi kabla ya ujauzito,wakati was ujauzito na baada ya kujifungua ni muhimu Sana,mazoezi kabla husaidia kuandaa mwili wako kupambana/ kukabiliana na mabadiliko yote ambayo hutokea wakati wa ujauzito,pia husaidia kuimarisha misuli ya mwili na kujenga stamina ili iwe rahisi wakati wa kujifungua pia mwili wako uweze kurudi kwa haraka zaidi Katika hali yake baada ya kujifungua,pia mazoezi humkinga mama dhidi ya kisukari ambacho hutokana na ujauzito.Kuna baadhi ya Wanawake hudhania wakati wa ujauzito ni wakati wa kupumzika tu hivyo hawatakiwi kabisa kujihusisha Katika mazoezi yoyote.Hata hivyo Kuna baadhi ya matatizo ambayo huitaji kufanya mazoezi kwa uangalizi au Kuacha kabisa kufanya mazoezi kutokana na athari ambazo zinaweza jitokeza, baadhi ya Mambo hayo ni pamoja na ugonjwa wa kisukari,ugonjwa wa kifafa,kuwa na historia ya kupata uchungu kabla ya wakati,mwenye historia ya kuharibika kwa mimba,shinikizo la damu,kondo la nyuma kujishikiza Katika njia ya kutokea mtoto n.k ,hivyo basi kabla ya kuanza kufanya mazoezi ni vema kuonana na mtaalamu ili aweze kukushauri mazoezi ambayo yatakufaa Kulingana na hali yako .

.Hakikisha una pata lishe bora.

Kula chakula bora haitakiwi tu wakati wa ujauzito pekee bali hata kabla na baada ya kujifungua,chakula bora wakati wa ujauzito husaidia kuupa mwili wako virutubisho bora kabisa tayari kwa kupokea ujauzito,siyo vema kushika ujauzito huku afya yako ikiwa imedhoofu kutokana na kukosa lishe bora kwasababu afya ya mtoto tumboni nayo itadhoofu kutokana na kukosa virutubisho vya msingi kutoka kwa mama.Vile vile kipindi Cha mwanzo ni kipindi muhimu Sana wakati wa ujauzito pia ni kipindi ambacho viungo vya  mtoto hutengenezwa hivyo kuhitaji zaidi virutubisho vya muhimu.

Pia wakati wa ujauzito  uhitaji wa chakula huongezeka kutokana na uwepo wa mtoto tumboni,kwahiyo utalazimika kuongeza idadi ya Milo ya chakula ambavyo vina kiwango Cha kutosha Cha madini ya chuma ,calicium na vitamini virutubisho hivyo ni muhimu Katika ukuaji na maendeleo ya mtoto.
Vile vile lishe bora husaidia uzalishaji wa maziwa ya kutosha baada ya kujifungua na kipindi chote Cha unyonyeshaji.Ulaji wa mboga mboga na matunda hushauriwa zaidi wakati wa ujauzito kwasababu ni vyanzo vikuu vya madini ya chuma na vitamini.

.Anza Kutumia folic acid.

Folic acid ni vitamin B9 ambayo hupatikana Katika baadhi ya vyakula pia hupatikana katika mfumo wa kidonge.Matumizi ya folic acid kabla ya ujauzito husaidia mtoto kuwa na afya bora,pia humsaidia mtoto asipatwe na upungufu wa damu.Kwaiyo Kama unatarajia kushika mimba ni muhimu Sana Kutumia vidonge vya folic acid angalau miezi miwili hadi miezi mitatu kabla ya kushika mimba hii husaidia mwili kuwa na kiwango Cha kutosha Cha vitamin B9 hivyo husaidia mtoto asizaliwe na tatizo la mgongo wazi(spinal bifida).Vile vile unaweza Kutumia vyakula ambavyo vina vitamini B9 lakini vyakula hivyo pekee havijitoshelezi kukupa kiwango Cha kutosha Cha vitamin hivyo ni lazima utumie vidonge mfano wa vyakula hivyo ni matunda(parachichi,machungwa ,papai n.k),mboga za majani,maharage,karoti n.k.
Licha ya kutumia folic acid kabla ya ujauzito ni lazima kuhakikisha unaendeleaje Kutumia dawa hizo Katika kipindi chote Cha ujauzito.


Kwa mambo mbali mbali yanayo husu  ujauzito,afya ya mama na mtoto karibu tukushauri.



Asante.
Share:

Nini husababisha Kipimo Cha mimba kutoa majibu chanya ya uongo?



Utangulizi.

Matokeo chanya ya uongo yamekua yakileta athari kwa Wanawake wengi hususani kwa wale ambao wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu kupata ujauzito,Wanawake wengi hufurahi baada ya kupata matokeo chanya lakini furaha hiyo hupotea baada ya kutambua majibu aliyo yapata haya kuwa ya kweli.

Kwa upande mwingine matokeo chanya ya uongo yaweza leta athari kwa Wanawake ambao hawapo tayari kubeba ujauzito, habari njema ni kwamba ni mara chache Sana hutokea matokeo chanya ya uongo lakini hutokea.

Kwahiyo ni muhimu Sana kujua Jinsi kipimo kinavyo tumika ili kuweza kubaini matokeo tofauti ambayo yanaweza onekana Katika kipimo.

Kama nilivyo eleza awali,kipimo Cha mimba kwa kutumia mkojo ndicho kipimo ambacho hutumika zaidi kutambua ujauzito,pia kipimo hiki kinaweza kutumika na muhusika kutoka katika duka la dawa na kujipima Kama anahisi ana dalili ya ujauzito,vile vile kipimo hiki hutumika Katika kituo Cha kutolea huduma na mtaalamu wa maabara kutambua uwepo wa mimba.

Kipimo hiki hutambua kichocheo Cha mimba kwenye mkojo,kichocheo hiki huzalishwa na kondo la nyuma baada ya yai lililo rutubishwa kujishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba,Kama kichocheo Cha mimba kipo tayari kwenye mkojo kipimo kinaonesha mistari miwili ikimaanisha uwepo wa ujauzito ,pia Kama kichocheo hakipo kwenye mkojo kipimo kitaonesha mstari mmoja ikimaanisha si mjamzito.



Je ,nini huweza sababisha majibu chanya ya uwongo?

Kuna mambo kadhaa ambayo huweza sababisha kipimo kioneshe majibu chanya ya uongo,miongoni mwa mambo hayo ni  pamoja na:

.Mimba kuharibika.

Kwa kawaida kipimo Cha mimba kitaendelea kuonesha kuwa kuna ujauzito kwa muda fulani baada ya mimba kuharibika au kutoka.Wakati wa ujauzito utengenezaji wa kichocheo Cha mimba huongezeka kadiri mimba inavyo dhidi kukua,baada ya mimba kutoka/ kuharibika kichocheo Cha mimba hupungua taratibu Sana.Pia Kama mimba ilitoka yenyewe Kuna uwezekano baadhi ya mabaki kuendelea kutengeneza kichocheo Cha mimba kwahiyo ni bora kwenda hospitali kuchunguza Kama Kuna mabaki yoyote, kwahiyo Kuna uwezekano mkubwa Sana kupata majibu chanya ya uongo baada ya mimba kuharibika/ kutoka yenyewe.

.Matumizi ya dawa .

Matumizi ya dawa za matibabu ya uzazi yaweza sababisha  kipimo Cha mimba kuonesha majibu chanya ya uongo,dawa za matibabu ya uzazi zina kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin ndani yake ,kwahiyo Kutumia dawa hizo husababisha kichocheo hicho kuwepo kwenye damu pamoja na mkojo,kwahiyo Kama ulikuwa unatumia dawa hizi na ukahisi una mimba ni vema angalau kusubiri kwa muda wa wiki mbili Kisha ukapima.Dawa zingine ambazo zinaweza kuchangia kipimo Cha mimba kuonesha majibu chanya ya uongo ni dawa za Magonjwa ya akili mfano Xanax,varium,cpz , phenobarbital n.k,dawa zingine ni methadone,lasix , promethazine.

.Kukiacha kipimo kwa muda mrefu bila kusoma majibu.

Maelezo yaliyopo Katika pakiti ya kipimo  yana maana kubwa sana Katika kutoa majibu sahihi,lakini endapo kipimo kitafanyika kinyume na maelezo Kuna uwezekano wa kupata majibu ya uongo. Kila kipimo Cha mimba kina maelezo ya muda ambao unatakiwa kusoma majibu kwahiyo endapo hujasoma majibu kwa muda ulio pangwa mkojo uliofyonzwa na kipimo hutoweka na matokeo yake baada ya kuonekana mstari mmoja itaonekana mistari miwili ,mstari wa pili unaweza ukawa hauonekani Sana au unaonekana kwa kufifia.Kwahiyo ili upate majibu sahihi ni lazima kuzingatia muda ulio pangwa mfano Kama unatakiwa kusoma majibu baada ya dakika mbili fanya ivyo,pia Kama ni dakika tano fanya ivyo.

.Kutumia kipimo kilicho isha muda wa matumizi.

Kipimo ambacho muda wake wa matumizi kikiendelea kutumika kinaweza sababisha kemikali iliyopo kwenye kipimo kutoa majibu ya uongo  hasi,chanya au batili, Kwahiyo Kama unachukua jukumu la kujipima nyumbani hakikisha unaangalia muda wa matumizi wa kipimo Kama umepita au bado Kama umepita ni vema kununua kipimo ambacho muda wake haujaisha.

.Mimba kutungwa nje ya uzazi.

Wakati mwingine yai lililo rutubishwa laweza tungwa nje ya mji wa mimba,kuna mambo mbali mbali ambayo huchangia mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi ,baadhi ya Mambo hayo ni uwepo wa makovu kwenye mirija ya inayo safirisha yai kutoka kwenye mfuko wa mayai kwenda kwenye mji wa mimba, Maambukizi kwenye via vya uzazi,kufunga kizazi n.k,mimba iliyo tungwa nje ya tumbo la uzazi haiwezi tena kuwa mimba ya kawaida kwa kuwa hakuna sehemu ya mimba iyo kuendelea kukua hivyo basi itatakiwa kuondolewa kabla ya kuleta athari kubwa,japo kuwa mimba imejishika sehemu ambayo siyo ya kwake itazalisha kichocheo Cha mimba na ukipma mkojo itaonesha majibu chanya.

.Magonjwa.

Kuna baadhi ya Magonjwa yanaweza sababisha kupata majibu chanya ya uwongo ,Magonjwa hayo ni Kama Maambukizi ya bakteria Katika njia ya mkojo,Magonjwa ya figo ambayo husababisha kuwepo kwa seli za damu kwenye mkojo,uvimbe kwenye mfuko wa mayai hususani kwenye corpus luteum, matatizo Katika tezi ya pituitary japo yaweza tokea mara chache Sana.

.Mimba ya kikemikali.

Hii ni hali ambayo mimba iliyotungwa hukadiriwa kutoka yenyewe kabla ya wiki ya tano ya ujauzito.Wanawake wengi ambao hupata aina hii ya mimba huwa hawatambui kuwa ni wajawazito bali huchelewa kupata hedhi.
Mimba ya kikemikali huelezwa hutokana na yai lilito rutubishwa kuwa na matatizo ya chromosome,kwahiyo mwili wenyewe huitoa mimba pindi unapo tambua kuwa siyo sahihi.Japo yai lina kuwa hali jajishikiza moja kwa moja hutengeneza kichocheo Cha mimba hivyo basi ukipima mimba utapata majibu chanya ya uongo.

.Kutumia kifaa kichafu kuweka mkojo.

Mkojo ambao umewekwa kwenye kifaa ambacho siyo kisafi unaweza ukawa umechanganyika na vitu mbali mbali matokeo yake kipimo kitatoa majibu yauongo chanya/ hasi.



Nini ufanye ili usipate majibu chanya ya uongo unapo fanya kipimo nyumbani?

.Hakikisha unaweka mkojo kwenye chombo kisafi ambacho hakina kitu chochote ndani yake.

.Hakikisha hutumii kipimo ambacho wakati wake umepita badala yake tumika kipimo kingine.

.Soma majibu ndani ya muda ulio pangwa kutokana na kampuni iliyo tengeneza kipimo ,ikiweze ana kama ni dakika tano au mbili weka alamu ili muda ukifika usome majibu.

.Pia usipime mimba muda mfupi baada ya mimba kuharibika au kutoka yenyewe.

.Kama unatumia dawa za matibabu ya uzazi ni vema kupima mimba angalau baada ya wiki mbili tangu Kuacha Kutumia dawa izo.

.Mwisho kwa wale ambao wanashindwa/ wata pima na kupata majibu ni vema kwenda hospitali ili kuthibitisha kutoka kwa wataalamu wetu.



KARIBU.
Share:

Nini husababisha kipimo Cha mimba kuonesha majibu hasi ya uongo licha ya kukosa hedhi?



Utangulizi.

Mara nyingi mwanamke  anapokosa hedhi japo kwa mwezi mmoja jambo ambalo humjia kichwani mwake ni kwamba huenda labda atakuwa mjamzito,anaweza akahisi kichefuchefu,kutapika ,maumivu kwenye maziwa/ anaweza akapata dalili zote za awali za uwepo wa ujauzito.

Baada ya kuhisi na kupata viashiria vya awali vya uwepo wa ujauzito ndipo huamua kununua kipimo na kujipima kabla ya kwenda kwa mtaalamu kutokana na vipimo kupatikana kwa urahisi kwa gharama nafuu,hata ivyo baada ya kupima majibu  huonekana kuwa hana ujauzito.

Hapo ndipo swali lingine huibuka je ,majibu aliyo yapata ni sahihi au siyo sahii? Wazo linalo kuja baada ya hapo ni kwenda Katika kituo Cha kutolea huduma ili kupata kuhakikisha/kuthibitisha Kama majibu hayo ni sahihi au siyo sahii.

Ni kweli kabisa kuna wakati kipimo kinaweza kikaonesha hauna ujauzito wakati kiuhalisia una ujauzito  na wakati mwingine kukosa hedhi lakini ukawa hauna ujauzito.

Kwa pamoja naomba fuatilia somo hili ili kupata kujua ni kitu gani ambacho huchangia kutokea kwa mambo haya yenye kuleta utatanishi.


Je Sababu gani hupelekea kipimo kioneshe hauna ujauzito licha ya kutokuona hedhi?

Kuna mambo kadhaa ambayo huweza kusababisha kipimo kitoe majibu hasi licha ya kuwepo kwa viashiria vyote vya ujauzito ,mambo hayo ni Kama ifuatavyo hapo chini:

.Kufanya kipimo mapema.

Mwili hauwezi kutengeneza kichocheo Cha mimba(human chorionic gonadotrophin) Kama bado mimba haijajishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba( uterus),mimba ikisha jishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba kondo la nyuma/ plasenta itaanza kuzalisha kichocheo Cha HCG.
Kwa kawaida toka mimba kutungwa huchukua takribani siku kumi hadi kumi na nne hadi kichocheo Cha mimba kuonekana kwenye mkojo.Kwaiyo endapo kipimo kitafanyika chini ya wiki mbili tangu kutungwa kwa mimba basi tegemea kabisa kupata majibu hasi hata kama unaujauzito,hushauriwa kupima mimba baada ya kukosa hedhi ya mwezi unao fuata.

.Kiwango kidogo Cha kichocheo Cha mimba kwenye mkojo(HCG).

Hushauriwa kupima mimba kwa Kutumia mkojo wa asubuhi kwa sababu kichocheo Cha mimba huwa kwa kiwango kikubwa kwenye mkojo wa asubuhi kuliko mkojo wa wakati mwingine.Mkojo wa asubuhi hukadiriwa kuchukua muda mrefu toka kukojoa kwa mara ya mwisho,kwahiyo endapo hautapima kwa Kutumia mkojo wa asuuhi Kuna uwezekano ukapata matokeo hasi licha ya kuwa na ujauzito. Kwahiyo Kama utaamua kupima mimba kwa kutumia mkojo ambao siyo wa asubuhi hushauriwa angalau kukaa masaa kadhaa bila ya kukojoa  kisha ufanye kipimo.

.Mimba kutunga nje ya mji wa mimba.

Ni mara chache mimba hutungwa nje ya tumbo la uzazi mara nyingi kwenye mirija ya falopia inayo safirisha yai hadi kwenye mji wa mimba.Hali hii husababisha kuchelewa kuzalishwa kwa kichocheo Cha mimba,hivyo kuna uwezekano ukipima mimba kipimo kikaonesha hauna wakati unayo.Nenda hospitali ukafanyiwe uchunguzi endapo kipimo kinaonesha hauna ujauzito lakini una dalili hizi, Maumivu makali chini ya kitofu au upande mmoja,kutokwa na damu,kuhisi kichefuchefu na kutapika pia kupata Kizunguzungu.

.Kutumia kipimo ambacho kimeisha muda wake.

Kila kipimo kina muda maalumu ulio pangwa kitumike ,endapo kinatumika baada ya muda wake kuisha basi Kuna uwezekano mkubwa kikatoa majibu hasi ya uongo,vile vile kila kipimo huelezwa kiifadhiwe Katika mazingira flani mfano kuna baadhi ya vipimo huelezwa visi hifadhiwe Katika mazingira ambayo yana joto ridi kiwango fulani na endapo kikahifadhiwa Katika mazingira yasiyo takiwa ufanisi wa kutoa majibu sahihi hupungua,kwahiyo kabla huja nunua kipimo/ kabla huja kitumia kumbuka kuangalia muda kipimo kimetengenezwa na muda wa kuisha kufanya kazi.

.Makosa Katika Utumiaji.

Vipimo huwa na maelezo tofauti tofauti Jinsi ya kutumia kutokana na kampuni inayo tengeneza vipimo hivyo,kuna vipimo vingine ili vitoe majibu sahihi huitaji kiwango kidogo Cha mkojo kwahiyo endapo utatumia mkojo mwingi basi tegemea kupata majibu ya uongo,vile vile Kuna vipimo ambavyo vinahitaji mkojo mwingi ili vitoe majibu sahihi kwahiyo endapo utaweka mkojo kidogo Kuna uwezekano mkubwa wa kupata majibu yasiyo sahihi,kwahiyo ni vema kusoma au kuomba ushauri Jinsi ya kutumia kipimo husika kabla hujakitumia.

.Mimba ya mtoto zaidi ya mmoja.

Kichocheo Cha mimba huzalishwa kwa kiwango kikubwa kwa Mwanamke ambaye ana mtoto zaidi ya mmoja tumboni,kwaiyo kutokana na kichocheo Cha mimba kuzalishwa kwa kiwango kikubwa kwenye mkojo Kuna uwezekano kipimo kikashindwa kutoa majibu yasiyo sahihi.

.Mzunguko wa hedhi unao badilika badilika.

Kwa wale ambao mzunguko wao una badilika badilika Mara kwa mara ni ngumu Sana kutambua siku gani yai linaweza kupevuka na Kuna uwezekano wa kupata mimba,mara nyingi wenye mizunguko ya namna hii wanaweza kupata mimba bila ya kujijua,kwaiyo kutokana na kuto kujua wanaweza jikuta wanafanya kipimo kabla ya wakati  na kuonekana hawana kumbe wana mimba.



Hata hivyo endapo ukafanya kipimo na  ikaonekana hauna ujauzito na ukachelewa/ hauja pata hedhi uwezekano wa kuwa mjamzito haupo,hedhi inaweza kuchelewa kutokana na msongo wa mawazo au Magonjwa.

Kama kipimo kimeonesha hauna ujauzito na haujafanya kwa kuwahi yawezekana Kuna mambo kadhaa Katika mwili wako yatakuwa yamechangia usipate hedhi/ uchelewe kuona hedhi mambo hayo ni pamoja na:


. Unyonyeshaji.

Wakati wa kunyonyesha mwili hutengeneza kichocheo Cha prolactin ambacho husaidia kuzalisha Maziwa kwa wingi,kuzalishwa kwa kichocheo hiki kwa wingi husababisha mayai yasipevuke  hivyo mwanamke anaweza asipate hedhi Kama ana nyonyesha kikamilifu au akachelewa kupata hedhi .


.Msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo unaweza sababisha kuvurugika kwa mfumo wa vichocheo vya mwili hivyo kusababisha mwanamke kukosa hedhi/kuchelewa kupata hedhi.

.Matumizi ya baadhi ya dawa.

Kila dawa huleta maudhi madogo kwa mtumiaji,kuna baadhi ya dawa zikitumika husababisha kukosekana kwa hedhi / kuchelewa kwa hedhi baadhi ya dawa hizo ni dawa za matibabu ya magonjwa ya akili.

.Mazoezi kupitiliza, husababisha kuvurugika kwa hedhi kutokana na matumizi makubwa ya nishati mwilini.

.Matumizi ya  njia za uzazi wa mpango.

Ni kawaida Sana kwa Wanawake wanao tumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kukosa hedhi au kuchelewa kupata hedhi.

Sababu zingine ni ,kuwa na uzito mdogo, kuwa na uvimbe kwenye tezi ya pituitary, uvimbe kwenye vifuko vya mayai,kubadilisha mazingira pamoja na aina ya chakula ambacho kinatumiwa.



Nini ufanye ili usipate majibu hasi ya uongo?

.Hakikisha unapima angalau baada ya kukosa hedhi ya mzunguko unao fuata.

.Hakikisha una tumia kipimo kwa usahihi kwa kufuata maelezo yaliyo tolewa na watengenezaji.

.Angalia kipimo Kama muda wake wa matumizi umeisha / bado kama umeisha usitumie badala yake kanunue kipimo kingine.

.Hakikisha unatumia mkojo wa asubuhi kujipima/ Kama hauto tumia basi angalau kaa kwa masaa kadhaa bila kukojoa kisha upime.

.Hakikisha haunywi maji mda mda mchache kabla ya kufanya kipimo ,kwasababu ukinywa maji utapunguza kiwango Cha kichocheo Cha mimba kilichopo kwenye mkojo.



Asante.
Share:

Utathibitishaje uwepo wa mimba na kwa wakati gani?



Kipimo Cha mimba.

Mimba hutokana na muunganiko unao tengenezwa baada ya mbegu ya kiume kukutana na yai,ili mimba iweze kutungwa ni lazima mayai/ yai liachiliwe kutoka katika moja ya vifuko vya mayai, mayai / yai huachiliwa katikati mwa mzunguko wa hedhi,pia mzunguko wa hedhi huto fautiana baina ya wanawake, kwa Mwanamke Mwenye mzunguko wa siku ishirini na nane tunategemea siku ya kumi na nne yai liachiliwe.

Kwa kawaida yai huachiliwa katikati mwa mzunguko wa hedhi wa Mwanamke,yai husafiri taratibu kupitia mirija ya uzazi kuelekea kwenye tumbo la uzazi,wakati yai linasafiri endapo Mwanamke atashiriki tendo la ndoa na mwanaume mwenye kutoa mbegu bora,basi Mwanamke atapata mimba.

Baada ya mimba kutungwa seli hugawanyika na kutengeneza seli zingine mpya,seli mpya nazo hugawanyika na kutengeneza kiini tete.Baadhi ya seli zilizo undwa hutengeneza maji Katika chupa ya uzazi na zingine huunda plasenta.


Nitajuaje Kama ni mjamzito?

Unaweza kutambua uwepo wa ujauzito kwa kuangalia dalili mbali mbali ambazo hujitokeza,dalili hizo ni pamoja na kuhisi kichefu chefu,kutapika, kukosa hedhi n.k.

Lakini hata hivyo huwezi kuthibitisha uwepo wa mimba kwa kuangalia dalili pekee kwa Sababu dalilli za magonjwa hufanana ,kwaiyo unaweza fikiri ana mimba kwasababu amekosa hedhi lakini ikawa siyo mimba,hivyo basi kipimo pekee kitathibitisha uwepo wa mimba.

Miongoni mwa vipimo hivyo ni pamoja na;

. Kipimo Cha mkojo (UPT)

Hiki ni kipimo ambacho kinaweza fanywa na muhusika Kwa kununua kutoka katika duka la dawa baridi,vile vile kipimo hiki hufanywa na wataalamu wa maabara katika kituo Cha kutolea huduma,na ndicho kipimo ambacho hutumika  zaidi kutambua mimba.

Kipimo Cha mkojo hufanya kazi kwa kutambua uwepo wa kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin kwenye mkojo, kichocheo hiki hutengenezwa na kondo/ placenta Mara baada ya yai lililo rutubishwa kujishikiza kwenye mji wa mimba na uzalishaji wake huongezeka kadiri mimba inavyo kuwa.

Kwa kawaida kichocheo hiki huanza kuonekana kwenye mkojo baada ya wiki mbili tangu kutungwa kwa mimba. Chemicali iliyotumika kuunda kipimo hiki hubadilika rangi pindi inapokutana na kichocheo kilichopo kwenye mkojo.

Kwaiyo ili kupata majibu sahihi hushauriwa kupima baada ya kukosa hedhi,pia hushauriwa kupima zaidi asubuhi kuliko mchana kwasababu mkojo wa asubuhi huwa na kiwango kikubwa Cha kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin kuliko wakati wowote hivyo uwezekano wa kupata majibu sahii ni mkubwa kuliko wakati ambao kichocheo hiki kina kuwa kwa kiwango kidogo kwenye mkojo.

.Kipimo Cha damu.

Hiki ni kipimo kinacho fanywa na wataalamu wa maabara ili kutambua uwepo wa kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin kwenye damu,vile vile kipimo hiki hutambua kiwango Cha kichocheo Cha mimba(HCG) kilichopo kwenye damu.



Jinsi ya kutumia kipimo Cha mkojo.

Kipimo hiki hupatikana kwenye maduka ya dawa,na pharmacy kwahiyo kutokana na kupatikana kwa urahisi na gharama zake kuwa nafuu  kina weza tumika hata nyumbani kwa kufuata maelezo bila uwepo wa mtaalamu wa maabara,lakini hata hivyo kutokana na kuto kuelimishwa namna ya kutumia kipimo hiki wakati mwingine kinaweza kutoa majibu ya uwongo, yafuatayo ni maelezo Jinsi ya kupima mimba kwa mkojo.

.Hakikisha unapima /unapimwa mkojo baada ya kukosa hedhi Katika mzunguko unaofuata.

.Hushauriwa zaidi kupima wakati wa asubuhi,japo unaweza kupima wakati wowote ule kwahiyo hakikisha unaweka mkojo Katika chombo kikavu pia kisafi.

.Kisha toa kipimo kutoka kwenye pakiti Kisha tumbukiza kipimo kwenye kifaa Cha mkojo upande wenye uelekeo wa mshale,hakikisha kipimo kina zama kwenye chombo hadi kwenye mstari,Kisha toa baada ya dakika moja.

.Subiri majibu kwa dakika chache,endapo ukatokea mstari mmoja Basi siyo mjamzito na ikitokea mistari miwili tambua ni mjamzito hivyo utalazimika kwenda Katika kituo Cha kutoa huduma ili wapate uthibitiwa na hatimaye uendelee na huduma zingine za clinic.


Usikose kufuatilia muendelezo wa somo hili wakati ujao.


KARIBU.


Share:

Lini naweza kujifungua baada ya kushika mimba?



Jinsi ya kutambua tarehe ya matazamio ya kujifungua.

Kwa kawaida huchukua takribani miezi tisa hadi kumi tangu kutungwa kwa mimba hadi kujifungua.

Mimba hukadiriwa kutungwa katika tarehe ya kuanza kuona damu/ hedhi kwa mara ya mwisho,tarehe ya kwanza ya kuona hedhi kwa Mara ya mwisho huchukuliwa Kama siku ya kwanza ya mimba japo uwezekano wa kushika mimba huwa ni wiki mbili tangu kuanza kwa hedhi.

Kukadiria siku ya matarajio ya kujifungua siyo sayansi iliyo kamili kwasababu kuna Wanawake ambao wanaweza kujifungua Katika tarehe ya makadirio na wengine kushindwa kujifungua Katika tarehe zilizo kadiriwa.

Japo kuwa siyo sayansi  iliyo kamili ,lakini ni vema kupata uelewa ni lini mtoto anaweza kuzaliwa,ili kuweza kuandaa mahitaji ya msingi ya Mama na mtoto mapema zaidi ,pia husaidia mama kujua ukuaji na maendeleo ya mtoto kulingana na mwezi.



Je nawezaje kujua tarehe ya matazamio ya kujifungua?

Unaweza kutambua tarehe ya matazamio kwa Kutumia njia kadhaa,njia izo ni:

.Njia ya hesabu.

Ni njia ambayo hujumuisha kukokotoa hesabu rahisi,hii hutumika kwa Wanawake ambao mizunguko yao ni siku ishirini na nane ,au yai huachiliwa katikati mwa mzunguko yaani siku kumi na nne,pia mizunguko yao haibadiliki badiliki.

Kuna kanuni maalumu ambayo hutumika kukisia tarehe ya matazamio ya kujifungua, kanuni hiyo huitwa naegele's rule.

Kabla ya kuitumia kanuni hii hakikisha unaijua tarehe ya kuanza kupata hedhi kwa mara ya mwisho,kisha andika kwenye karatasi ambayo utaitumia kufanya hesabu rahisi.

Baada ya kuandika tarehe husika kwenye karatasi /daftari lako ,ongeza/jumlisha Saba sehemu ya tarehe.

Sehemu ya mwezi toa tatu endapo ni zaidi ya miezi mitatu,yaani Kama itakua mwezi wa nne,tano,sita ,Saba na kuendelea,Kisha jumlisha moja sehemu ya mwaka.

Kama ni chini ya miezi minne yaani ni mwezi wa tatu,wa pili na wa kwanza, jumlisha tisa sehemu ya mwezi na sehemu ya mwaka usijumulishe namba yoyote,Bali utabaki mwaka uliopo.


Mfano,mteja "Y" alianza kuona damu kwa Mara ya mwisho tarehe 2/3/2019,je ipi ni tarehe ya matarajio ya kujifungua?


Tarehe ya  kuanza hedhi kwa Mara ya mwisho.                                        2/3/2019.

+ Saba tarehe,na Tisa mwez     7/9

Tarehe ya matazamio ni            9/12/2019.




Mfano 2,mteja "B" alianza ona damu kwa Mara ya mwisho tarehe 10/9/2019,je ipi ni tarehe ya matarajio ya kujifungua?


Tarehe ya kuanza hedhi kwa mara ya mwisho                                   10/9/2019 .

+ 7 tarehe,-3 mwez,+1mwk  7/-3/+1.

Tarehe ya matazamio ni      17/6/2020.                                   


Lakini hata ivyo Kama itakuwa siyo rahisi kufanya hesabu rahisi usiumize kichwa kwani mtoa huduma Katika klinic ya wazazi atafanya kwa ajili yako.


.Kipimo Cha tumbo.

Hiki ni Kipimo ambacho hupimwa ili kujua ukubwa wa tumbo la mama katika kila hudhurio,ukubwa wa tumbo huwakilisha  ukubwa wa mtoto kwa kwa wiki,Kipimo hiki hupimwa na mkunga au daktari.

Kuna Sababu nyingi ambazo zinaweza sababisha tumbo likawa kubwa au dogo, kwaiyo si vema kujifanyia Kipimo hiki mwenyewe Bali mtaalamu ndio atakupima.

Uwepo wa maji mengi katika mfuko wa uzazi,uwepo wa watoto zaidi ya wawili na uwepo wa uvimbe vinaweza sababisha tumbo kuwa kubwa zaidi,kwahiyo njia hii siyo sahii Sana katika kukadiria ukubwa wa mimba ivyo kusaidia kukadiria tarehe ya matazamio.

.Kipimo Cha utrasound.

Hii ni njia ambayo huweza kutambua umri wa mimba kwa usahihi zaidi ivyo ni rahisi kukadiria tarehe ya matazamio ya kujifungua .


*Kama nilivyo sema awali wachache Sana wanaweza wakajifungua Katika tarehe za makadirio,lakini wengi hawatojifungua Katika tarehe ambazo hukadiriwa,kwa kawaida uchungu unaweza kuanza kwa kuwahi wiki mbili kabla ya tarehe ya makadirio au wiki mbili Baada ya tarehe ya matazamio.



Pia unaweza ukajiunga barua pepe yangu kupokea makala mpya moja kwa moja kwenye simu yako pindi tu zikiwekwa.


KARIBU.




Share:

Tahadhari matumizi ya dawa Wakati wa ujauzito⚠️⚠️⚠️⚠️







Matumizi ya dawa Wakati wa ujauzito.

Kipindi Cha mimba ni kipindi ambacho hudumu kwa muda wa wiki 36 hadi wiki 42,katika kipindi hiki mtoto hutegemea kila kitu kutoka kwa Mama katika ukuaji na maendeleo yake tumboni.

Kipindi Cha miezi mitatu ya mwanzo mtoto hukua kwa haraka Sana na ndiyo kipindi viungo vya mwili hutengenezwa,Wakati huu mtoto huitaji virutubisho mbali mbali ili viungo vyake viweze kutengenezwa kiukamilifu.

Kwakuwa mtoto hutegemea kila kitu kutoka kwa mama yake ,basi kitu ambacho Mama hukitumia humfikia moja kwa moja mtoto bila ya kujali kizuri au siyo kizuri hivyo kuleta matokeo chanya/ hasi katika ukuaji wa mtoto.

Kuwepo kwa maduka ya dawa kumesababisha  matumizi ya dawa ya holela pasipo kupata ushauri kutoka kwa wataalamu,dawa zilizo nyingi huwa hazina madhara kwa mtoto lakini kuna baadhi ya dawa ni hatari endapo zikitumika na kwani huweza leta shida Katika ukuaji na maendeleo ya mtoto na pengine kusababisha ulemavu kwa mtoto.

Moja ya dawa ambazo hutumiwa  holela ni dawa za kutuliza maumivu,watu wengi hudhani dawa za maumivu haziwezi leta athari kwa mtoto, lahasha dawa hizi zinaweza kuleta athari Kama kawaida endapo mtumiaji hato pata maelezo kutoka kwa wataalamu.



Athari zitokanazo na matumizi holela ya madawa wakati wa ujauzito.

Utumiaji wa dawa holela unaweza ukamuathiri mtoto kwasababu dawa hizo humfikia mtoto moja kwa moja,athari ambazo zaweza tokea ni pamoja na:

.Kuharibika kwa mfuko wa uzazi (placenta) /makao ya mtoto,mfuko huu humsaidia mtoto kupata chakula,kupumua,kutoa taka mwili ,pia kumkinga mtoto dhidi ya vimelea vya magonjwa,kwahiyo kuharibiwa kwa mfuko huu husababisha mtoto kukosa mahitaji yake ya msingi Katika ukuaji wake hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto.

.Dawa huathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto hivyo kuongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu wa viungo kutoka na viungo kushindwa tengenezeka sawa sawa /kuzaliwa akiwa na afya iliyo dhoofu.

.Kuongeza uwezekano wa mimba kuharibika,kuna baadhi ya dawa hazishauriwi kabisa kutumika katika miezi fulani ya ujauzito na zingine Katika kipindi chote Cha ujauzito,endapo dawa hizo zikitumika huweza kusababisha mimba kutoka / kuharibika.

.Matumizi ya dawa pia yanaweza kusababisha Mama kupata uchungu na kabla ya wakati .


Hata hivyo kuathirika kwa mtoto hutegemeana na mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na:

.Aina ya dawa ambayo mama ameitumia, haimaanishi kila dawa yaweza leta athari kwa mtoto hapana ila Kuna baadhi ya dawa hazishauriwi kutumika na endapo zitatumika huleta athari moja kwa moja.

.Muda ambao dawa imetumika,Kadiri dawa ambazo hazishauriwi kutumika wakati wa ujauzito zinavyo endelea kutumika ndivyo kadiri athari kwa mtoto inavyo zidi kuongezeka.

.Kiwango Cha dawa ambacho kinatumika, daktari na wataalamu wengine wanajua kiwango cha dawa ambacho hutakiwa kitumike,lakini kutokana na kutumia dawa bila kupata ushauri unaweza kuzidisha kiwango Cha kawaida Cha matumizi ya dawa hiyo ,dawa inaweza ikawa haina madhara wakati wa ujauzito lakini endapo ikitumika kwa kiwango kikubwa inaweza leta athari kwa mama na mtoto.

.Dawa imetumika pekee yake au ime changanywa na dawa zingine,unaweza kutumia dawa moja/ mbili / tatu bila kuleta athari kwa mtoto endapo dawa hizo zitakuwa hazina madhara ,Lakini kadiri unavyo changanya madawa bila ushauri ndivyo uwezekano wa kutumia dawa isiyo sahii unavyo ongezeka.

.Ukubwa/umri wa mimba,Kuna baadhi ya dawa hazishauriwi kutumika katika miezi mitatu ya mwanzo,baada ya miezi mitatu ya mwanzo na zingine Katika miezi mitatu ya ujauzito,kwahiyo kadiri utakavyo tumia dawa wakati ambao siyo sahii kwa matumizi yake ,ndivyo kadiri itakavyo leta athari kwa mwanao tumboni.

.Afya ya Mama mwenyewe,ufinyu wa afya ya mama husababisha udhoofu wa ukuaji na maendeleo ya afya ya mtoto tumboni kutokana na kukosa virutubisho na uwezekano wa kushambulia na Magonjwa,vile vile utumiaji wa dawa Mara kwa Mara pasipo ushauri huleta athari kwa mtoto.



Nini ufanye Sasa kuondoa  athari kwa mtoto.

.Hakikisha ukiugua wakati wa ujauzito usitumie dawa yoyote bila kupata ushauri kwa daktari,mkunga au mtaaalamu wa dawa.

.Pia Kama ulikuwa unatumia dawa yoyote awali na ukahisi ni mjamzito ,ni vema Kuacha Kutumia dawa izo au ukapata ushauri kwa wataalamu ili kujua Kama ni salama/siyo salama kwa mwanao.

.Katika kipindi cha miezi mitatu ya awali ya ujauzito ni ngumu Sana kutambua Kama ni mjamzito lakini endapo ukatambua inashauriwa pindi unavyo kwenda hospitali kupata matibabu ni vema kumueleza daktari kuwa ni mjamzito ili asikupe dawa isiyo takiwa ,kwa kuto kujua.

.Ili kuepuka Kutumia dawa Mara kwa Mara hakikisha unakula mlo kamili Mara kwa mara ikiwa ni pamoja na mboga na matunda yakutosha,vile vile hakikisha unafanya mazoezi mepesi ili kuimarisha Kinga za mwili.

.Acha Kutumia madawa ya asili,kwa imani watu wengi hudhani kitu ambacho ni asili hakiwezi kuleta madhara,sawa kinaweza kisilete madhara,lakini ikumbukwe dawa za asili hazina kipimo maalumu Cha dawa,kwahiyo unaweza kuzidisha kiwango na ikamletea shida mtoto, kwaiyo ni vema zikaepukwa.

.Vile vile acha kutumia sigara,pombe na dawa za kulevya kwasababu athari zake hufanana na zile zitokanazo na Utumiaji wa dawa holela.



KARIBU.


Share:
Powered by Blogger.

Recent Posts